KACOU 19: MASWALI NA MAJIBU SEHEMU YA PILI NA MWISHO


( Maswali yaliulizwa tarehe tofauti pale Locodjro, Abidjan - Ivory - Coast)


1 S-J. N°1/ Ndugu Philippe, tunapaswa kufanya nini ikiwa tuko katika kanisa ambalo kuna fundisho moja tu la uwongo kama vile ubatizo au Mwanzo 1:26-27? 

 Ukiwa katika kanisa ambalo kuna fundisho moja la uongo, ni lazima utoke humo kwa sababu nyuma ya kila fundisho la uongo kuna pepo.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  Katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27, Biblia haisemi, “Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu... Mungu na malaika wakamuumba mtu” bali Biblia inasema, “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake. ".  Wana wa shetani waliojiweka kuwa manabii na wachungaji wanasema ni Mungu na baba yao Shetani ndio waliyemuumba mwanadamu pamoja.  Na wanachukua Ezekieli 28:12 na kusema kwamba Mungu aliumba na malaika pamoja na Shetani walimaliza kwa ukamilifu.  Hivyo ndivyo Louis Segond na matoleo mengine ya Biblia yanavyosema lakini sivyo Darby anavyosema.  Mnaona ?  

2  Biblia ya Louis Segond, chombo hiki cha Shetani kinasema kwamba Mungu aliumba na Shetani akaweka muhuri kusema kwamba ni kamilifu.  Huoni huo ni upuuzi?  Darby inasema, “Wewe (Shetani) ulikuwa umbo la ukamilifu, umejaa hekima na ukamilifu wa uzuri;  ulikuwa Edeni bustani ya Mungu” lakini Louis Segond inasema: “Uliweka muhuri kwa ukamilifu…”.  [Kc.20v3]

3 Nawaambia kwamba katika Mwanzo 1:26-27, Mungu hakuwa anazungumza na malaika yeyote vinginevyo damu ya Bwana Yesu Kristo ingeokoa pepo.  Malaika ni roho na hawako katika sura ya wanadamu.  Mnaona ?  Mungu mwenyewe ni Mwanadamu na Malaika.  Mnaona ?  Yeye mwenyewe ni Malaika wa Yehova.  Hatujui kilichotokea wakati wa uumbaji Mbinguni, Mungu angesema "Na tumfanye malaika kwa mfano wetu...".  Angesema hivyo, kwa maana  alipaswa  kudhihirishwa kama Malaika wa Yehova. 

4  Sasa hebu tuangalie Mithali 8, Mungu alizifanya tu sifa zake kunena.  Hakuna malaika aliyeshiriki katika uumbaji wowote, si Mbinguni wala duniani na hakuna malaika anayeweza kuumba.  Kusema kwamba Mungu alikuwa akizungumza na malaika katika Mwanzo 1:26-27 ni kuhusisha uwezo wa uumbaji na malaika na kumfanya kuwa sawa na Mungu.  Siamini kwamba mtu au kanisa ambalo lina Roho Mtakatifu linaweza kusema kwamba Mungu alizungumza na malaika!  Je, nilijibu swali?  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  "].Vizuri sana !  Na hili ndilo jibu la Mungu mwenyewe kupitia nabii wake.

5 Ni lazima Biblia iseme kwamba wakati kama huo, mahali fulani, Mungu atafanya jambo kama hilo.  Na hicho ndicho kitu pekee ambacho Mungu anaweza kutambua.  Kwa hiyo ukiwa ndani ya kanisa linalodai kuwa lina ukweli wote huo ni udanganyifu kwa sababu Roho na Neno wakisema tupo usiku wa manane, hapo ndipo unapopaswa kuwa ili kumpokea Roho Mtakatifu.

6 S-J. N°2/ Ndugu Philippe, katika Ufunuo 12:1 ni mwanamke gani?  Vema!  Hebu tusome : “…mwanamke aliyefunikwa na jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake”.  Haya! Juweni kwamba Yohana alimwona mwanamke huyu wakati fulani wa historia kwa sababu hapo mwanzo alifunikwa na mwezi, alitembea na sheria, ni Israeli na nyota kumi na mbili walikuwa wazee kumi na wawili lakini baada ya dhabihu ya milele, Yohana alipomwona ulikuwa ni Ukristo, Kanisa la Yesu Kristo na nyota kumi na mbili ni mitume kumi na wawili, fundisho la mitume kumi na wawili.  Mitume kumi na wawili na wazee kumi na wawili wanaleta wazee 24 wa Ufunuo 4:10.  

7  Yesu alisema katika Mathayo 19:27-28 kwamba mitume wangepokea viti kumi na viwili juu ya kuwahukumu Wayahudi.  Na juweni kwamba Ufunuo 12:5-6 inazungumzia Uyahudi na siku 1260 na inahusiana na Ufunuo 11:3 na Eliya na Musa lakini mwanamke katika mstari wa 14 ni Ukristo.  Kisha, kama katika aya ya kwanza, tunawapata wanawake hawa wawili katika mmoja.  Lakini wa kwanza hana tena umbo lake la mwanzoni la Kiyahudi kwa sababu imemkubali Kristo.

8 S-J. N°3/ Ndugu Philippe, katika 1 Samweli 28:7-20, mwanamke huyu mpandisha pepo aliwezaje kumfikia nabii Samweli?  

Jibu ni kwamba kabla ya dhabihu ya milele, Paradiso ilikuwa duniani na shetani angeweza kuwafikia watakatifu wote: Ibrahimu, Daudi, Adamu, Yusufu... Tunaona kwamba alitaka kuuchukua mwili wa Musa!  Yuda mstari wa 9. Damu ya mbuzi na kondoo ilikua ikifunika dhambi tu na haikuweza kuziosha ili tuweze kwenda moja kwa moja Mbinguni.  Paradiso ilikua ya kufungwa.  Lakini sasa baada ya dhabihu ya Bwana Yesu Kristo msalabani, kuingia ni mara moja. 

