KACOU 7: KULINGANISHA DARBY NA LOUIS SECOND

(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi mnamo novemba 02, 2003 pa Locodjro, Abidjan – Ivori-Coast)


 1  Nataka kufanya ulinganisho kati ya Darby na Louis Second. Tangu 2002 ambapo nilianza kuhubiri ufunuo kuhusu Biblia, wachungaji na manabii wajanja walipo kutana na Ujumbe, walianza kulazimisha Biblia Darby katika makanisa zao badala ya kuja kukubali Ujumbe. Ijapokuwa, wanaweza kubadilisha biblia na mafundisho lakini hawataweza kubadilisha iliyo ya muhimu ambayo ni roho ya uaguzi wanayoita roho mtakatifu na ndiyo itawapeleka jehanamu. Mnaona?   

2    Tangu 2003, mamia za ukurasa zimetumwa duniani kote juu ya intaneti. Na tunaona mara kwa mara wachungaji, manabii, wainjilisti wakiwa na biblia Darby. Wameacha vitabu vyao kubwa kubwa vya uchawi yaani Louis Segond, Scofield, Thompson, King James.   

3  Kwa hiyo naamini ya kwamba mapepo ya uaguzi tunayo fukuza hapa yanaweza kwenda kuwafunulia mambo yale kwa kuvuruga chanzo. Wengine pia huona kwamba nahubiri ukweli lakini ikiwa watakubali, ni hasara gani?... Kumbuka Matayo 8:28-34 ambapo Yesu alileta ufungulifu kwa baba wawili wa jamaa waliyo rudi nyumbani mwao. Ilibidi iwe karamu kwa utukufu wa Yesu, lakini watu walipoona kwamba wamepoteza zizi la nguruwe, haikuwapendeza, wakamfukuza Bwana Yesu...   

4  Haya! Kuna umati wa ukweli lakini moja tu ndio Ukweli. Kuna miungu nyingi lakini moja tu ndiye Mungu wa kweli. Kuna makanisa mengi lakini moja tu ndiyo Kanisa halisi. Kuna maroho takatifu mengi lakini moja tu ndiyo Roho Takatifu halisi. Kuna tafsiri nyingi za Biblia lakini moja tu ndiyo Biblia ya kweli. [[Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

5 Jua kwamba kuhusu nukta hiyo ya Ujumbe, mapingano mengi yametupwa duniani. Nitaambiwa: "Halafu wale wasiyo na tafsiri ya Darby katika lugha zao?"Mnaoma? Msiogope! Sitaki kuwanyanganya Biblia. Muda wa miaka 1500, baba zenu hawakuwa na Biblia lakini waliishi ukristo vizuri kuliko ninyi.   

6  Wanao tangaza tafsiri Darby, badala ya kutafuta kuitafsiri katika lugha nyingine, wanatafuta namna ya kuirekebisha. Wote walio sahihi matafsiri katika historia walikuwa wahubiri hodari, waliyojaa Roho. Siyo kundi la wataalamu bali mtu moja tu. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »]. 

7 Jua kwamba kiebrania ya kale haisemeki tena na ni lugha ngumu kuliko lugha zote, pasipo herufi za sauti, lakini nafikiri kwamba tafsiri Darby inaweza kugeuzwa katika lugha nyingine jinsi pia siku moja, Ujumbe huu utatafsiriwa katika lugha nyingine nisizoweza kufahamu! Mnaona? Ndicho iliwabidi kufanya. Hata hivyo, siamini marekebisho hata kidogo. Mabadiliko ya lugha yanahitaji kielezi cha chini,  hapana marekebisho. Mara kwa mara Lugha zitabadilika.   

