Kacou 20: Uhamisho wa roho
(Ilihubiriwa jumapili16, Novemba 2003, Huko Locodjro, Abidjan Ivort- Coast)
1 Asubuhi ya leo, ningependa kuzungumza juu ya somo: uhamisho wa roho. Hapo awali, ilikuwa ni kwa njia ya sinodi na mabaraza ya kiekumene ndipo uhamishaji wa roho ulianza, kisha kwa kukabidhi Kanisa kwa Serikali kupitia sheria na kanuni za ndani, kisha kupitia miungano, mashirikisho na mabaraza ya makanisa na sasa kwa makusanyiko, na hata kwa kumpa mimbari kwa yule ambaye haamini nukta kwa nukta au ambaye hana roho sawa na wewe; hata kama anahubiri vizuri.
2 Uhamishaji wa roho pia hufanyika wakati wa kubadilishana au kuazimana nguo na mtu ambaye si Ndugu au Dada. Pia kwa kushirikiana na watu fulani kama inavyoonekana katika 2 Mambo ya Nyakati 20:35-37 na 2 Mambo ya Nyakati 18 na 2 Mambo ya Nyakati 19:1-3.Yehoshafati lazima aelewe kwamba Mungu hataki tufanye urafiki na mtu asiyeamini au mwabudu sanamu.
3 Huna haki ya kwenda kwenye mkesha, kongamano au mkutano wa makanisa haya ya kikatoliki, ya kiprotestanti, ya kiinjili, misioni na huduma pamoja na wabranhamisti wote yaani wale ambao bado wanafuata Ujumbe wa William Branham hata katika usafi wake wote. Kwa sababu matokeo ni uhamisho wa roho.
4 Huwezi kuimba au kuomba na mtu kabla ya kukubaliana juu ya jambo la mwisho linalokutofautisha, kwa sababu nyuma ya Mbranhamisti, Mbaptisti au Foursquare, kuna pepo wengi kama nyuma ya Mkatoliki. Je, mnafahamu hilo? Nyuma ya Mkatoliki, Mprotestanti, Wakiinjili au Mbranhamisti, kuna pepo wengi sawa na yule anafuata Urusikrusiani, Ufremasoni au Vooduu. [Kc.89v3]
5 Mamia ya pepo wanaweza kusimama nyuma ya uwongo mmoja. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. Wala msiwahi kutamka kwenye ndoto ya watu hawa… usije kamwe pamoja kwa maombi hata kidogo. Ikiwa hali hiyo ilikushangaza, usifunge macho yako au utoke tu. Biblia inasema tusiwe na ushirika na pepo. [Kc.19v1]
6 Msijipendekeze kwa neno lolote kwa sababu ninyi si “ndugu” au “dada” katika Yesu Kristo yuleyule. Huna haki ya kumwita Mbaptisti au Mwadventista au Mbranhamisti “ndugu katika Kristo”, na msiwaruhusu wakuite hivyo. Ni majirani zetu na tunawapenda kwa sababu Biblia yasema: “Mpende jirani yako kama nafsi yako”. Tunaona maombi yao kama kelele katika jina la Yesu Kristo. Na tunayachukulia makanisa yao kama madhabahu za miungu ya Misri. Na lazima tuwe wakali kwao ili kuepuka uhamisho wowote wa roho katika maisha yetu. [Kc.67v30]
7 Na mtu yeyote akija kwetu kutoka katika makanisa haya, kwamba amebatizwa kwa jina la Yesu Kristo, au kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, kwamba amebatizwa kwa kuzamishwa au kwa kunyunyiziwa. lazima tu kabisa na kubatizwa tena.
8 Lazima mjue kwamba kuna mielekeo miwili duniani: wao na sisi. “Na asiye pamoja nasi yuko dhidi yetu, asiyekusanya pamoja nasi anatawanya. Luka 11:23. Chochote wanachofanya ni uchawi tu kuzipeleka nafsi za watu matekani ya jehanamu. Tunapochoma Biblia zao, vijitabu na kadhalika, ndivyo Mungu atakavyowatupa katika ziwa la moto.
9 Mungu wa Israeli ni tofauti na mungu wa Waarabu wanaozunguka Israeli. Na Mungu wetu ni tofauti na mungu wa makanisa yanayotuzunguka. Na hawa Wakatoliki, Wabaptisti, Wamethodisti, na hao wote mnaowaona karibu nasi, ni Wairaki, Wayordani, Walebanoni, Wasiria, Wapakistani, na Waarabu wanaotuzunguka.
