KACOU 72: MAAGIZO JUU YA UINJILISTI

(Ilihubiriwa Alhamisi 08 Mei, 2008 huko Anyama, karibu na Abidjan – Ivory Coast)

1 Nataka kutoa maagizo juu ya uinjilisti, lakini mniruhusu nizungumzie baadhi ya mambo!  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

2 Kwa wale ambao hawaelewi ninachosema kuhusiana na William Branham, jueni kwamba naamini kabisa kwamba William Branham ni nabii wa kweli aliyetumwa na Mwenyezi Mungu, kulingana na Malaki 4 na Ufunuo 10:7 na kwamba hata Maneno yake yana thamani sawa na maneno ya manabii wa Biblia, lakini siamini kwamba miaka kumi baada ya kifo chake, mmoja wa wale waliomfuata angeweza kupeleka nafsi moja Mbinguni.  Ujumbe wake ulikuwa wa wakati fulani na wakati huo umepita, zaidi ya miaka 40.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

3 Kuhusu maelfu ya vipeperushi vinavyosambazwa ulimwenguni kote kutoka Ulaya, nadhani ilikusudiwa tu kuandaa jukwaa kwa ajili ya huduma tukufu chini ya hema na kupitia hilo, ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo kama alivyojulisha mwenyewe katika Mihuri Saba.  Mnaona ?

4 William Branham alipokufa, ni Tommy Osborn, mtu ambaye kamwe hakuamini na kumfuata William Branham, ndiye wanabranhamisti walimweka mbele yao na Aprili 11, 1966, kwenye ibada ya mazishi ya William Branham, Tommy Osborn alihubiri.  Hawa wote Billy Paul, Lee Vayle, Joseph Coleman, Perry Green, Orman Neville na Ewald Frank walikuwepo wakati Tommy Osborn alipokuwa akihubiri na kuwapa maagizo na miongozo. 

5  Kiasi kwamba baada ya William Branham, kama Tommy Osborn angetaka, angeweza kuchukua mbele ya Ubranhamisti wote na hata kumruhusu mke wake Daisy kuhubiri kwenye Branham tabernacle!  Hakuna hata moja ya makanisa ya kiinjili ambayo William Branham alilaani inayoweza kukubali kwamba kuhani wa Kikatoliki au hata Papa wa Roma aje kuhubiri kwenye ibada ya mazishi ya rais wao.  Kamwe!

6 Tommy Osborn ameowa Daisy tangu 1942 na ni ono la mke wake analohubiri.  Na hilo, hakuna hata mmoja kati ya hao niliowataja asiyelijua.  Sasa mnaelewa kwamba mielekeo miwili mikuu ya Wabranhamisti ni kama pande mbili za sarafu moja!  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

7 Jumapili iliyopita, Mei 4, 2008, tulibatiza kusanyiko la wanabranhamisti huko Dabou.  Si muda mrefu uliopita, tulibatiza kusanyiko lingine la Wabranhamisti karibu nao. Kusanyiko ambalo lilikuwa chini ya uongozi wa Ewald Frank.  Hata makusanyiko ya kibranhamisti yanayotupinga ni mabirika yaliyopasuka kwa sababu watu wanatujia kutoka huko!  Oh Ujumbe mtukufu!  Nuru ya thamani ya mataifa!  Sambalati na Tobia hawana nguvu kwa sababu ni nuru kutoka Mbinguni na hakuna awezaye kuizuia.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].


8 Kama Adamu, Mungu alinipa uwezo katika kizazi hiki cha kuwapa wanyama majina.  Mungu alileta mnyama mbele yangu na nikamwita simba na hilo lilikuwa jina lake.  Niliwaambia Waprotestanti: nyinyi ni kondoo waume na hilo lilikuwa jina lao.  Niliwaambia wakiinjili: nyinyi ni mbuzi na hilo lilikuwa jina lao isipokuwa watubu.  Ikiwa wewe ni Mkatoliki, wewe ni mnyama na ndiyo maana huwezi kumwamini nabii aliye hai wa wakati wako.  Ikiwa wewe ni Mprotestanti, wewe ni mnyama na ndiyo maana huwezi kumwamini nabii aliye hai wa wakati wako.  Ikiwa wewe ni mwinjilisti, wewe ni mbuzi na ndiyo maana huwezi kumwamini nabii aliye hai wa wakati wako.  Ikiwa wewe ni mwabranhamisti, wewe ni mnyama wa Danieli ambaye hakutajwa jina na ndiyo maana huwezi kumwamini nabii aliye hai wa wakati wako.  Ninyi ni wanyama wa aina tofauti, lakini Nguvu za Mungu siku moja zitawafanya muelewane na kukusanyika pamoja.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

9  Kwa kumalizia na kuja kwenye maagizo ya uinjilisti, ningependa kuachia wa wabranhamisti sehemu ya barua ambayo Alexis Barilier alikuwa amemwandikia Ewald Frank mwaka wa 2006 ili watafakari. Ninaisoma.  Alexis Barilier anazungumza na Ewald Frank sasa: “… Kama mahubiri kutoka kwa Ndugu Branham ambayo tumepokea yangetuamsha, tungeamka muda mrefu uliopita.  Kumbuka kwamba mimi pia najiweka katika cheo sawa na wewe, kwa sababu sikuzote nimekuwa nikitafuta kuleta maneno yaliyoongozwa na Biblia tu, na ni wazi kwamba mahubiri yangu, hata yako hayakuweza kuzuia wanawali wasilale.  Baba yetu wa mbinguni alijua hilo na ndiyo maana alizungumza juu ya Kelele ambayo ilikuwa ya kuwaamsha wanawali, si katika zamu ya saba, ambayo ni ya mwisho, ambayo Roho na Bibi-arusi walio tayari wanaweza kusema: Njoo!  Lakini usiku wa manane kwa sababu wanawali wameacha kusonga mbele ...