8  Hivyo, Kwa neema niliyopewa, naona sasa ya kwamba, Tangu huduma hii ya Matayo 25:6 na ya Ufunuo 12:14, kuwa na tafsiri ya biblia inayo hukumiwa na Roho ni tendo la uasi. Na pia kuwa na tafsiri Darby niliyo amuru na kubaki mbali na kile ambacho Mungu iko anafanya ni bure. Wokovu iko tu katika kile ambacho Mungu iko anafanya hapa. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

9   Haya! Tuingie ulinganisho! Katika Isaya 35:8-9: njia ndiyo takatifu, hapana barabara. Katika Waamuzi 17:1-5, ni miungu yaani sanamu, wala siyo Mungu Mweza yote. Soma mpaka Waamuzi 18:23-24 ambapo Louis Segond anatambua kwamba ni “miungu” yaani sanamu. Katika Kutoka 32:4, Louis Second anakubali kwamba ndama ya dhahabu ni mungu na katika 1 Wafalme12:28, Louis Second anaandika “Mungu” na “M” kuu japo ni ndama za dhahabu.   

10  Katika Ezekieli 2:1; 3:1, na katika Ezekieli 4:1,... ni "mwana wa watu "maana yake nabiiwala siyo "mwana wa mtu "ambaye ni Yesu-Kristo, nabii mkuu sanakama vile katika Matayo 16:13. Pia, katika Ezekieli 3:12 na 14 vilevile katika Ufunuo 14:13, ni Roho ya Mungu ni kusema “R” kubwa kama vile katika Ezekieli 8:3.   

11  Naendelea. Katika Mwanzo 1:2 ; katika 1Samueli 16:14 ; katika Isaya 61:1,... "R" inabidi iwe herufi kubwa wakati ni Mungu Mweza yote. Japo, sababu ya kweli inayo sukuma Louis Segond kuandika “[r]oho” ya Mungu na “r” ni kwamba, kwa maoni yake, kuna roho nzuri ya Mungu na roho mbovu ya Mungu. Siamini mafundisho hayo. Na hiyo inafunuliwa katika 1 Samueli 18:10. Louis Segond anasema: "…roho mbovu ya Mungu ikashika Saulo"  japo Darby anasema:"...roho mbovu iliyo tumwa na Mungu ikashika Saulo." Louis Second anasema: “roho mbovu ya Mungu...” japo Darby anasema: “roho mbovu iliyotumwa na Mungu...” Si sawa. Ndivyo pia katika 1 Samweli 19:9.   

12  Katika Matayo 24:24, "K" ya makristo za uongo inabidi iwe kwa herufi ndogo kwani siyo Roho Mtakatifu wa kweli bali roho za uaguzi ambazo zitatenda kama roho mtakatifu. Hivyo inafaa kuandika: “makristo za uongo” na “k” ndogo wala sio ma Kristo za uongo”na “K” kubwa.   

13 Sasa katika Ufunuo 1:4, ni “Roho”na “R” kubwakwani ni Roho Mtakatifu katika vipindi saba. Lakini Louis Second anaiandika na “r” ndogo.   

14 Waliondoa “mwana mzaliwa wa kwanza”katika Matayo 1:25 ili kusema kwamba Maria hakuzaa watoto wengine baada ya Bwana Yesu-Kristo. Ni kwa makusudi walifanya mambo haya yote kwa shabaha za kidini.   

15 Herufi ndogo ya kristo au bwana Yesu hasa katika Agano Jipya… zinaheshimu lugha la kigiriki ambayo inaruhusu herufi kubwa tu wakati neno lina maana ya jina la upekee.   

16  Katika Matayo 4:10… Kusujudia ni tafsiri kihalisi ya neno la kigiriki proskïneo.   

17 Katika Ufunuo 1:20, ni taa saba yaani kinara moja wala siyo vinara saba vinavyo weza  kuleta taa arobaini na tisa; ndivyo pia kwa Ufunuo 11:4.   Katika Ufunuo 1:20, ni taa saba yaani kinara moja wala siyo vinara saba vinavyo weza  kuleta taa arobaini na tisa; ndivyo pia kwa Ufunuo 11:4. Katika Yoane 17:11 ni: "ninakuja Kwako”wala siyo "ninaenda Kwako”kwani Baba ni ndani Mwake; pia kwa shairi la 12, ni: “Jina lako ulilo nipa”.   

