KACOU 60: FILAMU YA HUKUMU YA MWISHO

(Ilihubiriwa Jumapili Machi16, 2003 huko Locodjro, Abidjan – Ivory Coast)


1 Vema! Hebu tuchukue Biblia zetu!  Nitasoma Mathayo 23:34-35 kisha nitasoma Ayubu 33:23-24 nitakayozungumzia wakati ujao.  Tusome katika Mathayo 23: “Ndio maana, tazameni, mimi nawatumia manabii, na wenye hekima, na waandishi;  na mtawaua na mtawasulubisha, na mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu, na mtawatesa kutoka mji hadi mji, ili damu ya wenye haki wote  iliyomwagwa duniani ihanguke juu yenu, kuanzia damu ya Abeli mwenye haki, hadi damu ya Zekaria, mwana wa Barakia, ambaye mlimwua kati ya hekalu na madhabahu."  

2 Tusome pia Ayubu 33:23-24: “Ikiwa yuko mjumbe kwake, mfasiri, mmoja katika elfu, ili kumwonyesha mtu kile ambacho ni haki kwake, atamrehemu, na atasema Mwokoe ili asishuke shimoni; nimepata upatanisho. "Amina!  Mtafakari juu ya andiko hili ya Ayubu 33, nitarudi kwa hili kama ninavyorudi kwenye Mathayo 23 leo.

3 Bila shaka, Nimesoma katika kitabu cha Mtakatifu Matayo, lakini mtu wa kwanza ambaye napenda kumtaja hapa ni Henoko.  Henoko aliishi kabla ya gharika.  Biblia inasema katika Yuda mstari wa 14 kwamba alikuwa wa saba. Kwanza ni Adamu katika Mwanzo 5 mstari wa 1, katika mstari wa 3 tuna Sethi, katika mstari wa 6 tuna Enoshi, wa nne ni Kenani katika mstari wa 9, wa tano ni Mahalaleli katika mstari wa 12, wa sita ni Yeredi katika mstari wa 15 kisha wa saba ni Henoko.  Mtu hawezi kuzungumzia watumishi watakatifu wa Mungu bila kuzungumzia Henoko.  Mwanzo 5:24 inasema : “Henoko akatembea na Mungu; na hakuwapo tena, maana Mungu alimtwaa.  Huu ni unyakuo wa kwanza ambao Biblia inataja.

4 Na huyu nabii Henoko alitabiri kwamba siku moja Mungu angeangamiza dunia kwa maji.  Mnasema : “Ndugu Philippe, je, Henoko alisema hivyo?  Ndiyo, Mungu aliifunua kwa ulimwengu kupitia Henoko.  Katika wakati wake, Henoko alikuwa nuru ya ulimwengu na haungeweza kuokolewa au kuwa katika mapenzi ya Mungu isipokuwa kupitia kwa Henoko.  

5 Henoko alikuwa nani?  Alikuwa mtu wa kwanza kabisa aliyetembea katika Roho na nguvu za Eliya.  Henoko alikataa makanisa yote, mifumo na mashirika ya wakati wake ili kubaki na ufunuo wa Mungu.  Hakutembea juu ya mafundisho ya kanisa au Biblia bali pamoja na Mungu.  Hapa ndipo Mungu alipomchagua Eliya kwa mara ya kwanza.  Mnaona ?

6 Ni huyu Henoko ambaye alikua akivaa ngozi za wanyama na ambaye walipaswa kutambua kupitia Eliya Mtishbi.  Ni mara ya kwanza kwa Roho wa Eliya kuonekana duniani.  Mtu huyu aliyepanda Mbinguni katika Mwanzo 5 ni Henoko.  Mtu huyu aliyepanda Mbinguni katika 2 Wafalme 2 ni Henoko.  Na mtu huyu ambaye atapanda Mbinguni katika Ufunuo 11 ni Henoko.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

7 Henoko alipoondoka duniani, ni nuru ndiyo iliondoka duniani kwa sababu makanisa hayakuitaka, ulimwengu haukuitaka [nuru]….  Na siku ambayo wana wa shetani walipomwondoa Bwana Yesu Kristo duniani ili kumtundika juu ya mti, giza iliifunika dunia kwa sababu alikuwa nuru ya ulimwengu.

8  Kilichomweka Nuhu katika ugomvi nakizazi chake ni kitendo cha kuwahukumu, aliwahukumu na kuwaita wachawi hadharani badala ya kunyamaza na kufanya kazi kwa utulivu upande wake.  Kwao, Nuhu alikua akiwadharau watumishi wazuri wa Mungu na kibaya ni kwamba alithubutu kusema kwamba hakuna mtu anayeweza kuokolewa isipokuwa kwa Ujumbe wake.  Nuhu alihubiri kwamba ili kuokolewa kutoka kwa gharika, ilikuwa ni lazima kuamini kile alichosema na kuja kwenye safina.  Nuhu alihubiri kwamba hakuna mtu angeweza kuwa katika mapenzi ya Mungu isipokuwa kwa Ujumbe wake. 

9  Watu wakamwambia kwa dhihaka : "Nuhu, unamaanisha kwamba Adamu na Henoko, baba zetu ambao hawakukuamini watakwenda kuzimu?".  Mnaona ?  Kulingana na ufahamu wao, alichokua akikisema Nuhu hakikuwa na mantiki kiasi kwamba hawakuogopa.  Lakini Nuhu alikuwa akisema : “Adamu na Henoko watahukumiwa pamoja na vizazi vyao lakini kizazi hiki, kitahukumiwa kulingana na Ujumbe wangu na kama ninyi ni uzao wa Adamu au wa Henoko, mtasema : '‘Amina’' kwa kila moja ya neno langu nanyi mtaingia kwenye mashua yangu."  Na watu wakacheka mpaka Nuhu na nyumba yake ndogo wakaona aibu.

10 Japo wakati huo Biblia haikuwepo na Mungu alizungumza na jamii iliyochaguliwa kama kwa Adamu katika Edeni.  Na Nuhu siku moja aliona, katika roho, tai akiruka katikati ya anga.  Tai akatazama kisiwani, na tazama, kulikuwa na kuku wengi ambao hakuna mtu awezaye kuwaesabu, na idadi yao ilikuwa kama nyota za angani na tai akalalamika akiambia kuku : "Bado siku 40 na samaki wa baharini wataogelea kwenye kisiwa hiki!  Hivi asema Bwana!  Rukeni na mje nami kwenye milima!". Na kuku wakajibu kwa pamoja wakisema : "Tunakataa, huo ni uongo!".  Na Nuhu alipokuwa akitazama, tazama, kiwango cha maji kilipanda na kuku walikuwa wakipiga kelele na kuruka huku na kule kwa nguvu zao zote.  Na baadaye kisiwa, kuku na miti ilishuka ndani ya vilindi vya maji. Na ono lile likaondoka akilini mwake na Nuhu akajisemea moyoni : "Lakini kama hawa kuku waliniamini, wangewezaje kuruka na wakati wao ni kuku?"

11 Na Mungu akamwonesha Nuhu kwamba si kwa sababu wachungaji hawa hawataki kuamini lakini ni kwa sababu ndani yao hakuna kitu kinachoweza kuamini… Hata kama wangetaka kuamini, hawangeweza.  Ni sawa na kuingia msituni kutafuta mti unaoweza kuvuja damu.  Na ni kama mtu anakuomba utoe kitu usichokuwa nacho.  Ni sawa na kumwomba Mwefraimu aseme “Shibolethi” wakati hawezi.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Mnaona ?

12  Na Nuhu alipoingia katika safina, Mungu akaacha muda kidogo upite, ndipo Mungu mwenyewe akafunga mlango wa safina.  Mnaona ?  Tangu siku mjumbe anapoondoka duniani njia ya kwenda Mbinguni huanza kuwa nyembamba kama piramidi mpaka njia ya kutoka isikuwepo ndipo Mungu anainua kizazi kingine cha watu kisha anatuma nabii mjumbe mwingine.  Mnaona ?

