KACOU 15: ANACHOKITRAJIA MUNGU KUTOKA KWETU


(Ilihubiriwa Jumapili asubui, 01 june 2003, pale Locodjro, Abidjan- Ivory - Coast)


1 …Tunapogundua ukweli usiopingika ulioahidiwa katika wakati wetu, kilichosalia ni sisi kupeleka ukweli huo popote pale mtoto wa Mungu anaweza kupatikana, awe tajiri au maskini, mbali au karibu. mwenye haki hataturuhusu tuingie Mbinguni bila kutudai damu yao. Ikiwa mwanadamu ni mtakatifu kama sheria ya wanadamu inavyosema, nafsi ni takatifu zaidi. Wajibu mkubwa upo juu yetu. Amri ya Mathayo 28:19 si kwa magazeti au vitabu bali kwa watu, sisi! Kitabu hakiwezi kujibu swali!  Mnaona?  [Kc.16v1-3] [Kc.72v18] [Kc.115v1]

2 Mungu alipoona kwamba wanadamu wanaelekea moja kwa moja upotevu, Alivua mamlaka yake ya Kimungu na utukufu wake wote kwa ajili ya kujitoa kama dhabihu kwetu sisi, ili tupate uzima wa milele kama yeye. kitu kikubwa ambacho Mungu alimpa mwanadamu ni  uhai wake mwenyewe. japo, anaketi katikati ya malaika, na kama hangeshuka, Yeye angebaki kuwa Mungu kila wakati, lakini alifanya hivyo ili sisi pia tupate uzima wa milele. [Ndr: Kusanyiko linasema, « Amina! »]

3 Sasa ni nini wanadamu wanaita utukufu, na inayo mzuia kumtumikia Mungu? Sijui! Katika Mathayo 4: 8-9, Shetani alimtolea Yesu yote lakini yeye aliikataa! Ndio maana hatujihusishi katika siasa […]

4 Mtu anapodai kumtumikia Mungu, tafuta kujua kwanza ukweli wa wito wake, agizo lake na mamlaka yake kabla ya kutaka kujua anachosema au kufanya ni kweli. Wakati Mungu hakumtuma mtu duniani, Hawezi kutambua juhudi na hata vitu vizuri vya mtu huyo. Kuhubiri kweli haimaanishi chochote kwani shetani mwenyewe anajua Neno. [Ndr: Kusanyiko linasema, « Amina! »] [Kc.3v39-40] [Kc.6v34-35] [Kc.28v13-14] [Kc.115v21] [Kc.118v33-36]

5 Mapenzi kamili ya Mungu ilikuwa kwamba nabii aongoze Israeli badala ya mfalme. Lakini Israeli alidai mfalme, 1 Samweli 8: 4-7. Mungu hasemi kupitia mfalme bali kupitia nabii. Kabla ya kifo cha Samweli, ilibidi ampake mafuta nabii mahali pake. Na ikiwa ujio wa mfalme aliyeteuliwa na nabii mjumbe siyo mapenzi kamili ya Mungu haitakuwa rais aliyechaguliwa na watu ambaye atakuwa. [Ndr: Kusanyiko linasema, "Amina!"] 

6 Katika 2 Wafalme 22: 11-14, Mfalme Yosia alimtuma kuhani Hilkia na mwandishi Akhikam kuuliza Neno la Mungu kwa nabii. Katika 2 Mambo ya Nyakati 20:20, Mfalme Yehoshafati aliwaambia Israeli, « Mwaminini Bwana Mungu wenu nanyi mtathibitika; waminini manabii wake nanyi mtafanikiwa. »  [Kc.41v36]

7 Mkristo ni kama askari anayepaswa kufa  siku moja kwa ajili ya nchi yake, ikiwa ni lazima. Siku ambayo wito unapofika juu ya kupita kwenye mashambulio, kila kitu hapa duniani hakina maana, siyo pesa au nyumba yake tu ambayo iko hatarini, lakini kile alicho nacho cha thamani zaidi, maisha yake. Kwa hiyo, mnapaswa kuwa tayari kwa wito wa jemadari. Na sio kwa mwezi au mwaka lakini leo. Bibilia na ono vinathibitisha hiyo, ndiyo sababu katika ono la 1993 mnamuona Mwana Kondoo ambaye ni alama ya dhabihu.

