KACOU 16: WITO WA KUPELEKA UJUMBE


(Ilihubiriwa jumapili asubuhi  Machi 9, 2003 huko Locodjro, Abidjan – Ivory  Coast)


1 Jueni kwamba  chochote tutakachofanya hapa duniani,  kitapotea hapa na hakitakumbukwa mbele za Mungu. Ni matendo yanayoingia kwenye mstari wa Wokovu tu ndio yatakayobaki hadi milele kwa sababu  ndio vazi la harusi kulingana na Ufunuo 19:7-8. Hili ndilo tuliloitiwa.[Mh: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].

2 Haya! Upanuzi wa Injili ambayo ni Habari Njema ya usiku wa manane  si lazima tu bali ni wajibu. Mafuta katika hifadhi ni kumbukumbu ya haya yote.  Kornelio alipokea Roho kama  malipo ya kumcha Mungu na sadaka zake za maisha yote. Ikiwa kweli umezaliwa na Mungu, jambo fulani  litatokea  ndani mwako utakapojua Ukweli kama yule mwanamke Msamaria , kwa maana kuna Uhai, kichocheo ambacho kitatokea.

3 Na dhambi kubwa zaidi katika jangwa ni  kugundua maji na kuyaficha kwa watu.  Sambazeni Ujumbe huu ili wale waliokusudiwa  waweze kuupokea. Hatutafuti kugeuza kaa  kuwa samaki au punda -mwitu kuwa wana-kondoo wa Mungu bali tunao wajibu wa kuwaonya bila ubaguzi. Hata wakiita "hukumu",  fanyeni hivyo! Msisumbuliwe! [Kc.15v1] [Kc.72v18] [Kc.115v1]

4 Zamani, Wakristo wa kwanza waliwashutumu makuhani wachawi.  Na wale waliokuwa wana wa Mungu walitubu, wakachoma uchawi wao na kuikubali kweli lakini wana wa giza,  uzao wa nyoka, wakasema: “Mungu anasema  tusihukumu...” Basi, kutoka karne ya 16 kuendelea, Waprotestanti walilaani Kanisa Katoliki.  Kondoo kwa mujibu wa Yohana 10 waliitambua sauti ya Bwana wao na wakatoka kuwa na Uzima wa Milele lakini wana wa shetani, mapepo yale yale ya kale walisema “Mungu anasema tusihukumu...”.  Leo, Waprotestanti na Wakiinjili wanatumia msemo huu.  Mnaona ?   mapepo hawafi.

5 Hata waseme nini, msisumbuliwe! Wanabeba Biblia kama ganda, hawajui chochote kuihusu.  Iwe wanataka kusikia au la, wahubirie!  Wataenda kuzimu lakini ni lazima wasikie hilo.  Amina!  Katika Mathayo 7:1 inasema, “Msihukumu” lakini vipi kuhusu Yohana 7:24?

6 .Na wakiwaona wajeuri,  nini maana ya: “ uzao wa nyoka-nyoka! Nyoka kwenye nyasi! Makaburi yaliyopakwa chokaa! Je, mimi ndiye mhubiri wa kwanza duniani   kuwataja wapinzani wa ukweli?  Wao ndio  hawana haki ya kuhukumu bali kwetu sisi, Mungu ametupa uwezo wa kuwahukumu kulingana na 1 Wakorintho 2:15! Si  ya kuwahukumu wao tu bali ya kuwahukumu pia malaika walioanguka ambao ni roho zao takatifu. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! Kwa vile Tangu Nuhu, manabii, Yesu Kristo na mitume, ikiwa tunaweza kuhubiri bila kuhukumu basi sijui! Ni Mungu aliye na haki ya kuhukumu na Mungu amenipa uwezo na mamlaka kwa  maandishi na kwenu ninyi mnaoamini Ujumbe huu kuwahukumu![Mh: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].