18  Katika Danieli 5:25, Louis Segond hakuonyesha andiko lililo chapwa juu ya ukuta yaani "Mene, Mene, Tekeli, Ufarsini!". Jua kwamba: Ufarsini ni wingi ya Peresi.   

19  Katika Danieli 9:25-27, kuna mchanganyiko katika tafsiri ya “wiki 70 za Danieli” kama vile Mika 1:10-15 ambayoLouis Segond hakuweza kuitafsiri.  Darby anasema katika Mika 1:10: "…katika Beti-Leafura, ujiviringishe mavumbini ". Louis Segond anasema: "…ninajiviringisha mavumbini katika Beti-Leafura ". Mnaona? Ni tofauti! Mmoja anasema : “ujiviringishe mavumbini” na huyu anasema: “ ...ninajiviringisha mavumbini...”.   

20 Katika Matayo 24:28, ni “tai” wala siyo “tumbusi”. Ni hapo nakazia kwamba matafsiri ya Louis Segond yanatofautiana... kwa kuwa mtafsiri hawezi kufahamu lugha zote za dunia, mtu aliye na Roho ya Mungu angepaswa kutafsiri kwa mfano Darby katika lugha ya kireneo na kihispania… kwani ya muhimu ni kwamba ifanyike katika lugha ya mjumbe na kwa neema ya Mungu, imetendeka hivyo.[Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

21 Katika Ufunuo 1:10, ni “mchana” yaani jumapili wala siyo “siku” ambayo inasemeka kwa siku ya unabii ambayo ni miaka elfu. Japo milenium peke ni miaka elfu.   

22  Katika Mwanzo 4:15, ni yule atakaye ua Kaina ndiye atahadhibiwa mara saba wala  si Kaina ndiye atalipishwa kisasi mara saba. Darby anaandika hivi: «Na Bwana akamwambia: ndio maana yeyote atakaye ua Kaina atahadhibiwa mara saba… »Louis Segond anaandika hivi:“Bwana akamwambia: kama mtu akiua Kaina, Kaina atalipishwa kisasi mara saba…". Siyo sawa. Na katika Mwanzo 4:23-24, mteolojia Lemeki aliitafsiri kwa faida yake ili kumwanga damu kama babu ya babu wake ambaye ni Kaina. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

23  Haya! Matayo 11:23:"hadese"siyo tu "makao ya wafu" kwani kwa upande moja kuna hadese ambayo ni pahali pa masumbuko na kwa upande mwingine kifua cha Ibrahimu.   

24 Katika Waebrania 13:17, Louis Segond anasena: «Mtiini viongozi wenu na muwe na unyenyekevu kwao, kwani wanakesha juu ya nafsi zenu… ». Lakini Biblia  halisi inasema kwamba kuna moja tu anaye kesha JUU ya nafsi zetu na pia JUU ya nafsi za viongozi wetu, na ni Mungu! [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »]. Hivi, tafsiri kamilifu siyo anayekesha juu ya nafsi zenu bali anayekesha kwa ajili ya nafsi zenu.   

25  1 Wakorinto 11:15 inamalizika na nukta wala siyo alama swali kwa kukata kauli kwamba nywele ndefu ndiyo utaji wa mwanamke. Kamati yalio rekebisha Louis Segond yaliitambua.   

26  Katika Waroma 16:1, siyo “shemasi mwanamke” bali “mjakazi”. Shairi la 2 linaionyesha. Mwanamke huyu aliwasaidia watakatifu, ndicho alichofanya.   Ufunuo 12:18 ni sehemu ya aya ya kwanza ya sura ya 13 na siyo: “akasimama” bali “nikasimama…”kwani siyo joka bali Yohana.   

