KACOU 11 : SEMA BASI !
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi, tarehe 01 december 2002, pale Locodjro, Abidjan – Ivory-Coast)
1 Mimi Kacou Philippe mtumwa wa Yesu kristo, sichoki kuwa alika muwe na hekima, na msifanye dhambi ile ile moja kama Israeli juu ya manabii, na ya Roma juu ya watakatifu ; mkinilaani, na mkinichukia kama pepo, mpinga kristo na mahubiri yangu kama nivakini, mjue kwamba ile yote mnamtendea Mungu.
2 Nilikuwa mpagani na tarehe 24 April 1993, kupitia ono nilipokea amri na kesho yake wakati nilikuwa nikikaa na jamaa yangu, nilichukuliwa katika ono nikapelekwa katika nchi yenye jangwa , na nikapokea amri ya kuhubiri hukumu ; na ni baaada ya yale maono mawili ambapo ni kaenda kwa mara ya kwanza kanisani.Na basi kama hamuwezi kuchukua biblia juu ya kupinga kile ambacho nina hubiri mkae kimya msijichagulie laana [Ndr: Kusanyiko linasema: « Amina! »].
3 Sijawahi bado kwenda kwenye seminari au kwenye mafunzo ya biblia yoyote, wala sisomi vitabu vya maduka yao mnayoyaita ya kikristo, kwa maana yule aliye nituma yupo pamoja nami ; Mungu ni mwenye mlalaka yote, anaweza kumtumia Mtu yeyote amtakaye, na kama yupo mtoto wa Mungu unalazimishwa kuitambua ile. Mwanzo wa kanisa aliacha Mitume na wafuasi wenye kujaa na Roho Mtakatifu na akachagua Sauli wa Tarsi, mtesi wa wakristo juu ya kusema na dunia mzima.
4 Na tarehe 24 april 1993 yuleyule Mungu mmoja alinichagua wakati nilikuwa bado ningali mpagani kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Na kama upo mtoto wa Mungu, utasema nini na kama si « oh ! Mungu mapenzi yako ifanyike » . [Kc.2v26] [Kc.3v27] [Kc.6v16]
5 Bustani ndogo ya wanyama ni dhambi kwa nchi; bustani kubwa ni halali ! lakini bustani ndogo ni dhambi ; Tai au Simba ndani ya nyumba inakuwa dhambi na ni namna moja na wale wanawafungia nyani ndani ya minyororo , hivi Bwana anasema, wafungueni hawa wanyama kama sivyo ni laana juu yenu.
6 Na tunaona wanyama wa mwituni, wanyama wakali ambao ni majitu ya zamani wanavamia miji wakiwa na nge, mazimwi na nyoka juu ya nguzo zao. Wanaume waliotobolewa masikio, nywele zisizo sahihi na lugha mpya, zote ni matunda ya dhambi. Kwa hivyo ni matunda ya uzinzi na uasherati, mimba katika hoteli, soko, ofisi, magari, nyumba ambazo hazijakamilika, na kadhalika.
7 Kufanya tendo la ngono kabla ya mahari ni kwenda dhidi yako na dhidi ya nchi yako na dhidi ya Mungu. Na ardhi imejaa na hayo. Mabweni ya chuo kikuu ni vituo vya ukahaba mkubwa.
8 Ibilisi ameifanya dunia Edeni yake na mwanamke kuwa chombo chake cha utangazaji. Na Ibilisi amewapa wanadamu alama nyingine za urembo. Lakini kulingana na Biblia, alama ya urembo ni uso. Tunaona kisa cha Rebeka katika Mwanzo 24:16, kisa cha Sara, mke wa Ibrahimu katika Mwanzo 12:11, kisa cha Raheli katika Mwanzo 29:17, kisa cha Abigaili katika 1 Samweli 25:3, kisa cha Tamari. 2 Samweli 14:27...
9 Lakini shetani amezua alama nyingine: matako kisha kitovu kisha rangi kisha vipodozi na kadhalika. Hii ni changamoto kwa ukamilifu wa kiungu: njia ya kusema kwamba « Mungu alipaswa kufanya mambo kwa njia hiyo ». Hatma ya Yezebeli imehifadhiwa kwa ajili yenu. Mkono wa uungu unawakamata mbwa ili wamle nyanya yenu Yezebeli. Na nini kilitokea kwa Yezebeli? Mbwa hawakugusa fuvu la kichwa, miguu na viganja vya mikono kwa sababu ya vipodozi na rangi ya kucha. Dada zangu wapendwa, Mungu anataka kuwaona jinsi alivyowaumba. Kaa hivyo! [Ndl: kusanyiko linasema: «Amina! »].
10 Na, piya roho yoyote ya kupinga Wafaransa ni ya shetani. Mungu yule asiyeweza kuliinua Kanisa dhidi ya Kristo au mwanamke dhidi ya mwanamume, Mungu huyu hawezi kuunga mkono uasi wa Ivory Coast dhidi ya Ufaransa au wa Kongo-Kinshasa dhidi ya Ubelgiji.
11 Na mnapotenda kwa njia hii, kabla ya kupokea bidhaa kutoka kwao, muwe na unyenyekevu na ujasiri wa kuwaomba msamaha. Sisemi kwamba Ufaransa haijawahi kufanya vibaya, lakini hamna haki ya kufanya mlichofanya. Na ni pepo huyu huyu ndiye aliyeingia Ivory Coast wakati Ahabu alipowekwa madarakani.
