KACOU 63: MUSA NA MWANAMKE MWETHIOPIA
(Ilihubiriwa Jumapili, Septemba 16, 2007 huko Adjame, Abidjan – Ivory Coast)
1 Vema ! Kuhusiana na maungamo ya uchi, ninabainisha kuwa haukutenda dhambi wakati macho yako yalipoangukia mwanamke aliyevaa vibaya ao picha mbaya na mara moja ukageuka bila kuangalia mara ya pili.
2 Vema! Nimeona maswali mawili hapa ambayo ningependa kuyajibu. La kwanza ni: “Ndugu Philippe , kwa nini Mungu aliumba wadudu?. " Mnaona ?
3 Hatuoni umuhimu wao katika maisha lakini kiuhalisia, wadudu wana umuhimu wao. Kwa mfano nzi, viwavi, funza na wengine hushiriki katika kuoza kwa kila kitu kilichokufa ili kurutubisha udongo tena kwa mbegu za baadaye. Hii ndiyo sababu hasa Mungu aliviumba. Mnaona ?
4 Wadudu huchangia katika maisha ya binadamu. Kufutilia mbali jamii ya wadudu hawa kutasababisha kuharibika kwa mpango wa Mungu.
5 Kama hapo mwanzo, Mungu angaliweza tu kumuua Kaini. Lakini hakufanya hivyo, kwa sababu Kaini na watoto wake wangehitajika mahali fulani. Ikiwa leo tuna magari, ndege, simu za rununu ... ni shukrani kwa Tubal-Cain. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! »] .
6 Biblia inasema katika Mwanzo 4:22, “Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua zana zote za shaba na chuma. Mnaona, yeye ni baba wa wanaviwanda, na yeye ni mtoto wa Kaini. Mnaona ? Mungu alipomlaani Kaini kwa mambo ya kiroho, alimpa zawadi ya vitu vya kidunia. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
7 Vivyo hivyo, angalia makuhani, wachungaji, manabii na viongozi wa kidini duniani kote. Zinatufaa kama vile wadudu na Tubal-Kaini. Unakumbuka kwamba huko Marekani, David Wilkerson, mmoja wao, aliwasaidia majambazi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Nicky Cruz akiwahubiri.
8 Kwa hiyo, kama Mungu hangemwacha Kaini aishi, makasisi na wachungaji hawa wa Kikatoliki, Kiprotestanti, kiinjili na kibranhamisti, wakiwemo wale wa Uislamu au Uyahudi, wasingalizaliwa kuwafuga hawa mamilioni ya wanyama wa porini na kuwathibiti katika makanisa haya na misikiti. Na tusingeweza kutembea kwa urahisi duniani. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Mnaona ? Wao ni muhimu kama wadudu. Makanisa na misikiti huchangia usalama wetu.
9 Vema! Swali la pili ni, "Ndugu Philippe , je, mtu anaweza kuokolewa nje ya Ujumbe unaohubiri?" ". Jibu ni hapana! Hili haliwezekani. Kwanza nitasoma Matendo 10, nitakuonyesha mistari miwili hapo. Kisha aya nyingine katika sura ya 11.
10 Wana wa Ibilisi hufikiri kwamba mtu anaweza kuishi vyema akiwa na moyo safi na kuokolewa bila ya lazima kukubali yale ambayo Mungu anafanya katika kizazi chake. Sasa katika kizazi kimoja ndicho Mungu anachofanya ndio mlango pekee wa Wokovu katika kizazi hicho. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
11 Kwa vile Kornelio alikuwa mtoto wa Mungu, Mungu hakumwacha afe pamoja na Mafarisayo, Masadukayo, Wahelenisti, Waherode, Waesene…kadhalika. Lakini alimpeleka kwenye Kweli ya wakati wake, kwa Petro, ambaye alikuwa na funguo za Ufalme katika kizazi chake. Na kama wewe ni mtoto wa Mungu leo, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya vivyo hivyo. Kwa nini? Kwa sababu ni yeye yule jana, leo, na hata milele.