9  Baada ya damu ya Yesu Kristo, kulikuwa utengano, Luka 16:22-23 inaonyesha vizuri.  Pia, wakati huo, ibilisi bado alikuwa anashikilia funguo za kuzimu hadi Bwana Yesu Kristo alipokuja kuzichukua kulingana na Ufunuo 1:18.  Kumbukeni kwamba alichofanya mwanamke huyu hakiwezekani tena leo.  Ukiona mtu aliyekufa kama mzimu, basi nafsi yake iko kuzimuni ndiyo maana Shetani aliweza kuufikia mwili wa

10  S-J. N°4/ Ndugu Philippe, katika ono la Aprili 24, 1993, Mwana-Kondoo alisema nini katika lugha isiyojulikana?  Ilikuwa ni siri kubwa ambayo haikupaswa kujulikana mpaka leo.  Ila sasa inajulikana na ni Ujumbe uliomo katika Kelele ya usiku wa manane.  Hata mwili wangu haukuweza kuufikia lakini ni nafsi yangu iliyoipokea kama muhuri.  Mahubiri haya ni tafsiri ya kile alichosema Mwana-Kondoo ambayo ni utimilifu wa siri ya ngurumo saba.  Shetani anajua kilichotokea katika bustani ya Edeni, pia alijua maana ya (ile) mihuri saba, lakini hakuwahi kufikiria kwamba, akichukua Jina la Bwana Yesu Kristo na kujificha nyuma ya biblia Louis Segond, King James au Scofield angefunuliwa.  Laiti angejua, angetumia ujanja mwingine zaidi ya huo.

11 Kwa kweli, Si kwangu mimi binafsi tu ndio urejesho huu ulitolewa bali kwa Kanisa.  Ikiwa ilikuwa katika Kifaransa na ningeshika kitu fulani, singesubiri miaka kumi.  Na siku iyo hiyo, siku ya ono, Roho alikuja juu ya Ujumbe huo, juu ya Neno.  Na matunda yalidhihirishwa: Nilikataa mafundisho ya ubatizo na hata ubatizo wa Utatu nilipokuwa na uongofu kwa miezi mitatu.  Roho Mtakatifu huja juu ya Neno pekee.  Bwana Yesu Kristo alikuwa Neno lililodhihirishwa, na Roho Mtakatifu akashuka juu Yake katika umbo la njiwa.

12 Na mtu yeyote akisema ana Roho Mtakatifu, haijalishi anatabiri jinsi gani, yeye hunena kwa lugha na kutenda miujiza, usibishane naye bali mjulishe Neno kwake, wasilisha Ujumbe huu kwake na umwambie ya kwamba lazima mtu kubatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo kulingana na Ujumbe wa wakati wake.  Akikataa basi mwambie kuwa roho aliyo nayo ni roho ya shetani na muwe safi na damu yake atakapokwenda kuzimu.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  Msimwache mpaka umwambie hivyo.  

13 Mwambie, hata kama ananena kwa lugha au kufufua wafu, hata kama jina lake ni Kaini, Joel Osteen, T.D. Jakes, Doug Batchelor, Billy Graham, Edir Macedo, Valdemiro Santiago, Silas Malafaia, Paula White au Joyce Meyer, fanyeni hivyo. ili Mungu asiwadai damu yao!  

14 Hata kama jina lake ni Chris Oyakhilome, David Owuor, Emmanuel Makandiwa, Uebert Angel, T. B. Joshua, David Oyedepo, Alberto Mottesi, Claudio Freidzon au Dante Gebel, fanya hivyo ili Mungu asikudai  damu yao! 

 15 Hata kama jina lake ni Benny Hinn, Manasseh Jordan, Jesse Jackson, John Hagee, Pat Robertson, Joaquim Gonçalves, Donald Parnell, Alejandro Bullón au Guillermo Maldonado, fanya hivyo ili Mungu asikudai  damu yao!  Wao ni wachawi na walozi kufuatana na  Yoeli 2:28 na 1 Wakorintho 2:4-5.  Fanya hivi ili Mungu asikudai  damu yao!  Narudia tena, fanya hivyo ili Mungu asikudai damu yao![Mh: Kusanyiko linasema: “Amina!  ”].

16 S-J. N°5/ Ndugu Philippe, je, mtu anaweza kuokolewa kwa utakaso wa mwili pekee?  Hapana Ndugu!  Leo hii haiwezekani tena.  Hili liliwezekana mpaka kwa  John Wesley lakini baada ya hapo, linahitaji utakaso wa kimwili na wa kiroho.  Ikiwa mtu leo anajiepusha na mambo yote ya ulimwengu, ibada ya sanamu, kupiga punyeto, uzinzi, uasherati, uwongo, mafundisho ya uwongo, ni sawa, lakini vipi kuhusu roho za uaguzi alizioipata kupitia mambo hayo?  

17  Na hakuna awezaye kufukuza roho hizi isipokuwa kwa uwezo wa Ujumbe utakao zifunua.  Huu ni utakaso wa kiroho.  Ni lazima kuwe na utakaso wa kiroho katika wakati huu.  Utakaso wa mwili pekee hautoshi tena.  Pia, haiwezekani kwa mshiriki wa makanisa haya ya Kikatoliki na ya kiinjili kufukuza pepo.  Wanachoita ukombozi ni maigizo, jukwaa la Shetani.

18  S-J. N°6/ Ndugu Philippe, unafikiri nini kuhusu maonyesho ya kiroho na unyakuo  wa Bibi-arusi utafanyika lini? 

Vema!  Ni kwa sababu kuna nabii mjumbe Duniani ndio maana  kuzungumzia  Kanisa.  Na huduma nne za Neno zinatoka kwa nabii huyu mjumbe.  Na huduma nne za Neno ni namna ya

juu kabisa ya udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika Kanisa la Yesu Kristo.  Na Kanisa la Yesu Kristo linatakaswa kwa kuungama hadharani na kumcha Mungu.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

 19 Na kuhusu unyakuo, maadamu Mungu hajatufunulia jambo lo lote, hebu tuzingatie kwamba unyakuo huo utafanyika leo, leo na leo hadi Bwana Yesu Kristo atakapokuja.  Utabiri juu tarehe  ulitoka kwa William Miller, baba wa kiroho wa Mashahidi wa Yehova na Waadventista Wasabato, naye akapitisha roho hiyo kwa Nelson Barbour na Georges Storr.  Na ni Nelson Barbour ambaye alipeleka roho hii kwa Charles Russell na njia bora ya kuepuka utabiri huu ni kutosoma maandishi yao.  Siamini katika utabiri wowote uliofanywa kutoka kwa mahesabu ya tarehe  na sijali kuhusu wao..

20  S-J. N°7/ Ndugu Philippe, je, tarehe ya ono ni kweli ya Danieli 10?  Ndiyo!  Tunaona katika Danieli 10:4 siku ya 24 ya mwezi wa kwanza.  Inarudi katika Biblia, kwa mfano, katika Hagai 2:10.  Kisha Mungu anazungumza tena na Hagai siku ya 24, Hagai 2:20.  Tazameni pia Zekaria 1:7, nk.  Kuhusu mwezi, ni kulingana na kalenda ya kale ya Kiebrania.  Aprili ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiebrania na yawezekana Bwana Yesu Kristo alizaliwa Aprili.  Hata maumbile yote yanashuhudia kwamba mwezi wa Aprili katika kalenda yetu ya sasa unalingana na mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiebrania.  Februari ni jangwa, yaani kifo, Machi ni maziko, Aprili ni kuzaliwa, ufufuo, Aprili ni kuotoa maua kwa zabibu na kuzaliwa kwa wana-kondoo.  Na yawezekana Bwana Yesu Kristo alizaliwa Aprili kwa sababu Yeye ni Mwana-Kondoo wa Mungu.