7 Someni 2 Timotheo 2:17 .  Mnaona? Tunaishi katika wakati wa udanganyifu na kughushi na hekima ya  wanadamu imetoa kifaa kidogo cha kupima noti. Wengine wana njia za kutambua noti halisi  na noti bandia. Kwa mfano, kwa kuangalia au kugusa, hii inaitwa karama ya kiroho. Lakini kuhusu roho, karama na mafundisho, Mungu ametoa njia ambayo si Biblia bali ni nabii mjumbe.[Mh: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].

8 Tunaanza kuona watu na vitabu vya William Branham zaidi na zaidi kwa sababu haviwezi tena kutoa Uzima wa Milele. Huo ulikuwa ukweli kwa kitambo. Na wanafanya uongofu zaidi na zaidi. Kwa nini? tumbusi, vikula mizoga na kunguru wanakusanyika huko, wakipiga kelele na kuruka-ruka,  wakati Tai wako kwenye Kelele ya usiku wa manane. Biblia inasema katika Ufunuo 16:13-14 kwamba hizi ni roho za vyura. 

9 Macho ya chura yako juu ya kichwa chake. Wanaona kile ambacho Mungu  alifanya huko nyuma, kile ambacho Mungu atafanya wakati ujao lakini si kile anachofanya Mungu kwa sasa: “Musa  alisema! Musa alisema!  Masiya atakuja"  Masiya alikuwapo! “John Wesley alisema hivi, Martin Luteri alisema vile, William Branham alisema hivi…” Mnaona! Inasikitisha! [Kc.9v33] [Kc.40v16] [Kc.131v5]

10 Mungu ameturuhusu kuona Ukweli ili tuakisi mwangwi wake! Warumi 10:14 inasema  “Watamwaminije mtu ambaye hawakusikia habari zake? Jihadharini na usumbufu wa nyakati hizi ambao ni uadui dhidi ya Wokovu. Mwisho wa kila wakati, Roho asema, " atakayeshinda,  nitampa. …”. Ikiwa tumezishinda dhambi za mwili, mafundisho ya uwongo, tusisahau kero za karne hii. Hebu tusome Mathayo 13:22 na Mathayo 25:24-30, mnaona?

11 Ni kweli  mmepokea Maneno ya Uzima wa Milele lakini mtafanya nayo nini ili  siku moja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu , wana wa Ibilisi wasiseme: “Sikujua  kwamba kulikua ukweli kama huo duniani vinginevyo ningeukubali! Tunapaswa kujua kwamba Mungu anatarajia mengi kutoka kwetu.  Itoke mioyoni.nasio kuhamasishwa kila wakati!

12 Kama mtu  anasema kwamba ana Roho Mtakatifu na anakataa mahubiri haya ninayoleta,  muonyeni kwamba ni  roho ya uaguzi aliyo nayo, hata kama  anasema kwa lugha na anafufua wafu,  mwambieni hivyo. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”] Msiwaache bila kuwaambia hivyo. Ninasema : msiwaache bila kuwaambia  hivyo. [Nh: Kusanyiko linasema: “Amina!”]. [Kc.20v15]

13 Ninapowaona wabranhamisti na wengine wakisema: "Tuna Neno", inanikumbusha sikukuu ya tumbusi.  Kitu ambacho tai hawezi kula tena ndicho tumbusi, mwewe na. Vikula mizoga wanavyoita, "Tuna neno,  tunafahamu maandiko." Vivyo ndivyo  Wamoabu walifanya  na Balaamu. Na ndiyo maana niliwaambiya msiende huko.[Mh: Kusanyiko linasema, Amina! ”].

14 Haya! Sasa turudi kwenye somo letu; na ningependa kuchukua mfano wa Mtakatifu Martin wa Tours mjumbe wa wakati wa Pergamoni. Akiwa na umri wa miaka ishirini, askari kijana, baada ya kubatizwa, alipewa likizo kwa ombi lake na hakurudi tena kwenye wadhifa wake kwa sababu alikuwa ametoka tu kukutana  si na kanisa bali   na mtu, mhubiri Hilaire de Poitiers. Huwezi kamwe kukutana na Mungu kanisani bali na mtu. Na manabii ni  watu. Ukisikia Isaya, Yeremia, Amosi, Habakuki na  wote hao, hayo si majina ya makanisa bali  ni majina ya manabii.