12 Ikiwa moyo wako ni msafi na wewe ni mwema kweli, haiwezekani Mungu asikuongoze hapa. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Katika siku za Nuhu, moyo wako ukiwa safi na mnyofu mbele za Mungu, utaingia katika safina ya Nuhu. Ukisema kuwa moyo wako ni safi, moyo wako ni sawa mbele za Mungu, ni wewe unayesema, lakini ni wakati unapoingia kwenye safina ya Nuhu ndipo tutaona kwamba moyo wako ulikuwa safi kweli. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
13 Sasa na tufungue Matendo 10:1-3, ni Kornelio. Fuata vizuri! “Basi huko Kaisaria mtu mmoja, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kiitwacho kiitalia, mcha Mungu, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima, aliona maono ya wazi,… Malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, Kornelio! Sala zako na sadaka zako zimepanda juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Na sasa tuma watu Yafa wakamwite Simoni aitwaye Petro”. Amina!
14 Biblia inasema Kornelio alikuwa mcha Mungu! Kisha Biblia inasema alimwogopa Mungu pamoja na nyumba yake yote. Ninabainisha kwamba alimcha Mungu pamoja na nyumba yake yote, pamoja na mke wake na watoto wake. Alitoa sadaka nyingi kwa watu, si kwa watu wa familia moja tu au wa sinagogi moja naye, bali kwa watu wote. Na ndipo Biblia ilisema aliomba na kufunga daima. Lakini katika Matendo 11:13-14, inasemwa juu ya Kornelio “Naye akatueleza jinsi alivyomwona katika nyumba yake malaika aliyesimama akamwambia, Tuma watu Yafa, wakamwite Simoni, aitwaye kwa jina lingine Petro. atakuambia mambo yale utakayookolewa kwayo, wewe na nyumba yako." [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
15 Malaika hakuja ili kumtia nguvu, au kumbariki au kumwekea mikono au kumwambia afunge siku nyingi zaidi au kumwambia kwamba ameokoka bali kumpeleka kwa mtu, Petro yeye aliyekuwa na funguo za ufalme wa mbinguni wakati ule duniani.
16 Na leo, hata kama wewe ni mchungaji wa kweli, nabii au chochote kile, na kile unachofanya kwa kweli kinapanda kwa Mungu, Mungu hatawahi kutuma malaika kukuambia ufanye chochote isipokuwa kuja kwa nabii aliye hai. yeye aliye na funguo za Ufalme na Maneno ya Uzima wa Milele ambayo kwayo utaokolewa, wewe na wale wanaokufuata. [Mhr: kusanyiko linasema, “Amina! ”].
17 Kila jambo alilofanya Kornelio lilikuwa jema, lakini lilikuwa Neno la yule aliyekuwa na funguo za mlango pekee wa Ufalme wa Mbinguni ambao lingeenda kumwokoa yeye na nyumba yake yote. Vinginevyo, angeishia kuzimu kwa urahisi. Ikiwa kornelio hangekubali kile ambacho Mungu alikuwa akifanya katika wakati wake licha ya unyofu wote wa moyo wake, angeishia kuzimu.
18 Petro hakufa msalabani Kalvari bali alikuwa Petro aliyekuwa na Maneno ya Uzima wa Milele na funguo za Ufalme wa Mbinguni. Kacou Philippe hakufa msalabani Kalvari kwa ajili yako, lakini ni yeye Kacou Philippe ambaye ana Maneno ya Uzima wa Milele na funguo za Ufalme wa Mbinguni kwa Wokovu wako leo. [Mhr: kusanyiko linasema, “Amina! ”].
