KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI
(Ilihubiriwa jumapoli asubuhi, May tarehe 16, 2004 huko Locodjro, Abidjan –Ivory Coast)
1 Tangu nyakati za jioni, dhambi ya asili si siri tena, ndiyo maana sitaeleza kwa undani. Nazungumza ili kuwafahamisha wasiojua...
2 Mti wa Uzima ni Bwana Yesu Kristo alikuwa anetembea juu ya uso wa maji na kusema na Adamu. Mwanzo 1:2. Alimfunika Adamu ambaye angeweza kuwapa wanyama majina na kutawala viumbe vyote. Kwa hiyo, Adamu alikuwa amekusudiwa Uzima wa Milele. Kisha tunaona mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao ni Lusifa, ambaye alitupwa chini kutoka Mbinguni kulingana na Ufunuo 12:7. Mmoja alikuwa akimshawishi Adamu na mwengine akimshawishi nyoka. Katika usemi wa kinabii, mti unaashiria mtu. Danieli 4:20, Mathayo 3:10. [Kc.24v7]
3 Nyoka alikuwa na sura ya binadamu zaidi, kuliko sokwe. Hapo mwanzo, nyoka hakuwa anatambaa, alikuwa akizungumza na Adamu na Hawa lakini laana ndiyo iliyoondoa miguu yake na mikono yake kulingana na Mwanzo 3:14. Alikuwa mzuri sana kama Ezekieli 28:11-15 inavyosema. Lakini Mwenyezi Mungu alimbadilisha kuwa kile alichokitumia kufanya dhambi, ngono. Lakini unapaswa kujua kwamba wakati wa uzinzi nyoka alikuwa na umbo lake kamili la kibinadamu.
4 Kwa hivyo, nyoka, mtambaazi anayetambaa porini, ndiye baba ya Kaini kama mimi ni baba ya binti yangu Grace; mfupa kwa mfupa, nyama kwa nyama. Kitambaazi huyo mnachokiona kwenye kichaka ni babu wa wale wote ambao Ujumbe huu unawahukumu na ambao hawatatubu. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Ninatoa changamoto kwa wanasayansi kufanya kipimo cha DNA na kuniambia ninachosema sio sawa! Nilisema kwamba nyoka akiuawawa, washiriki wa makanisa haya ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti ukiwemo na Uislamu na Uyahudi wanapaswa kuwa na mawazo ya uchamungu kwa huyo nyoka. [Kc.54v8]
5 Mnajua kwamba katika Afrika, makabila mengi hayali wanyama fulani kwa sababu yameambiwa kwamba zamani, babu yao, wakati wa jambo fulani, alibadilika au aligeuzwa kuwa mnyama huyu na ni kweli...Ni mnyama lakini ni babu wa kabila la mwanadamu. Hicho ndicho kilichotokea katika bustani ya Edeni. Katika usiku wa manane, ni sawa kwamba Mbranhamisti anainama juu ya maiti ya boa au chatu...
[Kc.1v13] [Kc.29v15]
6 Vema! Tunda lililokatazwa, ni tendo la ngono. Mwanzo 3 na Mithali 30:20 zinafanana. Hawa alifanya uzinzi na nyoka. Mungu alimwambia Hawa kwamba atazaa kwa mateso mengi kwa sababu, kama nyoka, ni kupitia ngono kwamba amefanya dhambi. Lakini kuhusu mwanaume, ni ardhi iliyolaaniwa, na miiba na michongoma na magugu yakaanza kuota. [Kc.81v26]
7 Biblia inasema kwamba Adamu na Hawa walikuwa uchi na hawakujua, lakini tendo la ndoa ndilo lililowafanya waone jambo hilo. Hakuna matunda, hakuna tufaha, hakuna machungwa, hakuna embe ... inaweza kufanya hivyo la sivyo tungegawa matunda haya kwa wasichana wadogo katika sketi ndogo ili wavae vizuri. [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”].
