KACOU 17: KUKIRI HADHARANI
(Ilihubiriwa jumapili , tarehe 10 August 2003 ,pale Locodjro, Abidjan-Ivory- Coast)
1 Vita kuu vya Ujumbe huu havikuhusisha tu kumfunua joka, udanganyifu bali pia kuvika taji kazi ya utakaso wa kimwili na wa kiroho. Na tunakuja kwenye kipengele cha kitume: kukiri hadharani. [Kc.1v16]
2 Na fundisho hili tukufu haliepukiki hata kwa dhambi ndogo, yaani bila hiari au kwa makosa. Kwa mfano mtu akikuomba pesa na kwamba ukampa bila swali na kwamba akaenda kucheza bahati nasibu, kununua sigara, kinywaji cha pombe... au ukinong'ona au kuimba wimbo wa kipagani... Una hatia.
3 Ukijihusisha hata kwa sekunde moja kuomba na mtu wa makanisa haya ya Kikatoliki, Kiprotestanti, kiinjili na kibranhamisti ikiwa ni pamoja na Uislamu na Uyahudi au misheni na huduma hizi, una hatia kama yule anayeenda kwa mganga au mchawi. Ikiwa uko mahali popote bila Biblia na japo hapo kuna toleo la Louis Segond au Scofield au Thompson au King James, utaliona hilo kama mtego wa Shetani.
4 Hamuwezi kutumia maneno ao misemo ya mitaani. Na si kwa kifo, au kwa karamu au Harusi, Bila sababu ... Hamutaingia katika makanisa haya, mikesha yao au vyumba vyao vya maombi. Mkitenda dhambi nyepesi kwa maneno na mtu unayemjua kuwa ni Mdhihaki au mkosoaji, ni dhambi Inayofanana na yule anayeingia katika nyumba ya kahaba. Hizi ni dhambi ambazo lazima tukabiliane nazo kwa sababu, katika hatua tuliyoifikia, mtu yeyote anayejitowa hata mara moja katika punyeto, uongo, uasherati, siasa, uzinzi, au asiyetoa zaka na sadaka, ... ni adui wa kutisha kwetu na lengo la matatizo yetu, yeye ni kama mwenye ukoma katika kambi ya Israeli.
5 Lakini jueni kwamba ikiwa mtu yeyote anatutesa kama Akani au anafuata Ujumbe huu isivyostahili, yuko chini ya laana ya 1 Wakorintho 11:27-30. Ikiwa umekaa hapo na dhambi na watu wanakiri kando kando yako na kwamba hilo halikuambii chochote, angalau ujue kwamba utajazwa mapepo na laana. Jueni kwamba mlikuja katika nyumba ya Mungu ili kutoka mumelaaniwa badala ya kubarikiwa.
6 Jihadharini kwa maana dhambi sio asili ya pili kwa wana wa Mungu na Mungu alimwambia Musa, "Wale walionijaribu mara kumi hawataingia nchi ya ahadi." Kila wakati unapoketi hapo ukiwa na dhambi ambazo hazijaungamwa moyoni mwako, hiyo inaenda mbele za Mungu mbinguni. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. [Kc.18v1]
7 Vivyo hivyo, Hamuwezi Kukiri na tabasamu midomoni. Na lazima uvue koti lako kabla ya kukiri. Matubio ya hadharani hayapashwi kuwa mahubiri, ushuhuda, kulipisha kisasi au kujitetea bali ni kukiri kwa majuto. Hepukeni Pia maelezo isipokuwa kama Kusanyiko linayaitaji. Ikiwa umetenda dhambi dhidi ya mtu na bado anaizungumzia, hata kama ilikuwa kabla ya ubatizo, utakiri kwake na kisha mbele ya Kusanyiko. Mnaona?
8 Na ikiwa umetenda dhambi, usije kusimama hapo na kusema, “Lo! Ndugu...mnielewe!, Biblia inasema mwili ni dhaifu, nimefanya kitu fulani...». Sio wewe unayeweza kuambia ndugu zako hivyo! Inapaswa kuwa kitu kama: "Ndugu, nimetenda dhambi dhidi ya Mungu na dhidi yenu, nimedhoofika, nimewasaliti, sistahili kuitwa ndugu!" Kitu fulani kilinitokea ..."