21 Tunajua kwamba 1993 ulikuwa mwaka wa matukio makubwa, hasa mazuri, duniani hasa mfumo wa vyama vingi barani Afrika na katika Ivory Coast, kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na USSR.  Kulitukia mabadiliko makubwa katika bara la Asia, Afrika Kusini na Angola ; amani kati ya Israel na Palestina ilisitawi pia.  Mambo haya yote yalizunguka mwaka wa 1993. Upepo wa uhuru na amani ulivuma duniani pote.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

22 Tangu mwaka 1963  ilipofunguliwa mihuri mpaka huduma hii imepita miaka 40, kizazi kimoja.  Amina!  Miaka 40 baada ya kutoka Misri, wateule walikuwa ng'ambo ya pili ya Yordani!  Nami niliwaambia wabranhamisti: “mlitoka Misri pamoja na nabii, mlivuka bahari ya Shamu, hampaswi kubaki jangwani, lakini lazima mvuke Yordani pamoja na nabii mwingine”.  Mahali fulani katika Afrika katika nchi ndogo, Mwenyezi Mungu amesema.  Hatuko tena wakati wa jioni, Roho amesogea mbele.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

23  Ilikuwa mwaka wa 1993 yaliposainiwa Makubaliano ya Oslo kati ya Israeli na Palestina na Yitzahk Rabin na Yasser Arafat wakapeana mikono mbele ya jumuiya ya kimataifa mbele ya Bill Clinton.  Ilikuwa ni mwaka 1993. Na pia ni katika mwaka 1993 ambapo Fréderic De Klerc na Nelson Mandela walipopokea Tuzo ya Amani ya Nobel.  Na ilikuwa ishara kubwa kwa jumuiya ya kimataifa.



24  Tuombe  sasa!  Bwana Yesu Kristo, Muumba wa mbingu na dunia, nimeleta Habari Njema Uliyonipa na sasa Uithibitishe Mwenyewe ya uthibitisho kwamba Wewe utapata kustahili na kwamba wateule wapate njia ya Ufalme.  Mimi mwenyewe, Ee Baba!  Neema yako na iwe pamoja nami daima, kwa maana mimi si mmoja wa wenye hekima!  Moyo wangu ukinitia moyo katika njia ya upotevu, mkono wako wa kuume na unirudishe!  Bwana, mwanadamu hawezi kuthibitisha kile kitokacho Mbinguni ukiwa hai.  Utujalie hilo, kwa kuwa katika Jina Lako, Yesu Kristo, tunaomba.  Amina!

25 S-J. N°8/ Ndugu Philippe, Biblia inapozungumzia kuvaa  shela, je ni nywele au kilemba?  Ni kuhusu nywele.  Angalia 1 Wakorintho 11:1-16, ukiona, onyo hilohilo katika mstari wa 16 linapatikana pia katika 1 Wakorintho 14:34-38 kuhusu tabia za wanawake.  Haya ni mapepo yale yale yanayotaka kuleta yale ambayo Mungu hajayaanzisha.  Wanafanya kazi za baba yao.  Waache wafanye!  Tayari katika mstari wa 6, Biblia inasema kwamba ikiwa ni vibaya kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, basi na azihifadhi.

26  Katika mstari wa 10 hii inaitwa alama ya mamlaka ya mwanamume na tunaona kwamba kuna tamaa ya ndani kwa kila mwanamke kuwa na nywele ndefu.  Paulo anasema nini katika mstari wa 15?  “Mwanamke akiwa na nywele ndefu, ni utukufu kwake kwa sababu nywele hizo alipewa kama mbadala wa kifuniko.  ".  Na mwishoni mwa aya hii inaishia na nukta nasio alama ya kuuliza.  Louis segond aliweka alama ya kuuliza kwa ombi la kampuni ya wachungaji wa Geneva. 

27  Kwa hiyo shela ya mwanamke si kilemba au kitu kingine chochote, ni nywele ndefu za mwanamke.  Na Paulo anasema katika mstari wa 16, mtu yeyote akitaka kubishia na abishie.  Mnaona ?  Katika kutaniko la Korintho, watu waliohuishwa na mapepo walitaka kuingiza mafundisho ya uwongo ndani ya kanisa.  Mambo ambayo Paulo wala mitume hawakufundisha.  Hata Musa hakuifundisha.  Mnaona ?

28  Na katika Luka 7 wakati mwanamke huyo alipokuwa akilowesha miguu ya Bwana Yesu Kristo kwa machozi yake na kuifuta kwa nywele zake, Bwana Yesu Kristo anapaswa kusema, “Wewe mwanamke, nenda kavae kilemba kichwani!  ".  Lakini hakufanya hivyo kwa sababu nywele ndefu ni kifuniko cha mwanamke.  Na Mungu alipomuumba Hawa, je, aliweka kilemba juu ya kichwa chake?  

29  Na kumbuka msichana mweusi katika Wimbo uliobora!  Sulemani angeweza kusema mbele ya Mshulami huyu mzuri: Akisema, "Wewe ni mzuri, rafiki yangu, ... Ondoa macho yako kutoka kwangu, kwa maana yananishinda."  Nywele zako ni kama kundi la mbuzi kwenye miteremko ya Gileadi;  ".  [Ndl: Wimbo Ulio Bora 6:4-5].  Sulemani hamwambii aende kuvaa kilemba, lakini anathamini hilo.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  Nywele ndefu ni utukufu kwa mwanamke.


30  Sasa fikiria 1 Wakorintho 11, mwishoni mwa mstari wa 15 neno la Kiyunani "Peribolaion" lilitumiwa na neno hili linamaanisha kufunika kwanza na kisha pazia.  Kwa hiyo tunaweza kuelewa kwamba ni kuhusu nywele ndefu katika mstari wa 5, 6 na 7.

31 Sasa kama hukubaliani na hilo, unaweza kuvaa kilemba chako.  Lakini sababu yako iwe mahali pengine.  Wakati wa ibada, dada akivaa kilemba kichwani kwa ajili ya kujifurahisha, hakuna shida, lakini akiona ni wajibu kwa sababu yuko kanisani, au anataka kusali, basi ni makosa, na kuna pepo amesimama nyuma. Ya hicho!  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

32  S-J. N°9/ Ndugu Philippe, je, Agano Jipya linazungumzia zaka?  Hapana Ndugu!   maana imepotea.  Tunazungumza zaidi juu ya uhuru. 