10 Sasa swali ni, je, tunafahamu kwamba wanawali wote walilala, hata sisi pia, na kwamba hii ilitokea baada ya wanawali kujibu mwito wa Ujumbe ulioletwa na Ndugu Branham?  Je, tunafahamu kwamba ikiwa mahubiri yetu yote hayakuweza kuwazuia wanawali wasilale, hayataweza kuwaamusha pia, lakini kwamba Bwana ameahidi kuwaamsha sio tu wanawali wenye hekima, bali pia wanawali wapumbavu Kelele ya usiku wa manane… Kelele pia ni Ujumbe kwa sababu labda ni Kelele ambayo inaonyesha Ujumbe wa furaha au wa dhiki, au Ujumbe wa wito wa kuamka na wa kukemewa, kama ilivyo katika Mathayo 25:6-7.

11  Ujumbe uliokabidhiwa kwa Ndugu Branham unapaswa kumtayarisha Bibi-arusi kwa ajili ya karamu ya Bwana Arusi.  Lakini ikiwa wanawali wamelala, watawezaje kujiandaa, wataweza je kutimiza Ufunuo 19: 7-8 na kuvaa matendo ya haki ya watakatifu waliyopewa ili kujivika wenyewe?  Tunachohitaji sana leo ni kuamshwa na Kelele la usiku wa manane iliyoahidiwa.  Je, inawezekana kua Bwana Yesu anamtumia mtu mwingine zaidi ya Ewald Frank au Alexis Barilier kuwaamsha mabikira?  Hakika ndio!".  Amina!

12 Haya ni maneno Alexis Barilier aliyomwambia Ewald Frank.  Na kama mbranhamisti anaweza kuelewa, na aelewe.  Kwa sababu ikiwa licha ya Ujumbe wenye nguvu wa William Branham, wanawali wote walilala usingizi ikiwa ni pamoja na Ewald Frank na Alexis Barilier, ni dhahiri kwamba yule ambaye atawaamsha wanawali hawa atatoka mahali fulani.  Na mnamo Aprili 24, 1993, Mungu alimwinua nabii kutoka mahali fulani kama manabii katika Biblia ili kumwamsha Bibi-arusi.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

13 Vema!  Ninakuja kwa maagizo!  Kuna nchi kadhaa ambazo ziko kwenye orodha ya nchi ambazo Ujumbe tayari upo!  Lakini haijalishi uko katika nchi gani, unapogundua Ujumbe huu, una wajibu na shurti mbele za Mungu, kulingana na Ezekieli 33, kufanya Ujumbe huu ujulikane karibu nawe.  Wazazi wako lazima waujue Ujumbe huu, wanaokufahamu lazima waujue Ujumbe huu; kila mtu anapaswa kujua Ujumbe huu.  Hata kama ni lazima wakukatae, lakini lazima waujue Ujumbe huu.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].

14 Kwa hekima na upole, lazima ujulishe Ujumbe huu kwa watu wote wanaokuzunguka.  Huwajibiki kwa miitikio ya watu bali unawajibika kuwafanya wausikie.  Hata kama wewe ni mwanamke, una jukumu.  Kama Maria Magdalene, Elisabeth, Suzanne na wanawake waliokuwa karibu na Bwana Yesu Kristo, unayo Maneno ya Uzima wa Milele ya kizazi chako mikononi mwako na lazima uhakikishe kwamba kila mtu anayasikia.  Ninyi akina dada, mnaweza kutoa ushuhuda au kueleza Ujumbe wanaowazunguka.  Lazima ujue kwamba uwezo wote ambao Mungu amekupa ni kwa ajili ya Wokovu.

15 Ikiwa wewe ni tajiri, ni kwa ajili ya wokovu.  Kila kitu kitaangamia duniani, lakini ulichofanya kwa ajili ya Mbinguni hakitapotea kamwe.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!].  Jengeni majengo, nunua magari mazuri, lakini yote ni wazimu mbele za Mungu.  Lakini cha muhimu ni kile ulichofanya kuokoa Wateule katika kizazi chako.  [Ndl.: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

16 Unapaswa kusoma au kusikiliza kila mahubiri na kulingana na imani ya aliye mbele yako, unajua ni mahubiri gani utampa na Mungu atashugulikia mengine.  Huwajibiki kwa majibu yake, si lazima aamini lakini una wajibu wa kumfanya agundue Ukweli huu.  Na katika hukumu, hatasema kwamba hakusikia jina la Nabii Kacou Philippe duniani.  Na mwenye masikio na asikie.  

Sura zinazofanana : Kc.15 ,Kc.16 , Kc.108]


Comments