15 Na Neno la Mungu humjia nabii kwa sababu Mungu yuko pamoja na manabii wake.  Na kukutana na Mungu, ilikuwa ni Hilaire ambaye Mtakatifu Martin wa Tours ilimbidi wakutane.  Na Hilaire alipokufa, jiji la Tours lilimwomba Martin awe askofu.  Na hapa ndio Rumi inajibu: "Hatuwezi kumfanya mtu wa sura ndogo kama hiyo, aliyevaa vibaya sana, ambaye hajachana nywele vizuri..."  Kuhitimisha kuwa mhusika asiye na sifa kama hiyo hastahili cheo cha juu kama hicho!  

16 Lakini kwa kweli, sikuzote Rumi iliona katika watu kama hao ambao haikuwafundisha,ni maadui hatari.  Lakini tayari ndani ya Mtakatifu Martin wa Tours moto ambao hakuna kinachoweza kuuzima  ulikuwa unawaka.  Hakuvunjika moyo.  Kwa miguu au kwa punda, kutoka kijiji hadi kijiji, kutoka mji hadi mji, makumi ya makusanyiko yalizaliwa, miujiza ilifuatana naye.  

17 Kanisa likamtambua mahali sawa na ile ya mitume.  Maaskofu walimwita lakini hakukutana nao hadi alipofariki mwaka wa 397. Zaidi ya makanisa 4000 ya parokia yalikuwa chini ya ulinzi wake, miji na vijiji 485 vina jina lake. Ni kuwekwa wakfu kwa namna hiyo ambayo lazima tufikie.  Amina!

18 Tunapendelea mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu kuliko Daktari wa teolojia.  Na niliwaonya dhidi ya teolojia ndogo, ndivyo Biblia inazungumza katika Mathayo 16:5-12.  Ni chachu ya Wafarisayo na Wasadukayo.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  Lakini tunashuhudia uamsho wa upesi kutokana na wasiwasi wa karne hii.  Lakini uamsho huu utafikia miisho ya dunia.  Dunia imejaa wajinga na mtu afadhali kuweka mali yake kununua gari au kujenga nyumba ambayo itaangamia duniani.

19 Na katika mahubiri, watu waligundua kwamba Hilaire alikuwa mzushi, hata ilimbidi kwenda uhamishoni kwa muda ili kuokoa maisha yake.  Na ni mtu kama huyo ambaye alikuwa bwana wa Mtakatifu Martin wa Tours.  Mnaona ?  Wakristo huweka ndoa, watoto, kazi mbele ya kazi ya Mungu.  Wanatafuta kujua watoto wao watakuwa nini duniani kabla ya kufikiria Ufalme wa Mbinguni na ikiwa kuingia Mbinguni lazima kuweka dhabihu juu yao kama mitume na watakatifu wa zamani, basi hawataki.  Wanataka Mbingu kama zawadi ya Krismasi.  Wanataka Ukristo kulingana na mfano wa kibinadamu!  Nje ya kile unachofanya kwa Neno la Mungu, kila kitu kingine ni ubatili wa kibinadamu na upumbavu.  Na mbali na yale ambayo nabii mjumbe hufunua katika kizazi, mengine yote ni ubatili na upumbavu wa mwanadamu.[Mh: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].  [Kc.6v18] [Kc.15v18] [Kc.16v31] [Kc.19v59]

20 Hata yule ambaye hana huduma, mwanamume au mwanamke, mara tu baada ya kuupokea ukweli huu ambao wengine hawana, lazima kila wakati, kwa hali yoyote na kwa nafasi ndogo, ijulikane kwa sababu ndani yake huchomwa Maneno ya Uzima wa Milele.  Hata unapotembea, unahisi kama unahubiri moyoni mwako, ukweli ndani yako umeishi kama mwanamke mjamzito, na kukufanya kuwa chanzo kisichoisha cha Wokovu kama Yesu alivyomwambia mwanamke Msamaria.(Mh : Kusanyiko linasema, "Amina! "  ”].