8 Kwa hivyo, si swala la miti ya asili katika bustani ya Edeni bali watu. Yohana Mbatizaji anaposema kwamba mti wowote usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni, si swala la mti wa asili. Na Mti wa Uzima unaonekana katika Ufunuo 22:1-2 na ni Bwana Yesu Kristo na wale mitume kumi na wawili. Kwa hiyo Ufunuo 22:1-2 ni urejesho wa Edeni. Musa bila kuwa na damu ya Yesu juu yake hangeweza kukaribia vya kutosha kuona kiti cha enzi wala mti wa Uzima kama Yohana anavyoeleza katika Ufunuo 22:1-2. Musa alisimama mbali sana na aliweza tu kueleza matawi manne ya mto wa Ufunuo 22:1. Nitarudi kwa hili katika mahubiri.
9 Kwa hivyo mwanzo Shetani alitupwa chini kutoka mbinguni na kutanga-tanga katika bustani, aliingia ndani ya nyoka na kumfanya anene kwa lugha na mwanamke. Vivyo hivyo mwisho wa nyakati, roho za chatu zinazotangatanga makanisani ziliingia ndani ya wana wa ibilisi ili kuwadanganya binadamu. Halafu Hawa ambaye ni jumla makanisa yote ya Kikatoliki, ya Kiprotestanti, ya Kiinjili na misheni na huduma pamoja na Wabranhamisti wote watatafuta kumdanganya Adamu yaani wana wa Mungu ambao wamefika usiku wa manane lakini wakati huu, ibilisi atashindwa. [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”]. Hatutakubali kamwe kongamano au ushirikiano wao kwa sababu tunajua ni nani anayewaongoza. [Kc.24v5-6]
10 Vema! Hawa anatumia neno “kudanganywa” katika Mwanzo 3:13, kwa hiyo ni tendo la ndoa. Na Hawa akachukua mimba kutoka kwa nyoka na kutoka kwa Adamu, mapacha. Ndiyo, Kaini na Abeli walikuwa mapacha. Biblia inasema nini: “Mwanamume akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini; akasema, Nimepata mwanamume kwa JEHOVAH. Naye akamzaa TENA Abeli nduguye. Abeli mfugaji, na Kaini mkulima. ". Mwanzo 4:1-2. Mnaona ? [Kc.24v18]
11 Biblia inasema Adamu alimjua Hawa na akapata mimba na kumzaa Kaini kisha Abeli kwa wakati mmoja. “Adamu akamjua mkewe TENA; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sethi;…”.
12 Ndugu zangu, hapo mwanzo kufanya tendo la ndoa haikuwa kama tunavyoona. Mwanaume alipaswa kufanya tendo la ndoa na mke wake siku fulani ya mwaka. Mnaona ? Na angalia mwanamke anapojifungua, kwanza hakuangi hedhi zake. Kwa kawaida, tunapaswa kufanya naye tendo la ndoa ya kwanza, baada ya kuzaa, tu baada ya hedhi yake ya kwanza. Lakini hii haipaswi kuja kwa matubio ikiwa hukufanya hivyo .
13 Na kuelekea unyakuo, wateule wataishi hivyo kikamilifu. Watakaa miezi mingi karibu na wake wao wenyewe bila hamu hata kidogo ya ngono, basi hawatasikia tena hamu yoyote ya ngono. Mnaona ? Itakuwa hivyo huku wana wa Ibilisi wakigaagaa katika ushoga na kuuruhusu. Biblia inasema, " Adamu akamjua Hawa, naye akachukua mimba, akazaa... Adamu akamjua Hawa tena, naye akachukua mimba, akazaa...". Mnaona ? Na kabla ya unyakuo, bado itakuwa hivyo. [Kc.58v3]
14 Na usishtuke kwamba Hawa alichukua mimba ya nyoka na ya Adamu kwa wakati mmoja. Sayansi inasema inawezekana. Ningependa kuzungumzia kisa kilichotokea kwa mwanamke mmoja huko Norwei mwaka wa 1964. Nitasoma kutoka kwenye hati hapa. Ninasoma: “Kuna uhusiano kati ya mwanadamu na mnyama: seli ya kiinitete kutoka kwa kijusi cha mnyama kilichochukuliwa na kudungwa ndani ya mwanamke, kisha seli za tezi ya mnyama zitaenda kwenye tezi ya binadamu; seli za figo zitaingia moja kwa moja kwenye figo za binadamu, kitivo huzikubali na kuzielekeza. Kwa hivyo mnyama huharibiwa lakini mshikamano unabaki. Kwa hiyo, mwaka wa 1964, mwanamke wa Norwei alipata mimba kutoka kwa mumewe mweupe na mpenzi wake mweusi. Mimba ilitenganishwa kwa wiki tatu. Kwa hivyo alijifungua mapacha: mtoto mmoja alikuwa mweupe kabisa na mwingine alikuwa mchanganyiko."
