KACOU 75: TULIONA NYOTA YAKE

(Ilihubiriwa Jumapili Asubuhi, Juni 1, 2008 huko Adjame kasha huko Anyama, karibu na Abidjan – Ivory Coast)


1 Akina ndugu, jueni kwamba Ukristo wa awali unaweza tu kuwa kurudi Edeni, ambako mwanadamu alianguka ili kumwinua milele! Hapo mwanzo, haikuwa mitala! Mungu alichukua ubavu mmoja tu kutoka kwa Adamu na kwa ubavu huo, akamfanya mwanamke moja na nyoka alipomwaibisha, Mungu hakuthubutu kubadilishia au kumuumbia Adam mwanamke mwingine ! Lakini mitala imetajwa katika Mwanzo 4 kuwa ni moja ya matendo ya wana wa shetani duniani. 

2 Angalia jozi hizi za njiwa, jozi hizi za wanyama, maumbile yote yanafundisha kwamba kuoa wanawake wengihaikuwa taasisi ya asili ya Mungu! Ni mjukuu wa Kaini aliyefanya hivi! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. Unaweza kuja hapa na wake wawili au watatu, lakini mara tu umejua Ujumbe huu na kupokea ubatizo wako, huwezi kuwa na wake wawili tena. Na kama ndugu akifanya hivyo, hawezi kamwe kukubaliwa katika Ujumbe huu hata miaka kumi au ishirini kutoka sasa.

3 Na nilisema kwamba baada ya miezi saba ya kuishi pamoja, ikiwa mwanaume anaenda zaidi ya mara tatu kwa wiki na mke wake, lazima aende kuungama! Mnaona? 

4 Vema! Ninakuja kwenye somo langu: Tuliona nyota yake ... Kwa hili nitasoma katika Mathayo 2: 1-2 ... "Basi, baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethlehemu ya Yudea, kwa siku ya mfalme Herode, tazama! Mamajusi kutoka mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa? Kwa maana tuliona nyota yake mashariki, na sisi tumekuja kumsujudia.”

5 Haya! Mungu wa Israeli alikuwa amewatumia Kora, Dathani na Abiramu kule jangwani lakini kosa lao lilikuwa ni kwenda kinyume na Musa na kufikiria kuwa wanaweza kuwa sawa na Musa. Sasa, kuwa sawa na Musa na kumfanya Mungu akubali hilo, hilo ndilo halipaswi kujaribiwa. Na kwamba nabii aliyeitwa Balaamu hakuelewa! Mungu wa Israeli alikuwa anazungumza naye kweli na alifikiri yeye ndiye nabii-mjumbe wa wakati wake lakini Musa alipokaribia, alipomwona Musa, ilimbidi aache nafasi na kukaa kimya kama Yohana Mbatizaji! Lakini hakuelewa hili na kusukumwa na fedha na umaarufu na sifa yake ya zamani, alienda kinyume na Musa!

6 Na ni Balaamu huyu aliyetabiri kwamba nyota ingetoka kwa Yakobo! Balaamu alisema katika Hesabu 24:17: “Nitaiona, lakini si sasa; Nitaitazama, lakini sio kwa karibu. Nyota itatoka katika Yakobo, na fimbo ya enzi itatokea katika Israeli, na kuzipenya ncha za Moabu, na kuwaangamiza wana wote wa ghasia.” Na hii ilifundishwa kutoka kizazi hadi kizazi! Unaona?

7 Ingawa Balaamu alichukua njia mbaya, Neno la Mungu kinywani mwake lilikuwa kweli. Na kama Balaamu, mbali na mpanda farasi Mwafrika, William Branham alizungumza habari zake, ni Waafrika wangapi hawakutangaza kwamba Mungu Mwenyezi siku moja angeipa Afrika ishara! Lakini badala ya kungoja hilo, tayari wako Yerusalemu pamoja na makuhani wakuu. Basi wataonaje ishara hii? 

