KACOU 76: NEEMA ILIYOTOLEWA AFRIKA
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi, Juni 15, 2008 huko Anyama karibu na Abidjan – Ivory Coast)
1 Kama kwa mataifa mengine ya dunia, Mungu ametoa neema kwa Afrika. Lakini kabla ya mahubiri, ningependa kuanza na maelezo. Ni kuhusu mahubiri. Natamani kwenye ibada za jioni au kwenye moja ya ibada ya jioni kwa wale walio wawili au watatu, mahubiri yawe kulingana na chaguo la mhubiri au mchungaji yasomwe na atoe maoni yake anaposoma.
2 Vema! Mtu ambaye alisikiliza mahubiri "Tuliona nyota yake!" akasema, "Ndugu Philippe , waandishi bado waliwajulisha Mamajusi kwamba Mfalme wa Wayahudi atazaliwa Bethlehemu!" "Nilisema hapana! Mamajusi hawakuhitaji! Ilikuwa nzuri tu kwa Herode na Wayahudi. Waandishi, licha ya mstari huu, hawakuweza kujua ni yupi kati ya watoto wote waliozaliwa wakati wa miaka miwili alikuwa Kristo! Na hakuna mstari ungeweza kuelekeza nyumba ila nyota ndio ilionyesha! [Mhr: Kusanyiko linasema, Amina! ”].
3 Biblia inasema, “Nao walipomsikia mfalme, wakaenda zao; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikafika na kusimama juu ya mahali alipokuwa yule Mtoto. Mnaona? Ni nyota pekee ingeweza kufanya hivyo! Na mtu yeyote, hata asiyejua kusoma na kuandika, angeweza kwenda kutoka Mashariki kumtafuta Masihi bila kumwandikia mtu yeyote au kutumia kitabu chochote!
4 Ikiwa wewe ni mteule na unaishi vizuri, utaona kwamba Wokovu ni jambo rahisi zaidi lililopo! Mnaona? Jambo kuu ni kuona nyota! Na tu kufuata nyota! [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”
5 Je! Tegemeo la Wayahudi na la Rais Herode, mjukuu wa Ahabu ilikuwa ipi? Mstari wa 3 na 4 inasema hivi: “Lakini mfalme Herode aliposikia alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye; Akawaita wakuu wote wa makuhani na waandishi wa watu, akawauliza, Kristo angezaliwa wapi”. Mnaona? Tegemeo lake ni wakuu wa makuhani na waandishi. Na tegeme la wakuu wa makuhani zilikuwa hati kunjo zile zile za zamani.
6 Sasa mtu mwingine aliniandikia akisema kwamba Marcus Garvey fulani anadaiwa kusema katika kanisa huko Kingston, Jamaika, "Tazama Afrika, ambapo mfalme atavikwa taji." Akaniambia tena, “Ninapokusikiliza, nabii mpendwa, ninaona kitu kikija ambacho kinaweza kuonekana kutoka pembe zote za dunia! Kitu kikubwa na kitakatifu kuliko Haile Selassie!”.
7 Ndugu, hayo yote ni mazuri sana! Lakini si suala la kuona hapa nabii wa Kiafrika au fahari kwa Afrika bali ni kutafuta Wokovu! Na nyie Waafrika msipokuwa makini wazungu watawatangulia katika Ufalme. Mimi siko na sitawahi kuwa mhamasisha Uafrika! Na Kelele ya usiku wa manane si ilani dhidi ya mashirika na mifumo ya dunia bali ni ufunuo wa Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu wa kila aaminiye! [ Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
8 Vema! Nataka kusoma kwanza kifungu katika 1 Wafalme 10:13…Nilisoma kwamba: “Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, [yote] aliyoyaomba, zaidi ya hayo aliyompa kwa kadiri ya uwezo wa mfalme Sulemani. Alirudi, alienda katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
9 Sasa, angalia ya kwamba aina mbili za mabikira hupokea mahubiri ya nabii aliye hai wa wakati wao, lakini ni wale tu wenye busara wanaopokea mahubiri ya maisha ya nabii ambayo ni siri nyuma wa Ujumbe. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
10 Nabii mjumbe anaweza kumtangaza Kristo, kuzungumza kwa niaba ya Kristo au kumdhihirisha Kristo. Yusufu alimdhihirisha Kristo na Biblia inasema Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini aliposimama mbele ya Farao na akapewa ufalme wote! Na kama Bwana Yesu Kristo, Yusufu aliuzwa. Na mle gerezani alikuwa upande wake wa kushoto mkuu wa waokaji aliyeuawa na kulia kwake mkuu wa wanyweshaji aliyeokolewa.