15 Vema! Kwa hivyo nyoka alikuwa na uzao wake kulingana na Mwanzo 3:15, Yohana 8:44 na 1 Yohana 3:11-12. Kaini ni mwana wa nyoka. Tayari kulikuwa na nyoka wakitambaa msituni, lakini nyoka huyo, ambaye alilala na Hawa, pia alikua mtambaazi baada ya laana. Mnaona ? Ni Abeli na Sethi ambao ni watoto wa Adamu. La sivyo, Kaini, ingawa pacha na Abeli, si mwana wa Adamu.
16 Ikiwa Kaini alikuwa mwana wa Adamu, na kwa kuongezea alitoka kwanza, kwa haki ya mzaliwa wa kwanza, jina lake lingetajwa katika Mwanzo 5:1-3, jina lake lingetajwa katika 1 Mambo ya Nyakati 1:1, jina lake lingetajwa katika Luka. 3:38... Mnaona? [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”]. Na mtoto wa Adamu hatazungumza na Mungu kama Kaini katika Mwanzo 4:9: “Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? ".
17 Mungu alichukua umbo la mwanadamu kuzungumza na Kaini na Kaini alijibu kulingana na mbegu yake. Kaini hakujua kwamba ni Mungu aliyekuwa akizungumza naye, kama vile leo watoto wa nyoka katika makanisa haya hawajui kwamba ni sauti ya Mungu inayosema nao kupitia nabii Kacou Philippe. Mnaona ?
18 Oneni kwamba ilikuwa baada ya hii ndipo Adamu alimwita mke wake Hawa kulingana na Mwanzo 3:20. Na ni kwa nini hivyo: "... kwa sababu yeye ndiye mama wa wote walio hai." Adamu si baba wa wote walio hai bali Hawa ndiye mama wa wote walio hai yaani mama wa watoto wa Mungu na mama wa watoto wa ibilisi. Mnaona ? Na leo, karibu kila nchi, mwanamke amechukua mimba ya mnyama, na Mungu aliyetuma UKIMWI kuhukumu wakaaji wa dunia ni mwadilifu. [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”].
19 Hapo mwanzo ilikuwa ni ngono iliyoleta laana juu ya dunia na mwishowe ni hiyo hiyo ngono ndiyo itaharibu dunia. Mwanzo wa uwizi na dawa za kulevya, ... ni ngono. Katika mwanzo wa UKIMWI na ongezeko la joto duniani... ni ngono.
20 Katika Mwanzo wa teolojia na makanisa ya Kikatoliki, Kiprotestanti, kiinjili na Kibranhamisti, ni ngono. Katika mwanzo ya makaburi na hospitali, ni ngono. Mwanzo wa mateso yote duniani ni ngono. Na daima itakuwa ngono hadi mwisho wa dunia. [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”].
21 Vema! Kama jambo la tatu, ningependa kugusia mada nyingine: Kaini alipata wapi mke wake? Jibu ni kwamba, Adamu na Hawa walikuwa na binti wengi na Kaini na Sethi walichagua wake zao miongoni mwao, kwa sababu kabla ya sheria ilikuwa inawezekana. Amina! Kabla ya sheria haikuwa dhambi; Abrahamu alimuoa dada yake mwenyewe, Sara. Rebeka ni mpwa wa Isaka... Mnaona?
