KACOU 64: TAFSIRI YA MAONO MAWILI


(Ilihubiriwa Jumatano jioni, Oktoba 17, 2007 huko Adjame, Abidjan – Ivory Coast)

1 Wakati nabii mjumbe anahudumu duniani, Mungu hutayarisha mazingira na wengi wa wale ambao majina yao yaliandikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu huanza kuzaliwa duniani.

2 Vema!  Napenda kuzungumza juu ya kitu kingine kabla ya kuanza. Malkia wa Sheba alipokuja kwa Sulemani, angalieni, kuhusu hekima ya Sulemani, Biblia inasema kwamba yeye mwenyewe alikuwa na hekima nyingi na hata kufikia hatua ya kumjaribu Sulemani kwa mafumbo na vitandawili.  2 Mambo ya Nyakati 9. Na kuhusu mali ya Sulemani, Biblia pia inasema kwamba alimletea manukato mengi na kundi kubwa la ngamia ndiyo waliyoibeba.  Alitoa zaidi ya tani tatu za dhahabu kwa Sulemani.  Hakuna mtu aliyekuwa ametoa dhahabu nyingi sana kwa Sulemani.  Alimletea mawe ya thamani kwa wingi sana.  Mnaona?

3 Mungu awabariki!  Jioni ya leo, natamani kusoma kwanza maono ya Aprili 24, 1993. Vema!  Ninasoma maono kwanza: “Nilijiona nikisimama juu ya mchanga wa bahari kisha juu ya piramidi ndefu kisha juu ya mchanga wa bahari tena mahali pengine na nikaona lori kuu la kijeshi likitoka kwenye vilindi vya bahari na kuenda nyuma yangu. Na nikageuka na kuona kwamba lina watu walio hai.  Walikuwa wanawake na mmoja wao alikuwa chotara. 

4 Kisha njiwa wawili wakanijia na kuondoka juu ya maji. Kukawa na kupatwa kwa jua kisha mtu aliyekuwa na mwonekano wa Wingu na mwenye upanga akashuka kutoka Mbinguni pamoja na Mwana-Kondoo na dunia ikaangazwa tena. Walisimama juu ya maji na Mwana-kondoo akaanza kusema nami katika lugha isiyojulikana.  Mlio wa sauti yake ikaniingia na nikaanguka kama mfu.  Nafsi yangu ikaenda kusimama pamoja nao juu ya maji huku mwili wangu ukiwa umelala juu ya mchanga wa bahari, alipomaliza kusema nami nafsi yangu ikaniingia na kuwa hai tena lakini sikuwaona tena. 

5 Kisha umati wa watu ulikuja kwangu kutoka upande wa kulia na niliwauliza ikiwa walimwona Malaika na Mwana-Kondoo.  Wakasema: “Hapana!".  Na nikasema: "Hamkuwaonaje Malaika na Mwana-Kondoo na yote waliyoyafanya"?  Wakajibu: "Hatukuona Malaika na Mwana-Kondoo na hatukusikia Maneno ambayo Mwana-Kondoo alinena lakini tunaamini kabisa maana kile alichotoa Mungu na ambacho shetani alichukua, sasa kimerudishwa kwako."  Nikatazama juu mbinguni na nikaona ngazi iliyosimamishwa kati ya mbingu na dunia juu ya maji na malaika wakipanda na kushuka.  Na maono yakaisha.  »  

6 Vema!  Yapata siku tano, nilikuwa nimekaa na dada mmoja. Saa tatu baada ya yeye kuondoka, nilihisi alikuwa na jambo muhimu sana kwa ajili ya Ujumbe.  Nilimpigia simu na ikawa hivyo.  Alisema: "Nilikuwa na maono mawili".  Na jioni iliyofuata alirudi kunieleza yale maono mawili.  Lakini alikuwa nayo miaka mingi iliyopita kabla ya kukutana nami.

7 Vema, Ninakuja kwenye haya maono mawili. Tazameni ono la kwanza: Yule dada akasema: “Nilikuwa nimekaa nyumbani na nikaona kama kibao mbele yangu na mtu aliyevaa mavazi meupe alikua wima juu ya mchanga wa bahari. Alikuwa mweusi, Mwafrika. Alikuwa akiangalia uso wa maji  kana kwamba alikuwa akingojea kitu na nilimwona kwa nyuma. 

8 Alipokuwa akitazama, samaki kama nyangumi aliinuka juu ya uso wa maji. Kisha muda muda kidogo baadaye, samaki huyu alishuka polepole ndani ya vilindi vya maji huku akivuta pumzi na kutoa mapovu ya hewa kana kwamba amekufa. Kisha samaki wa pili wa muonekano mmoja alionekana mahali pengine na kutoweka kwa njia sawa na wa kwanza. Kisha wa tatu, kasha wa nne, kisha wa  tano, kasha wa sita na was aba na wote walipitia kwa namna moja ili ile.