8 Na kulingana na Matendo 16: 6-10, Roho Mtakatifu ataongoza uamsho huu kwenye uwanja wa misheni. Lazima kila kitu kiwe katika mpango wa mapenzi kamili wa Mungu, vinginevyo ni dhambi. Na nafikiri kwamba ikiwa aliniita, basi alinijua kabla ya misingi ya ulimwengu na alijua uwezo wangu. Alipompa Petro funguo za Ufalme, alimjua Petro ni nani! Ujumbe huu utafika je mwisho wa mipaka ya dunia, Anajua. Na ni wale walio na imani ya Yoshua na Kalebu ndio watakaoingia. [Ndr: Kusanyiko linasema, « Amina! »]

9 Kitabu cha mchungaji wa Kibaptisti kitanifanyia nini kama si kunigeuza Mbaptisti mzuri?  Wakati Papa Innocent III ilipiga marufuku usomaji wa Bibilia, lengo gani Shetani alitaka kufilia? Ni lengo lile lile alilofikia leo kwa njia nyingine, ili kuwatiisha watu kwa mapenzi yake. Huku akiwaachia Biblia mikononi mwao, anawapa aina nyingi Zaidi ya matafsiri ya bibilia. Aina moja ya Wabaptisti, aina nyingine ya Pentekosti, aina ya mashaidi wa Yehova, Adventista, Mnazareti, Anabaptisti ... akifikia lengo lile lile moja na kwa ukamilifu.


10 Mtoto wa Mungu anayejali Wokovu na Uzima wa Milele, atatafiti hata mambo madogo sana ili ajue Ukristu ni nini. Panya hawezi kufugwa, mwana wa shetani hata akisikia ukweli atabaki jinsi  alivyo. Mwana wa Mungu akisikia uongo, atauliza maswali mpaka atakapoangazwa! Amina!  Mnaona? Kilindi kinaita kilindi. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. [Kc.43v32]

11  Kati ya 1540 na 1770, Wakristo milioni tisa walichomwa moto wakiwa hai, wakazikwa wakiwa hai, wakakatwa vichwa, si na Roma ya kipagani bali na Kanisa Katoliki la Roma. Kwa nini? … Mnamo 1415, John Huss, mkuu wa Chuo Kikuu cha Prague, alichomwa moto kwenye mti. Kwa nini? … John Wyclif, profesa katika Oxford alichomwa moto akiwa hai kwenye mti! Kwa nini? … Uchunguzi ulioanzishwa mwaka wa 1229 na Kanisa Katoliki la Roma uliwaangamiza kabisa Waalbigensia. Kwa nini? … 

12 Mnamo Agosti 1572, katika usiku mmoja, Wakristo 70,000 waliuawa katika Paris na mikoani. Kwa nini? … KWASABABU WOTE WALIPINGA HAYO  MNAYOYAITA MAKANISA LEO! [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. Walipinga mababu wa viongozi wenu Wakatoliki, Waprotestanti, wa kiinjili na wabranhamisti. 

13 Hawa viumbe wenye harufu ya dhambi na hatia, malaika walioanguka kutoka Mbinguni na ambao hukumu yao haikomi kupiga kelele, viongozi hawa wa Kikatoliki, Waprotestanti, Wainjilisti na Wabranhamisti waliowapotosha wale ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya misingi ya ulimwengu. Wale wasiojua kwamba kazi ya Mungu ni kumtambua na kumsikiliza yule aliyemtuma kulingana na Yohana 6:28-29. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”].

14 Na watu wanafikia hatua ya kusema kwamba roho ambayo  inatenda katika makanisa ya Wabaptisti, mikusanyiko ya miungu, Pentekosti, na kadhalika ni Roho Mtakatifu! Ni makufuru! Ikiwa mnafikiri kwamba roho inayotumika na Kaini, Joel Osteen, TD Jakes, Doug Batchelor, Billy Graham, Edir Macedo, Valdemiro Santiago, Silas Malafaia, Paula White, Joyce Meyer na Chris Oyakhilome ni Roho Mtakatifu, basi ! mnasema nini kwa ajili ya roho inayotenda juu ya yule mchawi wa asili wa kiafrika? 