8 Sasa, angalia jambo hili: Wakati wale mamajusi walipoiona hiyo nyota, walijiacha waongozwe na nyota hiyo kama vile Nguzo ya Moto ilivyowaongoza Wayahudi jangwani. Watu hawa wenye hekima walijua tu kwamba Yerusalemu palikuwa patakatifu zaidi, mahali pa kiroho zaidi duniani na kwamba Mungu wa Mbinguni alikuwa amefanya Jina lake likae humo!

9 Yerusalemu lilikuwa kitu cha kiroho na kitakatifu zaidi duniani. Zaidi ya kiroho na takatifu kuliko Jiji la Vatikani! Na ilikuwa katika Yerusalemu kwamba taasisi kuu za biblia zilipaswa kutafutwa na ikiwa Mungu alipaswa kukamilisha kazi duniani isingeweza kuwa katika mji mwingine isipokuwa Yerusalemu, mji wa Daudi.

10 Na wale mamajusi walipoona kwamba kundi la nyota lilikuwa limeelekea Yerusalemu... hapo mwanzo walikuwa wameifuata ile nyota vizuri sana lakini walipoiona Yerusalemu, wakasemezana: “Atukuzwe Mungu wetu! Ahsante Mungu, tupo hapa!!! ". Waliingia Yerusalemu lakini nyota haikuingia! Nyota haikuweza kuingia ndani yake! 

11 Na mara moja huko Yerusalemu, waligundua kuwa nyota imetoweka, wakasema: "Tupo hapo, kilichobaki kwetu ni kupata kituo cha kuzaliwa! ". Lakini kwa mshangao wao, wakati unaruka na hakuna chochote! Hawaelewi tena! Wakaanza kuulizana na kila mtu ili habari ziwafikie wakuu wa makuhani kisha kwa upande wao wakamjulisha Mfalme Herodiwalipokuwa pamoja naye mezani. Mamajusi watatu walikuwa wakimtafuta Mfalme wa Wayahudi ambaye angezaliwa chini ya ishara ya kimbingu! 

12 Biblia inasema kwamba Herodi na Ukristo wote, yaani, Yerusalemu lilichanganyikiwa! Unaona? Wakati fulani wachungaji walikuwa wamewaambia juu ya wimbo fulani wa malaika na walikuwa wamesema kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya shule yao ya uchungaji, kwa sababu ya makanisa yao ao ni kwa sababu ya ujumbe wa nabii fulani mwenye alikuwa amefika tu Yerusalemu. Lakini hapa , mamajusi walikuja kutoka mashariki ili kuwaambia kuhusu ishara ambayo walikuwa wameona huko. Zamani walikuwa wachungaji na sasa wao ni mamajusi. Herodi na Yerusalemu ilichanganyikiwa. Mnaona?

13 Sasa nini kilitokea? Mamajusi walipoona Yerusalemu, walienda kwa makuhani wakuu ili kujua kilichokuwa kikiendelea! Walikuwa na hakika sana hivi kwamba wakauliza, “Yuko wapi Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa?” Lakini wale Wayahudi wote waliojazwa na Roho Mtakatifu waliokaa katika Neno la Mungu hawakujua lolote kulihusu! 

14 Vivyo hivyo, wachungaji walipowaelezea kuhusu wimbo wa malaika, hawakujua lolote! Wachungaji wangeweza kusema, “Je, hii si kazi isiyo ya kawaida ya Mungu? Tunakumbuka kwamba Mungu alipomuumba Adamu, malaika waliimba katika nchi za Edeni! Je, si mtoto aliyezaliwa katika mazingira haya? ". Wakasema, “Hapana, hapana! Kuna mmoja, lakini ni mtoto wa mkulima asiyejua kusoma na kuandika ambaye haendi kanisani! Mkulima anaitwa Kacou Daniel na mkewe anaitwa Marie”. Mnaona? 