13 Kisha baada ya Nuhu kulikuwa na mtu, na jina lake aliitwa Musa.  Alipata umaarufu wake kwa neema ya Mungu pekee.  Katika enzi kuu ya kimungu, juu ya uso wa dunia, Mungu alimtazama kwa kibali.  Hakuwa na hekima, akili na umaarufu wa Kora, Dathani na Abiramu bali alikuwa kinywa cha Mungu. 

14 Ikiwa Musa alisema nenda kushoto, haijalishi ni ishara na maajabu ngapi Kora na Dathani na Abiramu wangefanya kusema nenda kulia, mnapaswa kwenda kushoto na Musa.  Hata kama kila mtu yuko upande wao, upande wa Musa, upande wa Mungu.  Na katika Hesabu 16, mamia ya watu, wote wasiojua kwamba juu ya uso wa dunia Mungu anazungumza kupitia mtu mmoja walimezwa.  Mnaona ?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

15 Kwa utofauti na Wayahudi, watu wa mataifa hawana uzoefu wa kiunabii ndiyo sababu wanajadiliana na nabii.  Siku zote waliongozwa na wafalme, watawala, watu waliokua wakiwaongoza kwa hekima zao.  Ni aina ya mchungaji.  Mnaona ?  Sababu iliyowafanya Wayahudi kumsumbua Bwana Yesu ni kwa sababu wanajua kwamba kumkataa nabii ni kumkataa Mungu.  Tangu Samweli, wanalijua hilo.  Lakini hiyo haimwambii chochote mtu wa mataifa.

16 Watu wa mataifa mengine hata hawajui kile tunachoita nabii.  Mtu fulani anaanza kuwafanyia miujiza, yeye ni nabii.  Mtu anajiita "nabii", kwa hiyo kwao ni nabii.  Mnaona ?  Lakini Wayahudi wanajua nabii ni nini.  Wayahudi wanajua kwamba nabii haji kuhubiri yale ambayo nabii mwengine amesema.

17 Na kama nabii anakuja duniani leo, tegemeo lake haitakuwa Biblia.  Nabii anakuja kuwaambia wanadamu kile ambacho hawajui.  Ni wa kipekee kwa wakati wake, katika kizazi chake.  Anakuja kama Nuru na Wokovu katika wakati wake.  Na katika wakati wake, yeye pekee ndiye anayeshikilia funguo za ufalme na hakuna anayeweza kuokolewa isipokuwa kupitia kwake.  Yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa kila nabii katika Biblia na ndivyo ilivyo leo kwa nabii Kacou Philippe. [Kc.2v8-9]

18 Mataifa hayajui hata nani anaitwa nabii na yatahangaika vipi? Myahudi anajua kwamba kuhani bora anaweza tu kudumisha imani ya watu, lakini ni nabii mjumbe pekee anayejua mapenzi ya Mungu.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

19 Na katika agano la kale, katika agano la kale mbele za Bwana Yesu Kristo, ukuhani ni mfano wa huduma za mtume, nabii wa kanisa, mwinjilist, mwalimu na mchungaji na askofu na wale wote mnaowaona leo.  Kuhani anapaswa kurudia tu kile nabii wa wakati wake alisema.  Hana haki ya kuleta fundisho jipya, ufunuo mpya.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

20 Vema…palikuwa na watu hodari wa Mungu duniani…Kulikuwa na Yeremia.  Lakini kabla ya Yeremia, kulikuwa na Uria.  Katika utoto na ujana wake, Uria alipokwenda kwenye masinagogi, macho yake yaliwaona makuhani wakuu tu, waliomcha Mungu...lakini Yehova wa Milele ambaye aliamini kuwa ni Mungu wa makuhani na manabii alipomwita, vita vilianza.  Vita vya ukweli dhidi ya uwongo vilianza na kumalizika kwa kifo chake.  Rehema! 

21 Uria alifanya nini?  Soma Yeremia 26:15-23.  Yeremia akawaambia, Ila jueni tu ya kwamba mkiniua, mtamwaga damu isiyo na hatia juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake;  kwani hakika Bwana amenituma kwenu kusema maneno haya yote masikioni mwenu.  Wakuu na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, Mtu huyu hastahili kifo;  kwa kuwa amesema nasi kwa jina la Bwana, Mungu wetu.

22 Basi baadhi ya wazee wa nchi wakasimama, wakanena na umati  wote wa watu, wakasema, Mikaya, Morashti, alitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na Hezekia mfalme wa Yuda, pamoja na Yuda yote walimwua ?  Na tungefanya madhara makubwa kwa nafsi zetu.  

23 Tena kulikuwa na mtu mmoja aliyetabiri kwa jina la Bwana, Uria, mwana wa Shemahia, wa Kiriath-yearimu;  naye akatabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;  naye mfalme Yehoyakimu, na mashujaa wake wote, na wakuu wote, wakayasikia maneno yake, mfalme akataka kumwua;  lakini Uria akasikia, akaogopa, akakimbia, akaenda Misri. 

24 Mfalme Yehoyakimu akatuma watu Misri, Elnathani, mwana wa Akbori, na watu pamoja naye, mpaka Misri, nao wakamleta Uria kutoka Misri, wakamleta kwa mfalme Yehoyakimu, naye akamkata kwa upanga, na kuutupa mwili wake ndani ya nchi makaburi ya wana wa watu.”  mnaona ?  Na Uria alipokimbia, lazima wapagani walisema, "Si ulisema ni Mungu aliyekutuma, kwa nini unakimbilia Misri?"  Kaa hapa na Mungu wako akutetee."  Mnaona ? [Kc.2v8-9]

25 Na Biblia ilisema kwamba kwa Yeremia, sasa ni wakuu na watu wanaosimama na kuwaambia makuhani na manabii wasimwue Yeremia.  Mnaona ?  Kuna umati wa manabii na makuhani upande mmoja lakini upande mwingine kuna Yeremia anayewahukumu...

26 Makuhani, wale ambao wana vitabu vya Musa mikononi mwao na manabii, wale wanaodai kwamba Mungu anasema nao, wanataka kumuua Yeremia.  Mnaona kwamba si Mungu mmoja wa Yeremia anayewaongoza na anayezungumza na manabii hawa?

27 Sasa tazameni!  Watu walianza kusema: Nuhu alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi.  Mika, Mmorashi, alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi wakati ilikuwa imekwisha pia.  Pia walikumbuka kwamba Uria, mwana wa Shemahia alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi wakati ilikuwa imekwisha pita.  Eliya alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi.  Amosi alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi.  Mnaona ?  

28 Watu walianza kuwa makini!  Mnaona ?  Isaya alikuwa peke yake dhidi ya wote na alikuwa sahihi.  Watu wakawaambia makuhani na manabii: hapana!  Lazima tutazame vizuri mara hii!  Siku zote kuna mtu ambaye anatupinga sote na baada ya kifo chake tunaona kwamba alikuwa sahihi, mara hii, lazima tuangalie vizuri! [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

29 Tuchukue Yeremia 26:7-8 .  Hebu tusome hiyo: “Makuhani, na manabii, na watu wote, wakamsikia Yeremia akisema maneno haya katika nyumba ya Bwana.  Ikawa, Yeremia alipomaliza kusema hayo yote Bwana aliyoamuru waambiwe watu wote, makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Hakika utakufa!  ".  Bado mnaona? 