21  Kila Ujumbe ambao Mungu alituma duniani ulikuwa  ukweli maalum ambao lazima uende hadi miisho ya dunia: Luteri akiwa na kuhesabiwa haki, John Calvin na kuchaguliwa tangu asili, John Wesley pamoja na utakaso, William Branham pamoja na nuru ya   jioni, urejesho.


22 Na kama mkiona, Wayahudi wanapomuua nabii na wakati wa nabii huyo unapita, wanajenga mnara katika kumbukumbu yake na kumtambua.  Vivyo hivyo Luter alipokuja alipigwa vita lakini wakati wake ulipopita kila mtu alimtambua.  Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa John Calvin, John Wesley na sasa na William Branham.[Mh: Kusanyiko linasema, Amina!  ”].

23  Kuipokea kweli na kuifanya mateka ni upumbavu kwa wale wanawali wa Mathayo 25 na Mungu anawezaje kumjaza mtu yeyote kwa Roho wake isipokuwa aende kupeleka Habari Njema hii ya Ufalme?  Katika Matendo 4 mitume na wanafunzi waliomba Roho zaidi ili kuwaangazia wale waliokuwa gizani na wakapewa. 

24 Ni upumbavu kuushikilia ukweli huu mkuu na kuwaacha watu wafe.  Ndiyo maana wanawali hawa walikosa unyakuo na ilibidi wapitie mateso.  Hivi ndivyo Mathayo 25:14-30 inazungumza;  mfano wa talanta ni mwendelezo wa ule wa wanawali kumi.  Haihusu makanisa ya Kiprotestanti na ya kiinjili, umisheni na huduma, wala Wabranhamisti bali wale wanawali kumi na kile watakachokuwa wamefanya na ile kweli ya Mungu ambayo wameipokea.[Mh: Kusanyiko linasema: “Amina!  ”].

25  Kwa maana wakiwa wametenda uovu kwa kushikilia kweli mateka, wataokolewa lakini kupitia mateso. Kulingana na Ezekieli 33:1-9 , tuna wajibu wa kueneza kweli hiyo “ili kuwaonya waovu juu ya njia zao.”  Haya makanisa yote yanaelekea kuzimu na utasubiri kuambiwa ili uwaonye?  Biblia inasema: "Mwovu atakufa katika uovu wake lakini damu yake nitaitaka tena kutoka kwa askari" lakini ukimwonya na akabaki katika kanisa lake, Katoliki, Kiprotestanti, kiinjili au kibranhamisti "wala hageuki katika njia zake, atakufa katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa nafsi yako."  Mnaona ?

26 Nyumba zetu, mazingira yetu, wilaya hizi, mashambani, vijiji, miji na nchi na makanisa haya yanamngojea nani?  Kila mmoja wetu siku moja atatoa hesabu mbele za Mungu.  Ikiwa tuna mitume kama baba, na tuzae kazi za mitume.  Mfano wa talanta unategemea kile ambacho kila mmoja amefanya na kweli aliyopokea.  Mnaona ?  Ukienda kazini, zawadi zitafuata.  [Kc.15v14] [Kc.15v20]

27 Hebu fikiria lori na mtu nje akipiga kelele, "Nyie wakaaji wa lori hili, jueni kwamba gari hili halina bima, magurudumu yake yamechakaa, breki imekatika na dereva hana leseni ya udereva!  ".  Huu ni utume wetu.  Mnaona ?  Mwenye busara atajaribu kuhakikisha anachosema kwa ukali kabla lori halijasogea inchi moja huku wana wa shetani wakimjibu: "Wewe ni polisi?  Huna haki ya kusema hivyo kwa sababu wewe si polisi!  ".  Mnaona ? 