 Kanisa halina haki ya kujua kama mtu hutoa zaka,  na ni katika mkutano gani hutoa zaka yake.  Ni kati yake na Mungu atakayemrudishia.  Pia, tusipitishe kapu la sadaka mbele za watu au kuwafanya wasimame kuja kuweka pesa mbele ya kila mtu.  Kikapu lazima kiwekwe kwenye mlango wa hekalu na washirika wataweka zaka na matoleo ndani yake kabla au baada ya ibada kutegemea  kila mshirika jinsi anaongozwa.

33 Huwezi kutoa zaka kwa mtu anayeitwa nabii au mchungaji.  Kwa upande mmoja ni kwa ajili ya Walawi wote, wale wote wanaofanya kazi ya Mungu kwa ajili ya kuendeleza Neno na kwa upande mwingine, kwa ajili ya ndugu au dada yeyote mwenye mahitaji. 

34  Pia, ni lazima uwasaidie wazazi kama ikiwezekana, lipia Ada ya shule ya ndugu na dada.  Siku moja, hawa Ndugu watakapokuwa watumishi wa serikali, si kwa Kanisa kwamba watatoa zaka na sadaka?  Kwa nini wazazi peke yao ndio wanaopaswa kufanya kila kitu. na bado, siku moja, ni wewe utakuwa miongoni mwa wakupokea zaka na sadaka?  Makanisa yote yako kimya juu ya hili lakini wanajua kwamba si sawa.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

35  Kwa hiyo kanisa si ushirika, haliwezi kuwekeza wala kufanya biashara.  Waaminifu, wanaweza!  lakini si mchungaji, mke wake, au kanisa.  Na kujenga shule, hospitali, na kadhalika... hiyo ndiyo kazi ya serikali.  Kanisa lina utume wa kiroho tu: kuokoa nafsi.  Pesa lazima zinyamaze kanisani, ni hatari sana.

36  Pia kuna zile zinazoitwa sadaka ya ustawi ambayo ni matoleo ya lazima ambayo unayatoa moja kwa moja kwa kaka au dada ambaye unajua kuwa ni mhitaji.  Ama kwa vitu au kwa pesa taslimu.

37 Na jueni kwamba hakuna mtu mwenye haki ya kutumia zaka. Ni kana  kwamba tulikula mnyama mwenye ishara mbaya, au tumetumia kitu kilichokatazwa, au chenye laana, , Ikiwa mlikuwa hamjui, sasa mnajua.  Pia, lazima jamaa na marafiki wajuwe kwamba sio kwa pesa mtu ataenda kumuona mtumishi wa Mungu.

38 S-J. N°10/ Ndugu Philippe, je, teolojia inaweza kuwa na vitu  nzuri?  Jibu ni kwamba Mungu akisema kwamba jambo fulani ni baya msitafute vitu vizuri ndani yake.  Kwanza, biolojia inamaanisha nini?  [Ndl: Ndugu anajibu: "elimu ya uhai "].  Vizuri sana ! Biolojia inamaanisha "masomo ya uhai"!  Sasa jiolojia inamaanisha nini?  [Ndl: Ndugu anajibu: “kujifunza juu ya udongo”].  Vizuri sana jiolojia inamaanisha "kujifunza juu ya udongo"!  Sasa tunajua kwamba neno la Kigiriki "Teo" linamaanisha Mungu na "lojia" maana yake ni kujifunza.  Kwa hiyo teolojia inamaanisha “elimu ya Mungu”.  Kwa ufafanuzi, teolojia  inajumuisha maarifa  yanayopatikana kwa njia ya akili.  Na Neno la Mungu ni  kweli zote zilizofunuliwa.  Kwa hiyo, teolojia ni mpango, madai ya kishetani kwa sababu tunajua kwamba ni Mungu Mwenyewe ambaye hujifunua au hulifunua Neno Lake kwa yeyote amtakaye.

39 Ndio maana hatuwezi kwenda kwenye makanisa haya ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti, ikiwemo misheni na huduma hizi na hatuwezi kutumia matoleo ya biblia kama Louis Segond, Thompson, Scofield na mengine kwa sababu ni kazi ya wanateolojia.  Ikiwa mchawi alitatafsiri Biblia, hata kama aliifanya vizuri, nitakaa mbali nayo kwa sababu siamini uchawi na roho ilio nyuma ya ile ni shetani.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”]. 

40 Tazameni alivyosema Origen, mwanafunzi wa mitume, na ambayo mwanahistoria  Daniel-Rops aliripoti.  Origen alisema: “…Teolojia ni sayansi ambayo msingi ni vitu vya imani lakini ambayo hutoa matokeo yake katika mpango wa kiakili na ambayo inapaswa kutenganishwa na kweli zilizofunuliwa”.  Kwa hiyo Neno la Mungu na teolojia si kitu kimoja. Kile Kinachotoka kwa Mungu kupitia nabii na kile kinachotoka katika shule ya uchungaji, au taasisi ya Biblia, si kitu kimoja.  [Kc.2v16-17]

41 S-J. N°11/ Ndugu Philippe, nje na wanawali  wenye busara na wanawali wapumbavu, je, kunaweza kuwa  kitu kingine chochote hapa kati yetu?  

Ndiyo, bila shaka!  Mtaona matunda yao.  Wakati tunatumika  kwa ajili ya ukamilifu, mawakala wa shetani wameketi hapa ili kuzuia na kuharibu kile tunachofanya.  Usikengeushwe.  Kama mnaamini kwamba Mungu aliniita na kuniagiza, zingatieni hilo.  Wanaketi hapa, lakini wao ni wana wa Ibilisi.  Na mioyo yao inawaambia hivyo.

 42  Mwana wa Mungu au binti wa Mungu hawezi kuabudu, huku kila mtu akikiri karibu naye, ana dhambi inayoficha moyoni mwake.  Anaomba pamoja nanyi, na ana dhambi anayoficha moyoni mwake.  Anaimba nanyi, na ana dhambi anayoficha moyoni mwake.  Mnaona ?  Mnakiri karibu naye, naye anaketi pale  na dhambi iliyofichwa moyoni mwake.  Hivyo ndivyo Yuda alivyofanya  alipokuwa akila pamoja na Bwana Yesu.  Ni wana na binti za shetani.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

43 Jueni kwamba kila mtu ameketi hapa akiwa na utume wa kinabii nje ya nia yake mwenyewe.  Sasa, angalia jambo hili: kama yule mwovu hana budi kuchukua jukumu hapa, Mungu atampa kuamini Ujumbe huu;  ukweli wa kuamini katika Ujumbe huu haimaanishi kuwa wewe ni mtoto wa Mungu.  Unaona?  Kutakuwa na miiba na michongoma hapa,  Kutakuwa na m kansa, maadui ndani  wenye kushiriki na kula karamu  pamoja nasi.  Lakini wataiishia kufichua walivyo.  Mtoto wa Mungu hawezi kumtesa mtoto wa Mungu au mtoto wa shetani.