30 Tunapoona kutokana na historia kwamba nabii Isaya alikatwa vipande-vipande, tunaelewa kwamba uwezo wa kutokunyenyekea kutoka kwa uzao wa Kaini unabaki kwa Mungu pekee.  Yeremia anapofikia hatua ya kulia kama ilivyoandikwa katika Yeremia 20:14-18, wakati kuhani mkuu Pashuri anampiga kofi na kumfunga gerezani, wakati katika Yeremia 38:7 hawa wachungaji na manabii wanamshusha Yeremia shimoni, jinsi Mungu hajaamua kimbele kwa misheni hii ataweza kushikilia?  Na kama wewe ni nabii kutoka kwa Mungu, makanisa yanawezaje kukubariki?  Mnaona ?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

31 Baada ya hayo, nabii Eliya.  Na vita vile vile vikaanza, vita dhidi ya roho ya upotovu ambayo iliishia katika kunyakuliwa kwa Eliya.  Alikuwa peke yake dhidi ya makuhani, manabii na watu katika wakati wake.  Mtaona kwamba katika 1 Wafalme 18 hapakuwa na nabii kando yake na katika 1 Wafalme 19:10 alisema : “Nalimwonea wivu sana Bwana, Mungu wa majeshi;  kwa maana wana wa Israeli waliliacha agano lako;  waliyapindua madhabahu yako na kuwaua manabii wako kwa upanga, nami nilibaki peke yangu, na wananitafuta kuyaondoa maisha yangu.”  Lakini kwa Wayahudi hawa, ni manabii waasi na wasio na adabu kama Eliya ambao waliwaua kulingana na vile Musa aliwaambia.  Hawakujilaumu lolote.

32 Baada ya Eliya, napenda kuzungumza juu ya Mikaya mwana wa imla katika 1 Wafalme 22. Wakati huo, kulikuwa na manabii mia nne wenye nguvu katika Israeli. Manabii kama Billy Graham, Baruti Kasongo, Ushe Praise, Tommy Osborn na Yonggi Cho. Kwa muda mfupi, walikusanyika. Walikua wanafahamiana, na wanatembeleana na wanafanya makusanyiko pamoja. Walikuwa ndugu katika Kristo licha ya tofauti zao za kimafundisho. Lakini Mikaya alikuwa peke yake na alipokuja alikuwa peke yake.

33 Na katika 1 Wafalme 22:24 Mikaya akamwambia Ahabu : "Na sasa, tazama, Bwana ametia roho wa uongo vinywani mwa manabii wako wote hawa, na BWANA alinena mabaya juu yako.  Naye Sedekia, mmoja wa manabii, akaja, akampiga Mikaya shavuni akisema : "Roho ya Bwana ilipita wapi nje yangu ili kusema nawe? ".  Na tunajua kwamba Mikaya alifungwa gerezani kwa ajili ya jambo hilo na pambano hilo lilipaswa kuishia katika kifo chake.

34 Kisha Mungu akamtuma Amosi, twasoma hili katika Amosi 7:10 : “Ndipo Amazia kuhani wa Betheli akatuma watu kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, kusema, Amosi alifanya fitina juu yako katikati ya nyumba ya Israeli;  nchi haiwezi kubeba Maneno yake yote”.  

35 Mstari wa 12 unasema, “Amazia akamwambia Amosi, Mwonaji, nenda zako;  kimbilia nchi ya Yuda, ukale mkate huko, na kutabiri huko, lakini usitabiri tena katika Betheli, kwa maana ni patakatifu pa mfalme, na nyumba ya ufalme.  Amosi akajibu, akamwambia Amazia, Mimi sikuwa nabii, wala sikuwa mwana wa nabii;  lakini mimi nalikuwa mchunga mifugo, mkusanya  matunda ya mikuyu, naye BWANA akanitwaa hapo nilipofuata kundi, BWANA akaniambia, Enenda ukawatabirie watu wangu Israeli.  ".  Mnaona ?

36 Sikuwa nabii wala mwana wa nabii, sikujua chochote kuhusu Mungu lakini mnamo Aprili 24, 1993, niliitwa na kuamriwa kutimiza misheni kulingana na Mathayo 25:6 na Ufunuo 12:14.  Mnaona ?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Elisha alisema: Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa nikilima shamba langu na kura ya Bwana ikaniangukia.

37 Mtu wa kiroho zaidi, kuhani mkuu wa Betheli anamfukuza nabii Amosi kwa makubaliano ya taifa na mfalme.  Rehema!  Tazamani anachosema na mtaona kwamba ndivyo tunavyopitia [leo].  Anasema : "...nchi haiwezi kuvumilia Maneno yake yote"...

38 Kinachotufurahisha ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu daima huishia kwa ushindi na Kelele ya usiku wa manane itashinda.  Ikiwa huwezi kusimamisha tetemeko la ardhi basi huwezi kusimamisha Ujumbe huu wa kinabii kutoka kwa Mungu kufika ulimwenguni kote... [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

39 Kisha Mungu akamtuma Yohana Mbatizaji.  Baba yake alikuwa kuhani lakini alienda nyikani ili kupokea chochote kutoka kwake.  Mungu ndiye aliyemtuma, hakuwa na cha kupokea kutoka kwa mwanadamu.  Mnaona ?  Nabii anafanya nini katika kizazi chake?  Anashambulia ukuhani wote.  Lakini kwa kuwa Mungu hawainui wajumbe wawili kwa wakati mmoja, Yohana Mbatizaji ilimbidi aondoke kwenye eneo  ili kutoa nafasi kwa ajili ya Bwana Yesu.  Na ndivyo ilivyotokea.

40 Kisha Bwana Yesu Kristo akaanza kuchunga Israeli kwa fimbo ya chuma.  Lakini makuhani, Mafarisayo, Masadukayo, Waesene waliona mambo kwa namna nyingine.  Kwao, ikiwa Yesu Kristo anaona wanakosea, basi ajenge sinagogi lake mwenyewe na kuwatabiria wale wanaotaka kumsikiliza na kwenda Mbinguni na ni watakapo fika Mbinguni ndipo wataona aliyefanya vema au vibaya.  Lakini Bwana Yesu hakuona hivyo.  Kwake, alikuwa nuru ya ulimwengu na hifadhi ya ukweli na alidhamiria kwenda mwisho katika mapambano ambayo mwisho wake tunaujua, yaani kifo cha mjumbe.  Kisha hatimaye, Alijikuta peke yake dhidi ya wote.  Peke yake dhidi ya taifa.  Peke yake dhidi ya Herode.  Peke yake dhidi ya Pilato.  Na Yohana 9:22 inasema kwamba : "...Wayahudi walikuwa wamekwisha kupatana ya kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi."  Mnaona ?

41 Na leo, hawa wana wa ibilisi wako hapa duniani.  Na hawasemi lolote kwa sababu wanadhani kwamba kwa kuzungumzia Kelele ya usiku wa manane, wanajiweka katika hatari ya kuieneza na kuifanya iwe maarufu.  Lakini hatimaye watawaonya watu dhidi ya kitabu hiki.  Tazama, mmeonywa.  Wengine watasoma ili kupata maarifa na wengine hawatazungumza juu yake kama tahadhari kwa sababu wanafikiri kuwa jambo hilo linaweza kutoka kwa Mungu.  Lakini fahamuni ya kuwa hawa wote ni watoto wa shetani.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

42 Wakati Bwana Yesu Kristo alikuwa akihubiri, Mafarisayo walisema katika masinagogi yao... Ndugu, Mafarisayo walimwalika rabi mkuu, mwanateolojia mkuu mbele za Bwana na siku hiyo, katika vazi lake refu, na ndevu zake ndefu, baada ya kusoma katika kitabu cha Musa, alionyesha kwamba Bwana Yesu Kristo ndiye nabii wa uwongo zaidi ambaye Shetani alimtuma duniani tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

43 Alinena maneno ya kuwafanya watu wawe wagumu, kuifanya Waisraeli iwe ngumu. Alisema maneno kama : "Ni nani aliyetoa dhabihu ili kututoa Misri?" Musa au Yesu?... Na wote wakajibu Musa.  Akasema Musa huyu angali hai, na yeye ndiye nabii wetu.  Naye alionyesha kuwa Musa hakufa na akauliza ni nani aliyeliona kaburi la Musa?... Musa hajafa, Mungu alimficha. 