9 Na samaki wa saba alipotoweka, palikuwa na mwangaza juu ya maji, mbele ya mtu aliyevaa mavazi meupe. Mwangaza huo ulitoa sauti kubwa kama sauti zenye chehe.Haikuwa mwangaza wala ngurumo bali ni umeme uliotoa kelele hizi kama nyufa zenye nguvu zenye cheche. 

10 Na nuru ya sauti za umeme zikavipiga viumbe vyote, na upepo ukavuma juu ya maji na juu ya miti. Na mawimbi yakagonga miamba. Na ilikuwa kana kwamba ndivyo mtu alivaa mavazi meupe alikuwa akingojea na maonoyakaisha.”

11 Na mnaona ono hilo la kwanza, nyangumi saba wenye sura moja wanatokea mahali tofauti. Nyakati saba za kanisana wajumbe saba wakijidhihirisha katika sehemu mbalimbali za dunia, Huko Asia, na Paulo, huko Ulaya na Martin Luther, John Wesley, Ulrich Swingli, kadhalika, kasha Marekani na William Branham na sasa Afrika na nabii Kacou Philippe. Na itakuwa hivyo daima hadi mwisho wa nyakati za mataifa. Samaki saba na samaki hawa wanatoweka hadi was aba ili kuonnyesha pia kwamba wakati wa William Branham utapita. Na kwamba baada ya hapo, Mungu atamwinua Mwafrika ili ulimwengu uokolewe kupitia yeye. [Mhr: Kusanyikolinasema, “Amina ” ]

12 Sasa, tunafika kwenye ono la pili.  Baada ya ono la kwanza, dada alisema : “Inamaanisha nini?  Na mara ono ya pili likafuata.  Mwafrika yule yule, mtu yule yule aliyevaa mavazi meupe niliyemwona wima juu ya mchanga wa bahari alikuwa ameketi juu ya farasi mweupe juu ya mlima mrefu sana.  Na mlima huu ulikuwa wazi kama piramidi. Maji yalitiririka juu ya piramidi hii.  Mlima huu ulikuwa peke yake, si katika mlolongo wa milima. 

13 Na nilitamani kuona sura ya huyu mwafrika lakini haikuwezekana maana nilimuona kwa nyuma.  Alikua akishuka pole pole na aliposonga mbele, mlima aliokuwa amekalia, alipokua wima pa nafasi yake lakini milima mingine yote na vilima vyote duniani vilikua vikianguka na kugeuka mawe madogo mbele yake na miti yote, mikubwa na midogo ikajipinda kama upinde hadi majani yao yaligusa chini mbele yake na akaenda kwa mwanamke mzee sana mweusi. 

14 Ilikuwa ni kana kwamba mwanamke huyu mzee sana mweusi alikuwa akimngoja mwanamume huyu kwa muda mrefu. Alikuwa ameinama kwa uzee, mikunjo usoni ilikuwa na mikubwa, mwendo wake ulikua wa polepole sana.  Alimtazama mpanda farasi akija, kama mtu anatazama tumaini pekee na pia ilikuwa ni kama ni kwa sababu yake ndio alikuja.  Na yule mtu aliyevaa mavazi meupe akiwa amepanda alienda mpaka kwake.  Na alipomgusa yule mzee, akawa msichana mzuri sana. Hata nguo zake zilibadilika. 

15 Na kwa muujiza uliotukia, umati mkubwa wa watu ukaja tena, ukimsifu na kumwabudu Mungu kwa sababu ya muujiza huo.  Na umati ukawa mkubwa sana.  Na walikuwako wanaume na wanawake, wadogo na wakubwa, weupe na weusi, watu wa kila kabila za dunia wakipiga kelele : “Atukuzwe Mungu wetu!  Atukuzwe Mungu wetu!  Tumeokolewa!  Tumeokolewa!  ".  Na habari hiyo ilienea duniani na umati wa watu ukaja kutoka kila mahali. Mpanda farasi akaendelea mbele na umati ukamfuata.  Na ono likaisha na nikasumbuka kwa siku kadhaa.  Amina!

16 Ndiyo yanayotendeka hasa duniani kwa sasa na wanadamu hawayaoni. Katika siku za Bwana Yesu Kristo, wanadamu walifikiri kuja kwa Bwana Yesu Kristo kungekuwa kubwa sana kiasi kwamba vituo vya televisheni vingeitangaza.  Lakini Mungu anajifunua kwa urahisi na watoto wa Mungu wanatambua hilo.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!”].  Lakini ono linasema kwamba miti mikubwa ya dunia na milima mikubwa itainama mbele ya tendo hili la kimungu duniani.