44  Sasa jambo lingine: …haijalishi mtakachoona ndani mwangu, nataka kuitwa “ndugu”, hivyo tu.  Na mke wangu, mwiteni "dada".  Sio "mama", lakini mwiteni "dada".  Amina!

45  S-J. N°12/ Ndugu Philippe, je, kuchaguliwa tangu asili  ni ya kibiblia? 

 [Ndl: Ndugu Philippe alihubiri juu ya kuchaguliwa tangu asili.  Tazameni Kc.21].  

Ndiyo, Biblia nzima inazungumzia juu hili.  Warumi 8:29-30 na Matendo 13:48 inazungumzia hili.  Kuchaguliwa tangu asili ulikuwa ni Ujumbe wa John Calvin katika historia ya Kanisa.  Alikuwa ni Mjumbe mkuu aliyehubiri juu ya kuchaguliwa tangu asili.  Aliita hii “kuchaguliwa kati ya sehemu tangu asili ” yaani kuchaguliwa kwa wokovu au kuchaguliwa kwa upotevu.  Kuna watu ambao wamechaguliwa kwa uzima wa milele, na watu ambao wamechaguliwa kupotea.  Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu, tayari umechaguliwa kwa uzima wa milele.hii ipo katika damu yako, katika mbegu yako.  [Kc.21v7]

46  Israeli ilipitisha miaka 430 huko Misri bila kuwa wa misri kwa sababu hapo mwanzo Wayahudi hawa hawakuwa Wamisri.  Lakini uzima wa milele Mungu alipokuwa akishughulika na Israeli, watu kama Ruthu na Rahabu kati ya mataifa... waliupokea kwa neema.  Mkiangalia, katika Ufunuo 7 makabila ya Dani na Efraimu yalifutwa kwa sababu ya kuabudu sanamu.  1 Wafalme 12:25-30, Hosea 4:17.  Nafasi yao ilichukuliwa na Manase na Lawi.  Lakini Mungu alijua kabla ya misingi ya ulimwengu ya kwamba ingekuwa hivyo, kwa nini?  kwa sababu ya kuchaguliwa tangu asili .

47  S-J. N°13/ Ndugu Philippe, Ujumbe wa jioni unachukua nafasi gani katika ujumbe wa usiku wa manane?  Ni Jumbe mbili tofauti kwa nyakati tofauti lakini za Roho moja na za nyakati moja.  Ningesema upeo mwingine wa Ujumbe wa kwanza.  Wakati John Calvin alipoanza kuhubiri matengenezo, Ujumbe wa Martin Luther ulikuwa umepita na wakati.  Japo ilikuwa ni wakati moja, Roho moja, na Luther alibaki kuwa baba wa matengenezo kama William Branham leo.

48  Hamwezi tena kurudi wakati wa jioni kwa sababu mana iliyochacha haipaswi kuliwa, haipaswi ichanganywe na ya leo.  Kulingana na Esta 2:15, chukueni tu kile kilichompendeza Mungu kuwapa kwa wakati wako.  Ikiwa  tunasoma maandishi ya John Wesley leo, utakua mkanganyiko kamili.  Kwa mfano tendo tu la kuona Wapentekoste, Wamethodisti, Wabaptisti ... wanazungumzia ujio wa pili wa Yesu Kristo, William Branham anawaona kama wanawali kulingana na Mathayo 25. Hili lilikubalika katika wakati wa jioni lakini sio usiku wa manane kwa sababu tuna ufunuo ulio wa juu zaidi na makanisa ambayo Biblia inayaita makahaba hayawezi kuwa wanawali.  Mnaona ?

49 S-J. N°14/ Ndugu Philippe, uamsho wa Bibi-arusi unakusudia nini?  Amina!  Nimejazwa.  Vizuri sana !  Mnaona ?  Zawadi tunayompa msichana mdogo ni midoli kwa sababu anapaswa kuwa mama. Lakini  wavulana wadogo, tunawapa bunduki kwa sababu wanapaswa kuwa askari. Kwa hivyo natazama ndugu wote wanaokuja hapa kama wahubiri wa siku zijazo. 

50  Baada ya mwaka mmoja tu, ndugu watapita hapa mimbarini na nje.  Na kila ndugu atafanya kazi hii ya kijeshi kwa sababu kuna vita kubwa ya kiroho ambayo tutakabiliana nayo.  Hivi ndivyo Bwana Yesu Kristo alivyofanya na hivi ndivyo tai na simba hufanya na watoto wao, kwa nini?  Kwa sababu wanapaswa kuwinda.  Kueni na tabia ya wanaume, walivyo wanajeshi nje ndivyo tulivyo.  Hatujui hatima gani Mungu ametuwekea lakini tutaikubali.  Hii ndiyo injili niliyoleta!

51  Kila wakati ninapozungumzia uamsho, ninajazwa.  Siku moja mtakumbuka mambo haya wakati mtapitisha usiku wenye kupotea kwenye kichaka bila kula, bila kuoga, awamu nyingine ya ukamilifu.  Mungu ameilaza dhamiri ya makanisa haya mpaka wakati fulani kabla ya kuyaamsha dhidi yetu.  Huu ndio wakati ambao Bwana alisema, "Na walitayarisha taa zao."  Yote yanapitikana sasa.

52  Neno hili ni kwa ajili ya anguko la wamojawapo na kuinuliwa kwa wengine.  Gharika ile ile iliyomwokoa Nuhu na walio wake iliangamiza wasioamini.  Tuwe hodari, sisi ni uzao mwingine wa wahubiri na Neno la Mungu lapaswa kua kama fimbo ya chuma kinywani mwetu, kuhukumu.  Ni jeshi hili ndilo linaloonekana katika Ufunuo 19. Na Biblia inazungumzia hilo katika Ufunuo 12:16, dunia hii ni mwana wa kiume.  Amina!  Roho Mtakatifu ataliongoza Kanisa takatifu katika uamsho huu ambao Kelele ya usiku wa manane italeta.  Ufunuo 19:11-16 inapitikana mwishoni mwa wakati wa Laodikia. [Kc.3v29]

53 Makanisa mnayoyaona yatachochea mamlaka, mashirika, ... dhidi yetu kulingana na Ufunuo 12:15, lakini mwana wa kiume yaani wanawali wenye busara, atadhibiti mashambulizi haya!  Haleluya!  Tunaona nini juu ya kichwa cha mpanda-farasi huyu wa Ufunuo 19:11 ?  Vilemba kadhaa, si taji za wafalme bali vilemba vya malkia, wanawali  wa Mathayo 25. Huu ndio wakati ambao nilisimama juu ya piramidi ya nyakati saba  katika ono la Aprili 24, 1993 nilipokea Jiwe lake la kifuniko.