44 Musa alisema: Siku moja mtu akija kuwaambia kwamba nilikufa, msimsadiki.  Manabii hawafi.  Maneno yao ni ya uzima na ya milele.  Na Mfarisayo huyu alisema Mungu alimpa Musa ishara mbili.  Na Yesu, Mungu alimpa ishara gani?  Ni mdanganyifu maana maandiko yanasema Masihi atakuwa Mchungaji wa Israeli, kuhani mkuu Melshisedeki japo makuhani wanapaswa kuwa wa kabila la Lawi lakini Yesu huyu ni wa kabila la Yuda jambo ambalo haliendani na yale Musa aliyotuambia.  Sio ya kibiblia.  Isitoshe, yeye hashiki Sabato na wanafunzi wake hula bila kunawa mikono. 

45 Na huyu Yesu hasemi neno jema ila kuwatukana watu wa Mungu na masinagogi.  Ujumbe wake ni kutaja majina: uzao wa nyoka, nyoka kwenye majani, makaburi yaliyopakwa chokaa, na kadhalika.  Ujumbe wake ni matusi, Mungu hawezi kumtuma mtu wa Mungu kuwatukana watu.  Na Wayahudi wote wakafurahi.  Walikuwa wakipiga kelele kwa furaha, walikuwa wakiruka…Mnaona?  Walisema: Huyu Yesu hasemi neno jema ila anatumia makosa na udhaifu wa masinagogi na kuwapotosha wanyonge bali Mungu atukuzwe, kwa maana sisi ni wajuzi wa maandiko!  Haleluya!!!…”.  Na watu wakapiga kelele, "Amina!  Amina!!  Amina!!  ".

46 Rabi huyu aliendelea akisema : “Huyu Yesu anataka kuwaongoza watu wote kwake peke yake, lakini Mungu anachotaka kwetu ni kushika sheria ya Musa!!!  Na hii inaweza kufanywa kutoka mahali popote, kutoka katika sinagogi lolote, iwe Farisayo, Masadukayo, Essene, Hellenisti au Herodia.  Tofauti za mafundisho si kitu!!!  Cha muhimu ni Musa, ni kuishi vizuri!!!  Mafarisayo, Masadukayo, Wahelenisti, Wazeloti, Waesene na kadhalika, ni kama jamii ya watu weusi, wa njano na weupe.  Mbinguni tutakuwa na rangi moja tu!!!  Sisi ni bustani ya mboga ya Mungu yenye maua mbalimbali!!!  Haleluya!  … Sisi ni wa Musa!!!  Musa pekee!!!  Musa alisema yote!!!  Musa alifunua yote!!!…”.  Mnaona ?

47 Huyu Mfarisayo alipiga kelele kwa nguvu zake zote na taifa lilishangilia.  Walihakikishiwa kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa nabii wa uongo.  Mnaona ?  Lakini Yesu huyu anayezungumziwa katika masinagogi yote ni nani?  Lakini ni nani huyu ambaye wanafunzi wake walitoka katika masinagogi yote na makabila yote ya Israeli?  Ni nani huyu Kacou Philippe ambaye makanisa yote yanamzungumzia, ambaye wachungaji wanahubiri katika makanisa yao? 

48 Kila mtu anapingana naye, kila mtu anajaribu kumtesa, kila mtu anataka awe gerezani, afe.  Yesu huyu ni nani?  Ni nani huyu nabii ambaye wanafunzi wake wanatoka katika mataifa yote ya dunia, kutoka katika lugha zote za dunia.  Nabii huyu ni nani?  Nabii huyu ambaye wafuasi wake wanatoka katika makanisa yote ya ulimwengu ni yupi?  Nabii huyu ni nani?  Ni historia inayojirudia.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  

49 Ndugu, rabi huyu alikuwa na ufasaha sana, mwenye kuaminika sana, alikuwa wa kibibilia sana na baada ya saa moja ya kuhubiri, ilikuwa pointi kuu. Ilikuwa ni kukumbatiana kwa furaha.  Walimtukuza Mungu maana hawakumfuata Bwana Yesu Kristo na waliomba Mungu awakomboe wale ambao waliwaona kuwa walidanganywa na Yesu Kristo.  Na ndivyo watakavyofanya hadi leo.

50 Lakini mimi, nabii Kacou Philippe, ninajibu pia kwa kuwaambia kwamba wao ni bustani ya mboga ya Ahabu na kwamba ni kwa ajili ya bustani hii ndio walimuua Nabothi, manabii na Yesu na kwamba wanatafuta kusulubisha ujumbe huu tena.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. Ni bustani ya damu na laana!  Ni kwa ajili ya bustani hii ndio Wabranhamisti walichanganya Ujumbe wa William Branham.

51 Mnaona?  Katika ujumbe wa rabi huyu kuna mapepo kadhaa, ambayo ya mwisho ni: "Musa alifunua yote!".  Ni pepo wa zamani!  Wakati Paulo alipokuwa akijifanya nabii, pepo huyu wa zamani alisema : "Yesu alifunua yote!". Wakati William Branham alipokuwa akihubiri, shetani yule yule alisema : “Biblia ilifunua kila kitu!”. Na wakati Kelele ya usiku wa manane inapolia leo, pepo huyu huyu wa zamani atasema kupitia uzao wa nyoka : “William Branham alifunua yote!". Wanapaswa kusema hivyo kwa sababu mababu zao walisema hivyo.  Iko ndani ya damu yao.  Mnaona?  Nazungumzia damu ya nyoka anayetambaa msituni!

52 Kama vile kuna vikundi tofauti vya damu na rhesus tofauti, vivyo hivyo kuna tofauti ya uhusiano kati ya wale ambao hawawezi kuamini Ujumbe huu na sisi.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

53 Lakini kwa kweli, Musa hakufunua yote, ndiyo maana Mungu alituma manabii!  … Mnaona ?  Je, Paulo hakufunua yote, hata jinsi unyakuo ungefanyika kulingana na 1 Wathesalonike 4:16-18?  Na je, Paulo hakuwaambia watu wajifariji kwa hilo mpaka Bwana atakapokuja?  Sasa ilikuwaje basi Mungu alimtuma John Wesley, Martin Luther na William Branham na inakuwaje kwamba Mungu hawezi tena kutuma nabii duniani?  Mnaona ?

54 Lakini kitu cha ajabu, Ujumbe wa Bwana Yesu ulikuwa ukishika kasi na maadui zake walipoona maslahi yao yakitishwa, wakashauriana.  Mnaona ?  Lakini Alichosema kilikuwa kweli juu ya msingi wa ufunuo wa kinabii ambao Wokovu ulijengwa juu yake, si katika Mathayo 16:18 bali tangu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  Japo, hata ikiwa yale ambayo Yesu alisema hayakukubaliana na yale aliyosema Musa, lazima tuamini!  Hata kama wanafunzi hawanawi mikono kabla ya kula, lazima tuamini!  Hata kama Yesu hashiki Sabato, inabidi tu kuamini!  … [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

55 Na Biblia inatuambia kwamba ni makuhani waliowashawishi watu wamchague Baraba!  Hebu tusome Mathayo 27:20: “Lakini wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano wamchague Baraba na kumwua Yesu.  Mnaona ?  Kama vile katika siku za manabii wote.  Na ni wachungaji na manabii ambao wataonya watu dhidi ya nabii Kacou Philippe leo.  Ni historia inayojirudia.  Mnaona ?  

56 Na Bwana Yesu Kristo alitabiri katika Mathayo 23:34-35 kwamba atatuma manabii na ukweli duniani na ulimwengu wa kidini utawakataa na kuwatesa.  Ulimwengu wote utawakataa na kuwajengea makaburi baada ya kifo chao.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

57 Sasa turudi kwenye Mathayo 23 ili kumalizia: “ndio maana, tazameni, mimi nawatumia ninyi manabii, na wenye hekima, na waandishi;  na mtawaua baadhi yao, na kuwasulubisha, na mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu, na mtawatesa kutoka mji hadi mji, ili damu yote ya haki iliyomwagika juu ya duniani, kuanzia damu ya Abeli mwenye haki hadi damu ya Zekaria, mwana wa Barakia, ambaye mlimwua kati ya hekalu na madhabahu ianguke juu yenu  ».

