KACOU 75: TULIONA NYOTA YAKE
(Ilihubiriwa Jumapili Asubuhi, Juni 1, 2008 huko Adjame kasha huko Anyama, karibu na Abidjan – Ivory Coast) 1 Akina ndugu, jueni kwamba Ukristo wa awali unaweza tu kuwa kurudi Edeni, ambako mwanadamu alianguka ili kumwinua milele! Hapo mwanzo, haikuwa mitala! Mungu alichukua ubavu mmoja tu kutoka kwa Adamu na kwa ubavu huo, akamfanya mwanamke moja na nyoka alipomwaibisha, Mungu hakuthubutu kubadilishia au kumuumbia Adam mwanamke mwingine ! Lakini mitala imetajwa katika Mwanzo 4 kuwa ni moja ya matendo ya wana wa shetani duniani. 2 Angalia jozi hizi za njiwa, jozi hizi za wanyama, maumbile yote yanafundisha kwamba kuoa wanawake wengihaikuwa taasisi ya asili ya Mungu! Ni mjukuu wa Kaini aliyefanya hivi! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. Unaweza kuja hapa na wake wawili au watatu, lakini mara tu umejua Ujumbe huu na kupokea ubatizo wako, huwezi kuwa na wake wawili tena. Na kama ndugu akifanya hivyo, hawezi kamwe kukubaliwa katika Ujumbe huu hata miaka kumi au ishirini kutoka sas...