27  Hii kazi juu ya Louis Segond ilifanyika pia juu ya tafsiri King James, Ostervald, David Martin, na zingine nyingi kwa kuwa kila moja ya hizo tafsiri inatawala mahali fulani duniani. Kuna nchi ambapo, hata kwa wakiinjili, Louis Segond  haijulikani. Shetani alifanya kazi maalum na watu hawajui. Mnaona?   

28  Pia, Louis Segond ilirekebishwa mara kadhaa, kesi hii haijawahi kupata Darby. Japo tunajua ya kwamba jambo fulani linarekebishwa kwa kuwa si nzuri. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].  Hivyo, kamati za marekebisho hazikuheshimu aya zilizo katika zile za awali za kiebrania na kigiriki. Na umati wa mashairi yaliongezwa kwa upatano.   

29  Ninaripoti kwamba tafsiri ya Scofield na ile ya Thompsonni masalio, ni  yenye kutokana na tafsiri ya Louis Segond. Kuhusu tafsri  King James yaani mfalme Yakobo, mfalme Jacques IV wa Scotland alipo chukua madaraka Uingereza kwa jina la Jacques 1er, akaomba kwa watafsiri hodari hamsini na nne wa London, wapagani kama vile wa kidini, wafanye tafsiri inayo itwa kwa jina lake, namna ya kuwavuta  wakristo kumpenda. Ni kama vile wangepatia dunia nzima tafsiri nzuri sana ya Biblia inayoitwa: Tafsiri Fidel Castro wala Tafsiri mtawala Bokassa 1er. Japo mambo yale yote ni kazi ya theolojia.   

30 Kwa mfano chukua Louis Segond, sehemu ya kwanza isiyo patana ni: «Louis Segond, mwalimu mkuu wa theolojia» kwa ukurasa wa kwanza wa ile biblia. Kukubali hiyo, ni kukubali theolojia kwani ninapo jua kwamba uchawi si nzuri, namna gani ninaweza kusoma biblia iliyo tafsiriwa na mchawi na inayo kwa ukurasa wake wa kwanza: «Tafsiri ya Zérédji, mchawi mkuu» hata kama imefanyika vizuri? 

31 Angalau pande hii, nasifu waprotestanti na wakiinjili kwani, walipo washutumu wakatolika, hawatumii kamwe biblia Tob. Wakiinjili na watheolojia watasimama siku ya hukumu kwa kuhukumu wabranhamisti. Mnaona? Wabranhamisti wanapenda kuonyesha wanadamu kwamba mti mbaya wa teolojia ambao William Branham alishutumu unaweza kutoa matunda mema sana kama vile Biblia Louis Segond. Na watajibu mbele ya Mungu. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

32  Ikiwa muumini fulani wa haya makanisa hajui kwa nini hizi mabiblia Louis Segond, King James na zingine ni za shetani, nawasihi mumweleze vizuri tangu teolojia hadi kufikia ulinganishi wa mashairi. Lakini ikiwa mbranhamisti fulani, mwana wa Beliali anapinga Ujumbe huu, inatokana na nia mbaya au kiburi tu, kama sivyo ni mchawi kwani hawezi kusema kwamba haelewi…[Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

33  Kuhusu kukata Biblia kwa sura na mashairi, kwanza kwa karne ya IX,  wamasora (marabi na wasomi wa kiyahudi) wakaingiza nambari pembeni katika gombo za Agano la Kale wakiacha aya namna zilizo, mzima, bila kuzibadilisha. Tena kwa karne ya XIII, watu wawili: kardinali moja aitwaye Hugo na askofu mkuu muingereza aliye itwa Langton wakakata matafsiri za kwanza kwa sura. Ni katika mwaka wa 1520 ndipo Sanctès Pagnin aliweka nambari pembeni katika tafsiri yake ya kilatini Kama vile katika gombo za kiebrania sawa na Darby, bila kutofautisha mistari.   