58 Vema!  Bwana anasema nini?  Nimewatumia, manabii?  Hapana!  Lakini: natuma kwenu katika siku zijazo, manabii!  Je, umewaua ?  Hapana!  Lakini… “Baadhi yenu mtawaua na kuwasulubisha, na mtawachapa mijeledi katika masinagogi yenu, nanyi mtawatesa kutoka jiji hadi jiji.  Bwana Yesu Kristo atatuma manabii duniani, manabii kama wale wa Agano la Kale.

59  Nabii anamaanisha nini?  Kwa asili ya Kiebrania, neno nabi linamaanisha "msemaji".  Wingi ni Nebiim, kumaanisha: "wasemaji".  Sio wabeba upako au watenda miujiza bali wasemaji!  Nabii ndiye kwanza kabisa mbebaji wa Ujumbe kutoka kwa Mungu kwa wanadamu. 

60 Na Mungu anapomtuma nabii mjumbe duniani, ina maana kwamba hakuna ukweli tena duniani.  Naye hunena, na kuhukumu na kuhukumu kwa ajili ya Mungu, kwa mamlaka pekee ambayo ni ya Mungu peke yake.  Wakati nabii mjumbe yuko duniani, kuna ukweli na Wokovu tu kwake.  Na hakuna awezaye kumtumikia Mungu ila pamoja naye.  Na Mwenyezi Mungu anauthibitisha ujumbe wake kwa ishara na maajabu.  Na ikiwa ni kweli, ulimwengu wa kidini utaikataa.  Naye atakuwa peke yake dhidi ya wote.  Kwa nini?  Kwa sababu analeta tishio kwa maslahi na mamlaka ya watu wengi.  Na hakuna mtu anayeweza kumwamini bila kupoteza, angalau kwa muda, kile alichokuwa.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  

61 Na tazama katika kusanyiko!  Unamwona Ndugu Oscar ameketi pale, miezi mitatu iliyopita, alikuwa mchungaji msaidizi katika kanisa la kiinjili.  Mchungaji Akobé na wengine wengi.  Kutoka kwa wachungaji walikuwa, watakuwa waumini wa kawaida?  Sio rahisi lakini lisilowezekana kwa wana wa shetani linawezekana kwa wana wa Mungu.  Mnaona ?  Je, hawa wachungaji na manabii pamoja na familia zao, wanaolishwa na kuwekewa nyumba na makanisa yao watafanyaje?  Mnaona ?

62 Ikiwa mtu anajiita nabii na anaenda kushirikiana na manabii wengine kwa semina, makongamano na mikutano, kimbia, yeye ni mbwa mwitu!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

63 Sasa, sikilizeni mfano huu ambao Mungu wa mbinguni anawaambia wanadamu: Kondoo akienda mbali na zizi lake, akawaachia watoto wake maagizo akisema, “Fungeni mlango, mlale, wala msiufungue mpaka nitakaporudi!  ".  Wakasema, "Mama, tunaelewa, lakini utuletee nyasi nyingi unaporudi!"  …Aliwanusa kwa upendo na kuondoka. 

64 Mara moja, mbwa mwitu aliyekuwa anatazama alikaribia na kusema, “oh!  Je, tayari mmelala?  Fungueni mlango mimi ni mwana-kondoo kama nyinyi, nina kuja  kwa niaba ya mama yako kwa nyasi mlizoomba.  Fungueni mlango !  ".  Mnaona ?  Alikuja na neno la mama yao, neno la ukamilifu wao.  Alikuja na Neno la Mungu.  Lakini wana-kondoo walitazamana na kusema, "Je, wewe ni mmoja wetu?"  ".  Mbwa mwitu akajibu: Mimi ni miongoni mwenu, nifungulieni mtaona sufu yangu nyeupe na mtaona kuwa mimi ni mmoja wenu...".  Kisha mmoja wa wana-kondoo alikuwa na hekima ya kutazama chini ya mlango na aliona nini?  Sio kwato bali makucha ya mbwa mwitu yenye makucha ambayo yalionyesha kidogo chini ya ngozi nene ya kondoo.  Naye akalia, "Ni mbwa mwitu!"  Angalia makucha yake chini ya mlango!  ".  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Na mbwa mwitu, akihisi kufunuliwa, akakimbia.  Mnaona ?

65 Ni kweli kwamba tunahitaji nyasi, yaani miujiza na Neno, lakini tujue kwamba tutaugua tena na hata kufa.  Tusijishughulishe nafsi zetu na miujiza ya udanganyifu.  Bwana Yesu Kristo anataka Kanisa lenye hekima kulingana na Mathayo 25 kwa sababu Yeye mwenyewe ndiye utimilifu wa hekima. 

66 Kwa mujibu wa yale tuliyojifunza kutoka kwa Nuhu, Yeremia, Eliya na manabii wote wa kweli wa Mungu, mara nabii anapokaribia na kusema kwamba amepitia mafunzo ya kiteolojia, yeye ni mbwa-mwitu!  

67 Mara nabii anapokaribia si na Ujumbe ambao ni nuru ya kizazi chake bali na kanisa, yeye ni mbwa-mwitu!  Mara nabii anapokaribia na utume, huduma au maneno ya maarifa na si ujumbe wa kinabii wa wakati wake, yeye ni mbwa mwitu!  Ni lazima aje na Ujumbe wa kinabii ambao utafungua macho ya wateule wa kizazi chake.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

68 Neno la Mungu humjia nabii pekee na nabii huwajia watu akiwa na Neno kwa maana hapo mwanzo kulikuwa na Neno na kama sisi ni watoto safi wa Mungu, mazao safi ya Neno, tutaamini huku kila mtu akikataa hilo. 

69 Kanisa ni kwa ufafanuzi wote wa wale wote walioacha makanisa kukusanyika karibu na Ujumbe wa wakati wao.  Mnaona ?  Mara nabii anapotokea na kuanza kushirikiana na nabii mwingine huku wakiwa wameanzisha makanisa, misheni au huduma mbalimbali, wao ni mbwa-mwitu na msiache kuwaambia kwamba ni roho ya shetani inayowaongoza.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

70 Mara tu mtu anaposimama na kusema yeye ni nabii, muulize wito wake, utume wake na ni wapi kwenye Biblia Mungu alisema kuna mtu anakuja kutimiza kile anachofanya kwa sasa.  Kwa mfano: Isaya 40:3 ilitangaza kwamba Yohana Mbatizaji angekuja na Yohana Mbatizaji mwenyewe alisema hayo katika Mathayo 3:1-3. 

71 Isaya 61 alimtabiri Bwana Yesu na Bwana Yesu Kristo alisema hayo katika Luka 4:16-21...Na Isaya 49:6 ilikuwa inamzungumzia Paulo inasema, “Nimekuweka uwe nuru ya mataifa, ili uwe wokovu hata miisho ya dunia” na Paulo alisema hayo katika Matendo 13:47… 

72 Kwa kumalizia, ningependa kusema hivi: Kila mtu anatambua akiwemo Ewald Frank kwamba tuko usiku wa manane na William Branham mwishoni mwa huduma yake alisema kwamba tulikuwa dakika moja kufika usiku wa manane.  Na ni miaka arobaini baada ya William Branham, jinsi gani tusingekuwa usiku wa manane?  Mnaona ? Na kulingana na Danieli 12, huhitaji Mathayo 25:6 kuamini.  Na kulingana na Ufunuo 12:14, huhitaji Mathayo 25:6 kuamini lazima kuwe na Kelele ya usiku wa manane.  Mnaona ?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

73 Wakati wa jioni Shetani alisema kwamba Nguzo ya Wingu ilikuwa ni wingu la kawaida kutoka Tucson, ikiwa usiku wa manane anakuambia kuwa Mathayo 25:6 ni mfano wa kawaida, mwonyeshe hilo.  Mwonyeshe Yoshua 6, mwonyeshe 1 Wafalme 19, mwonyeshe Esta!  Mwonyeshe Isaya 30. Mtambulishe kwa Biblia nzima!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

74 Sasa, angalia katika ono, William Branham alikusanywa kwa watu wake.  Nini kingetokea atakapokufa, Mungu alimruhusu alione hilo.  Lakini ona kwamba William Branham hakumwona Musa, hakuona Yeremia, wala Paulo, wala Martin Luther, wala John Wesley.  Mnaona ?  Kila mjumbe alikuwa pamoja na kundi lake.  