9 Pia, Wale wote walio na jambo la kukiri na walifanye pamoja mmoja baada ya mwingine na kuwe na sala moja kwa ajili ya wote. Baada ya maungamo yote, yule anayeongoza Kukiri hadharani atakabidhi kusanyiko neno ili kusanyiko liingilie kati maungamo hayo. Lakini ndugu ambaye amekiri hastahili kuingilia maungamo ya mwingine. [Kc.71v28]
10 Lakini, kuna mambo ambayo hayawezi kuja kwa matubio. Kwa mfano kama hukuweza kuongea mbele ya mtu ambaye anajaribu kupinga Ujumbe, suluhu sio kuja kwenye matubio ya hadharani bali ni lazima umpigie simu mtu huyo ili umwambie kile ambacho hukuweza kumwambia kabla ya kuja kukiri. Kadhalika, yule ambaye hajalipa fungu la kumi atakiri ikiwa tu ameirudisha.
11 Vema ! Kukiri masikioni, yaani Kukiri dhambi mbele ya kuhani au mbele ya mchungaji, ni taasisi ya kibinadamu. Mitume tangu wakati wa Bwana Yesu Kristo walianzisha kukiri hadharani kulingana na uwezo ambao Bwana Yesu Kristo mwenyewe alikuwa ametoa katika Yohana 20:23.
12 Kukiri hadharani kulikomeshwa kuelekea mwisho wa karne ya 3 na nafasi yake ikachukuliwa na kukiri kwa sikio ambako kulianzishwa na Mtakatifu Benedikto, mwanzilishi wa utaratibu wa Wabenediktini lakini si kwa ondoleo la dhambi. Katika mwaka wa 1215, Kukiri masikioni kuliwekwa kwenye Baraza la Laterani na kufanywa kuwa lazima kisha, miaka miwili baadaye, kwenye Baraza la Trento, likawa fundisho la sharti kabisa. Ilikuwa katika mwaka wa 758 ambapo kuungama kwa sikio kulianzishwa katika nchi za Magharibi kwa utaratibu wa kidini wa Mashariki ili kuchukua mahali pa kuungama hadharani.
13 Na baada ya kukiri masikioni, kuhani alisema: "Ninakusamehe kwa kadiri niwezavyo na unavyohitaji." Badala ya kusema, “Mungu akusamehe dhambi zako na zangu! »
14 Na kwa kushirikiana na makuhani, wafalme na maliki walichukua fursa ya kukiri masikioni ili kutenda uhalifu. Mfalme Louis wa 11 alienda kuungama mara tu alipofanya uhalifu mkubwa na akawa, tangu wakati huo, mwenye moyo wakutulia na dhamiri huru. Alikiri mara nyingi, lakini kama ingekuwa kukiri hadharani, asingelifanya huvyo. Na wakati huo huo, mazoezi haya yalilinda kiti chao cha enzi. Huko Normandy, kijana mmoja alikiri mbele ya kuhani akisema kwamba alitaka kumuua Mfalme Francis wa Kwanza. Kuhani akamjulisha mfalme na yaliyofuata mnayajua. Lakini kama ilikuwa ni katika matubio ya hadharani, mfalme hangeweza kufanya lolote kwa kijana huyu. Mnaona ?
15 Kukiri dhambi mbele ya mtu, awe kuhani au mchungaji, si sahihi. Hilo linatoka kwa shetani. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. [Kc.18v10]
16 Chunguza historia na utaona kwamba katika Israeli, kwenye mfungo wa Yom Kippur, yaani msamaha mkubwa, kukiri kulikuwa hadharani. Siku hiyo, Wayahudi wote walikusanyika pamoja na kukiri dhambi zao hadharani kwa robo ya siku! Si robo saa bali robo ya siku, wamoja baada ya wengine... Someni Nehemia 9:1-3 mtaona hilo! Mnaona?