54  Ilisemwa kwangu, “Kama vile Mariamu alivyochukua mimba bila kumjua mwanamume, kama Musa alivyopokea kwa undani kile kilichotukia wakati wa uumbaji, wewe pia umepokea Maneno ya Uzima wa Milele tarehe 24 Aprili 1993 na imeamriwa na Mungu.  Kwa wakati wake utaelewa na kufundisha yale ambayo hukujifunza, ili kila aaminiye awe na uzima wa milele."  Unaona ?  Haijalishi kipi kitakugharimu, usiende mbali na hayo.

55 S-J.  N°15/ Ndugu Philippe, kutakuwa na wito maalum kati yetu? Wito binafsi, hapana!   Unachohitaji tu ni Neno na ubatizo wa Roho Mtakatifu.  Lengo lako na wasiwasi wako lazima uwe mahiri katika Biblia na Ujumbe huu, ili uweze kufunga kinywa cha mtu yeyote.  Kwa hiyo ni lazima uwe na angalau ujuzi wa jumla wa makanisa, matendo yao na mafundisho yao.  Wanajeshi husoma mbinu za kijeshi za kila nchi.  Biblia na Ujumbe wa nabii aliye hai lazima viwe karibu zaidi na wewe kuliko mkeo kama mkeo hayuko katika mstari na Roho wa Ujumbe.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].


56 Usijiingize kwenye mjadala wowote bali tafuta kutuliza, usijitie katika majaribu.  Ibilisi anajaribu kuwafukuza, kujaribu kuwarudisha nyuma.  Lakini kwenye uwanja wa misheni katika mkesha wa unyakuo, itakuwa ni kitu kingine.  Roho akikuambia upige kwa ukoma, upofu, kupooza, kifafa, … piga!  Kwa maana hiyo ndiyo miujiza pia katika uamsho.  

57 Kutakuwa na mahubiri ya hukumu kama kule Misri pamoja na Musa.  Hivi ndivyo mambo yatakavyokuwa haswa!  Natabiri ili usishangae.  Unaona ?  Nchi ya Ufunuo 12:16 ni mwana wa kiume.  Kwa hiyo sio aina za uamsho na miujiza ambayo tumezoea kuona, lakini itakuwa miujiza ya kipekee.  Na hii ndiyo miujiza ileile ambayo wale watiwa-mafuta wawili wa Ufunuo watafanya.

58 S-J. N°16/ Ndugu Philippe, wewe ni mjumbe wa 8 kama wengine wanavyosema? 

 Ikiwa kuna mjumbe wa nane, basi mnijulishe.  Biblia yangu haikutaja.  Mtu akiwaambia kwamba Kacou Philippe anasema yeye ni mjumbe wa 8, mumuulize hii imeandikwa wapi katika Biblia na ni wapi nilisema hili.  Kama anasema aliisikia mahali fulani, mtajua kuwa mpo mbele ya mwana wa shetani.  Sikuwahi kujifanya nisivyo.  Ni Ujumbe ninaohubiri ndio unaonishuhudia.  Ninachojua ni kwamba mimi ndiye sauti ya Mathayo 25:6.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

59 S-J. N°17/ Ndugu Philippe, je, kuna fumbo katika Mathayo 17:1-8 linalozungumzia kugeuka sura?  

Ndiyo, haya ni mambo ya Milenia.  Kutoka kwa mwili huu unaoharibika, tutapita kwenye mwili wa mbinguni baada ya ufufuo na kisha kwenye mwili wa utukufu katika Milenia.  Katika kifungu hiki kutoka Mathayo 17, tunaona Musa na Eliya wakitokea.  Musa ni torati lakini zaidi ya yote tunapaswa kuona wanawali waliolala ambao watafufuka, kwa upande mwingine Eliya anafananishwa na watakatifu walio hai ambao hawatapitia kifo.  Katika mstari wa 8, torati na manabii vimeshikamana ndani ya Yesu.  Na tunaona hapo mashahidi watatu wa mbinguni: Musa, Eliya na Bwana Yesu.  Na pia mashahidi watatu wa kidunia: Petro, Yakobo na Yohana ambao wanafananishwa na Wayahudi.  Umati ulio chini ya mlima ni mataifa.  Yote hayo ni mambo ya milenia.

60 S-J. N°18/ Ninaona kwamba hauongelei sana juu ya Yesu!  Je! hayo tu umepata kutokana na yale niliyohubiri?  Jueni basi kwamba sikuja kusema habari za Yesu bali nilikuja kusema kwa niaba yake, mimi ni msemaji wake.  Kila mtu anaweza kumzungumzia Rais wa Jamhuri lakini anayemtuma hamzungumzii bali anazungumza kwa niaba yake na ndivyo ilivyo kwa Bwana Yesu Kristo na mimi.  Mimi ndiye msemaji wake.

61 S-J. N°19/ Ndugu Philippe, “Narudi mkono wa kuume wa Baba” inamaanisha nini?  Ndiyo, usemi sahihi ni “Narudi” na si “naenda” kwa sababu Baba ni Yesu Kristo Mwenyewe.  Yesu Kristo ni Mungu Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi, Baba, Mwana, Roho Mtakatifu, Yehova, Malaika wa Yehova, Melkizedeki, Yehova, Nguzo ya Wingu na Nguzo ya Moto... Unaposoma Zaburi, badilisha kila kitu "Milele" pamoja na Yesu Kristo.  

62 Na anaposema, “Narudi kwa Baba,” maana yake anarudi kwenye nafasi yake ya kiroho, ile nuru iliyotangulia mbele ya wana wa Israeli, Kut 13:21-22.  Katika Matendo 9, nuru hii ilimwambia Paulo, "Mimi ni Yesu."  Na Anaposema, “Narudi Mkono wa Kuume wa Mungu,” Mkono wa Kuume ni uweza na Nguvu;  na Nguvu za Mungu ni Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe.  