15 Yerusalemu lilikuwa likifanya kazi zake nyingi zisizo za lazima! Na baada ya kuingia mitaani, mamajusi walitaka kuuliza lakini watu walikuwa na haraka sana ili wasichelewe kazini, kwa shughuli zao, kwa mkutano wa maombi au kwa mazoezi ya kwaya! Kama vile babu na babu zao walivyofanya katika siku za Noa.

16 Makuhani waliposikia hayo, walitazama juu angani na hawakuona kitu, wakasema, “Ni lazima museme kwamba muliona nyota! Ni kwetu sisi makuhani kuonyesha kama hii inahusiana na kuzaliwa kwa Mfalme wa Wayahudi au la. Katika hili hukuwa na hekima”. Makasisi wengine walisema, “Si jambo la pekee; ni kutokana na hisia kwamba ulifikiri hivyo. Ni nyota kubwa tu. Na wakati munatembea, mulihisi kama anasonga. Sio hivyo! ".

17 Kisha wale mamajusi wakatambua kwamba walikuwa wamefanya kosa kwa kuacha ile nyota. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. Mamajusi walikuwa wameanza vizuri! Kama Musa na Israeli kule jangwani, ile nyota ilikuwa tegemeo yao! Nyota ilipokuwa ikienda kasi, walienda kasi, nyota ilipokuwa inazunguka, walikuwa wanazunguka! Nyota iliposimama, walisimama! Ilikuwa ni tegemeo wao ! Tegemeo yuko hai ! Tegemeo ya wana wa Mungu ni hai! Wakati mtu amekufa, hata awe mkubwa kiasi gani, hawezi kuwa Tegemeo aliye hai! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

18 Mayahudi walipotoka Misri, pamoja na wana wa Ibilisi, walisema: Tegemeo letu ni Nabii. Ni Musa!” lakini Mungu aliona mioyo yao. Bado hapakuwa na Biblia wala gombo na walilazimika kusema kama wana wa Mungu kwamba tegemeo wao ndiye nabii aliye hai kati yao! Lakini Mungu alijua kwamba kama vile malaika hawakujitiisha Kwake Mbinguni kwa sababu Yeye ni malaika kama wao, wana wa Ibilisi hawangejitiisha kamwe kwa nabii aliye hai kati yao kwa sababu nabii huyo ni mtu kama wao! 

19 Waliposema “Tegemeo yetu ni Musa, Nabii aliye hai miongoni mwetu! Mungu alijua huko Mbinguni kwamba ni uwongo. Wana wa Ibilisi hawawezi kumkubali kiumbe hai kuwa tegemeo. Ndipo malaika wa mauti akasimama lakini Mungu akamwambia, “Waache! Kwa wakati uliowekwa, watatengwa”. [Ndl: kusanyiko linasema: “Amina! "].

20 Wana wa Ibilisi wanapendelea kitabu kuwa tegemeo kama vile baba zao siku zote walivyopendelea kichawi, vitu iwe tegemeo kwao. Mwana wa Ibilisi anaweza kuwa na kipande cha chuma kuwa tegemeo lake, anaweza kuwa na kitu kama tegemeo kwake, na kwa njia hiyo hiyo Mungu alijua ya kwamba siku moja kitabu kingekuwa tegemeo yao. Wanapendelea manabii waliokufa kwa sababu ya bidii yao kwa imani ya mizimu ambayo tunaiona sana hapa Afrika. Ndiyo maana mara tu Musa alipokufa walisema: “Sisi tumetokana na Musa! Tegemeo yetu ni gombo la Musa”, yaani vitabu vitano vya Musa. Na pepo huyu amefanya kazi duniani mpaka leo! 

21 Isaya aliponena, walisema, “tegemeo yetu ni Biblia. hatuamini mwanadamu ! Tunaamini katika Biblia!” Yohana Mbatizaji alipozungumza, walisema: “Tegemeo yetu ni Biblia. hatuamini kitu kingine chochote!” Na wana wa shetani waliokuwa pale wakipiga kelele, “AMINA! ". Naye Yohana Mbatizaji hakujua la kusema! Lo jinsi manabii walivyoteseka! Wakati wa uhai wa nabii, alianzisha wana wa Mungu karibu naye lakini wakati hayupo, ni wana wa shetani ambao wanakamata ukuhani ili kuharibu njia yoyote ya Wokovu. Mnaona?