75 Wakati mjumbe anaporudi, Mungu anafunga mlango kwa sababu neema kwa kizazi hiki inapungua na kuisha na giza linaingia tena.  Mnaona ?  Nuhu alipoingia katika safina, upanuzi wa neema ulitolewa kwa dunia kwa siku saba!  Lakini hii sio dhahiri kila wakati kwa sababu, Musa alipojiunga na kundi lake, mlango ulifungwa.  Musa aliporudi kutoka katika huduma yake, mlango ulifungwa kwa Musa na kundi lake.  Kuanzia Yoshua na kuendelea, hakuna mtu aliyeweza kuingia pamoja na Musa.  

76 Huu ni ufunuo maalumu.  Wote waliokuja baada ya hayo, Musa aliwaambia waende kwa yule aliyeuza mafuta baada yake, yaani Yoshua.  Mungu daima amekuwa na mtu duniani ambaye tunapaswa kumwamini kulingana na Yohana 6:28-29, ili tuwe na Uzima wa Milele.  Kazi na mapenzi ya Mungu ni kumwamini yule ambaye amemtuma.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. [Kc59v58]

77 Walimwambia William Branham pale, “Paulo yuko pamoja na kundi lake!  Ukimaliza huduma yako, utakusanywa kwetu na utahukumiwa sawasawa na yale uliyohubiri…”.  Na Paulo atakapokuja, hatasema alichofanya alipokuwa chini ya sheria bali kila kitu kitaanza kwa Paulo siku ile nuru hii ilipomulika njiani kuelekea Dameski na sauti hii ikazungumza naye.  Na ikiwa sauti hiyo ya Matendo 9 inatoka kwa Mungu basi heri wale wote waliomfuata na ole wao wote ambao hawakumfuata.  Mnaona ?  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  

78 Paulo atakuja na kundi lake.  Atajitambulisha na kusema, "Bwana, uliniita katika maono sawasawa na agizo la Isaya 49:6 nami nikapokea kutoka Kwako yote niliyohubiri...".  Ikiwa Mungu hakumtambua Paulo, yote yalikuwa yamekwisha kwa wale waliomfuata Paulo. 

79 Musa atakapopanda mpaka kwenye kiti cha hukumu kwenye Kiti Cheupe cha Enzi, atasema, “Bwana, siku moja tulipokuwa tungali kule Misri, malaika aliniita kutoka kwenye kijiti kilichokuwa kinawaka moto na kuniagiza ...”.  Na vivyo hivyo, wote watakaribia pamoja na kundi lao, wale waliowajua duniani: Martin Luther na kundi lake... John Calvin na kundi lake... John Wesley na kundi lake... ambaye walitembea naye duniani.

80 Na baada yao, sasa tunaona Walutheri wakija.  Walutheri walisema, “Bwana, sisi pia tulimwamini Martin Luther, mtumishi wako mtakatifu!  ".  Na waliposema hivyo, Luther akapaza sauti, akasema, “Mimi!!!  Sikuwahi kuwajua!!!  Mliniona wapi?  Mliamini mwaka gani?  ".  Walisema, "Mwaka 1560."  Lakini Luther alisema, "Mwaka 1560 alikuwa John Calvin!"  Wapelekeni kwa John Calvin."  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

81  Lakini John Calvin akiwaona alisema, “Bwana, wote hawa walijiita Walutheri nilipokuwa nikihubiri duniani,” na John Calvin akawarudisha kwa Martin Luther ambaye aliwahukumu.  Katika Luka 23:7 na 11: “Pilato aliposikia ya kwamba Yesu yu ndani ya mamlaka ya Herode, akamrudisha kwa Herode.  ".

82 Nini kitatokea kwenye Kiti Cheupe cha Hukumu?  Kwanza Mafarisayo walikuja na badala ya Musa waliwaona mitume kumi na wawili na Yesu wa Nazareti kulingana na Mathayo 19:28.  Waliogopa na kusema, “Sisi ni wanafunzi wa Musa!  ".  Mnaona ?  Hivi ndivyo walivyomwambia Yesu katika Yohana 9:28.  Na Yesu akasema, "Basi wapelekeni kwa Musa."  mnaona ?  Na walipofika kwa Musa, Musa akawauliza, "Lakini sikuwajua ninyi duniani, mlikuwa pamoja nami jangwani?"  Wakati kora, Dathani waliponiasi, mlikuwa upande wangu?  Mnawafahamu haruni na Miriamu?  ".  Mafarisayo wakasema, hapana!  ".  

83 Musa akastaajabu, akasema, Kwa hiyo mlikuwa pamoja nami huko Misri, lakini hamkutoka ?  ".  Mafarisayo wakasema, hapana!  Tuliishi duniani mwaka wa 30, mwaka wa 40 huko!  Lakini tulikuwa waaminifu kwako, sisi ni wanafunzi wako!  ".  Musa alisema, " mwaka wa30? , huyo ni Yesu Kristo!"  Lakini!!!  Kwa nini basi mnasema kuwa nyinyi ni wangu?  ... Je, sikuwaambia ya kwamba Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi?  Nendeni kwa Yesu!  ".  Wakasema, Samahani, Musa, usitufanyie hivi.  Tulikutetea duniani!  Kwa hivyo tunakuomba utukubali pamoja nawe!  Lakini Musa akawaambia, "Lakini mlipokuwa duniani ni nani aliyekuwa nabii wakati huo?"  Ni mimi au Yesu?”  Walisema, “Tulijua kwamba Yesu alikuwa akihubiri duniani.  ". 

84 Musa akasema, “Lakini ndivyo hivyo.  Alikuwa nabii wa wakati wako.  Alikuwa hai duniani mnamjua!  Lakini hamnijui.  Hamuwafahamu Haruni, Miriamu.  Hamumtambui mtu yeyote wa kura yangu, wewe si wa kura yangu.  Wewe ni sehemu ya Yesu Kristo na mitume.  Ni ndani yao kwamba ulipaswa kuamini ili kuokolewa.  ".  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!!]. 

85 Na Mafarisayo waliogopa waliposikia Jina la Yesu na mitume, walijua ya kwamba wale walio duniani waliwahukumu na kule Mbinguni wangewahukumu.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Mafarisayo waliposikia Jina la Yesu, mioyo yao iliruka!  Baridi iliwapitia.  Walikumbuka Yesu aliwaambia duniani katika Yohana 5:45, “Msidhani ya kuwa mimi nitawashitaki mbele za Baba;  yuko anayewashitaki ninyi, Musa ambaye mnamtumaini.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

86 Tunajua kwamba Neno la Mwenyezi Mungu ni hukumu kwa wana wa shetani, na wanapo sema: Sisi ni wa Musa.  kumwita mtu ambaye tayari amekufa ni kusema kwamba wamepoteza jaribio mbele ya walio hai.  Sisi ni wa nabii fulani na  nabii fulani ambaye tayari amekufa!  Mnaona ?  Mafarisayo walipokata rufaaa kuja mbele ya Musa, kusikilizwa, kulikubaliwa lakini Bwana Yesu Kristo aliwaambia kwamba Musa angewahukumu.

87 Kwa hiyo ili kurahisisha kila kitu, Mungu alitoa hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi ambacho ni mfano wa Sanhedrin ya Kiyahudi, mfano wa Mahakama yetu Kuu hapa.  Mnaona ?  Ili wasimkubali Yesu, walijiandikisha kwenye orodha ya wanafunzi wa Musa.  Walisema katika Yohana 9:28, “…sisi ni wanafunzi wa Musa.”

