KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI


(Ilihubiriwa Alhamisi jioni, Septemba 04, 2008 huko Anyama, karibu na Abidjan – Ivory Coast)


1 Niliposikia kuwa faili langu la ombi la viza lilipelekwa Ubelgiji ili kuchunguzwa na viongozi wa Ubelgiji, nilitarajia chochote na nilipoona kwamba ilichukua muda mrefu, nilianza kuelewa!  Mimi si mwanasiasa na sijawahi kushirikiana na mtu yeyote na faili yangu ya kuomba viza ilipelekwaje Ulaya?  Japo, hatujasikia kamwe walimkatalia mchungaji viza.

2 Baadaye, nilipokea simu kutoka Ubelgiji ikiniambia kwamba walinikatalia visa! Na kwamba ni Abidjan ndio inapaswa kunieleza sababu!  Nilisema ndani mwangu : Iwe hivyo, lakini sio wavuta sigara wanaopaswa kusema kwamba mimi ni nabii wa kweli au wa uwongo!  

3 Waliowachagua wameshasema kwamba mimi ni nabii wa uongo na najua amtasema vinginevyo!  Ila tu, Ivory Coast, makanisa yake na wakaaji wote wa dunia wanipende kabla ya kuniua!  Hata wakininyima viza mara elfu moja, hiyo haitaniondoa chochote kwa kile niko au ninachotaka kusema! Naweza kumwogopa yule aliye na funguo za Ufalme wa Mbinguni na ambaye anaweza kutoa viza ya Mbinguni!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

4 Maono yanasema kwamba kulikuwa wanaume na wanawake, wadogo na wakubwa, weupe na weusi, watu wa mataifa yote ya dunia wakilia kwa sauti kubwa, “Atukuzwe Mungu wetu!  Atukuzwe Mungu wetu!".  Na umati wa watu ulikuwa ukija kutoka kila mahali. Mpanda farasi alikua akisonga mbele na umati ukimfuata.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  Nilikamilisha misheni yangu kama Mshindi katika mawazo ya Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kabla hata sijaianza duniani!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Kwa hivyo sikengeushwi!  Walitaka kutupiana jukumu la kukataa!  Lakini kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, Mungu alijua kwamba mngefanya hivi!

5 Na tunaujua huu mchezo wa Herode na Pilato!  Walijaribu kunawa mikono kwa kutuma faili huku na kule!  Ijapokuwa nilikuwa tayari nimepewa taarifa kwa siri kutoka Ubelgiji, wale wa Ivory Coast hawakunipigia simu na nilipoenda huko walitaka kuniambia nirudi siku nyingine kana kwamba hawakuwa tayari!  Mnaona ?  Je, wanatuma faili za mapadri na wachungaji ili zikachunguzwe nchini Ubelgiji?  Je, mnatuma faili ya rais wa baraza la makanisa ya Kiprotestanti na kiinjili ya Ivory Coast nchini Ubelgiji?  Mpaka sasa sijawahi kufika mahakamani!  Sijawahi kwenda jela!  Na isitoshe mimi ni mtumishi wa Mungu na mnahamisha faili yangu huku na kule!

6 Na ripoti ilisema kwamba sitapata viza kamwe!  Mnaona ?  Ikiwa nilisema kwamba nitaenda huko [Ubeljiji] kama mgeni kama nilivyoonyesha kwa Ubelgiji, nitakua mgeni hatari kwao!  Ikiwa ningesema kwamba nitaenda huko kupumzika kama nilivyosema kwa Uswisi, hawatakubali kwa sababu ni nabii Kacou Philippe!  

7 Ningesema naenda kama mtalii wasingekubali!  Haijalishi ningesema nini, hawangekubali!  Wana wazo kamili, hawataki kuelewa chochote!  Mungu alijua kwamba wangefanya hivyo!  Na lazima wafanye hivi ili kuongeza haki yangu ya hukumu juu yao mbele za Mungu!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

8 Na nilishangazwa kuona katika faili langu, sababu za kukataa viza yangu.  Ilikuwa imeandikwa: "Umeripotiwa kuwa  hustaili kupata viza" na tena, iliandikwa: "Unafikiriwa kuwa na uwezo wa kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa ya moja ya vyama vya mkataba!"  ".  Mnaona ?  Na waliniambia niweke wakili nchini Ubelgiji ikiwa sikubaliani na uamuzi wao.  Mnaona ? 

9 Mtu wa Mungu anawezaje kuchukuliwa kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa kati ya nchi wakati wachungaji majambazi, manabii  wafanyabiashara wa hekalu huenda huko kwa uhuru?  Na  wengi wao wana pasipoti za kidiplomasia!