10 Israeli ni bonde la manabii na mwana wa Mungu anafuata nabii aliye hai kwa sababu nabii ni kinywa cha Mungu duniani. Biblia ni kitabu cha vitabu vya manabii na mtoto wa Mungu hawezi kuishi mbali na nabii aliye hai. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. [Kc.114v20]
11 Tekelezeni mambo haya, nami nasema ya kwamba zile roho mlizozitoa kwao hapo awali zitarudishwa kwao. Na katika Jina la Yesu Kristo, itakuwa hivyo! Kuwa na ustadi wa somo hili: "Uhamisho wa roho". Chomeni hizo biblia za uongo na shetani atajua hana sehemu na nyinyi. Wajulishe watu hao kuwa hamko katika hali sawa!
12 Kwa ninyi mnaotoka kwenye Ujumbe wa jioni, kuna baadhi ya wabranhamisti waliowekeana mikono wakati wakati wa kuoshana miguu. Kwa usiku wa manane, hii haiwezekani tena kutokana na uhamisho wa roho. Ni sawa na makanisa, makusanyiko ambapo watu huomba kwa kushikana mikono au kuwekeana mikono.
13 Usiweke kamwe haya yanayoitwa viwakilishi vya Yesu Kristo nyumbani pako. Hata ile ya Hofmann. Mitume na wanafunzi walipinga hili. Yusebia pia, yule aliyechagua vitabu 27 vya Agano Jipya kati ya 62, alipinga uwakilishi wa Yesu. Ilikuwa ni kwenye Baraza la Konstantinople katika mwaka wa 692 ambapo uwakilishi wa Yesu uliidhinishwa.
14 Ikiwa Bwana Yesu Kristo ni Mungu, basi Anaweza kutokea kwa namna nyingi, na ni chukizo kujaribu kumwakilisha Bwana Yesu. Wanafunzi wawili waliokuwa njiani kuelekea Emau hawakumtambua. Katika Yohana 20:11-16, Maria Magdala hakumtambua. Na Biblia husema kwamba Bwana Yesu Kristo alionekana mara nyingi katika namna mbalimbali. Kwa hivyo utamwakilishaje? Katika kujaribu kumwakilisha Bwana Yesu Kristo, Mungu atamfanya Yuda ambaye utamwakilisha na kumweka katika nyumba yako.
15 Jitengeni na chochote kilichochafu . Mnaona? Bado hatujakaa pamoja kwa miaka mitatu lakini nikirudi baada ya miezi mitatu kusafiri, je hamtanitambua? Ni vipi basi siku tatu baadaye, mchana kweupe, Simoni Petro, Tomaso, Yohana, Yakobo na wanafunzi wengine waliokuwa wakivua samaki hawakumtambua Bwana Yesu? Yote ni sawa! Mnaona?
16 Na Marko 16 inasema …hebu na tuisome, “Na baada ya hayo akawatokea katika sura nyingine wawili wa wale waliokuwa njiani, wakienda ushambani. Kwa nini? Kwa sababu Yeye ni Mungu Mwenyezi! Na nyie wana wa ibilisi mliishia kumpa uwakilishi! Lakini nina hakika kwamba picha hii inayodaiwa kuwa ya Yesu iko karibu na Yuda Iskariote kuliko Bwana Yesu. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
17 Na nitamalizia na hili: Epuka kusema “Mungu aliniambia” kwa sababu ikiwa si Mungu, basi umemwita Shetani mungu wako. Kwa hivyo wale wote wanaokusikiliza watapokea roho hii. Unaweza kuona ufunuo ya haki na yaliyo wazi na hiyo ni ya shetani.
18 Na ikiwa mtu yeyote anajiita Mkristo na kudai kuwa ana Roho Mtakatifu, ikiwa anakataa Kelele ya usiku wa kati, usiogope kumwambia kwamba yeye ana roho ya uaguzi kulingana na Ezekieli 33: 1-9 na kuwa safi na damu yake siku ya hukumu. [Kc.16v11]
19 Nanyi mjua kwamba ni bora zaidi kwenu kuwahubiria wazazi wenu na watu wa ukoo wenu Ujumbe ili wasije wakatafuta kusali pamoja nanyi mfikapo nyumbani kwao… Tangulieni! Na kuwa safi na damu yao. Amina!
Sura inayofanana: Kc55
Comments
Post a Comment