17 Kumwambia kuhani au mchungaji dhambi zako hakuitwa kukiri bali kuficha siri. Ulimweleza kuhani au mchungaji ili kutuliza dhamiri zako lakini usizungumzie kukiri. Kukiri masikioni au kibinafsi ni urithi wa Kikatoliki.
18 Hivi ndivyo kamusi ya Littré, Buku la 2, ukurasa wa 633 inavyosema: "Kukiri masikioni au kibinafsi: ni maungamo yanayofanyika sikioni mwa kuhani, kinyume na matubio ya hadharani ambayo yalikuwa yakitumiwa katika Kanisa la kwanza". Sasa, haya ndiyo yale ambayo kamusi ya karne ya ishirini, juzuu ya 2, ukurasa wa 404, inavyosema: "Ukiri wa kibinafsi au wa sikio: ni maungamo yanayofanyika kwenye sikio la kuhani, kinyume na matubio ya hadharani, ambayo yalikuwa yakitendeja katika Kanisa la kwanza. ". Mnaona ?
19 Tangu mitume hadi karne ya nne, ilikuwa ni kukiri hadharani. Kisha kanisa la Kikatoliki la Roma lilikomesha hilo na kuanzisha ukiri wa sikio. Mungu hawezi kukusikiliza isipokuwa kukiri kwako kuwe hadharani kwa sababu ni amri. Usichanganye kuficha siri na kukiri.
20 Katika Injili, katika Yohana 8, mwanamke mzinzi alipaswa kupigwa mawe lakini aliweza kufikia njia panda ya sheria na ya neema na hapo, neema ikashinda. Mnaona? Watu wote walitaka kumpiga kwa mawe kulingana na yale yaliyotukia chini ya sheria tangu Musa. Ni Musa ndiye aliyeamuru hayo kwa sababu dhambi zote ni dhidi ya watu. Kwa nini Wayahudi walitaka kumpiga kwa mawe mwanamke huyu ikiwa dhambi yake haikuwa dhidi yao? Mnaona?
21 Watu wote walimpiga mawe Akani katika Yoshua 7. Dhambi ya Akani iliwaletea madhara kwa sababu ilikuwa dhambi yao pia. Dhambi ya Akani ilihesabiwa kwao. Na ni vivyo hivyo leo. Mara tu unapoamini Ujumbe na ya kwamba umepokea ubatizo, wewe ni viungo vya mwili wa Kristo. Sisi sote tunajenga mwili wa Kristo, na dhambi ya kiungo kimoja ni dhambi ya mwili mzima. Na kwa hiyo kama mshirika anaficha dhambi zake na anakuja kuketi hapa, yeye ni adui kama Akani. Mnaona ?
22 Musa aliwapa Wayahudi uwezo wa kupiga mawe, lakini Bwana Yesu Kristo alitupa sisi uwezo wa kusamehe. Lakini tunaweza kusamehe tu ikiwa mnakiri mbele ya kusanyiko, mbele ya kila mtu. Ikiwa mnaogopa au kulionea haya kusanyiko, basi msitende dhambi. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
23 Tunaamini kwamba baada ya ubatizo, tunajenga mwili mmoja na kwamba dhambi ya kiungo kimoja ni dhambi ya mwili mzima. Na Mathayo 18:18 inasema, “Amina, nawaambia, lo lote mtakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lo lote mtakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Na katika Yohana 20:23, Bwana Yesu Kristo aliposema, “Kwa yeyote mtakayemsamehe dhambi, atasamehewa; na yeyote mtakayezuwia, atazuwiliwa,” Alikuwa akizungumza na wanadamu. Na wanadamu hawa ni sisi, Kanisa lililo hai. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
24 Katika Mathayo 16:19, Bwana Yesu Kristo alimpa Petro uwezo huo wa kusamehe. Lakini mara tu Kanisa lilipoanzishwa, uwezo huo ulihama na kwenda Kanisani. Hivyo Mathayo 16:19 inazungumza juu ya yule aliye na funguo za Ufalme duniani. Yeye aliye na funguo za Ufalme; mtu wa pekee ambaye maombi yake hupokelewa mbele za Mungu, yenye nguvu zaidi kuliko maombi ya dunia yote yakiwekwa pamoja.