19 Uthibitisho kwamba Kornelio alikuwa mwema ni kwamba alikubali kile ambacho Mungu alikuwa anafanya katika wakati wake. Mnaona ? Kinachookoa ni Neno la Mungu lililo hai kwa wakati wako. Na Neno Hai; ni neno linalotoka kwa nabii aliye hai. Neno la Mungu lililo hai leo, Neno la Mungu lililo hai katika kizazi, ni Neno la Mungu litokalo katika kinywa cha nabii wa kizazi hicho wakati nabii huyo anaishi duniani. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
20 Hapo mwanzo kulikuwako Neno! Halikuwa kanisa bali Neno! Na kama Neno lilikuumba kweli, hutasema kamwe, "Natafuta kanisa zuri." lakini utasema, “Yuko wapi nabii aliye hai wa wakati wangu, iko wapi injili ya wakati wangu? [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
21 Hapo malaika akamwambia Kornelio, “Yote unayofanya ni mazuri. Unaenda kanisani, unaomba na unafunga sana, wewe ni mcha Mungu, haufanyi uovu, unamcha Mungu, unachangia.. lakini utaingia motoni usipoifanyia kazi Yohana 6:28-29. inasema kwamba kazi ya Mungu ni kumwamini yeye aliyemtuma” [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
22 Katika siku za Nuhu, kazi ya Mungu ilikuwa kumwamini Nuhu, nabii aliyeishi miongoni mwa watu wake. Katika wakati wa Musa, kazi ya Mungu ilikuwa kumwamini Musa, nabii aliyeishi katikati ya watu wake. Katika wakati wa Bwana Yesu Kristo, kazi ya Mungu ilikuwa kumwamini Bwana Yesu Kristo, Nabii aliyeishi miongoni mwa watu wake.
23 Na leo, kazi ya Mungu ni kumwamini nabii Kacou Philippe, nabii anayeishi katikati ya kizazi hiki. Kazi ya Mungu ni Yohana 6:28-29. Na ndivyo inavyosema katika maono ya 1993: "...Kwa wakati uliowekwa mtaelewa na kufundisha yale ambayo hamjajifunza, ili kila aaminiye awe na Uzima wa Milele." ".
24 Na katika "Yeyote" atahesabiwa kila mtu bila kujali wewe ni nani na jinsi ulivyo, bila kujali imani yako na usafi wa moyo wako, hata kama Mwenyezi Mungu atakuletea malaika kutoka mbinguni, ni kwa ajili ya kukuongoza kwenye kile anachofanya kwenye wakati wako. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
25 Na ndani ya juma hili, nilimwuliza mchungaji, nikamwambia, “Bwana, katika siku za Nuhu, je! kungekuwako na mtu mahali fulani duniani ambaye pia alikuwa anafanya kazi ya Mungu?”". Na hakuweza kujibu. Nikaendelea tena, “Bwana, ninamaanisha katika siku za Bwana Yesu Kristo, wakati Bwana Yesu Kristo alipokuwa akihubiri duniani, je, kunaweza kuwa na mtu mmoja popote pale juu ya uso wa dunia? ambaye pia alikuwa anafanya kazi hiyo ya Mungu? ".
26 Na kinywa chake kilifungwa, na hivyo vinywa vyao vitafungwa duniani na mbinguni milele na milele! Ni swali linalowangoja kwenye hukumu na watalijibu! [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Mungu ni wa pekee mbinguni na kinywa chake ni cha pekee duniani na kinywa cha Mungu ni nabii mjumbe aliye hai. Funguo za Ufalme zinaweza kupatikana tu na mtu mmoja duniani kwa wakati mmoja. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
27 Vema! Tunajua kwamba Roho wa Danieli lazima atende katika wakati wetu. Akizungumzia lugha isiyojulikana, awamu kuu ya huduma, ni Roho wa Danieli. Sasa Roho wa Mungu huhudumu katika mazingira. Hiyo ndiyo inavyomtambulisha Yeye. Mnaona ?
28 Roho ya Danieli ilipokuwa ikitenda upande ule, ilikuwa Babiloni. Na wakati Roho wa Danieli inapotenda leo, ni Babiloni pamoja na ikulu ya Nebukadneza, ambako kuna jengo la kidini la kifahari sana ulimwenguni. Na Danieli alizungumzia milki nne: milki ya Babiloni, milki ya Umedi na Uajemi, milki ya Wagiriki na milki ya Kirumi iliyokuwepo kama ilivyofunuliwa kwetu katika mahubiri: “Siri ya wale wanyama wanne uliyewaona".
