Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6
(Maneno ya mwisho ya Ndugu Philippe kufuatana na mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6)
1 Kaka na Dada, Jumamosi hii, Mei 11, 2024, mimi, Ndugu yenu Philippe, nawatumia, kwa noti hii, maneno ya mwisho ninayotamka kufwatana na utume wa Mathayo 25:6 ambao nilikabidhiwa Aprili 24. 1993. Mnamo Januari 21, 2024, nilipopaza sauti: “pandeni wote kwenye chumba cha juu! ", Sikujua kwamba mimi pia ilibidi ninyamaze na kukomesha misheni yangu.
2 Ujumbe wa Mathayo 25:6 umekamilika. Na ni kwa ruhusa ya Mungu ninawajulisha maneno haya ya mwisho. Sasa ni kwa yule ambaye Mungu atamkabidhi mwenge kutuingiza katika uamsho wa wanawali kumi. Lakini hilo halinizuii kuwatembelea ninyi ikiwa Mungu ataniruhusu, kwa sababu ninawapenda na nina hilo moyoni mwangu.
3 Tunapohubiri na kudumu katika Ujumbe wangu, hebu sasa na tujingojee kwa mtu huyu mwengine na hatua hii inayokuja. Lengo la Ujumbe wangu halikuwa kuwaongoza kwangu ila kuwaongoza kwa Mungu. Kuanzia sasa, mtazame Mungu. Nilikuwa tu ishara ndogo ya kuja kuwaelekeza kwa Kristo. Nilikuwa tu mwongozo wa kuwaonyesha mnakoenda. Mimi sio mwisho wa safari.
4 Kwa hivyo nendeni kwa Kristo wala si kwangu mimi Kacou Philippe, maskini mwenye dhambi aliyeokolewa kwa neema ambaye alikuwa chombo tu mikononi mwa Mungu. Aliyekufa pale Kalvari ili kuwakomboa wanadamu wote, Pamoja na nyinyi nami, na ambaye inatupasa kumfuata, ni Bwana Yesu Kristo.
5 Ninafurahi kwa kuwa nimewapeleka nyinyi mbali na uso wa nyoka, mbali sana na roho takatifu za uwongo. Nina furaha kuwa nimewaelekeza kwenye Roho Mtakatifu wa kweli.
6 Na katika ono nilikuwa na watoto wadogo juu ya mwamba mkubwa. Nilishuka kutoka kwenye mwamba pamoja na watoto. Kisha tukatembea kutoka mwamba hadi mwamba juu ya mto, ambapo mto wa utoto wangu unatoka. Kisha tukashika uelekeo mwingine na tukaelekea pande za juu, mahali nisiyoijua. Na tulikuwa tumefikia tambarare zenye miamba ambapo kulikuwa na mawe mengi yaliyochongwa na kuainishwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
7 Na kulikuwa na mwamba uliokuwa unatikisika tulipokuwa tukiusukuma. Ilikuwa na umbo la mraba, karibu sentimita 50 kila upande. Na urefu wake kutoka ardhi ulikuwa karibu sentimita 70 . kifuniko cha mwamba kiliondolewa. Na tazama, ndani yake palikuwa na chombo cheupe na tupu. Nami nikasema: “Acheni mwamba huo! Huu ni mwamba wa Abraham Mazel. Ni lazima tuende ngambo ingine.” Na ono likaniacha.
8 Kwa maji ya mto wa utoto wangu ambayo ni Ujumbe, tumepitia ukuaji hadi ukomavu na kukomaa. Na baada ya hayo, ilikuwa ni hasa juu ya miamba tulilazimika kutembea kwa hatua ifuatayo. Miamba ilipangwa kwenye mipaka ya mto.
9 Abraham Mazel ni kiwango cha unabii wa akina Camisard na Cévenols, wakifasiri vibaya ufunuo wao. Na walikuwa na manabii wa kiume na wa kike wengi. Na zawadi kubwa sana ya kinabii ya wakati wao ilikuwa ni mchungaji mdogo wa kike wa miaka 15: nabii wa kike Isabeau Vincent.
10 Na mara ya mwisho nilienda Rikédiba nikitembea na Akina Ndugu, ilikuwa Januari 16, 2024. Na nikiwa njiani, nilikuwa nimechoka, na mhubiri Atchui Vincent, mwenye asili kutoka Locodjro, alikuwa amenisaidia kubeba mkoba wangu. Mnamo Agosti 2022, alimwoa dada Rose Isabelle ambaye alikuwa karibu nami sana tangu alipokuwa chuo kikuu, hadi dada Rosine alipokuja mwaka wa 2018. Aliolewa akiwa bikira na umri wa miaka 28.
11 Kutembea katika ukomavu ni kwa njia ya miamba ambayo ni ufunuo. Huduma za manabii wajumbe hupitika juu ya milima, wakati Ujumbe wao ni mito au mito kuu yanayotiririka katika mabonde ya milima.
12 Popote pale Kelele ya Usiku wa manane imefika, mto mmoja au nyingi ni ishara za ujumbe, hata kama mito hii haiitwi Rikediba. Na Ujumbe wangu ambao ni mto wa utoto wangu unadumu milele kama vitabu vya manabii wengine walionitangulia kwa sababu Ujumbe wangu ni kazi ya mikono ya Mungu mwenyewe.
13 Sasa mwisho wa misheni yangu umefikaje? Alasiri ya Jumatano Februari 28, 2024, nilienda kumsalimia mtume Martin nyumbani kwake. Kisha tukashuka na kutembea kidogo uanjani. Kisha nikarudi chumbani kwangu. Na nilipofika kwenye balkoni, nilikuwa nikaishi mambo ya kigeni.