34  Lakini katika mwaka wa 1551, Robert Estienne, katika tafsiri yake ya kiingereza ya Agano Jipya iliyo tokea Geneva, aliifanya kama vile Louis Segond, akivunja-vunja maandiko kwa mashairi na kila shairi kwa mistari, hivyo akaharibu zile aya za gombo za kiebrania na za kigiriki. Robert Estienne alifanya hivyo kwa kutangaza vulgati yake iliyotokea mwaka 1555. Mfumo huu wa kishetani ukakubaliwa kwanza na viongozi wa kidini wa Ufaransa na vyama kuu vya  kiinjili vya wakati ule. 

35  Ndivyo kupitia Darby inajulikana ya kwamba Ufunuo 12:18 ni shairi ya kwanza ya Ufunuo 13. Ufunuo 12:18 inasema hivi: “Na nikasimama juu ya mchanga wa bahari” na Ufunuo 13:1 inasema: “na nikaona kutoka bahari mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake taji kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru”. Na ndani ya Darby, nyota ndogo zinaonyesha mwanzo wa sura katika awali za kiebrania. Kwa hivyo, Mwanzo 2:4 ni mwanzo wa sura  ya pili ya Mwanzo, na vivyo hivyo katika Biblia nzima. Mnaona ya kwamba Mwanzo 2:1 inasema: “Ndivyo ikawa mwisho…”.Na mnaona kwamba ni mwanzo wa kumalizia sura ya 1.   

36  Kufwatana na historia, John Nelson Darby alizaliwa London mwaka 1800 na baba wa Irland. Yeye ni wa Irland sawa vile William Branham na Colomban. Baada ya masomo mengi ya haki katika chuo kuu cha Dublin pa Irland, akawa wakili, kabla ya kuacha baraza la wanasheria kwa kumfuata Bwana. 

37 Kama vile John Wesley mwaka 1725, akawa shemasi mdogo wa kanisa la anglikani mwaka 1825, kiisha, akawa mchungaji mwaka uliyo fwata katika vijiji vya Wicklow huko Irland kabla ya kuachana na kazi hiyo baada ya kukosa makubaliano na wakuu wake. Baada ya masomo mengi ya mwanasheria, kitu moja ambacho Darby alijifunza ni malugha kwa namna aliongea kiebrania na kigiriki ya kale kama lugha yake ya kuzaliwa.  Kujifunza lugha siyo teolojia!  

[Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

38 Baadaye, rafiki wake John Gifford Bellett, yeye pia wakili, akajiunga naye. Tangu hapo, akitegemea tu Roho Mtakatifu, Darby akaanza kuhubiri katika vijiji na mashambani tangu Irland, kupitia Ulaya, Asia na Amerika akishutumu tengenezo la kanisa, urais wa mwanadamu juu ya kanisa, anasa na teolojia na hapo kuonyesha kwamba “Yesu Kristo ndiye Yehova wa Agano la Kale”, akialika makanisa zote kurudilia msingi ya mitumena manabii. Darby aliongea kiingereza, kifaransa, kiebrania, kiyunani, kijerumani, na kiitaliano. Alitafsiri Agano Jipya na la Kale karibu mwaka 1859 baada ya ile ambayo Louis Segond alitafsiri kwa ombi ya kampuni la wachungaji wa Geneva.   

39  Tafsiri Darby ikapita ile ya King Jams ambayo mfalme Yakobo aliomba ifanyike kwa jina lake, na iliyo fanyika mwaka 1611, tafsiri ambayo ilitawala kwa muda wa karne mbili na ilikuwa ni kurejea ile ya William Tyndale.   

