KACOU 8 : MKUTANO WA KIEKUMENIKA

(Ilihubiriwa Jumapili, mnamo januari, 12, 2003 pa Locodjro, Abidjan – Ivory-Coast)


 1    Ningependa kuzungumzia mkutano wa kiekumenika. Manabii waliizungumzia, na imefika hii tarehe 09 januari 2003. ishara ya kihistoria imetolewa. Biblia na kurani zimekutana. Wakatoliki, waprotestanti, wa kiinjili, makanisa yaliyofunuliwa ao za urejesho, waislamu, wabudha, wamahikari, warosikrusia, dini za kienyeji, wa eckankar, imani baha’ie, wanasiasa, orodha za kisiri… Wote wamekusanyika katika jumba la michezo la Treichville kwa kusali. Kumwomba nani? Sijui! Hii ni mbali na ufahamu wangu. Hii ni mbali na shirikisho la makanisa. Ni jambo ambalo mwanadamu hangeweza kufikiria.   

2    Na, kwa mfano  wa manabii, kwa mfano ya wale waliyo nitangulia katika nyakati za kale, nilikuwa pale! Nilifikiria kupata pale manabii, lakini hawakuweko. Ni wapi watu wa ukweli kwa hiyo miadi ya kihistoria? Katika ufunuo niliona ngurumo, na umeme wa hasira didhi ya jumba la michezo. Kisha, nikaona patwa jua(-mwezi). Wakristo na waislamu na orodha za kisiri walikusanyika pamoja na rais wa Jamuhuri na waliombea amani. Walisali mungu gani ? Sijui!   

3    Kesho yake, niliona juu ya gazeti ya kiinjili, kichwa hiki cha makufuru: « Biblia inaungana na Kurani » ;kardinali Bernard Agré, imamu Idriss Koudouss, reverend Ediemou Jacob aliye mpotevu mkuu wanganga na wachawi wa Ivory-Coast, reverend Benjamin Boni, rais wa kanisa methodisti… Wote walikuwa pale, kwenye jalada la gazeti mkono mkononi. Sikusema siku zote kwamba shetani ndiye mungu wa makanisa haya, na popo ndio mfano wao wa kiroho? Mungu hakuweka mapopo katikati ya mahali ambapo picha zinapigwa, ambayo ndiyo katikati ya Abidjan na ndio moyo wa Ivory-Coast? [Kc.3v20] 

4    Basi nini ilipitika mnamo januari 09. Mapema basi mnamo januari 09, nilikuwa pale pamoja na polisi na tayari, Biblia iliinuliwa didhi ya jumba, nilipaza sauti bila kuchoka kwa megafoni: «Ni asubuhi hii ndipo maadui za Mungu watakusanyika nafasi hii! Ni asubuhi hii ndipo maadui za Mungu na za nchi watakusanyika hapa!». Na watu walinisihi niseme: «marafiki na maadui za Mungu…» na walipoona kwamba siwasikii na ya kwamba hawawezi kunisukuma kubadilisha, wakachochea polisi dhidiyangu wakisema: «neno lake linatusumbua, hatuta weza kuomba pamoja na neno hilo nyuma yetu! Mumkamate!». Polisi walijaribu lakini sikuacha.   

5    Karibu saa 3 asubuhi, mkuu wa polisi alitoka jumbani kwa kuja kunikamata alipo sukumwa lakini sikuacha. Tulijadiliana ndipo akaelewa. Nilimwambia: «Bwana, wewe ni hapa kwa kutii bwana wako, nami pia nipo hapa kwa utiifu kwa Bwana wangu». Na tena polisi wengine wawili wakaja lakini sikujiona kuachilia kabla saa nne ya mchana kutimia. Na ilikuwa hivyo hivyo hadi saa 4 na nusu ya mchana.  

6   Ndipo, mtu mmoja akajionyesha kwangu kwamba yeye ndiye katibu la taifa wa shirika la makanisa, alitoka jumbani mwenyekuvaa kanzu nyeusi. Tayari alikuwa amesikiya wakisema kuhusu Kacou Philippe lakini hakujua kwamba ni mimi. Alisema: «Tangu asubuhi unarejea tu maneno yale. Rais wa jamuhuri na wakuu watakuwa hapa na hiyo itaonesha mfano usiyofaa kwa makanisa zetu». Tena akawaomba polisi wanikamate ikiwa nitaendelea. Mkuu wao akawaambia watu wake: «akarejea, akamatwe». 

7   Nilimwambia: «kama ninapenda kuendelea, nitaifanya kwa kuwa Biblia haiwezi kutii mavazi ya askari! Je! ni wewe ulinituma hapa?». Na nilizingirwa na polisi waliyokuwa tayari kunikamata na nikasema kwa ukali mno hata akabadilisha akisema «Musimkamate ila chukueni megafoni yake!». Sijui mara ngapi nilinyanganywa megafoni yangu.   