10 Na nikaambiwa :  Nchi yako inafikiri kuwa  unaweza kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa.  Kama tu Ahabu na Yezebeli wangemwambia Eliya!  Kama Herode na Herodia wangemwambia Yohana Mbatizaji!  Kama vile Herode na Pilato wangemwambia Bwana Yesu!  Na kama wangemwambia kila nabii katika Biblia. Kama wao wangemwambia Paulo! Inamaanisha nini?  Ni historia inayojirudia.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

11 Kama nabii Eliya Mtishbi aliomba visa ya kwenda Ufaransa, Ufaransa ingeuliza Israeli na kikundi [sanhedrini] cha Kiyahudi kama Eliya anastahili kupata visa ya kwenda Ufaransa?  Na faili yake ingetumwa Ufaransa ili ichunguzwa. 

12 Na Israeli ingesugua mikono yao ikisema : “Naam, uko mikononi mwetu sasa!”.  Na Ufaransa ingemwambia Eliya : "bwana nabii, nchi yako inaonyesha kwamba hupaswi kupewa viza, yaani, wewe sio aina ya mtu ambaye tunapaswa kumpa viza na nchi yako inafikiri kuwa unaweza kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa kati ya Ivory Coast na sisi!  ".  Mnaona?  Wakati huo makuhani wakuu na manabii wa Baali walikuwa na pasipoti za kidiplomasia!

13 Na nilisikia kwa njia ya siri kwamba katika maisha yangu yote, sitakuwa na viza ya kusafiri na kwenda katika nchi yoyote duniani.  Ni uamuzi wa makanisa na serikali ya Ivory Coast na hautabadilika kamwe.  Katika maisha yangu yote, sitapata viza kamwe.  Lakini ninajua ya kwamba kama mimi ni nabii wa kweli kutoka kwa Mungu, Ujumbe ambao Mungu amenipa utaenda hata miisho ya dunia.  Sijui ni jinsi gani lakini Mungu anajua na Mungu atasababisha Ujumbe huu ufikie miisho ya dunia.  [ Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

14 Tangu Abeli, kila nabii katika Biblia ametambulishwa pamoja na Kristo na kila nabii ambaye Mungu atamtuma duniani atatambulishwa pamoja na Kristo!  Chukua Biblia na unionyeshe nabii mmoja ambaye hakuweka ishara ya kunyimwa visa!  Nionyeshe nabii mmoja ambaye hakufikiriwa kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa, na mahusiano ya kimataifa!  

15 Israeli wanawezaje kutoa ushahidi mzuri juu ya Yeremia, Hagai, Zekaria, Sefania, na Habakuki?  Je, Babeli inawezaje kutoa ushuhuda mzuri juu ya Danieli kama Mungu hangekuwa ameweka jambo hili juu yake?  Je, Israeli inawezaje kutoa ushahidi mzuri wa nabii wa kweli?  Yesu angeweza kupaza sauti: Yerusalemu, Yerusalemu unaowaua manabii!  Ni nabii yupi ambaye Israeli walimheshimu wakiwa hai?  Je, inawezekana kwa nabii wa kweli aliye hai kuheshimiwa na taifa lake?

16 Na kama Israeli wangefanya hivyo, je, taifa lolote la kipagani lingefanya kinyume chake?  Hapana!  Lakini kinyume na hayo, manabii wa uongo wametendewa mema sikuzote hata Yezebeli na Ahabu walitaka kulipiza kisasi mbele ya Eliya!

17 Vema!  Sasa nitasoma Yeremia 26:23 : “Kulikuwa pia mtu mmoja aliyekua akitabiri kwa jina la Bwana, Uria, mwana wa Shemahia, wa Kiriath-yearimu;  naye akatabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;  naye mfalme Yehoyakimu, na mashujaa wake wote, na wakuu wote, wakayasikia maneno yake, mfalme akataka kumwua;  lakini Uria akasikia, akaogopa, akakimbia na akaenda Misri.  Mfalme Yehoyakimu akatuma watu kwenda Misri, Elnathani, mwana wa Akbori, na watu pamoja naye mpaka Misri;  wakamtoa Uria kutoka Misri, wakamleta kwa mfalme Yehoyakimu, na akampiga kwa upanga, na kuutupa mzoga wake katika makaburi ya wana wa watu.  Amina! Hili ilifanyika kwa maskini nabii Uria.