40 Na kuzungumzia tafsiri King James, mfalme Yakobo mwenyewe alikubali wasomi 47, watafsiri mashuhuri ambao kwa hesabu yao inabidi kuongeza hesabu fulani ya marabi wakuu wayahudi waliyo kuwa na maandiko bora zaidi na wote waligawanywa kwa makundi kubwa kubwa tatu. Kundi moja kwa chuo kuu cha Cambridge, kundi lingine kwa Oxford, na kundi la mwisho huko Westminster. Na kila kikundi kiligawanywa pia kwa kundi ndogo ndogo mbili. Kwa jumla vikundi sita. Kundi la kwanza lilipomaliza lilipitisha kazi kwa kundi la pili ambalo pia lilipitisha kwa kundi lifwatalo… Na japo hivyo, ilisahihishwa mara kumi na nne kabla ya onyesho la kwanza la King James mwaka 1611. Japo kila moja wao alijua sana kiebrania kuliko haizuru muyahudi fulani.   

41  Na ilisemeka kwa moja wa watafsiri wa King Jams ya kwamba alikuwa msujaa sana katika lugha zote, hasa zile za mashariki, kwa namna angekuwepo kwa mchanganyo wa lugha wakati wa mnara wa Babeli, angeweza kuwa msaada kwa kutafsiri. Na babu ya babu ya mtu kama huyu alikuwa mjenzi wa mnara wa Babeli na tazama mjukuu wa mjukuu wake ni mjenzi wa mnara wa Babeli mpya uitwao “biblia King James” katika hiyoEdeni ya Shetani. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

42  Lakini kwa maongozi ya Mungu Darby, mtu mmoja tu, akasimama kutoka Mungu kwa kutafsiri Biblia. Je! Mungu Mweza yote anahitaji wajuzi hamsini na nne kwa kutafsiri Biblia? Je! Mungu hutumika na wenye akili?...   

43  Tafsiri Darby ikapita ile ya mwana theolojia mwenye nguvu Ostervald ambalo linategemea marekebisho ya mwana falsafa na mwana theolojia David Martin kwa ombi la sinodi ya makanisa ya walloni kwenye Biblia ya Lemaistre de Sacy. Niligundua kwamba Jonh Nelson Darby alikuwa ameenda mbali zaidi katika utafsiri wa mafumbo ya Biblia. Tayari akionyesha katika karne ya 19 kwamba wazee ishirini na nne waliozunga kiti cha enzi walikuwa wote mitume kumi na mbili na wazee kumi na mbili, na kwamba Mwanzo 1:27 haikuhusu wa malaika. 

44 Biblia moja tu duniani iliyoshinda na ambayo haijaguswa wala kurekebishwa hata na mtafsiri wake na ambayo haikuwa rejeo au tafsiri kutoka matafsiri mengine ni hii ya wakili John Nelson Darby. Hii ndiyo Bibilia inayofaa kwa ujumbe wa kurudisha upya [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

45  Na nilipata ufunuo kwamba ndiyo Biblia ya Bibi Arusi wakati hii ya mwisho kabla yangu kupata habari hizi. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].   

46  John Nelson Darby alifariki mnamo Aprili 29, 1882 na tazama maneno yake ya mwisho: “Mungu ahimidiwe, sizani ya kwamba nina lolote la kuondoa, wala la kuongeza. Sina la kuongeza ila tu shukrani na upendo wangu wa kweli kwake” Barua ya mnamo Machi 19, 1882. Maneno haya yawe pia yangu kwa mwisho wa Ujumbe huunanipewe kama vile ninyi pia mulioamini, sifa za ushindi na huu ndiyo msimamo wetu! [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »]. 

47 Nasema nilicho ona na kile Mungu alicho niamuru kusema kama vile kwa Musa, Paulo na manabii wote waliyo nitangulia... niliitwa kwa namna isiyo ya kawaida na nilitumika kama wao, ikiwa wao wanaingia, sisi pia tutaingia [kusanyiko linasema: “Amina!”].   