8   Na asubuhi ile, dini zote zilikuwa pale. Katika mustari, niliona waislamu katika kanzu, wakatoliki, wa Eckankar, na kadhalika... Na waliniangalia wote kama watu ambao hawakuja kusali. Waliniangalia kama vile mimi ndimi shetani wao japo walikuja kusali.   

9   Na neno la katibu wa shirika la makanisa lilikuwa kama ambukizo la mapepo kwa askari polisi kwani walisisimuka. Kulikuwa na askari, na polisi. Na kati ya wale askari kulikuwa na mbranhamisti, baba wa ndugu Fabrice. Japo, mapema niliona andiko la makanisa haya yote juu ya mlango wa jumba.   

10    Kama wewe ni mwanamemba wa kanisa ambayo yenyewe ni mojawapo kati ya shirika la makanisa halafu wewe ni mwenye makosa mbele ya Mungu hata ikiwa wewe hukuwa jumbanisiku ile.   

11   Makanisa yaliongezwa mapepo hii januari 09 na ni kwa ajili ya uamsho ya watakatifu ambao tayari upo duniani, kupitia huduma hii ya Matayo 25:6. Na tayarindani mwetu kuna huoupakoutakao anzishauamsho huu. Na niliwaambia kwa neno la Bwana ya kwamba uamsho huu utapiganishwa na shirikishola makanisa, hiuo mchorowa kishetani ambao ni tu vikundi vyawachawi katika ngozi ya kondoo.   

12   Mkitambua, mkuu wa shirika la makanisa nayule aliyevaa kanzu nyeusi walitoka jumbani, kaburini pamoja na umati wamapepo ambazo walipitisha kwa polisi.Mnaona?Angalia Matayo 8:28-34, Bwana Yesu-Kristoalipo mponya huyo mwenye pepo wachafu huko Gadara,  mapepo yakaingia ndani ya nguruwe, kisha ndani ya maji… kisha ndani ya wachungaji… kisha ndani ya wakaaji wa kijiji na hao wakamfukuza Bwana Yesu.   

13   Tangu nyakati za kale, wote ambao Mungu alituma walifanya hivyo hata bila mapato, kwani kazi ya Mungu haifungwena pesa,piakubaki hekaluni kwa kulaumu au kushutumuna kusemaya kwambawewe ni bora,hii siyo kazi ya Mungu bali fomu ingine ya udanganyifu. Sicho tulichofundishwa na manabii, wala mitume hata na Bwana YesuKristoMwenyewe katika huduma yao. Ukweliunakaidina kushindainje, hapana ndani ya kanisa wala ndani ya makesha ya maombi bali inje.   

14   Ikiwa huna pesa, tembea kwa miguu! Nilihubiri popote hadi leo bila kupokea lolote kutoka mtu isipokuwa tu mtu mmoja aliye niletea mchele kidogo nyumbani. Japo, sijawahi kuona mwinjilisti, nabii wa makanisa haya ambaye hakupokea hundi, nyumba za kifahari, magari, na vinginevyo. 

15 Usitamani ambacho huna. Kwa Injili hiyo, nimechagua njia nyembamba pamoja nanyi basi tusimame imara! Ikiwambingu imefungwa kwao si mali yao ndiyo itapata njia ya mbingu. Ikiwa haikupewa kwako toka mbinguni kabla kuwekamsingiwadunia, huwezi kumpa mchaguliwa hicho kikombe cha maji cha Matayo 25: 32-35. Ambacho walitendea mti mbichi ndicho watatendea mti kavu. Mtumishi si mkuu kuliko bwana. Mnaona?   

16  Hii januari 09, kisha kupaza sauti tangu saa moja hadi saa nne ya mchana, nilitamani baki ya maji waliyokuwa wakitupa lakini kama mtu angejaribu kunipa, makutano wangemgeukia. Mnaona? Waliniangalia wote kwa chuki kama watu ambao hawakuja kusali. Macho ya Kaina! Mnaona? Kulikuwa na waislamu katika kanzu, wametodisti, wakatoliki, wabatisti ambao nilitambua nyuso zao. Shemeji yangu, mume wa Claudine binamu wangu, ambaye ni mhubiri mmetodisti alikuwa kwenye mstari. Na nyuma yake kulikuwa na muislamu aliyevaa kanzu. Mnaona? Mbuzi, Nguruwe,kuku, mbwa wote pamoja.   

17 Ndugu, hubirieni na msiogope wanao jidai kuwa manabii. Ni yaleyale maroho za uchawi ndiyo yamejiweka ndani ya makanisa. Biblia iliitabiri katika Matayo 24:24. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »]. Nabii gani? 

