Kacou 162: Noti kwa mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6
(Maneno ya mwisho ya Ndugu Philippe kufuatana na mwisho wa Ujumbe wa Mathayo 25:6) 1 Kaka na Dada, Jumamosi hii, Mei 11, 2024, mimi, Ndugu yenu Philippe, nawatumia, kwa noti hii, maneno ya mwisho ninayotamka kufwatana na utume wa Mathayo 25:6 ambao nilikabidhiwa Aprili 24. 1993. Mnamo Januari 21, 2024, nilipopaza sauti: “pandeni wote kwenye chumba cha juu! ", Sikujua kwamba mimi pia ilibidi ninyamaze na kukomesha misheni yangu. 2 Ujumbe wa Mathayo 25:6 umekamilika. Na ni kwa ruhusa ya Mungu ninawajulisha maneno haya ya mwisho. Sasa ni kwa yule ambaye Mungu atamkabidhi mwenge kutuingiza katika uamsho wa wanawali kumi. Lakini hilo halinizuii kuwatembelea ninyi ikiwa Mungu ataniruhusu, kwa sababu ninawapenda na nina hilo moyoni mwangu. 3 Tunapohubiri na kudumu katika Ujumbe wangu, hebu sasa na tujingojee kwa mtu huyu mwengine na hatua hii inayokuja. Lengo la Ujumbe wangu halikuwa kuwaongoza kwangu ila kuwaongoza kwa Mungu. Kuanzia sasa,...