17 Tazameni maono ya kwanza!  Maono ya kwanza ni maono makubwa zaidi yanayohusiana moja kwa moja na Ujumbe baada ya yale ya Aprili 24, 1993. Na yanatukia pembeni ya mto mkubwa wa Hidekeli kuhusiana na lugha isiyojulikana ya Danieli 12:10. Hii ni picha nyingine kabisa ya maono ya Aprili 24, 1993 kama moja ya vitabu vya Mathayo, Marko, Luka na Yohana kulingana na kile Bwana Yesu Kristo alifanya duniani.  Na karama ya unabii, iwe kubwa kiasi gani, haiwezi kuwa sawa sawa na hiyo.  Mnaona ?

18 Naye alipoona ono la pili, alisema : "Mtu kama huyu atatembea je duniani"? Mnaona? Ni kwa yule ambaye alipewa uelewa wa hilo tangu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio atakayeelewa na kuamini.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”]. Na hawa, kabla hawajawa na mwili, kabla hawajadhihirishwa duniani, walikuwa tayari wameamini katika mawazo ya Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. [Kc.139v27]

19 Sasa tuchukue ono la kwanza.  Wale nyangumi saba ni makanisa saba ya mataifa ambayo yatatokea katika sehemu mbalimbali duniani.  Maji ni mataifa kama inavyoonekana katika Ufunuo 17:15.  Pepo nne ni nguvu na mapepo ambayo yatachochea mawimbi, yaani umati na mataifa dhidi ya watakatifu kama inavyoonekana katika Ufunuo 12:14-17.  “Nyoka akalusha maji juu ya mwanamke. ..” yaani kanisa.  Mnaona ?

20  Na nyangumi wa kwanza ni Kanisa la Efeso na ni nyangumi huyu huyu anayeonekana na kutoweka hadi wa saba.  Kitendo cha nyangumi wa saba kutoweka kabisa inamaanisha kwamba Ujumbe wa jioni utapita kabisa kabla Kelele ya usiku wa manane kusikika kama inavyoonekana katika mahubiri : Siri ya wale wanyama wanne uliowaona. Nyangumi wa saba anatoweka kabisa na Wabranhamisti wanakuwa mnyama wa nne wa Danieli 7 kabla Kelele ya usiku wa manane haijasikika duniani.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”]. Baada ya Laodikia inakuja huduma ya mpanda farasi wa Ufunuo 19. Mnaona?

21 Na baada ya nyangumi wa saba, umeme unapiga, si mbinguni, bali juu ya maji.  Hasa mahali na kwa mbali ambapo Malaika na Mwana-Kondoo wa Aprili 24, 1993 walisimama. Dada aliona umeme lakini nabii Kacou Philippe aliona wazi wazi Malaika na Mwana-Kondoo. 

22  Dada huyo alisikia milio mikali ya milipuko kama sauti, kama vile Danieli pia aliisikia hapo, lakini nabii Kacou Philippe alisikia Maneno kwa uwazi hadi kusema : lugha hiyo ilikuwa karibu na Kiarabu kwa sababu sijawahi kusikia mtu yeyote akizungumza Kiebrania.  Katika Yohana 12:28-29, Biblia inasema umati wa watu ulisikia ngurumo lakini ilikuwa ni Maneno: "Nilimtukuza na nitamtukuza tena."  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

23 Na dada huyo anasema kwamba nyangumi wa saba alipotoweka, mtu huyo alikuwa akijitayarisha kwa ajili ya jambo fulani kisha umeme ukaja.  Na sauti iliyotoka katika ule umeme ikatoa zile pepo nne juu ya maji, maji yakainuka kuipiga miamba na nafasi ya nyuma ya yule mtu aliyevaa mavazi meupe palikuwa kama jangwa nililoliona katika maono ya pili ya 1993.

24 Kulikua miamba;  na palikuwa na mmoja kabla yangu kwa maana Bwana Yesu Kristo Mwenyewe ndiye Mwamba wa nyakati. Na katika kitabu cha Ufunuo, ambapo inazungumza juu ya umeme, inazungumza pia juu ya sauti na ngurumo.  Umeme na cheche zinashuhudia kwamba ni sauti na Ayubu 37:4 inasema kwamba Yeye hazuii umeme Wake anapoisikilizisha sauti yake.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

25 Ono la pili ni lile la huduma tukufu.  Dada anabainisha kuwa mlima ulikuwa wazi, maji yalitiririka juu yake. Ilikuwa wa mrefu na pekee, si katika mlolongo wa milima. Na huo mlima mrefu ni Kanisa lile lile la kale tangu mitume.  Alikuwa peke yake, si katika mlolongo wa milima; si pamoja na makanisa mengine yaani haijawahi kuwa na kamwe haitaunganishwa na mlima mwingine wowote, yaani kanisa.