48  Sasa, jua kwamba Bibilia yatoka katika maandiko ya kale. Maandiko tatu ya mkono yanayo julikana sana yanayokusanya karibu kanoni yote, kwa jumla vitabu vilivyo julikana vya agano la kale na agano jipya ni: Sinaïticus iliyo gunduliwa kwa karne ya 4 katika monasteri mtakatifu Katherine ya mlima Sinai. Ina Agano Jipya na la Kale nzima; leo imechungwa katika British Museum ya London. 

49 Kisha inakuja Alexandrinus iliyo gunduliwa kwa karne ya 5 huko Alexandrie katika Misri, ina Agano la Kale na Agano jipya na ya kushangaza, Agano Jipya inaanza na Matayo 25:6. Hii yapatikana katika encyclopedia ya kibiblia ya Frank Reisdorf-Reece. Kwetu sisi, siyo kubahatisha tu. [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »]. 

50 Kisha ya 3, Vaticanus, ambayo asili yake haijulikani, isiyo na maana, haina 1 na 2 Timoteo, Filemono, Tito na Ufunuo. Imechungwa huko Vatikano.   

51 Tunakadirisha kwamba maandiko haya ya mkono iliyoletwa kwa waafrika na inayoanza na Matayo 25:6 ni alama ya unabii. Na tazama ripoti ya wateolojia kulingana na ile ile encyclopedia, kwa ukurasa ule ule. Imeandikwa: “tafsiriya kwanza ya kiprotestanti, ilikuwa ile ya Olivetan, 1535. Ikasahihishwa na Jean Calvin katika mwaka 1550 na baadaye ikasahihishwa na Theodore de Bèze na ikachapishwa na Corneille Bertram, Geneva 1588. Tangu wakati ule, ilirekebishwa na David Martin, 1707 tena na Jean Frédéric Ostervald. 

52 Zile tafsiri zote leo zinabadilishwa na tafsiri zile za Louis Segond Geneva 1874-Oxford 1880, ile inayoitwa ya mtaguso iliyo rekebishwa katika mwaka wa 1926, na ile tunayo kadirisha kuwa aminifu zaidi kwa maandiko za awali, ni ile ya J.N. Darby”. Amina! Je! Mnaelewa ? Nina soma tena huu msemwa wa mwisho: “ ...ile tunayo kadirisha kuwa aminifu zaidi kwa maandiko za awali, ni ile ya J.N. Darby”.[kusanyiko linasema: “Amina!”]. Lakini namna gani basi mnajua ya kwamba tafsiri Darby ndiyo aminifu sana kwa maandiko za asili na mnaiacha na kwenda kutumia tafsiri za King James, za Scofield, Thompson, na kadhalika... ? Sielewi ! Lakini mimi napendelea tafsiri aminifu sana hata kama ni ngumu kuelewa.   

53  Tazama kwa mfano tafsiri King James, ilitafsiriwa na kundi japo Mungu hatumii kundi bali hutumia mtu moja tu! Na kulikuwa na marekebisho na marekebisho na marekebisho.  Na rekebisho la mwisho la King James lilifanyika mwaka 1881. Kabla ya Kelele ya usiku wa manane, mambo haya hayakujulikana, lakini sasa yamejulikana, msibishanie! Muipokee kama amri ya Mungu. Amina!   

54  Mungu alisema katika Matayo 25:6 na Ufunuo 12:14 ya kwamba Ujumbe fupi utakuja kwa kupeleka wachaguliwa mbali na uso wa nyoka: mbali na makanisa haya ya kikatolika, kiprotestati, kiinjili na kibranhamisti, pamoja na islamu na uyahudi… 

55 Mbali na roho takatifu inayotenda katika makanisa hayo… mbali na hao wa Kaina, Tomy Osborn, Kenneth Hagin, Ushe Praise, Morris Cerullo, Yongi cho! Mbali na Aki na Joel Osteen, T.D Jakes, Doug Batchelor, Billy Graham, Edir Macedo, Valdemiro Santiago, Silas Malafaia, Paula White, Joyce Mayer, Chris Oyakhilome! Mbali na Hao wa David Owuor, Emmanuel Makandiwa, Uebert Angel, T.B. Joshua, David Oyedepo, Alberto Mottesi, Claudio Freidzon na Dante Gebel. 