15 Ikiwa mnafikiri kwamba roho inayo kuwa juu ya David Owuor, Emmanuel Makandiwa, Uebert Angel, TB Joshua, David Oyedepo, Alberto Mottesi, Claudio Freidzon, na Dante Gebel ni Roho Mtakatifu, Mnasema nini kwa ajili ya maroho inayotenda ndani ya vyama vya kimataifa rose-croix, franc macon na wengine?

16 Ikiwa mnafikiri kwamba roho inayokuwa juu ya Tommy Osborn, Morris Cerullo, Benny Hinn, Manase Jordan, Jesse Jackson, John Hagee, Pat Robertson, Joaquim Gonçalves, Donald Parnell, Alejandro Bullón na Guillermo Maldonado ni Roho Mtakatifu, mnasema nini basi kwa ajili ya roho inayowachezesha Wahindu kule? [Kc.22v4] [Kc.32v27-28] [Kc.40v9] [Kc.108v16] [Kc.116v9] [Kc.118v13]

17 Sitaki watoto wa Mungu walale pamoja na wale ambao walizaliwa ili wasitubu. Unapoona kanisa la foursquare, kanisa la zamani toka 1922, ambalo hubatiza kwa namna moja hivi,na kanisa lingine ambalo linabatiza namna nyingine na wote wawili wako kwenye shirikisho moja la makanisa . ! Mtoto wa Mungu ataenda kufanya nini huko?

18 Kanisa, kwa jinsi lilivyohanza na Yohana Mbatizaji  na Mitume na maendeleo yake katika historia, haina uhusiano wowote na kile (unachokiita) mnachoita "kanisa" leo.  Ingekuwa rahisi sana kubandika mwili wa Kibaptisti kwenye kichwa hiki na kumdanganya mtoto wa Mungu .  Huwezi kubandika kichwa cha mwanamke kwenye mwili ambao si wake na  kumkubalisha mwanaye kuwa huyu ni mama  yake.  Ataangalia majina, urefu, rangi, umri na mengine yote.  Hivyo ndivyo watoto wa Mungu watakavyofanya siku zote.  Maelfu ya makanisa lakini Biblia inasema kwamba wateule hawatadanganywa!  Amina!

19 Na ni kwa ajili ya mambo yote hayo ndio Mungu anatuita kwenye uwanja wa misheni.! Kwa nini? Ili kuzuia udanganyifu na kufunua hila za shetani . [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. Wito wa mwisho na mkuu wa Mungu husikika kwa kila Mkristo. Ikiwa nyinyi mna Mitume kama baba zenu na mnadai kuwa mnafuata nyayo zao, basi pokeeni wito huu kama sauti katika mioyo yenu, haijalishi iwe ngumu kiasi gani.


Na kama sisi ni matajiri ni kwa ajili ya kuendeleza Neno. 

20 Mungu hatuiti tena kukaa ndani ya kuta nne bali katika uwanja wa misheni. Huu ndio wakati ambao ukweli lazima uende kutoka mji hadi mji, kutoka kijiji hadi kijiji, kutoka nchi hadi nchi! Habari njema za Ufalme kwa wakati wetu lazima zihubiriwe kwa wagonjwa, kwa maskini, kwa matajiri,  na kwa wakaaji wote wa dunia. Kwa nguvu, njia na uwezo ulio nao tenda kwa ajili ya kuendeleza Neno. Usifanye hesabu yoyote! Mungu wa Eliya aliyewaongoza baba zetu mitume na wanafunzi yeye Mwenyewe atakuongoza.[Mh: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. [Kc.16v28]

21 Mnamo 1415, John Huss, mkuu wa chuo kikuu aliacha kazi yake, akawa  mwanafunzi wa mhubiri mdogo ambaye alipokea maandishi kutoka kwake na kisha kujazwa na fundisho hilo, alienda kutoka mahali hadi mahali akihubiri kile ambacho watu waliita uzushi na ambacho kilikuwa ni  kweli. Kwamba hakuna mtu angeweza kumpinga mpaka akateketezwa akiwa hai.