25 Wakati wa taabu, katika 2 Wafalme 19, Mfalme Hezekia alimtuma Eliakimu kuhani mkuu na Shebna mwandishi na wazee wa makuhani kwa Isaya, nabii, ili kuinua maombi kwa ajili ya Israeli. Na walipaswa kusema: "Ee mfalme, tunakujulisha kwamba makuhani wote wa Israeli wameamua mfungo Yehoshafati kwa ajili ya nchi nzima na mfungo Esta na kwa kuzingatia makubaliano ya makanisa yote na wasimamizi wao hadi kwa manabii mia nane waliona mafanikio mapema’’.
26 Lakini mfalme alisema: Mimi napendelea Isaya. Nendeni kwa Isaya, nabii aliye peke yake dhidi ya watu wote wa Mungu! [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. Ninampendelea Isaya, ambaye kila mtu anapigana naye. Katika historia, nilielewa kwamba yule ambaye kila mtu anapigana naye, ni yule aliye na Maneno ya Uzima wa Milele. Amina! Wafalme wema wa Israeli wamefanya hivyo sikuzote.
27 Sasa turudi kwenye somo letu! Kukiri hadharani ni jinamizi kwa watenda dhambi katika makusanyiko. Ndio maana hawaitaki! Wana huzuni tunapozungumzia kutubu hadharani. Na mshirika wa Kanisa la kusanyiko la miungu aliniambia: "Ujumbe ni wa kweli na ninataka kuja lakini mkiondoa kukiri hadharani, mtawafanya waongofu wengi zaidi!"
28 Wengine husema, "Nikikiri hadharani, wanafunzi watazungumza juu ya matubio yangu nje!" Lakini ikiwa ndivyo, basi Msitende dhambi! Mnaona? Kinachoitwa matubio yanayoelekezwa moja kwa moja kwa Mungu ni ya shetani. Mnaona? Kila ungamo lazima liwe hadharani mbele ya kusanyiko. Ni amri ya Mungu leo. Huu ndio Ujumbe na ufunuo wa Yesu Kristo leo. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
29 Na kusema kuhusu kukiri hadharani, Ayubu asema nini? Hebu tusome hilo, Ayubu 31:33-34: “Ikiwa nalifunika kosa langu kama Adamu, nikiuficha uovu wangu kifuani mwangu; kwasababu niliogopa umati mkubwa, na dharau ya familia ilinitisha, na nikakaa kimya… Sasa nitasoma mstari wa 40, sikiliza kwa makini: "... Miiba na ikue badala ya ngano, magugu badala ya shayiri!" " Mnaona?
30 Ayubu anasema ikiwa, kwa sababu ya wingi wa watu, ikiwa kwa sababu ya kudharauliwa na watu, ameuficha uovu wake moyoni mwake, ikiwa anafanya jambo, basi lishindwe! Ikiwa ulikuwa na nguvu za kutenda dhambi na unaona aibu au unaogopa kukiri hadharani kama Ayubu, basi laana itakuwa juu yako na juu ya chochote utakachoweka mikono juu yake! [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
31 Na kuhusu kuingilia kati baada ya kukiri hadharani, sisi hatuko darasani na hatutaki wachambuzi mashuhuri wa matubio ya hadharani, watu ambao ni kama wamelazimika kutamka juu ya kila ungamo, hatuwataki. Uingiliaji kati wowote lazima uwe wa upole, kwa lengo la kumrudisha mtenda dhambi. Lakini ikiwa inaonekana kama shambulio, basi uingiliaji huu ni wa kishetani.