12 Nami nikasema kwamba ikiwa kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa amani na atatawala juu ya jimbo lote basi mimi si mtu wa Mungu na Mungu hajasema nami. [Kc.19v7] [Kc.59v38]
13 Ikiwa Ivory Coast ingekuwa na chaguo kati ya Mungu na Shetani, ingemchagua Shetani na makanisa yake na manabii wake. Mungu anapotoa kiti cha enzi anakiweka imara. mlifanya chaguo hili dhidi yenu. Na nasema hivyo kwa nguvu niliyopokea kutoka kwa Mungu.
14 Ahabu na mkewe Yezebeli ni watoto wangu, na watumishi wote wa Ahabu ni wajukuu zangu. Lakini kabla sijaingia kwa watu kama hao kwa wema, lazima wawafukuze hadharani marais na manabii wote wa Baali wanaokula mezani mwao na kuahidi kutoshiriki tena pamoja nao. [Ndl: kusanyiko linasema : «Amina! »].
15 Na tunamwona Yezebeli, mke wa rais akijiweka kama nabii mke, akitoa maagizo kwa Wakristo hata akiwaomba wachungaji kutumia kondomu na kuwashauri waaminifu wa makanisa yao. Hawa wapumbavu hawathubutu kumziba mdomo huyu mpagani mdogo ambaye yuko hapa leo na ambaye atatoweka kesho.
16 Na ninyi, mashirikisho ya makanisa, ninyi ndugu wa wachawi katika ngozi ya kondoo, Yesu Kristo amewashinda! Mnataka kula kwa meza ya Mungu na kwa meza ya Kaisari? Upanga utakuandama mchana kweupe na kuzimu itawapokea. Mnanichukia nikifa, Mungu atamtuma Kacou Philippe mwengine.
17 Israeli walimkata Isaya vipande vipande lakini Isaya mwengine alikuja katika mtu wa Yeremia. Nikifa hamtamaliza kushangilia kuwa Mungu atamtuma nabii mwengine kwa sababu ya watoto wake duniani. Adui wa dunia ni nyinyi! Kwa sababu mnatafuta kujenga himaya za kifedha,kwa hivyo mthamini dhambi? Jueni kwamba Mungu atawaangamiza na kuzimu itawapokea!... Nyinyi, Goliathi wenye miguu ya udongo, Ujumbe huu utawapiga. Ni Mateso yenu yameanza.
18 Ninyi! Wachawi! Mbwa mwitu kwa nyama na wanene! Nyoka walifugwa! Makao ya Shetani, mmelewa kwa damu ya watu wasio na hatia wanaotafuta Wokovu, bado mtaishi duniani hadi lini? Na kuzimu na ziwa la moto na jahanamu hupiga kelele dhidi yenu, « Hatia! hatia! Hatia ». Kwa nini? Kwa sababu utaifa wako ni kuzimu. [Ndl: kusanyiko linasema: «Amina! »].
19 Mnajiingiza katika siasa na mnasema: hatufanyi siasa! Ni kama mtu anayesema, « Sili nyama ya nguruwe lakini nakunywa mchuzi wa nguruwe.»
20 Mnamo 1993, kwa ajili ya mchezo wa kandanda kati ya Asec na Kotoko, nchi hii iliibuka dhidi ya Waghana, watu masikini waliofika katika nchi inayoitwa ya ukarimu kutafuta chakula. Niliona wanadamu wakifa mbali na nchi yao katika hali ambayo mtu hawezi kutamani itendewe hata mnyama.
21 Huko Yopougon, karibu na Sagudiba, mwanamke alikufa kwa mchi iliyosukumwa kwa sehemu yake ya siri hadi tumboni. Huyu mwanamke alifanya uovu gani? Na ni kusihi gani na msamaha gani mwanamke huyu hakuomba? Ni huruma gani mwanamke huyu hakuonyesha mbele ya hii Ivory Coast katili ambayo leo inalilia nchi mbalimbali kwa masemi ya mwana kondoo? Kwa nini Ghana ilikuwa kimbilio wa kwanza, hospitali wa kwanza ya Ivory Coast baada ya Septemba 19, 2002 ?
22 Tangu 1993, damu hizo zisizo na hatia hazichoki kumlilia Mungu: « Ee Mungu mwenye haki na Kweli, hadi lini utakawia kuhukumu na kulipiza kisasi damu yetu juu ya wakaaji wa Ivory Coast?». [Ndl: kusanyiko linasema: «Amina! » ]. Na baada ya hapo, Ivory Coast kupitia mwanawe Yodé alitoa kaseti ya muziki kusifia uhalifu wake na nchi nzima ikacheza.
23 Kuenda dhidi ya mgeni, mjane au yatima, Mungu hawezi kuachilia bila kuadhibu. Kama ningekuwa mwanajeshi, nisingeweza kamwe kubeba silaha kwa ajili ya nchi kama hiyo, kwa ajili ya Sodoma na Gomora. Sitakubali kamwe kufa nikiwa adui wa Mungu. Mimi ni Mkristo kabla ya kuwa raia wa Ivory Coast.
24 Kila mtu hufa akiwa na taji na maandishi juu ya taji hiyo, kilichotawala maisha yake…
25 Umemtesa mjane na yatima, umemtesa mgeni, na sasa unamtesa nabii wa Mungu ijapokuwa nyinyi ni nchi ya matumaini, nchi ya ukarimu, nchi ya baba ya undugu wa kweli? Mungu ni upendo lakini pia ni Mungu wa haki na hukumu. Mti unaanguka upande ulioegemea!
Sura inayofanana : Kc.103
Comments
Post a Comment