28  Nafsi hazina bei sawa...Nafsi za wana wa shetani hazina maadili.  Wanaweza kufia katika kanisa katoliki, la kiprotestanti, la kiinjili au la kibranhamisti.  Wanaweza kufa kwa ajili ya siasa, kwa ajili ya soka, wanaweza kufa bure, ni wana wa shetani.  Ni lazima waende kuzimu lakini lazima wasikie ujumbe huu.[Mh: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

29 Tunapoona Mathayo 13:22 , tunaelewa kwa urahisi sababu za tabia hiyo.  Roho anahimiza waziwazi kwamba yeye aliye na masikio ya kusikia, asikie.  Katika ono hilo, kulikuwa na kupatwa kwa jua na kisha mwanga ukaja.  Mnaona !  … 

30 Ujumbe unaposhuka, nuru yake lazima iangazie dunia yote na hivi ndivyo mabikira wenye busara walielewa na hii ndiyo sababu sehemu kubwa ya mafuta ilitolewa kwao.  Kwa nini kiasi kikubwa hivyo cha mafuta apewe mtu ambaye hajui thamani yake na wala hafanyi chochote nacho?  Kufanya nini ?  Iwe ni katika Agano la Kale au Jipya, ni kufanya kitu ambacho Mungu hutoa Roho au mafuta.

31 Wanawali wenye busara au wanawali wapumbavu, ni tangu mwanzo kutengana hufanyika.  Mnaona ?  Wanawali wapumbavu hawako nje tu bali wameketi hapa wakiwa na msururu wa wasiwasi wao vichwani.  Lakini mtoto wa Mungu anapofanya kazi, wasiwasi wake si kile ambacho ameweza kukusanya katika akaunti yake ya benki hadi sasa bali ni kile ambacho amemfanyia Mungu ili kuchangia katika upanuzi wa Neno.[Mh: Kusanyiko linasema. , “Amina!  ”].  [Kc.6v18] [Kc.15v18] [Kc.16v22] [Kc.19v59]

32 Wakati Mtakatifu Martin alipoomba likizo hii na hakurudi tena kwenye wadhifa wake kutumikia nchi yake.  Mara tu alipoanza kuhubiri mashambani, hakukuwa na ugonjwa au udhaifu ambao ulipinga sala yake.  Wafu walifufuka…mnaona?  Hakukubali zawadi yoyote, kama Bwana Yesu alivyopendekeza. 

33 Hatuwezi kukubali zawadi kutoka kwa mtu kwa sababu Mungu amefanya muujiza katika maisha yake kupitia sisi.  Na hatujioni tukitumia pesa kama tungekuwa na pesa kununua ardhi na kujenga mahekalu mazuri yenye viyoyozi kwa mazulia wakati watu wanakufa kutokana na Neno.  Mnaona ?  Juhudi zetu lazima ziende kwanza katika mwelekeo wa upanuzi wa Neno.  Hii ndiyo sehemu ya pili ya Neno iliyoshuka juu ya Mawingu.

34 Sehemu ya kwanza imekwisha na tunamaliza sehemu ya mwisho.  Maneno ya kwanza yalikuwa ni Maneno ya hukumu na ya pili yaliambia Kanisa kubadili maisha yake.  Nilikuwa nimesimama hivi na nikaona upande wa mashariki  maandishi ya Kifaransa yakishuka kwenye Mawingu.  Ni kwa wateule nao wataamini.  Walisema, “Hatujamwona Malaika na Mwana-Kondoo bali tunaamini KAMILI…” Mnaona?

35 Kunyakuliwa si kwa kunguru wanafiki, vyura na tumbusi;  wala kwa wale wanaoionea haya Injili.  Hata nyie dada shuhudieni!  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

36 Sasa turudi kwenye Ezekieli 33, jinsi baba zetu mitume walivyopiga tarumbeta, kwa hiyo kila mmoja wetu ameitwa kufanya.  Kuwa Mkristo ni kutambua thamani ya nafsi zinazoangamia wakati zina haki ya kusikia ukweli ili kuokolewa.  Kuwa Mkristo ni kuwa na uzito na huruma ya nafsi.  Mwenye masikio na asikie!  [Kc.15v17]


Sura zinazofanana: Kc15, Kc 72 na Kc 108


Comments

Popular posts from this blog

KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI

KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI

Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6