88 Mnawezaje kuwa wanafunzi wa mtu ambaye hamkumjua duniani na ambaye hata hajaishi katika kizazi kimoja nanyi?

89 Baada ya Musa, Baruku mwana wa Neria alikuwa mfuasi wa Yeremia na Elisha alikuwa mfuasi wa Eliya.  Mnaona ?  Na zaidi ya miaka elfu moja baadaye, walijiweka wenyewe kuwa wanafunzi wa Musa ili wasimkubali Yesu Kristo, nuru ya wakati wao.  

90 Na leo, wajukuu wa wale Mafarisayo, ambao kuzimu inawangojea, wamepanua na kuendelea kupanua orodha ya mitume na wanafunzi wa Yesu.  Leo, katika mwaka wa 2003, wao ni mitume na wanafunzi wa Yesu wa Nazareti ambao walitembea katika barabara za Yerusalemu na waliokuwa na mitume kumi na wawili na wanafunzi sabini waliohesabiwa vizuri.  Mnaona ?

91 Lakini Ibilisi anaweza tu kumdanganya mtu aliyezaliwa ili kudanganywa.  Maana Biblia inasema kama ingewezekana wateule wangedanganyika lakini haiwezekani!  Mungu ni mwema na kwa wema wake siku moja ataruhusu magamba ya upofu yatoke machoni petu.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!  ”].

92 Wanaomba kuonekana mbele ya kiti cheupe cha enzi lakini kuhusu wale walioamini Ujumbe wa wakati wao, hawatakuja hukumuni, tayari wamehukumiwa kupitia kusulubiwa kwa Yesu Kristo.  Musa atakuwa kama rais wa Mahakama Kuu ya wale wote walioishi huko katika jangwa la Sinai kama vile William Branham atakavyokuwa kwa wale walioishi alipokuwa nuru ya ulimwengu kulingana na Yohana 9:5. 

93 Na mimi Kacou Philippe ninayezungumza nawe, nitakuwa wa kizazi hiki.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Kila mtu duniani leo, iwe ananiamini au la, yuko chini ya mamlaka yangu!  Na siku moja mbele za Mungu, kwenye hukumu ya kile kiti kikubwa cheupe cha enzi, tutatokea kule mbele za Mungu.  Ninaona filamu ya hukumu ya mwisho.  Amina!  Haleluya!

94 Makanisa ya Kiinjili, wazao wa Mafarisayo wakaja na kumwambia Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi: "Sisi ni wa Yesu, hatukuamini chochote ila katika Yesu!"  ".  Lakini Bwana Yesu Kristo atawaambia, “Je! wewe ulikuwa katika Israeli nilipokuwa duniani?  Nilipokuwa duniani, hata niliwaambia wanafunzi wangu wasiende kwa watu wa mataifa kwa sababu huduma yangu ilikuwa kati ya ndugu zangu Wayahudi, basi inakuwaje ninyi, watu wa mataifa, mnasema: Sisi ni wa Yesu, tulikuwa wanafunzi wako. duniani?  … Kwanini mnasema hivyo?  Je! sikukuahidi nyota saba ambazo ni malaika saba ili uwasikilize ili uokolewe?  Kwa nini hukuwasikiliza?  Ondokeni kwangu, enyi watenda maovu!  ".  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Mnaona ?

95 Bwana Yesu alisema, “Je, sikusema katika Yohana 9:5 ya kwamba ‘WAKATI niwapo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu’ hamkusoma katika Biblia kwamba kabla Yangu kulingana na Yohana 5:35 . Yohana Mbatizaji alikuwa nuru ya ulimwengu?  Na kwamba, nitakapokuwa sipo tena duniani, manabii wengine watakuwa nuru ya ulimwengu ili kukuangazia kama Paulo?  ".  Mnaona ?  Watafungwa midomo!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

96 Baada ya Bwana Yesu Kristo, Paulo alisema, Mungu ameniweka KUWA nuru ya ulimwengu.  Sio nuru ya ulimwengu bali KUWA nuru ya ulimwengu.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Na kanisa fulani likatokea na jambo lile lile.

97 Rais wa kanisa la Kipentekoste atakaribia akiwa na Biblia kubwa iliyoshikilia moyoni mwake na atasema, "Bwana, mimi ni Mtume Yao Bio, nimefanya miujiza mingi kwa jina lako."  Bwana Yesu Kristo atamwambia: “Wewe unasema kuwa wewe ni mtume lakini ulikuwa mtume wa yupi kati ya wajumbe wangu ?  ".  Atasema: “Bwana, kwa tahadhari , sikumwamini yeyote ila Wewe, ni katika Injili yako kwamba mimi nilikuwa mtume”.  Bwana atamwambia: Mitume wangu walikuwa kumi na wawili katika hesabu, wewe ulikuwa yupi?  [Mhr: Kusanyiko linapaza sauti, "Amina!"  », Ndugu Philippe anasimama kwa muda] ... 

98 Na Yao Bio mkuu na mashuhuri, rais wa kanisa kuu la Pentekoste alifungwa kinywa chake na Bwana akasema: "Mfungeni miguu na kumtupa nje, ambapo kutakuwa na kilio cha  kusaga meno.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Je! sikuwaambia ya kwamba saa imefika ambapo ibada itakuwa katika roho na kweli, na kwamba si katika Israeli mtu atazame?  sikukuambia ya kwamba nitatembea kati ya mataifa, kati ya taa saba za dhahabu?

99 Je! sikukuambia kwamba kama vile umeme unavyotoka mashariki na kuonekana magharibi, ndivyo nitakavyojidhihirisha kwa mataifa yote ya dunia?  Je, sikuwaambia katika Mathayo 23:34-35 kwamba nitatuma manabii duniani tena?  Na wakati Paulo alipokuwa huduma huko Mashariki,je! hakuwa Mimi?  Na wakati Antipa alipokuwa kwenye huduma kulingana na Ufunuo 2:13, je! hakuwa mimi? 

100 Wakati mtumishi wangu Martin de Tours alipokuwa kwenye huduma huko Ufaransa, je! hakuwa Mimi?  Na wakati John Calvin alipokuwa kwenye huduma huko Uswizi, je!hakuwa Mimi?  Na wakati Jean Huss, Saint Patrick, John Wyclif... walipokuwa kwenye huduma, je! hawakuwa Mimi?  

101 Na wakati Martin Luther alipokuwa kwenye huduma huko Ujerumani, je!   hakuwa Mimi?  Na wakati John Wesley alipokuwa kwenye huduma,je! Hakuwa Mimi?  Na wakati William Branham alipokuwa kwenye huduma,je! Hakuwa Mimi?  Na Mathayo 25:6 ilipotimizwa katika Kacou Philippe, je! haikuwa mimi? Kwa nini hamkuwaamini?  Kama vile nilivyomtuma Eliya Mtishbi, Yeremia, Habakuki, Hagai, Hosea, Zekaria, Amosi, Sefania, Isaya ... na manabii wote kwa Wayahudi, ndivyo na kwenu pia, kama vile ahadi yangu ya Mathayo 23. 34 nanyi mmewakataa!  Ondokeni kwangu, enyi watenda maovu!  ".  [Mhr: Kusanyiko linapiga kelele kwa furaha, Ndugu Philippe anasimama kidogo].

102 Na kisha Joel Osteen, T.D. Jakes, Doug Batchelor, Billy Graham, Edir Macedo, Valdemiro Santiago, Silas Malafaia, Paula White na Joyce Meyer wakakaribia kama Mtume Yao Bio na ilikuwa hukumu na sentensi ile ile!  Na Chris Oyakhilome, David Owuor, Emmanuel Makandiwa, Uebert Angel, T. B. Joshua, David Oyedepo, Alberto Mottesi, Claudio Freidzon, na Dante Gebel walikaribia kama Apostle Yao Bio na ilikuwa hukumu na sentensi sawa! 

103 Na Benny Hinn, Manase Jordan, Jesse Jackson, John Hagee, Pat Robertson, Joaquim Gonçalves, Donald Parnell, Alejandro Bullón na Guillermo Maldonado walikaribia kama Mtume Yao Bio na ilikuwa hukumu sawa na sentensi sawa!  Na malaika watakatifu na viumbe vyote vilivyoko mbinguni vikapiga kelele kwa furaha wakisema: Aleluya!  Hosana!  Haleluya!  Hosana!  [Mhr: Kusanyiko linapiga kelele Haleluya!  Hosana!].