56 Mbali na wale wa Benny Hinn, Manasseh Jordan, Jesse Jackson, John Hagee, Pat Robertson, Joaquim Gonçalves, Donald Parnell, Alejandro Bullon na Guillermo Maldonado! Walozi na wachawi kama imeandikwa katika Yoeli 2:28 na 1 wakorinto 2:4-5. Mbali na Next Generation Alliance. Mbali na Carlos Annacondia, Paul Ayoh, Benjamin Boni, Jean-Baptiste Nielbien, Bernard Agré... Mbali na haya maduka ya vitabu na vyombo vya habari vya kikristo… Mbali na hizo miungano na mashirikisho za makanisa… 

57 Mbali na hizi vitabu vya uchawi viitwavyo biblia Louis Segond, King James, Tob, Scofield, Thompson… Mbali na hao manabii wanao zunguka duniani na, ni Ujumbe huu ndiyo mabawa mawili ya Tai kubwa ya Ufunuo 12:14 na ambayo inapaswa  kuwapeleka wachaguliwa jangwani mbali na uso wa nyoka. Jihadharini nao! Kwani hakuna wokovu nje ya Ujumbe huu. Tambueni siku na Ujumbe wake! Ni walozi na wachawi kama ilivyoandikwa katika Yoeli 2:28 na 1 wakorinto 2:4-5. [kusanyiko linasema: Amina!]. [Kc.22v35] 

58  Tuinamishe vichwa! Ninyi mliyo pale kwa mara ya kwanza, baada ya kusikia Ujumbe huu, je! Kuna anaye amini kabisa na anaye tamani kuikubali?... ikiwa ndivyo, anyanyue mkono wake kwa upole!... inakubidi kuifanya kwa uhuru kwani hitaji letu siyo kwamba Mungu ageuze kaa ya pwani kuwa samaki! Ikiwa ataifanya, itakuwa vizuri, lakini kutakuwa na samaki nyingi hapa, lakini samaki zilizo na mwenendo wa kaa na tutapata wote shida. 

59 Ikiwa mtu fulani anasema nitanunua Biblia Darby lakini nitabaki katika kanisa langu la katolika, protestanti, kiinjili ao branhamisti,  mwacheni! Mnaona? Ni kaa ya pwani. Lakini kile anacho tafuta Mungu asubui hii, ni samaki; ni wateule. Amina! Kuna anaye tamani kukubali Ujumbe huu asubui hii ? [Ndl: mtu moja ananyanyua mkono]. Kaka, Mungu akubariki! Ndiyo, kaka pale! Dada pale, Mungu akubariki pia!... Acheni mikono yenu juu ninapo waombea! Mungu akubariki pale! Mungu akubariki pia pale...   

60 Bwana Yesu Kristo, Wewe Bwana na Mwokozi wangu, naomba ili katika uamzi huu, ushikilie imani yao! Kukata shauri yao itajaribiwa na shetani na hatuta kuweko kwa kuwashikilia lakini tunawakabidhi kwa neema yako ya uungu! Na wakati tunaenda kumaliza ibada ya asubuhi hii, ninakabidhi kila kaka na kila dada mikononi mwako ili, tunapo tengana kimwili, tuungane kila mara katika Roho moja na imani moja mbali na dhambi mpaka tutakapo kutana tena! Bwana Yesu-Kristo, utupe nguvu na utupe ushindi juu ya dhambi na juu ya shetani na hata heshima, utukufu na ukubwa viwe kwako milele na milele, Amina!   



Sura inayofanana : Kc.42

Comments

Popular posts from this blog

KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI

KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI

Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6