63 Yesu Kristo alidhihirishwa katika mwili...na kwa kuwa yuko kila mahali, mjuzi wa yote, na muweza wa yote, Anaweza hata kwa sifa moja kujidhihirisha katika sehemu arobaini tofauti, kwa wakati uleule, tofauti, kwa namna mbalimbali.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

64  S-J. N°20/ Ndugu Philippe, mwaminifu anayeteswa au ambaye amekataliwa na familia yake kwa sababu ya Ujumbe anapaswa kuwa na tabia gani?  Haijalishi umri wako, hali yako ya kijamii;  hali ya hewa au hali yoyote;  chochote kinachokugharimu, usirudi nyuma, usikatae Ujumbe.  Ikiwa kuna jambo moja la kipaumbele, si maisha yako au maisha yako ya baadaye bali ni Neno.  Kila kitu kitapita lakini Neno ni la milele.  Na siku moja tutatoa hesabu kwa Mungu.  Ikiwa hii inapaswa kuwa msalaba kwako, ubebe!  

 65 Unapokutana na ukweli, usifanye mahesabu, toka kwenye makanisa haya machafu!  Unaweza kupoteza utu wako, kufa na kuzikwa kama mbwa, lakini hii pia ni njia nyembamba ambayo mitume walichagua na matokeo yake ni utukufu wa milele.  Usiguse matapishi.  Na kwa yale yanayoishughulisha nafsi yako, usikubali kushindwa na majaribu au upinzani wa mtu yeyote hata kama unamtegemea.  Ikiwa kweli umegundua ukweli na ukakubali, huna udhuru mbele za Mungu.  [Kc.6v18] [Kc.15v18] [Kc.16v22] [Kc.16v31]

66  Na nisingeweka upinzani kutoka kwa wazazi kama mateso, ni majaribu tu ambayo hayawezi kushinda imani yetu.  Na ikiwa ndugu atakataliwa na wazazi wake kwa sababu ya Ujumbe huu, ninawaomba wanafunzi wangu wote wamtunze ndugu huyu mpaka ndugu huyu awe na hali ya kijamii duniani.  Ndugu huyu asiende tena kwa wazazi wake kwa hitaji lolote lile.  Sio lazima hata kuwatembelea.  Na ikiwa siku moja wazazi wake watatubu, ni mbele ya Kanisa kwamba wazazi wake wanapaswa kujieleza wenyewe.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”]. 

67 Katika Biblia, manabii, mitume na watakatifu daima wamepinga mpaka kufa.  Ikiwa Kanisa halipaswi kujinyenyekeza kwa Shetani, kwa nini Mkristo ananyenyekea chini ya wajibu mbaya wa familia yake?  Njia pekee ya kumkataza mtu kwenda kanisani ni kumwonyesha kwa Biblia kwamba kanisa hili ni la shetani. [Kc.50v13]

68  Katika historia ya kanisa, maelfu ya vijana wamekufa mara kwa mara katika mateso ya kutisha na ya kikatili. Wakakatwa miguu, mikono, ndimi zao, wakawachoma moto wakiwa uchi, wasichana na wavulana waliofungwa kwenye miti, wakawamiminia risasi iliyoyeyushwa masikioni, puani, midomoni mwao mpaka kifo kikafuata.  Unaona ?  Matendo yako siku moja yatakumbukwa mbele za Mungu, ndio maana lazima umpe utukufu.  Mungu anatarajia mengi zaidi kutoka kwetu ambao tumefika mwisho wa nyakati.

69  S-J. N°21/ Ndugu Philippe, nimekuja kutoka wakati wa jioni na nina wasiwasi;  William Branham alisema katika brosha ya Unyakuo kwamba Kelele ya usiku wa manane ni Ujumbe wake.  Pia alisema kwamba Roho wa Eliya atakuja duniani mara tano.  Unazungumziaje kuhusu hilo?  

70 Vema!  Sehemu ya kwanza ni: “William Branham anasema katika brosha ya Unyakuo kwamba Kelele ya Usiku wa manane ni Ujumbe wake”.  Kelele ya usiku wa manane inasema nini?  “Ujumbe huu unasema kwamba hatuko tena wakati wa jioni bali usiku wa manane  Hata hivyo ni wakati ule ule na Roho yule yule wa Eliya lakini ni Ujumbe “Mpya” ambao ni kiwango cha juu zaidi ya  wakati wa jioni”.  

71 Na malaika akamwambia William Branham katika Mto Ohio alipokuwa karibu kumbatiza mtu wa kumi na saba: “…Umetumwa na Ujumbe MMOJA ambao utanitayarisha kwa ajili ya kuja kwangu mara ya pili”.  Unaona ?  Sio Ujumbe bali Ujumbe MMOJA kwa sababu ni sehemu tu ya Ujumbe wote.  Lakini katika haya yote, kama wewe si mwabudu wa William Branham, unapaswa kujua kwamba "wakati wa jioni" ni tofauti na "usiku wa manane" na Biblia inasema katika Mathayo 25:6 kwamba Kelele ni usiku wa manane.  Kwa sababu tu William Branham anasema Ujumbe wake ni Kelele ya usiku wa manane haimaanishi kwamba lazima uchukuliwe kihalisi.

72 Wakati Isaya aliposema, “Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;  na Jina lake litaitwa: Mshauri wa Ajabu, *Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Enzi, Mfalme wa Amani,’ je, haikuwa lazima kungoja miaka mia nane ili kuona utimizo huo?  Unaona ?  Wabranhamisti hawaelewi na hawakubaliani juu ya kijitabu hiki cha William Branham, hii ndiyo sababu Ewald Frank bado hajachapisha.  Wabranhamisti hushika maneno yanayoweza kuwaharibu na kukataa yale yanayoweza kuwaokoa.  

73 William Branham alisema hawezi kujibu mbele za Mungu kwa kizazi asichokijua, lakini atajibu kwa ajili ya wale wa wakati wake, wale alioishi nao.  Na imeandikwa vizuri sana katika vijitabu vya William Branham lakini mnaikataa.

74 Vema!  Sehemu ya pili ya swali ni, "Pia alisema kwamba Roho wa Eliya atakuja duniani mara tano."  Mungu akubariki kaka kwa imani yako ilishinda haya yote kukuleta hapa kabla hujayaelewa.  Ndugu, labda Roho wa Eliya atakuja mara tano duniani kama William Branham alivyosema lakini si wewe wala William Branham wala mimi tunajua ni watu wangapi Roho huyu atawainua atakapokuja duniani.

75  Mimi ni wa wale wanaoamini kwamba William Branham amekufa lakini Roho ya Eliya, Nguzo ya Moto na Nguzo ya Wingu, ingali duniani.  [Ndl: Ndugu anasema, “Amina!  ”].  Na mpaka Bwana atakapokuja kwa ajili ya unyakuo, itakuwa daima ni Roho ya Eliya kwa sababu Roho ya Eliya ni Roho ya unyakuo.

76  Na wakati Ufunuo 22:17 inaposema ya kwamba “Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo, Bwana Yesu,” ni Roho wa Eliya.  [Ndl: Ndugu anasema, "Amina!"].  Biblia ilitangaza tu wajumbe saba kwa ajili ya Kanisa la mataifa lakini hao ni Roho saba za Mungu na hatuwezi kuhesabu ni watu wangapi kila Roho, kila Nyota itatuma duniani.  