22 Wale mamajusi walipoiacha ile nyota, walikuwa sasa pamoja na makuhani na Mafarisayo na Masadukayo na hao walitumia muda wao kuwaeleza wale mamajusi jinsi kivuko cha Bahari ya Shamu pamoja na Musa kilivyokuwa na utukufu na kile ambacho Musa alikuwa amefanya. Musa alikuwa amefanya huko Misri. Na nabii kama huyo alikuwa amefanya hivi, nabii kama huyo alikuwa amefanya vile. Walikuwa wakieleza historia. Walikuwa wakikunja gombe, wakionyesha hili, wakionyesha hilo. Yote haya! Badala ya kuwauliza mamajusi wawaeleze kuhusu nyota iliyo hai na kila kitu walichokiona pale. 

23 Kwao, mamajusi ni wa pagani hawana kitu cha kuwafundisha. Na ikiwa Mungu atasema na dunia, ni kupitia kwao makuhani, walio wa kiroho zaidi duniani. Je, unaona kiburi kinachorudiwa leo? Na badala ya kuwasikiliza hawa watu wadogo waliopata nyota katika wakati huu tunaoishi, badala ya kuwaambia hawa watu wadogo: “Tuambie kuhusu nabii Kacou Philippe. Yeye ni nani? Anatuletea nini ya mpya ?     Je, maono makubwa ya Aprili 24, 1993? Tunataka kuelewa. Tunataka kujua. ". Badala yake, wanasumulia historia: Yesu alifanya hivi, mtume fulani na fulani alifanya vile, na kadhalika ... Wao ni wana wa Ibilisi. Na hii ni historia ambayo inarudiwa. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

24 Lakini yale ambayo hao marabi wakuu hawakuweza kufanya, kafiri alikuwa amefanya. Mnaona? Mfalme Herodi alikuwa amefanya hivyo, lakini kwa nia mbaya. Alikuwa amewauliza mamajusi kumwambia tangu wakati nyota ilipotokea na mambo hayo yote. Lakini waandishi na Mafarisayo na watu wote hawakujua. Unaona? Wachungaji hawa wakuu, waheshimiwa hawa, maaskofu hawa hawakuwa na wazo hili kwa sababu ya kiburi chao. Na hili ndilo linaloendelea hadi leo duniani kwani Mungu alirudisha tena nyota iliyo hai inayosonga kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

25 Sasa sikilizeni hili: Ni kweli kwamba Biblia ilisema kwamba nyota ingetokea, lakini kama wale mamajusi wangeichukua kwa tegemeo Biblia ile ile iliyowaambia kwamba nyota ingetoka kwa Yakobo, hawangeenda kamwe kupata lengo walilokuwa wakitafuta! Lakini tegemeo yao, kiongozi wao na alama yao kuu, ilikuwa nyota iliyo hai! Walikuwa wakitembea na nyota, walikuwa wakizungumza na nyota na nyota ilikuwa ikiwajibu na uwepo na anga ya nyota ilikuwa nzuri sana! [Ndl: kusanyiko linasema: “Amina! "]. 

26 Biblia ni ushuhuda wa tegemeo kwa sababu nabii ndiye tegemeo ambayo Mungu amewapa wanadamu! 2 Mambo ya Nyakati 20:20, Hosea 12:14 na Amosi 3:7 hazisemi kutumaini Biblia au nabii ambaye tayari amekufa.  

27 Sasa ona hili: wimbo wa malaika ulisikika nje ya Yerusalemu na wachungaji waliokuja kuwajulisha wakuu wa makuhani! Vivyo hivyo, nyota hiyo ilionekana kwa mamajusi badala ya kuwatokea makuhani! Kwa nini Mungu anafanya hivi kiasi kwamba anawadharau watumishi wake makuhani? Ni kusema kwamba Neno la Mungu hasije kwa kuhani. 