32 Na kuhusu kusamehe, kutaniko liko huru kusamehe au kutosamehe kwa sababu ya uwezo ambao Mungu Mwenyewe ametoa kwa Kanisa katika Mathayo 18:18 na Yohana 20:22. Hakuna anayepaswa kusema, “Sisi sote tu wenye dhambi; kwa hiyo ni lazma tusamehe." Chini ya sheria, ni kwa wanadamu kama sisi kwamba Mungu aliwapa uwezo wa kupiga mawe. Na hatuna haki ya kupotosha Neno likilinganishwa na sisi wenyewe!
33 Hadi miezi saba katika Ujumbe, yule anayekiri daima ataishia kupokea maombi ya kusanyiko. Lakini baada ya miezi saba katika Ujumbe, ikiwa ndugu ambaye hana fikira kwaajili yetu na kwaajili ya Ujumbe ataenda kufanya dhambi ya ngono, naomba kwamba mwezi mmoja hadi mitatu baada ya kukiri, aje na msichana kabla hatujaomba na ni sahihi.
34 Mnasema, “Itakuwaje kama hataki kuja? ". Atakuja! Kwa nini asije? Maadamu, huyu ndugu alikuwa na busara kumpeleka hotelini, atakuwa na busara kumleta hapa. Na ikiwa alikubali kwenda hotelini kuvuliwa nguo na kuchafuliwa, sio kwenye hekalu ambako atakataa kuja kutakaswa! Ana wajibu wa kumleta hapa ili atuambie kwamba hana mimba na yakwamba hakuna tatizo lolote kabla hatujamuombea ndugu huyo.
35 Lakini kama ni dada, hawezi kumleta huyo mpagani. Lakini atakuja baada ya muda wa adhabu na tutamuombea ikiwa katika wakati huo wa idhini alibaki msafi. Lakini angalau ndugu au dada atatoa sababu za kitendo chake kwasababu dhambi ya ngono haiwezi kushangaza. Kumhukumu kuwa ni mdhaifu, anaweza kupewa muda wa uchunguzi ambapo atabaki ndani ya kusanyiko na kuungama dhambi atakazofanya. Lakini kwa dhambi hii, ataiungama tena baada ya muda wa uchunguzi. [Kc.70v2] [Kc.112v3]
36 Lakini ikiwa ni kisa cha uzinzi na mwanamume aliyeoa au mwanamke aliyeolewa, ndugu au dada atamwendea kwanza mwenzi wa mtu huyo na kumwomba msamaha kabla ya kuja kukiri katika kusanyiko. Lakini ikiwa ndugu au dada ameolewa, kwanza atakiri kwa mwenzi wake na kisha ataambatana na shahidi pamoja na mwenzi wake kwa wanandoa wengine. Na ni baada ya hatua hizi ndipo atakuja kukiri katika kusanyiko. Nami nawaambia kwamba, hii ni amri kutoka kwa Bwana, ufunuo wa Yesu Kristo kwa kizazi hiki. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].
37 Kwa ajili ya matubio, mtu ambaye amekiri katika ibada ya kwanza baada ya dhambi yake hawezi kutupwa inje, atatumia wakati wake wa malipizi katika kusanyiko na ikiwa ni kuhusu ngono, wizi, ulaghai au kubadilishana picha au video zisizofaa. ni kusema juu ya ngono, hii lazima ichapishwe kama habari katika kundi la nchi.
38 Si kwa sababu sisi ni wenye nguvu kwamba tunafuata Ujumbe huu, lakini kwa msaada na neema ya Mungu, kama Yoshua na Kalebu tunasema kwamba kwa imani tunaweza! Msifuni tu! Hebu tuimbe na kulisifu jina lake! Amina!
39 Mungu ameketi katika utakatifu, na malaika hulalamika usiku na mchana, "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana." Ikiwa mnapenda utakatifu na utakaso, hamta tupiliambali kukiri hadharani. Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu, kwa sababu ya kukiri hadharani, utasema, “Ee Mungu! Ikiwa ningekutana na Ujumbe huu tangu utotoni mwangu, nisingeishi maisha mabaya, kuna dhambi ambazo singefanya kamwe’’. Kwa mtoto wa Mungu, kukiri hadharani ni zawadi kutoka kwa Mungu na wateule wanasema Amina kwa hilo.
Comments
Post a Comment