26 Na mpanda farasi aliposonga mbele, makanisa ambayo ni milima na vilima vya dunia yalikua yakiinama, hata miti ilijukunja mbele yake.  Na miti ni watu wakuu wa kidini, wanateolojia na wafalme wa dunia.  Na itatokea kwamba mameya, manaibu, mawaziri na hata marais na wafalme wa dunia watatokea ili kutimiza maono haya na itasemwa kwamba Mungu wa mbinguni amemtumia mwafrika, sio kubeba msalaba wa Bwana Yesu bali kusema kwa niaba ya Mungu kwa wakaaji wote wa dunia kama alivyofanya zamani na Musa na manabii ili kwa muda, kusiwe hata mtu awezaye kuokolewa katika uso wote wa dunia isipokuwa na Mwafrika huyu.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

27  Ndiyo!  Wateule watakuja kutoka Mashariki na Magharibi, kutoka Kaskazini na Kusini juu ya mbawa za tai;  kutoka Asia, Ulaya, Marekani, Afrika kwa ajili ya ubatizo, kuwekwa wakfu na kadhalika, akishirikiana nasi, kwa maana tulikuwa na furaha pamoja Naye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  Mabara yametutenganisha, utajiri umetutenganisha, rangi na makanisa yametutenganisha lakini nabii anatukusanya pamoja chini ya 2 Mambo ya Nyakati 20:20 na Hosea 12:14.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

28 Na huyu mwanamke mzee si chochote ila Kanisa lile lile la mitume linalotokea hapa usiku wa manane, mara hii kama Mwafrika.  Naye hangeweza kuwa na mzungu kama nabii mjumbe kwa sababu Biblia inahukumu mchanganyiko.  Na Nabii wa wakati  wake ndiye aliyemfanya upya kama ilivyokuwa kwa vizazi vilivyopita.

29 Na katika yale maono mawili, dada hakuona uso wa mtu aliyevaa mavazi meupe.  Kila mara alikua akijiweka  ili asiweze kuuona uso wake.  Kwa sababu, hawezi kuwa mtu mwingine isipokuwa yule wa Mathayo 25:6 ambaye atamwona siku moja duniani.  Na kama angelimwona, angaliamini leo kwa sababu alimtambua na si kwa ajili ya Ujumbe.  Japo inapaswa kuwa kwa sababu ya Ujumbe na hivyo ndivyo hasa hufanyika.  [Mhr : Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

30 Mnapoona ono la Mungu, hata miaka kumi baada ya ono hilo, mtakumbuka ono hilo kana kwamba ilikuwa jana. Na angejua kwamba ni mimi. Lakini aliponiona upande huu, hakuweza kufikiria kwamba mimi ndiye mtu aliyevaa mavazi meupe ambaye alikuwa amemwona katika maono, kwa sababu mtu huyu alikuwa mkuu mbele za Mungu na asiye na maana mbele ya wanadamu. 

31 Maana kilicho cha maana mbele ya wanadamu si cha maana mbele za Mungu, na kilicho kikubwa mbele ya Mungu hakina maana mbele ya wanadamu.  Mnaona?  Na kabla sijahubiri, Mwenyezi Mungu amefunua ya kwamba Mwafrika atakuja na Ujumbe, na kwa Ujumbe huo, watu wa rangi zote za dunia wataokolewa.  [Mhr : Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

32 Na uwe Mwasia, Mzungu, Mmarekani au Mwafrika, Ni lazima ujue kwamba kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, hakuna anayeweza kuokolewa isipokuwa kupitia Mwafrika huyu.  Kulikuwa na wakati ambapo ilikuwa ni Paulo, Mwasia. Kisha huko Ulaya na Martin Luther, John Wesley, Ulrich Swingli na wengine wengi.  Na kisha, Marekani pamoja na William Branham.  Na sasa Mungu anamwinua Mwafrika, ambaye nje yake hakuna Wokovu. 

33 Kama vile Nuhu kwa wakati wake, kama Bwana Yesu Kristo wa wakati wake, kama kila nabii wa wakati wake, leo ni nabii Kacou Philippe.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”]. Na huwezi kuokolewa nje ya yale ambayo Nabii Kacou Philippe anahubiri.  Na mwenye masikio asikie!

Sura zinazofanana:  Kc.1 Kc.36  Kc.130 na  Kc.133


Comments