28 Na leo, mitume, manabii wa kanisa, wainjilisti, madaktari, wachungaji, na wote unaowaona ni ukuhani katika Agano jipya. Hata mtume, nabii wa kanisa, mwinjilisti, mwalimu au mchungaji au askofu ana uwezo gani, Neno la Mungu haliwezi kumjia. Unaona? Yesu Kristo alikuwa Neno la Mungu na alipokuja duniani alikwenda kwa Yohana Mbatizaji ambaye alikuwa nabii. Ukuhani napaswa kuwa mwangwi ya kile ambacho nabii aliye hai wa siku yake anasema.

29 Na leo, kama wewe ni mtume, nabii wa kanisa, mwinjilisti, daktari, askofu, mchungaji, na kadhalika…unaweza tu kumtumikia Mungu ikiwa unarejea kile nabii Kacou Philippe anasema. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. 

30 Na ni vivyo hivyo leo kwa viongozi wa Kikatoliki, Waprotestanti, Kiinjili na Wabranhamisti kwa kile ambacho Mungu anafanya hapa. Na inapokuwa hivyo, wakuu wa makuhani wanaharakisha kukataa! Na mnamo Aprili 24, 1993, Malaika wa Bwana anashuka! Malaika wa Mungu anashuka na kuja kuzungumza na mpagani mdogo ambaye hajawahi kufungua Biblia! Lakini je, hufikia Mungu kubadili jinsi anavyotenda? Hapana! Kwa maana ni yeye yule jana, leo, na hata milele!  [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

31 Wimbo wa malaika waenda kwa wachungaji wadogo maskini wasiojua lolote juu ya Mungu badala ya kwenda kwa makuhani. Nyota hiyo inaenda kwa watu maskini wenye hekima ambao hawajui lolote kuhusu Mungu badala ya kwenda kwa makuhani. Na mnamo Aprili 24, 1993, Malaika na Mwana-Kondoo wanakwenda kwa watu wasiojua kusoma na kuandika huko katika mikoa ya Ivory Coast badala ya kwenda kwa makuhani wakuu wa Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

32 Haya! Ni wangapi wanaoamini kwamba Neno la Mungu katika kinywa changu, mimi nabii Kacou Philippe, nihalali, ni thamani sawa na lile la Isaya, Yeremia na manabii wote wa Biblia? Hata ikibidi niseme hivi na kusema vile… na sasa narudi kusema hivi, je nilishindwa? [Ndl: Kusanyiko linasema: “Hapana!”]. Ufunuo ni gumu sana lakini Mungu huwapa wale ambao umekusudiwa.

33 Sasa! Kwa nini mamajusi walikuwa wanaendelea? Mamajusi waliendelea kwa sababu walikuwa na mwongozi hai,tegemeo lililo hai! Na tunataka tegemeo ulio hai kwa sababu Amosi 3:7 haisemi kwamba Mungu hafanyi neno lolote bila kufunua siri yake kwa makuhani ambao leo ni huduma za Waefeso 4:11 lakini Mungu hafanyi neno lolote bila kuwafunulia siri zake kwa watumishi wake manabii walio hai! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

34 Ikiwa Mungu anataka kufanya jambo lo lote leo, hatamfunulia Martin Luther katika kaburi lake kule Ujerumani, hatamfunulia William Branham katika makaburi ya Jeffersonville. Lakini atamfunulia nabii Kacou Philippe anayeishi na kutembea kati yenu. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. Na ikiwa hana nabii wa kuongea na Mamajusi, Mungu anawatumia si Biblia bali nyota! Unaona? 