11 Jueni kwamba umeme unapokuja kutoka Magharibi pamoja na kanisa la Kibranhamisti na kugusa Afrika, hauwezi kumpata isipokuwa huyo tu! Na watu wa mataifa yote ya dunia wanaokolewa pamoja naye. Kama vile vile, wakati wa kila nabii, watu wa kila jamii ya dunia wanaokolewa pamoja na nabii huyu. Na kwa upande huu, ni katika maana hii ya kiroho kwamba Bwana anamwita "Malkia wa Kusini", ambayo ni kusema mwanzo wa Kanisa la Afrika kuwa na chapa za Kristo. [ Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!”].
12 Si kazi ya umeme bali ni kile ambacho umeme unapaswa kusafisha, kukifanya cheupe na kutakaswa ili kuwasilisha bila doa au kunyanzi kwenye unyakuo! Kwa hiyo Makanisa yatainuka na kuinuka na kuinuka tena lakini kiroho bado ni Kanisa lile lile tangu siku za mitume, likijidhihirisha kulingana na mataifa ya dunia. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
13 Ni kipindi cha kwanza kabisa kwa Afrika na hakuweza kuita isipokuwa kwa namna hii. Kutakuwa na aina na aina mpaka wanaonekana mwisho wa kuwika kwa jogoo, si kama huyu bali kama bikira safi, asiye na doa wala kunyanzi.
14 Yeye atatokea na kutokea tena na tena kwa namna tofauti na kuonekana mpaka ukamilifu, katika hatua hiyo ya kuwika kwa jogoo! [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Israeli katika sura yake ya kwanza, wakiwa wametoka nje ya uaguzi wa Wamisri, hawakuweza kurithi nchi ya ahadi! Kimwili kizazi kimoja kilianguka na kizazi kingine kikainuka lakini kiroho ilikuwa ni Israeli sawa kupitia Danieli 12:8-10.
15 Kumbuka, Musa alipoenda mbali kwa siku arobaini tu, Israeli walipotoka. Kusema kwamba mbali na nabii mjumbe aliye hai, kanisa haliwezi kamwe kuwa katika mapenzi ya Mungu pamoja na makuhani, ambao ni mitume, manabii wa makanisa, wainjilisti na walimu. [ Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Kwa hiyo, baada ya Bwana Yesu Kristo, Paulo angeweza kuja. Na, hata wakati wa uhai wa Paulo, tuliona ugumu katika kanisa.
16 Na Paulo alipoondoka eneo la tukio, kanisa lilipotoka tena. Na Mungu akainua watumishi kadhaa, mmoja baada ya mwingine. Mtumishi wa Mungu aliinuka juu ya uso wa dunia mahali fulani, na alipokufa, kanisa likageuka tena kuwa upagani. Na Mungu alikuwa akimwinua nabii mwingine. Kwa hiyo, tumejua majina kama John Wesley, Ulrich Zwingli, Martin Luther, John Calvin, John Huss, John Wyclif… Hawa wote walikuwa ni wajumbe ambao Mungu aliwatuma duniani kuliongoza kanisa kutoka katika upagani.