22 Sasa jueni kwamba kuna siri katika kifo cha Abeli: Mungu ndiye aliyemwondoa Abeli kwa sababu yeye ni tunda la dhambi ya Adamu na Hawa na haikuwa kawaida kwa binadamu kutoka kwa tunda la dhambi hata kama yeye ni mwana wa kweli wa Adamu. Yaani mwana wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu alifanya dhabihu na kisha Sethi akazaliwa. [Kc.6v36] [Kc.137v59]
23 Vema! Ningependa kusisitiza jambo lingine: nyoka alikuwa ameumbwa na jike lakini laana pia ilimpiga jike na watoto wao. Pia ni laana iliyowakumba aina ya nyoka. Na ingawa laana ambayo ingemwangukia mwanadamu ilienda chini, mwanadamu mwenyewe hakuachwa. Aina za rangi, vikundi vya damu, nk. Ona Mjerumani, mrefu, mwenye nywele nyekundu, mwenye macho ya bluu na pigmi mweusi wa Gabon au Mwaeskimo… Na vipi kuhusu nyoka? Tazama aina hizi tofauti za makanisa na sumu zao ambayo ni teolojia! Mnaona ?
24 Kwa kumalizia, nataka kusema hivi: Wakati Abeli na Kaini walisimama pale ili kutoa dhabihu, ilikuwa ni uwakilishi mkamilifu zaidi wa ulimwengu wa kidini siku hizi. Abeli alikuwa baba wa wote ambao watakuwa wanatembea kwa ufunuo wa kiungu, na kwa ajili ya sadaka yake Mungu alimfunulia kwamba dhambi ya asili ilikuwa ni tendo la ndoa na kwamba kulikuwa na damu. Kwa hiyo ilikuwa ni damu iliyopaswa kujibu.
25 Lakini Kaini akiunga mkono nadharia yake ya tufaha, akisema kwamba Adamu na Hawa walikula tufaha za asili, akamtolea Mungu tufaha. Zaidi ya miaka 2000 kabla ya Musa kuja kuandika Kumbukumbu la Torati 12:6 , Mungu alimfunulia Abeli kile ambacho angetoa ilikua katika ono. Mnaona ? Abeli alitoa wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake na Mungu akakubali hilo.
26 Hapo awali, Mungu alikuwa amemfunulia kila kitu katika maono. Mnaona ? Alichokuwa akifanya mbele ya Kaini ni kuigiza tu ufunuo aliopewa na Mungu. Na Bwana Yesu Kristo alisema katika Mathayo 16, "Nitalijenga Kanisa Langu juu ya ufunuo wa kiroho." Alisema, “Mwili na damu havikukufunulia hilo, hukujifunza hilo kutoka katika kitabu au kutoka katika shule ya uchungaji, lakini Baba yangu aliye Mbinguni alikufunulia hilo. Na juu ya ufunuo wa kiroho nitalijenga Kanisa Langu.” [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. Na leo, kila kitu tunachofanya, kila kitu ninachohubiri, hayo yote, Mungu Mwenyezi, Mungu yule wa Abeli tayari ameyafunua mnamo Aprili 24, 1993 ni maonyesho tu. Mnaona ? Watoto wa ibilisi hawaelewi, lakini watoto wa Mungu wanaelewa hilo. Amina!
27 Ikiwa hukuwa miongoni mwa umati wa watu wa Aprili 24, 1993, huwezi kuamini Ujumbe huu na Matendo 13:48 inasema kwamba Paulo alipokuwa akihubiri, wote waliokusudiwa Uzima wa Milele waliamini. Na kabla ya kudhihirishwa duniani, umati huu ulipaza sauti katika ono la Aprili 24, 1993: “Hatujamwona Malaika na Mwana-Kondoo na hatujasikia Maneno yaliyotamka Mwana-Kondoo lakini tunamwamini kikamilifu…”. [Ndl: Kusanyiko linasema, Amina! ”].
28 Kwa kweli, hili lilifanyika katika akili ya Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Mnaona ? Sio yule anayetaka au mwenye hekima au mwenye akili lakini ni yule aliyechaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu katika akili ya Mungu.
29 Haidhuru uko wapi sasa, katika Afrika, katika Asia, katika Ulaya, katika Amerika, hakuwezi kuwa na mapepo wa kutosha kukuzuia kuusikia Ujumbe huu na kuukubali. Na haufi mpaka umsikie na kumkubali...
30 Mungu anajua kabisa ni Wachadi wangapi, Wazimbabwe, Waghana, Wamartinika na Wareno wangapi walikuwa kwenye umati ule mkubwa tarehe 24 Aprili 1993. Na mwenye masikio ya kusikia asikie. !
Comments
Post a Comment