35 Hata kama hakuna nabii duniani kwa miaka mia tano, Mungu hatafunua Neno lake kwa kuhani, mtume, nabii wa kanisa, daktari, mchungaji, au mwinjilisti! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "]. Na nabii anapoondoka duniani, hiyo ndiyo nyota ambayo imesimama na mradi uishie hapo, uko katika mapenzi makamilifu ya Mungu na Mungu yuko pamoja nawe. Nabii akiondoka duniani, simama pale wapi alipokuacha mpaka uone nyota nyingine inatoka kwa Yakobo! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

36 Je, tegemeo ya mtu aliye hai leo inaweza kuwa mfu? Je, tegemeo ya mtu aliye hai leo inawezaje kuwa kitabu cha Isaya aliyekufa miaka 2,800 iliyopita? Tegemeo ya mamajusi hawa ilikuwa nyota inayosonga! Ikiwa tungewapa Mamajusi tani nyingi za gombo, hawangeweza kuchukua hatua hata moja na juhudi zao zote zingewapeleka mbali na Mungu! Ndio maana, ijapokuwa gombo zilizokuwa humo, Mungu aliwapelekea nyota, tegemeo iliyo hai ! [Ndl: kusanyiko linasema: “Amina! "].

37 Unapotaka kufika huko bila nabii, utasoma kila aina ya vitabu vya dini, utafunga sana, utaomba sana, lakini kila moja ya mambo haya yatawajaza pepo tu na kuwapeleka mbali na Mungu. utaota ndoto mara kumi kuliko nabii! [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

38 Kwa kumaliza, acheni tusome shairi ya 9 na 10 ya Mathayo sura ya 2. Nisoma hivi: “Nao walipomsikia mfalme, wakaenda zao; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikafika na kusimama juu ya mahali alipokuwa mtoto. Nao walipoiona ile nyota, wakafurahi kwa furaha kubwa.” [Ndl: kusanyiko linasema: “Amina! "]. 

39 Nimeipenda hiyo sentensi ya mwisho, naipenda! Unaona? Biblia inasema wakaenda zao na walipofika nje ya Yerusalemu waliona ile nyota tena! Biblia inasema kwamba walipoiona tena ile nyota waliyoiona Mashariki, walifurahi kwa furaha kubwa. Hawakuiacha nyota hata ilipofika kusimama juu ya mahali alipokuwa mtoto mdogo. Amina! 

40 Walipowaacha makuhani, makanisa, Yerusalemu na vyote hivyo, wakaiona ile nyota na walipoiona ile nyota, wakafurahi kwa furaha kubwa. Unaona? Huwezi kuona nyota ndani ya Ukristo huu wa kishetani, makanisa haya ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti, ndani ya misheni na huduma hizi. Huwezi kuona nyota katika ufalme huu wa Shetani lakini inabidi utoke humo. [Ndl: Kusanyiko linasema: “Amina! "].

41 Ndugu, daima weka macho yako kwenye nyota na hutatoka katika mapenzi makamilifu ya Mungu! Kuwa na gombo zote za manabii unazotaka na uzisome lakini tegemeo lako iwe daima nyota hai ya kizazi chako! Ikiwa nyota inakwenda sawa, nenda sawa! Ikiwa nyota itaenda kushoto, nenda kushoto! Ikiwa nyota inasonga mbele, songa mbele nayo. Lakini usiseme, "Isaya alisema hivi, Paulo alisema hivi!" ". Hapana, nenda mbele na nyota!

42 Kama hapo mwanzo kwa Musa, wengi wetu tulitoka Mashariki, lakini kuna watu wenye busara hapa ambao wanafuata nyota na wale ambao hawaifuati! Ni kweli kwamba walifurahi walipomwona mtoto mdogo, lakini Biblia inasema kwamba walipoiona ile nyota, walifurahi sana! Na ninaweza kuwazia furaha kubwa waliyokuwa nayo. Na hii ndiyo furaha ambayo ubinadamu ungekuwa nao kama hasingejitoa kwa makanisa ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti leo. Hii hapa furaha ambayo wanabranhamisti wangepata ikiwa hawakusonga mbele wakati nyota iliposimama mnamo Desemba 24, 1965. Na yeyote aliye na hekima ya kuelewa, aelewe!


Comments