17 Na leo, angalia upagani huu wote juu ya uso wa dunia, Shetani mwenyewe anaketi katika Ukristo. Shetani ameufanya Ukristo kuwa ufalme wake duniani. Roho yake inatenda kazi katika makanisa ya kikatoliki, kiprotestanti, kiinjili na kibranhamisti na watu wanaiita roho takatifu. Wanawake wenye hedhi na pedi chini yao, wanaweka mikono juu ya wanaume, wana hubiri katika makanisa ... Ni nini? Ufalme wa Shetani uko duniani. Na Ukristo ni ufalme wa Shetani. Lakini kama kawaida, kwa sababu ya wateule, Mungu daima atamtuma nabii aliye hai duniani. Na nabii huyo atatoka mahali fulani kupigana na ufalme huu wa Shetani. [ Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
18 Musa na Wayahudi walipotoka Misri, ni Mungu wa Wayahudi ndiye aliyekuwa anaenda kuwashinda wanadamu. Na miungu ya Misri pia ilitoka na kwenda kuwashinda wanadamu. Hivyo, popote Mungu wa Wayahudi anahubiriwa, miungu ya Misri pia itaweka madhabahu zao. Na kulipokuwa na Eliya katika Israeli, kulikuwa na mamia ya manabii wa Baali katika Israeli.
19 Na miaka 2000 iliyopita, Yohana, kwenye Kisiwa cha Patmo, alikuwa ameona kwamba Israeli ingekuwa Sodoma na Misri. Sodoma, kwa sababu ya ushoga. Yohana alikuwa ameona, miaka 2000 iliyopita, kwamba mashoga wangetembea katika mitaa ya Yerusalemu. Na kwamba miungu ya Misri iliyo leo, Wakatoliki, Waprotestanti, wainjilisti na Wabranhamisti wangeenda kuhiji Israeli. Israeli ilipaswa kuwa mahali pa utalii pa pepo. Yohana alikuwa ameliona hilo. Na miaka 2000 baadaye, tunaona hii ikitokea mbele ya macho yetu.
20 Wakatoliki, Waprotestanti, wakiinjili na Wabranhamisti, wana wa pepo wanaenda kuhiji Israeli. Inafurahisha kuona hili! Unabii unaotimizwa mbele ya macho yetu! Mapepo, wana wa shetani wakienda kuhiji na mashoga wakiandamana katika Israeli. Oh! Inapendeza kuona mambo hayo yakitimizwa duniani! Na wakati huo huo, Mungu wa Eliya, Roho wa Eliya pia anatenda duniani akipigana na manabii wa Baali na Yezebeli, akipigana na miungu ya Misri, akipigana na mapepo wa Misri ambao sasa wameimarishwa katika makanisa.
21 Mungu anamwinua nabii mdogo katika mikoa ya Afrika kusema kwa niaba yake. “Wewe, Bethlehemu ya Yuda, si mdogo kabisa kati ya maliwali wa Yuda, kwa maana kwako atatoka mtawala ambaye atawachunga watu wangu Israeli.” [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Unabii unatimizwa duniani lakini ubinadamu hauoni hili. Mnaona ?
22 Mwanadamu ana mapenzi yake ambayo si lazima yawe mapenzi ya Mungu! Lakini Mungu, Mwenyewe, analiangalia Neno Lake ili kulitimiza! Na Neno la Mungu linatimizwa leo kwa ajili ya Wokovu wa wanadamu. [ Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
23 Ulimwengu mzima lazima uandike upya historia ya Wokovu wa wanadamu, lakini wakati huu na Afrika. Si jinsi anavyotaka, si ladha yake bali kulingana na mapenzi ya Mungu! Kwa wale walio nje, ngurumo za radi na hukumu lakini kwa wale walio ndani, kuendelea kupitia dhoruba ya upepo ambayo ni maalumu kwa wakati wa manabii! Na mwenye masikio na asikie!
Sura zinazofanana: Kc.6 na Kc.67
Comments
Post a Comment