22  Kutoka kwa mitume hadi kwa John Wesley, sijaona mtu wa Mungu akiweka huduma yake ndani ya kuta nne. "Nendeni popote..."  Iwe ni eneo la Kikatoliki, la Kiislamu, la kiinjilisti, ya huduma, hubirini kila mahali! Sio lazima kuomba kwa mtu yeyote ruhusa. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wahubiri wakuu katika miaka hii ya 1900. Mnaona ? [Kc.5v43] [Kc.6v17]

23 Watu wanafikiri wao ni wakristo  wakati si wakristo. Na Tunapaswa kuwaambia hivyo kulingana na Ezekieli 33:1-9 ingawa wanaiita hukumu. Hatuwajibiki kwa majibu yao. Mungu alimwonya Kaini akijua atamwua  Abeli. Katika Agano la Kale, Mungu alifanya hivyo kupitia manabii kwa gharama ya damu yao. Katika Kanisa, Hakufanya hivyo Kupitia malaika wala  kupitia nafsi yake bali  kupitia Wakristo. Kwanza na baba zetu mitume na wanafunzi na sasa, na sisi. Hivyo ndivyo anavyofanya Mungu  siku zote. Na hili si jambo jipya! [Kc.16v35]

24  Ndiyo maana nawasihi msiweke kipaumbele mambo ya kimwili kuliko ya kiroho! Wana wa  shetani wanahangaikia watakachokua duniani, na hata maiti zao zitakavyo kua nyuma yao . Msiwaige! Ikiwa  mtatendewa kama mbwa na kwenda Mbinguni,  msirudi nyuma!

25 Ikiwamnatamani Mbingu na  mnatambua kwamba ni Mwenyezi Mungu aliyezungumza nami mnamo Aprili 24, 1993,  pokeeni hii kama wito kutoka kwa Bwana Yesu Kristo Mwenyewe. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. Mungu alijitoa kwa ajili yetu na ni kwa sababu nzuri  ndio anaomba maisha yetu! Hebu tufe kwa ajili ya dunia na tuishi kwa ajili ya Mbingu! Kumkopesha Mungu  alichotupa isichukuliwe kuwa ni dhabihu kubwa sana! [Kc.6v18] [Kc.16v22] [Kc.16v31] [Kc.19v59]

26 Mnaona? Siachi kusema kwamba kwa Ujumbe mpya kama huu, kusanyiko  lililo mjini, haliwezi kupitisha miezi mitatu bila kuongosha nafsi mpya.  Na kama kusanyiko haliendelei wa kulaumiwa ni kiongozi. Na  ikidumu, lazima akubali  kuketi kwa unyenyekevu, peke yake . Nitarudilia kwa hiyo.

27 Lakini,  ninyi wanafunzi wangu, kumbukeni mfano wa talanta na msiwe kama mitini isiyozaa! Ndugu na dada, kama yule mwanamke Msamaria,  hakikisheni kila mtu anasikia Ujumbe huu karibu  yenu. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina!”]. [Kc.16v28]

28 Pia, wale wote walio na mali au fedha lazima watende kwa namna hiyo, wakiweka mali zao katika kazi ya Mungu kulingana na Ezra 1: 5-6.  [Kc.10v61]

29 Mungu awabariki, mkutano umekwisha.  Ukiwa nyumbani usisahau kuniombea.  Na kwamba, tukitenganishwa katika mwili, Mungu atuhifadhi daima katika Roho yule yule hadi tutakapokutana tena.  Amina!


Sura zinazofanana: Kc.16, Kc.72 na Kc. 108

Comments

Popular posts from this blog

KACOU 23: UFUNUO JUU YA DHAMBI ASILI

KACOU 79: KUNYIMWA VISA NA MARUFUKU YA KUSAFIRI

Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6