14 Nilikuwa tu nimefika kwenye balkoni, na mtu akaja kwangu akitembea, kana kwamba ananifuata. Na nilipokuwa karibu na mlango wa balkoni, aliinama chini ili nisiweze kumgusa ikiwa ningenyosha mkono. Naye akaenda kuingia kwenye balkoni. Alikuwa ni mzungu mrefu. Na akaniagiza nikae pale bila kuondoka nyumbani. Na nilikaa humo, peke yangu, hadi Mei 10, 2024 kabla ya kuweza kutoka kulingana na neno lake.
15 Na mnamo Machi 26 adhuhuri, katika ono, Malaika aliniomba nisome tena Ujumbe wangu wote. Hii ilikuwa katika shabaha ya kuupunguza kama mto mdogo baada ya kufurika baada ya mvua kubwa. Niliona katika maono mto wa utoto wangu ukiwa umefurika.
16 Nilimaliza kazi ya kusahihisha jioni ya Jumanne Aprili 2, 2024, kabla ya giza kuingia. Ilikuwa chini ya usaidizi Wake, hivyo kwamba niliacha sehemu nyingine na akaniambia nizifute na nikazifuta. Pia, sehemu zote za Ujumbe ambamo nilikuwa nimeweka nafasi kwa waganga pamoja na Mungu, nilizifuta. Hii ni kinyume na imani ya kinabii. Kwa muujiza, sio kwetu kukimbilia waganga kwa uthibitisho, lakini ni kwa adui zetu kufanya hivyo.
17 Hatuwezi kuzungumzia imani ya kinabii na wakati huo huo kuzungumzia waganga au kitabu cha ushuhuda wa uponyaji. Sisi si wakiinjili wala wapentekoste. Tusipoteze utambulisho wetu kwa sababu ya yake yatakayosemwa na maadui zetu. Ikiwa unataka kutenda kulingana na kile watu watasema, unaweza kufanya makosa mengi.
18 Na usiku wa Jumanne, Aprili 2, 2024, niliota ndoto. Katika ndoto hiyo, nilikuwa nimemaliza kazi ya kusoma upya na kuondoa sehemu nyingine. Na malaika mwingine, tofauti na yule aliyenitokea Februari 28, alikuja kwangu, akiwa na muhuri wa posta. Aliniomba nimpe bahasha nyeupe iliyokuwa mbele yangu ili abandike muhuri juu yake.
19 Na nilipompa bahasha hiyo, bahasha hiyo ikawa pakiti la bahasha. Na alipoweka mhuri, nikaona kwamba pakiti ya bahasha imekuwa kitabu kidogo ambacho ni kitabu cha Ujumbe wangu. Naye akakitia muhuri kitabu ili kisifunguliwe. Naye akatoweka na kile kitabu kilichofungwa.
20 Nilipokuwa nikitafakari juu ya ndoto hiyo, nikasema: “Ah!, ndivyo katika Ufunuo 6 kile kitabu cha mihuri saba kilitiwa muhuri! ". Na bado nikitafakari juu ya ndoto hiyo, nikiwaza nitafanya nini katika uamsho ujao ikiwa sitalazimika kuhubiri tena, nilipata maono. Mtu mmoja na mtumishi wake walikuja na chombo kikubwa kilichojaa divai iliyotengenezwa kwa asali. Na wakaweka chombo karibu na mahali alikuwa anaketi mtoto mdogo. Na nikaona kuwa mtoto ni mimi. Na divai ilikuwa na rangi na mwonekano wa asali safi ya asili.
21 Naye bwana akampa mtoto divai iliyo ndani ya sehemu ndogo sana ya nta ya nyuki. Nta ilikuwa ya rangi nyeupe na ilikuwa na umri wa siku moja. Na yule bwana akiwa ameshika sehemu mbili za nta, nilipopokea sehemu ya kwanza, nilimwomba pia anipe sehemu ya pili aliyokuwa ameshika. Nami nilinyoosha mkono wangu hadi mwisho wa ono bila yeye kunipa sehemu ya pili.
22 Na nilielewa kwamba sehemu ya kwanza ilikuwa ni tume chini ya hema kwa kupaza Kelele ya Mathayo 25:6; na kwamba sehemu ya pili ingekuwa tume la usambazaji wa divai kwa Ujumbe mwingine ambao msingi wake ni Ujumbe wangu, kama pia Ujumbe wangu uliweka msingi wake juu ya Ujumbe wa William Branham.
23 Na kwa noti moja niliwajulisha wanafunzi wangu wote maono haya pamoja na ndoto ya kutiwa muhuri kwa kitabu changu kuashiria mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6. Na niliomba kukomeshwa kwa wakfu na kuanzishwa tena kwa ibada.
24 Kuanzia na wale ambao tarehe 2 Aprili 2024 walipatikana katika kuwekwa wakfu, wanaweza kuchukua majukumu na shughuli zote tofautitofauti katika Ujumbe ikiwa ufunuo yao yanawaruhusu kufanya hivyo. Tenda hasa kulingana na Kacou 1 hadi Kacou 154, lakini bila dakika 30 za maombi kwa sasa. Na ninaomba barua hii isomwe katika makusanyiko kesho Jumapili, Mei 12, 2024.
25 Nasema asante kwa Mungu na asanteni nyote kwa yote mlionitendea wakati wa mamlaka haya. Mbele ya Mungu na mbele ya malaika Wake watakatifu na mbele yenu na mbele ya wanadamu, ninathibitisha kwamba nilitenda kwa uaminifu kamili na unyofu. Na Kitabu hiki kilichotiwa muhuri na kupelekwa kwa Mungu na malaika huyu kitafunguliwa siku ya mwisho kwa hukumu ya wale wote ambao waliishi duniani katika wakati wangu hadi nabii mwingine atakapokuja.
Comments
Post a Comment