104 Kama kuna tumbusi hapa, na anyamaze kwa sababu tai wanakula.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Sisi ni samaki, tulizaliwa samaki na hatuombi kaa wawe samaki kama sisi, wala kunguru wawe tai kama sisi!

105 Mtu anainuka, na kujenga shirika la kidini na kuliita kanisa na kujitangaza kuwa yeye ni mtume, mchungaji, mwalimu, mwinjilisti au mfuasi...si  nabii mjumbe wa wakati wake bali ya Yesu wa Nazareti ambaye hakumjua na baadhi ya watu wanamfuata kama wanyama .  Mnaona ?  Sasa haya, ni mazoea ya zamani ya kipagani.  Ninatoa mifano miwili tu: Nitaisoma hiyo!  [Mhr: Ndugu Philippe anatafuta ukurasa]... 

106 Ni Daniel-Rops, Historia ya Kanisa la mitume,... ukurasa wa 157, nitasoma hivi: "Na wakati Mfalme Konstantino anapohisi mwisho wake unakaribia, akajenga kanisa kwa heshima ya mitume watakatifu pamoja na makaburi yenye Vito vyekundu kumi na mbili yakaandikwa  kumbukumbu zao,la kumi na tatu lilihifadhiwa kwa ajili yake".

107 Na mnajua kwamba hekalu kubwa zaidi ulimwenguni lipo katika Ivory Coast yenye picha kumi na tatu, ile ya Houphouët Boigny, inayowakilisha mtume wa kumi na tatu wa Yesu.  Mnaona ?  Na kama Constantine na Houphouët, uko huru kuongeza orodha ya wanafunzi na mitume wa Yesu, kama vile baba zako walivyokuwa wanafunzi wa Musa badala ya kumkubali Bwana Yesu Kristo, nuru ya wakati wao. 

108 Ninyi Wakatoliki, Waprotestanti, Wainjilisti na Wabranhamisti, ninyi, misheni na huduma Mungu akimwokoa mmoja wenu au mmoja wa wale wanaowafuata, lazima awaombe msamaha Mafarisayo na kuwaokoa wote akiwemo Yuda Iskariote!  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

109 Lakini tunajua ya kwamba Mungu kamwe hatumi kanisa duniani bali Ujumbe na wale wanaotoka katika madhehebu hukusanyika kuuzunguka Ujumbe huo ndio wanaounda Kanisa.  Lakini kwanza Ujumbe, kitu kipya ambacho ulimwengu haujui na ambacho kinakuja kama nuru ya ulimwengu.  Mnaona ?  

110 Pamoja na Musa, Yeye alileta torati, na kila nabii alikuja na Ujumbe... si na sinagogi bali Ujumbe uliomo katika kitabu.  Huwezi kamwe kuona kanisa au sinagogi la nabii namna hiyo ila Ujumbe…Na ni kwa Ujumbe huu ambapo kizazi chake kinahukumiwa duniani na kwamba kizazi chake kitahukumiwa mbele za Mungu Mbinguni.

111 John Wesley angewaambia Walutheri waliokataa Ujumbe wake duniani, “Msidhani ya kwamba Mimi, John Wesley, nitawashitaki ninyi mbele za Baba;  yuko mmoja anayewashitaki, Martin Luther ambaye mnamtumaini”.  William Branham angeweza kuwaambia Wamethodisti, “Msidhani ya kuwa mimi, William Branham, nitawashitaki mbele za Baba;  kuna anayekushitaki, John Wesley ambaye mnamtumaini”. 

112 Na ninaweza kuwaambia Wabranhamisti: “Msifikiri kwamba mimi, Kacou Philippe, nitawashitaki mbele za Baba;  kuna anayekushitaki, William Branham mnayemtumaini”.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Katika hukumu, wale wabranhamisti waliosikia Kelele ya usiku wa manane na kukataa walikuja na ilikuwa vivyo hivyo.  Ni unabii!

113 Ikiwa uliishi duniani mwaka wa 2002, uko chini ya mamlaka ya Mathayo 25:6.  Ikiwa ninyi ni Wakatoliki, Waprotestanti, Wainjilisti na Wabranhamisti au washiriki wa Uislamu au Uyahudi au misheni na huduma, ikiwa ni Mungu aliyenipa Ujumbe huu ... Kama Isaya na Yeremia, yule aliyewahukumu duniani tangu 2002 atakuwa hakimu  wenu mbele za Mungu.  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].

114 Ndipo, Mafarisayo wakavuta hati zao ndefu za kukunjwa hadi kwenye Baraza la hukumu na kusema, “Sisi ni wa Musa.  Wangesema leo, "Sisi ni wa Yesu!"  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Ni wakati huu ambapo wengine miongoni mwa wabranhamisti walikuja kwenye Baraza la hukumu!  Na walisema: "Bwana, hatukumkataa nabii Kacou Philippe lakini kama tahadhari, tulikuwa tukingojea uthibitisho wa ili tuungane naye ... ". 

115 Na Bwana atawaambia: “Lakini ninyi mlio na Ujumbe wa jioni, mlikuwa mkingojea ishara gani?  Ni uthibitisho ulioje!!!…Watasema, “Bwana, hukumthibitisha William Branham kwa Nguzo ya Moto?”  …Na Bwana atawaambia, “Ni uthibitisho gani uliokubaliwa na Yeremia, Isaya, Hagai, Hosea, Yoeli, Danieli, Sefania, Habakuki… Martin Luther, John Wesley, na wengineo?  Nyie wenye dhana ya nabii mlikuwa mnasubiri uthibitisho huku makahaba wa Baptisti, Methodisti, katholiki na wapentekoste wakiingia ndani???  Je, nimetia saini mkataba wa uthibitisho na wewe???  Je, Biblia inasema nilipaswa kufanya hivyo???  Ondokeni Kwangu na muende kwenye moto ambao umetayarishwa kwa ajili yenu tangu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu!!  !  ".  [Mhr: Kusanyiko linasema: Amina!].  Na William Branham mwenyewe ndiye aliyewahukumu mbele za Mungu kulingana na Yohana 5:45!

116 Jua kwamba ukishaikataa Injili ya wakati wako, imekwisha kwako!!!  Mifungo na maombi yako ni machukizo!  Bidii yako, matunda yako ya Wagalatia 5:22 ni machukizo na zaidi ya yote, Yesu wako ni Shetani.  [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!”].

117 Wakati nabii mjumbe anahubiri, mchungaji, mwalimu, nabii, mwinjilisti au mtume yeyote ambaye hachukui Ujumbe wake anatoka kwa ibilisi.  Unalazimika kuwa mwangwi wa Ujumbe wake vinginevyo unamtumikia shetani

118 Wakati Nuhu alipokuwa akihubiri, ungeweza tu kumtumikia Mungu kwa kuwafanya watu waamini Ujumbe wa Nuhu.  Yeremia alipokuwa akihubiri, ungeweza tu kumtumikia Mungu katika masinagogi yako kwa kuwafanya watu waamini kile Yeremia alikuwa akisema.  Wakati Bwana Yesu Kristo alipokuwa akihubiri, ungeweza tu kumtumikia Mungu kwa kuwaongoza watu kufuata Ujumbe wa Yesu.  Amosi alipokuwa akihubiri, Mungu angeweza tu kuutambua ukuhani wa Amazia ikiwa angemtambua Amosi kwa sababu Biblia inasema katika Yohana 6:28-29 kwamba... tusome hivi: “Wakamwambia, Tufanye nini tupate kuzitenda kazi za Mungu?  Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa naye.  Mnaona ?

119 Hungeweza kumtumikia Mungu isipokuwa kama ungemwamini yule Aliyemtuma kwako leo.  Mwenye masikio na asikie!

Sura zinazofanana: Kc.59, Kc 85, Kc 88 na Kc 117


Comments