18  Naam, mtu kama huyo angepata viza ya kwenda Misri?  Hapana!  Israeli na makanisa yake mengi yangeiakikisha kwamba hapaswi kupewa viza.  Na makuhani walipofika huko, wakawaambia viongozi wa Misri: “Ndugu wenzangu wa Misri!  Tunakuja kwa niaba ya mfalme.  Hatutaki uhusiano mzuri wa muda mrefu unaounganisha mataifa yetu mawili uharibike kwa sababu ya mtu mmoja!  Ni kondoo mpotevu!  Lakini kwa kuwa ni mtoto wetu, hatuwezi kumwachilia!  Tunashughulika naye!  Na tumekuja kumtafuta kwa niaba ya mfalme”.  Wamisri wakamkabidhi Uria kwa makuhani.  Wakamchukua kama mfungwa na kwenda pamoja naye mpaka Israeli.

19 Na siku moja, mtu aliyesikia au kusoma Ujumbe Ufaransa aliniandikia akisema : "Samahani, sijui kama hiyo ina uhusiano wowote nayo, lakini nataka tu kujua kama wakati wa Vurugu huko Ivory Coast, hujapigwa na kitako cha bunduki kichwani?  Kwao, kama vile Paulo mbele ya Agripa na Festo, ninachosema kinaweza tu kutoka kwa mtu ambaye ana tatizo la akili!  Lakini maneno yangu yanawezaje kuwa na maana yoyote kwenu wakati mimi ni nabii wa kweli?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

20 Na hivi majuzi nilikuwa nikizungumza kwenye redio na nikasema : “wewe bwana, una huduma ya Waefeso 4:11 kama kuhani wa Agano la Kale, unachosema ni kizuri kwa kusanyiko lako!  Biblia haikutangaza hivyo huna haki ya kuandika kitabu au kusambaza mafunuo yako... Lakini kile ambacho mimi, nabii Kacou Philippe, nasema kina thamani sawa na kile Isaya au Musa alisema na kinaweza kuongezwa kwenye Bibilia.  Na muhimu zaidi kwa wakati wetu kuliko vile Isaya au Musa walisema…”.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

21 Na nilipokuwa nikizungumza, mwandishi au mtu fulani alisema : “Kuanzia sasa, tutakuwa na madaktari wa magonjwa ya akili kwenye seti hii hapa kwa sababu kuna vichaa ambao hutoroka kutoka kwa vituo vya magonjwa ya akili na kuwa manabii".  Kwa hivyo ikiwa mtu anayeitwa mwalimu wa Neno anasema hivyo, je, ni Ivory Coast au Ubelgiji ambayo itasema kitu kingine?  Na wanasema kwamba nikipewa viza, ninaweza kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa kitaifa na uhusiano wa kimataifa kati ya nchi.  Je, nitahatarisha vipi mahusiano ya kimataifa, mimi ambaye ni mtumishi wa kawaida wa Mungu?

22 Vema!  Nitasoma andiko lingine la Mathayo 8 kuhusu Bwana Yesu Kristo Mwenyewe... “Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu;  nao walipomwona wakamsihi aondoke katika pwani yao.  Akapanda mashua, akavuka ng'ambo, akapanda merikebu, akavuka na akafika katika mji wake."  Mnaona ?  Alikuja katika mji wake wa nyumbani!  Watu walisema : Anasema yeye ni mtumishi wa kweli wa Mungu, Anasema Yeye ni Masihi lakini kwa nini watu waliweza kumtupa kwa urahisi hivyo?

23 Baadhi ya wanafunzi walitarajia ataita moto kutoka mbinguni kama Eliya.  Mnaona?  Sasa alitupwa nje ili afananishwe na manabii wote!  Yeye mwenyewe alionekana kuwa angeweza kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa lakini leo, nyote mnajidai kuwa wake huku mkimkataa yule aliyewatumia kwenu kulingana na ahadi yake katika Mathayo 23:34-35!

24 Kila nabii wa kweli wa Mungu anafananishwa na Kristo na siku za unabii wake zinafananishwa na siku za Kristo na mfalme au Rais na taifa ambalo anatoa unabii ndani yake litafananishwa na Israeli na wafalme wa Israeli!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Ndio maana tuliona serikali ya Marekani ikiinuka dhidi ya William Branham japo William Branham alikua akishirikiana na makanisa yote ya wakati wake ikiwemo Wakatoliki.  Ni lazima iwe hivyo, ili Maandiko yasilete mkanganyiko.

25 Hapo walinipa nafasi ambayo wangempa Musa, Yeremia, Bwana Yesu Kristo, Paulo au nabii yeyote wa Biblia!  Kwa tendo hili, walijifananisha wenyewe na Israeli na mbele ya Kelele ya usiku wa manane, kila taifa duniani litatambulishwa na Israeli!  Makanisa yao yatatambulishwa na Mafarisayo, Masadukayo, Waessene na Wagiriki...na miungano yao, mabaraza na mashirikiano ya makanisa lazima yatambulishwe na Sanhedrini ya Kiyahudi!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

26 Na tunakumbuka Paulo ambaye aliburutwa mbele ya mahakama. alipigwa na Wayahudi mara tatu. Mara tano alipokea mapigo arobaini kasoro moja... Hakuna nabii hata mmoja katika Biblia ambaye alitendewa tofauti! Na maadamu Mungu anatuma manabii duniani, itakuwa hivyo. 