29 Na katika Afrika…Nimekuwa nikisema daima ya kwamba Malkia wa Sheba mwenyewe hakuwa sehemu ya Afrika. Uthibitisho ni kwamba wakati Mungu anapowatembelea Waafrika, ni wakati huu ambapo Falashas, watoto wa Malkia wa Sheba wanarudi Israeli. Kwa hiyo Malkia wa Sheba hana uhusiano wowote na Afrika. Hakuna kuchanganyikiwa kwa Mungu.
30 Vema! Hebu tuangalie vizuri : malkia wa Sheba, huyu Mwethiopia anaenda kwa mtu mkuu zaidi wa wakati wake. Mwanzo 2:13 inasema kwamba Kushi yaani Ethiopia ilikuwa katika bustani ya Edeni na kupatwa kwa jua Machi 29 kuliipitia. Kushi ni Ethiopia, Mwanzo 10:6. Ethiopia ilipaswa kuwa na umaarufu duniani.
31 Sasa nini kilitokea kwa mwanamke huyu wa Kiethiopia? Na tena Ethiopia inarudi kwenye tukio pamoja na nabii Musa. Kuna mwanamke wa Ethiopia alimwendea Musa na ukafunuliwa upumbavu wa Haruni na Mariamu. Sulemani hakuwahi kumjali mwanamke huyu wa Kiethiopia hadi alipokuja kwake. Musa hakuwahi kumtilia maanani mwanamke huyu wa Kikushi hadi alipokuja kwake.
32 Vema! Narudi kwa Sulemani na Malkia wa Sheba. Vema! Biblia ni kitabu kilicho wekwa alama yasiri. Katika kitabu cha Mwanzo, Mungu alisema tunda wakati ni tendo la ndoa. Na Biblia inasema Malkia wa Sheba alikwenda kwa Sulemani kuona ukuu wake lakini ufunuo ni kwamba alikwenda kuona ukuu wa Sulemani mtu mwenyewe. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
33 Naye akapata mimba ya Mfalme Sulemani, na kutoka huko ukatoka uzao wa Falashas. Na inaonekana, Mwethiopia huyu alikuwa anaenda tu kuona ukuu wa nabii Musa. Na hawa Falashas walikuwa watu mashuhuri nchini Ethiopia kama Haile Selassie, lakini wasio na maana katika Israeli. Waisraeli hata hawawaangalii hawa Falashas kuwa ni Wayahudi kama wao.
34 Wakati huyu mwanamke wa Ethiopia anapoonekana katika Agano la kale la Musa, ni wale waliomwona shetani ndani yake ambao walianguka katika Hesabu 11. Walimwita "Ibilisi" Mwenyezi Mungu aliyemwongoza mwanamke Mwethiopia kwa Musa. Hii ndiyo sababu halisi ya kifo chao na iliendelea kwa Haruni na Miriamu katika sura inayofuata. Mnaona ? Walikua wamekwisha kasirika mbele ya mana ileile, joto, na kiu ya jangwa na Musa alipofanya hivyo, hawakuwa hata makini! Mnaona ? Lakini hilo halikuwapa udhuru kwa sababu lilikua taifa la Mungu, na walipaswa kumtambua Mungu kupitia hilo, waliona mkono wa Mungu na Neno la Mungu pamoja na Musa na walipaswa kumtambua Mungu kupitia hilo. [Kc.98v28] [Kc.127v25-30]
35 Kwa mfano tusome katika Kutoka sura ya 19 : “Na Mlima Sinai wote ulikuwa unafuka moshi, kwa sababu Bwana alishuka juu yake katika moto; na moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuru, na mlima wote ukatikisika sana. Na sauti ya tarumbeta ilipozidi kusikika, Musa akasema, na Mungu akamjibu kwa sauti.” Mnaona ? Na Mungu alimkumbusha Haruni jambo hili katika Hesabu 12.
36 Na mara mbili, Musa alibaki katika uungu na Mungu na malaika watakatifu na Biblia inasema kwamba hata wana wa Israeli hawakuweza kuutazama uso wake kwa sababu ya utukufu. Amina! Tusimame sasa kwa maombi.
Comments
Post a Comment