77  Ndugu, kama ulivyoamini kabla ya kujaribu kuelewa, nilitaka pia kukujibu kama ndugu.  Bwana Yesu Kristo angeweza kusema, "Huyu pia ni mwana wa Ibrahimu."  Unaona Malaki 4 inazungumza juu ya kuja kwa Eliya lakini katika utimilifu sio Eliya wa Tishbi au mtu mmoja au hata wakati huo huo.

78  Na sasa sitaki kupingana na William Branham, bali ninyi Wabranhamisti, mnasema ya kwamba Roho ya Eliya inakuja mara tano na mnasema: “Mara ya kwanza ni Eliya Mtishbi, mara ya pili ni Elisha, mara ya tatu ni Yohana Mbatizaji, mara ya nne ni William Branham, na mara ya tano itakuwa ni Eliya pamoja na Musa katika Ufunuo 11,” hizo ni mara tano.  

79 Lakini nataka kukuuliza jambo fulani: Henoko aliyekuja kabla ya Nuhu, Henoko pale ambaye alinyakuliwa kabla ya gharika, je, huyo naye ni Roho wa Eliya?  Ndiyo au hapana?  Naacha hilo kwa tafakari yako.  Na sasa usiku wa manane, nikisema Roho wa Eliya atakuja mara sita au saba, hiyo ni nini kwako?  Mungu ndiye mfasiri wa neno lake mwenyewe na leo umemkataa nabii mjumbe wake aliye hai, kinywa chake juu ya nchi, nyamaza tu![Mh: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

80 S-J. N°22/ Ndugu Philippe, sielewi Ufunuo 21:9-10.  Yohana aliona nini kwenye Kisiwa cha Patmo? 

 Ufunuo 21:9...Hebu tusome : “Na mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vikombe saba vilivyojaa  mapigo saba ya mwisho, akaja na akasema nami, akisema : Njoo , nami nitakuonyesha Bibi-arusi, Mke wa Mwanakondoo.  Na akanichukua katika Roho mpaka kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, wenye utukufu wa Mungu.  Mnaona ?  

81 Sasa jueni kwamba  malaika alimwambia Yohana aje kuwaona kikundi cha wanawali wenye hekima wakishuka kutoka Mbinguni kwa Utawala wa Miaka Elfu.  Hawa ni watu ambao malaika alikuwa akimuonyesha Yohana.  Lakini Yohana aliona kwa mbali sana, Yohana alituona tukiwa mbali sana juu ya mawingu kiasi kwamba hakuweza kutofautisha maumbo yetu ya kibinadamu.  Mnaona ?  Na hao maelfu ya watakatifu walichukua umbo la mji na ndivyo Yohana anavyoeleza.  Kwa hivyo sio suala la nyumba au jiji la kawaida.  

82 Mmeona picha ya Nguzo ya Wingu?  Inasemekana kuwa ni wingu la ajabu la maili kadhaa kwa urefu na maili kadhaa kwa upana juu ya Flagstaff, Arizona lakini nabii aliona malaika saba.  Nadhani… vipimo vya wingu hili… urefu wa kilomita 80 na upana wa kilomita 48.  Mnaona ?  Waliona nini Tucson, Arizona?  Kutimia kwa Luka 21:27.  Bwana arusi akishuka juu ya Mawingu kwa nguvu na utukufu mkuu. Mnaona ?  Kwa karibu, Jean angeona watu.  Na maumbile yenyewe yanatufundisha jambo hili: kuna ndege ambao, wakiruka kwa vikundi, huunda picha nzuri mbinguni.  Hivyo ndivyo tu Yohana alivyoona.

83  S-J.  N°23/ Ndugu Philippe, je, Shetani anaweza kumpa mtu wa Mungu aliyejazwa na Roho Mtakatifu ufunuo?  

Ndugu, kupokea Roho Mtakatifu hakutuweki juu ya Mungu!  Je, mlisoma Ayubu 1?  Subirini!  Chukueni Mathayo 4, nini kilitokea?  "Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kilele cha hekalu, akamwambia hiki na kile...".  Mnaona ?  “Ibilisi akamchukua tena mpaka juu mlima mrefu sana, akamwonyesha milki zote za ulimwengu na fahari yao, na akamwambia hiki na kile…”  Mnaona ?  Inamaanisha nini ?  Ni katika maono tu ndio shetani alionyesha mambo haya kwa Bwana Yesu.  Na kama amuelewi, jueni kwamba mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.  Ikiwa shetani alimnyanyua Bwana Yesu Kristo, akimpeleka haku na kule, akimuonyesha maono, basi mimi ni nani, mimi nabii Kacou Philippe niliyeokolewa kwa neema?

84  S-J. N° 24/ Ndugu Philippe, tuna televisheni ambayo, zaidi ya magazeti, ripoti na makala, inatumiwa kwa kungalia video za Ujumbe.  Je, ni sahihi ?  Haya... Ni sawa ikiwa ni mwanamume na mwanamke ndio watu pekee wa kuwasha au kuizima televisheni hiyo. [Kc.50v13]

85 S-J. N°30/ Ndugu Philippe, hutokea kwamba wasio Wakristo wanataka kutuoa.  Je, tunapaswa kufanya nini? Kwanza fahamu kwamba mpo katika dunia mbili tofauti.  Na kwamba mnyama wa kufugwa hatamchukua jike wake porini.  Lakini kwa wanaume, hakuna kitu kizuri na wapole zaidi kuliko wanyama wa porini.  Wawindaji wanajua hili vizuri.  

86 Lakini ona kwamba Mungu hapendezwi na wanyama hawa wa mwituni kwa ajili ya matoleo ya kuteketezwa.  Unaona ?  Ni dunia mbili tofauti sana.  Sisi, tunaona tu kwenye nuru lakini wanaona gizani kwa sababu ni wana wa giza.  Na sioni nikiwapa binti yangu kwenye ndoa.  Lakini, akina dada, ninachoweza kukuambia katika ushauri ni kwamba usiwadharau.  Hatujui Mungu anaweza kufanya nini.  

87 Waambie waje kwenye Ujumbe kama wanataka kukuoa na wachungaji wako watashughulikia hayo mengine.Ninabainisha kwamba Ndugu anaweza kuoa Dada kutoka nchi nyingine au kabila nyingine.  Hapo mwanzo hakukuwa na rangi au lugha tofauti.  Tulikuwa kitu kimoja katika Adamu.  [Ndl: Dada huyo anasema: “Asante Ndugu Philippe”].


Comments

Popular posts from this blog

KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI

KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI

Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6