27 Lakini je, Biblia haisemi lazima iwe hivyo?  Je, hakupaswi kuwa angalau nabii mmoja aliye hai duniani ambaye anaambiwa kwamba hapaswi kupewa viza?  Je, kusiwe na angalau nabii mmoja ambaye anafaa kuchukuliwa kuwa anaweza kuhatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa huku hata wanasiasa, wapinzani wa kisiasa na waasi wa tawala zilizopo wana viza?  Je, kusiwe na nabii anayepaswa kufananishwa na manabii wa Biblia?  Lakini pamoja na yote, yeye ndiye atakuwa nabii mkuu wa nchi yake, wa bara lake na wa dunia yote kwa kizazi chake!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

28 Ni wakati wa Eliya na Mungu yuko hapa.  Na kabla ya kwenda Israeli, tuliona njiwa wawili wakiwa na Malaika wa Aprili 24, 1993 wakishuka kwa Ibrahimu kama katika Mwanzo 18!  Wawili kati yao wanaelekea Sodoma na Gomora, yaani Jerusalem na Tel Aviv ambayo ni miji mikuu ya mashoga na wasagaji wa dunia nzima kama nilivyosema! 

29 Sasa, baada yangu, wakati Eliya na Musa watakapoinuka katika Israeli, watakuwa na viza ya kwenda popote wanakotaka duniani?  Hapana!  Manabii wa uwongo watakuwa nayo lakini wale wa kweli, Eliya na Musa, hawatakuwa nayo ili wafananishwe na manabii wote ambao Mungu amewatuma duniani hadi leo tangu Abeli!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

30 Mnaona?  Sitaki msaada wenu wala ruzuku yenu, lakini mnanitakia mabaya.  Siku moja mahali fulani duniani, mtasema kwamba mko hivi au vile!  Na mtaambiwa: “Ah, ni kwenu ambako Mungu alimwinua nabii mkuu kwa jina la Kacou Philippe! ".  Mtakuwa kichwa chini!  Na mtakumbuka mabaya yote mnayonifanyia si kwangu mimi bali kwa Mwenyezi Mungu aliyenituma.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  

31 Siku moja nitakuwa faida kwenu kama vile Yesu Kristo ni faida kwa Israeli iliyomsulubisha!  Nitakuwa nabii zaidi kwenu mda utakapo pita!  Na Ubelgiji na Uswizi watawaambia wajukuu wao kwamba walikuwa wepesi sana juu ya uamuzi huu!  Lakini inaweza kuwa vinginevyo?  Hapana, haikuwezekana.  Ilibidi iwe hivyo ili nifananishwe na watangulizi wangu!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Ndugu walitaka kujua kama tunaweza kupata mwanasheria au kukamata vyombo vya habari? Nikasema hapana!  Kamwe !  Eliya, Elisha, Yeremia, Bwana Yesu Kristo au yeyote kati ya manabii hawangeajiri mwanasheria.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

32  Sasa tusome Amosi 7:10 ili kumaliza!  “Ndipo Amazia kuhani wa Betheli akatuma watu kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, kusema : Amosi amefanya fitina juu yako katikati ya nyumba ya Israeli;  nchi haiwezi kuyavumilia Maneno yake yote.  Maana Amosi asema hivi : Yeroboamu atakufa kwa upanga, na Israeli hakika itaondolewa katika nchi yake.  Amazia akamwambia Amosi : Mwonaji, nenda zako;  kimbilia nchi ya Yuda, ukale mkate huko, na kutabiri huko, lakini usitabiri tena katika Betheli, kwa maana ni kimbilio la mfalme, na nyumba ya ufalme."  Mnaona ?

33  Amosi aliambiwa aondoke mjini, huku manabii wa uongo, wachungaji wa uongo, walimu wa uongo na makuhani wa uongo kama Amazia mwenyewe wakijionyesha pale!  Lakini mamia ya miaka baadaye, Kitabu cha Amosi kilikuwa kando ya kitabu cha Musa!  Isaya alikuwa alipiganishwa, akifikiriwa na nchi yake kama atahatarisha utulivu wa umma, usalama wa taifa na mahusiano ya kimataifa, na mwishowe  akakatwa vipande-vipande lakini miaka mia nane baadaye kitabu chake kilikuwa pamoja na kitabu cha Musa!  Na mwenye masikio na asikie!


Comments