18   Katika huduma zote, maishaya kale ya nabiimjumbeyanahesabiwatangu kuzaliwa kwake. Hatamaisha yamchungaji! Mtu aliye na mtoto nje ya ndoa au kabla ya ndoa,hawezi kuwa mchungaji. Anaweza kufanya kazi ya uchungaji lakini hawezi kuwa mchungaji. Mwinjilisti Haya; lakini hapana mchungaji au nabii. Vivyo hivyo kama mke wake si mtiifu au ikiwa ana mtoto nje ya ndoa. Angalieni Yeremia 1:5, Waamuzi 13:3-4, Luka 1:13-15… 

19  hupaswi kuwa zamani mtenda maovu, kujua wanawake, kunywa pombe ya kulevia, au kuvuta sigara na baadaye kuwa mchungaji au nabii wa Mungu; haidhuru maono unayo. Anaweza kufanya kazi ya uchungaji kwa muda lakini yeye hawezi kuwa mchungaji. Ndivyo.   

20  Na nabii au mchungaji, inalazimika ushuhuda bora… inakubidi kutimiza shurti kama sivyo, baki kimya! Mnaona? Kama baada ya kusikia watu wakisimulia kuhusu nabii Kacou Philippe, unapatikana katika hali hizo, huwezi kuwa tena mchungaji katika Ujumbe huu. Siongei kuhusu wale walio kuja wakiwa katika hali hii. Lakini tangu wakati ulisikia wakisimulia kuhusu nabii Kacou Philippe wala kama ulikuja katika Ujumbe huu na baadaye unarudi katika dunia kwa kutenda mambo haya, huwezi tena kuwa mchungaji katika Ujumbe huu. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

21  Pia, kama wewe ni mchungaji kabla ya ndoa, sheria inasema ya kwamba kuhani atakuwa na mwanamke ambaye hajaguswa bado. Walawi 21:13-14 / Ezekiel 44:22.   

22  Usitamani ambacho hukupewa na Mungu kutoka mbinguni. Kumbuka ya kwamba kule mbinguni, malaika wote waliotamani kuwa na huduma kubwa kama ile ya Gabrieli walitupwa duniani. Ikiwa Mungu alikutuma duniani kwa ajili ya kazi fulani, atakulinda katikati ya hivi viozo. Huduma silo jambo la kuhubiri vizuri au kupaza sauti au kuruka ruka mbele ya watu, balini pia maisha.   

23  Sasa sikilizeni mfano huu ambao Mungu wa mbinguni analeta kwa wanadanu. Mungu akapiga kwa upofu Kijiji kilicho kosa uaminifu kwake. Lakini katika rehema yake, akatuma nabii kwa kuwaponya. Lakini wakamwambia nabii: «Hatutaki tena kuona kwani tangu tulipofushwa, tuna yote kwa bure, na dunia nzima inatushughulikia. Basi umwambie Mungu atuweradhi! Na ni nini inaonyesha kwamba ni Mungu ndiye alikutuma?». 

24 Basi siku moja, watu wa kijiji jirani wakasemezana kati yao na kusema: "tunalima, tunateseka na udongo hautupatii tena kitu. Tunafarikikwa njaa ijapokuwa kijiji mpofu kina yote kwa wingi. Twendeni, tuwaue na tutwae udongo wao na yote waliyopewa". Wakatwaa magongo mchana kati, wakaenda katikati ya kijiji kipofu na wakaanza kupaza sauti: "Njooni! Tumekuja na mifuko za mchele, mafuta, na mavazi. Sisi ni shauri na shirikisho la makanisa, sisi ni ndugu zenu katika Kristo". Basi wakatoka. Lakini, nabii alipo waona akajiokoa na jamaa yake. 

25 Na jirani wao walipo wavizia wakatoka na kuanza kuwaua… wamoja walilalamika: "Mturehemu! Ô Rehema!". Walilia mikono mbele namna hii! Wengine walilia: "lakini iko nini? Muwakamate!!! Muwakamate!!!Muwakamate!!! ". Ndugu, ilikuwa huzuni. Kijiji kipofu kikaangamizwa. Lakini katika uchungu wao, walilia wote: "Tunataka kuona, tunahitaji huyo nabii, yule nabii yuko wapi? tunatamani kuona tena…". Hata wale ambao hawakutoka inje waliuawa. Mnaona?   

26    Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, vivyo hivyo itakuwa kwa kizazi hiki kikaidi na makanisa zake. Aliye na masikio kwa kusikia asikie!   



Sura inayofanana : Kc.40


Comments

Popular posts from this blog

KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI

KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI

Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6