KACOU55 KUJITENGA NA KUTOKUAMINI


(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi, Agosti  07, 2005 Huko Locodjro, Abidjan - Ivory  Coast)

1 Asubuhi ya leo napenda kuzungumza juu ya mada: "Neno la Mungu linaamuru kujitenga na kutokuamini".Hebu tuchukue Bibilia zetu katika 2 Mambo ya Nyakati 19. Mfalme Yehoshafati alikwenda kwa Ahabu na wote wawili wakaenda vitani kuuchukuwa Ramoth-Gileadi na hiyo ilimalizika kwa kifo cha Ahabu. Tunaona hilo pia katika 1 Wafalme 22. 

2 Hebu tusome 2 Mambo ya Nyakati 19: 1-3 basi : "Na Yehoshafati mfalme wa Yuda alirudi nyumbani kwake, kwa amani, Yerusalemu. Na Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kwenda kumlaki na akamwambia Mfalme Yehoshafati, Je! Unawasaidia waovu, na unawapenda watu wamchukiao Bwana? Kwa sababu ya hilo, kuna gadhabu juu yako kutoka kwa Bwana. Mnaona?

3  Mfalme Yehoshafati alikuwa peke yake na Mungu lakini alitaka kushirikiana na mtu ili kumaliza upweke wake. Alikuwa amechoka na maisha yake ya kawaida. Alijua kwamba wafalme wa makanisa yaliyokuwa karibu walikuwa waabudu sanamu na maadui wakubwa wa Mungu. Lakini, alitaka hata hivyo rafiki na akampata Ahabu, mfalme pekee ambaye alikiri Mungu mmoja kama yeye. 

4 Lakini nini kilitokea? Mungu akamkasirikia Yehoshafati! Na nabii alipaza sauti: "Je! Unawasaidia waovu, na unawapendaje watu wanaomchukia Bwana? Kwa sababu ya hilo, kuna ghadhabu juu yako kutoka kwa Bwana ..." Mnaona? Unawasaidiaje Waovu? Unawapendaje watu wanaomkataa Yesu Kristo, Neno la wakati? Je! Yesu Kristo katika mwili alishirikiana na Mafarisayo waliokataa Ujumbe wake? Mnaona? Mungu alikuwa akitaka Yehoshafati awe na tabia ya manabii Watakatifu wa Mungu na ambayo huwaongoza kila mara milimani, mbali na wapinzani na maadui wa Mungu. Lakini mapenzi haya, Yehoshafati alikuwa hayaelewi.

5 Na hata kabla Musa hajatangaza amri, kusanyiko lilitakaswa kutoka kwa Kora na Dathani na Abiramu. Vivyo hivyo na Mitume, kabla ya Roho Mtakatifu kushuka, kusanyiko lilitakaswa kutoka kwa Yuda Iskariote na wengine. Na kabla ya sisi kuona utukufu, Yuda wote watatoka kati yetu. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

6  Hebu tuone mstari mwingine, 2 Mambo ya Nyakati 20: 35-37: "Na baada ya hayo Yehoshafati mfalme wa Yuda alijiunga na Ahazia mfalme wa Israeli, ambaye alifanya maovu sana. Akajiunga naye ili kufanya meli za kwenda Tarshishi; walitengeneza meli huko Ezioni-geberi. Na Eliezeri mwana wa Dodava, wa Maresha, alitabiri juu ya Yehoshafati, akisema: “Kwa sababu umejiunga na Ahazia, Yehova ameangamiza kazi zako.” Na meli zilivunjika, na hazikuweza kwenda Tarshishi. " Mnaona?

7 Mungu atuzuie tusijiunge na kanisa au mchungaji, mtume, mwinjilisti au mwalimu au mwingine! Jueni kwamba hawa waeshimiwa wote, hawa maaskofu wakubwa ulimwenguni, ni mashetani. Hawawezi kumtumikia Mungu isipokuwa waje hapa kwa unyenyekevu kubatizwa na kuwekwa wakfu na nabii Kacou Philippe. Hakuna Mungu mwingine nje ya Yesu Kristo na Kacou Philippe ndiye nabii wake pekee duniani. Na kila mwana wa Mungu anasema "Amina!" kwa neno hili. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"]

8 Na wakati mtakapoamini Ujumbe huu na mtakuwa wahubiri au wachungaji wa Ujumbe huu, msifanye ukahaba na makuhani wa mahali pa juu pa wakatoliki, waprotestanti, wa kiinjili na Wabranhamisti. Kaeni na Mungu! Kaeni na Neno lake! Haijalishi mateso, kaeni na Mungu na nabii wake! Kwa sababu nje ya nabii aliye hai wa wakati wenu, jueni kwamba ni njia ya upotevu! Bwana Yesu Kristo hakuteseka msalabani ili muwe Wakatoliki. Bwana Yesu Kristo hakuteseka msalabani ili muwe Waprotestanti. Bwana Yesu Kristo hakuteseka msalabani ili muwe wakiinjili, Wabranhamisti, Waislamu na wengine. Na vile Yeye ni yule yule jana, leo na hata milele, kama kila wakati, katika wakati wenu pia, atatuma nabii mmoja kama Nuhu ambaye mnapaswa kumuamini ili muwe na Uzima wa milele. Na tegemeo la nabii huyu litakuwa Mungu Muweza wa yote aliyemtuma. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"]

9 Jueni kwamba tegemeo langu sio Musa au Yesu Kristo wa Nazareti, au nabii mwingine wa Biblia. Bwana Yesu Kristo anaweza kunitokea katika maono au ndoto kama vile Musa na Eliya walivyomtokea wakati wa huduma yake lakini hiyo haiwaweki Musa na Eliya juu yake. Kila nabii ndiyo ukweli katika wakati wake. Mnaona?

10 Vema, Bwana Yesu Kristo alikuwa na awamu mbili katika huduma yake. Kwanza, alikuwa Mwana-kondoo wa Mungu na kupitia dhabihu yake msalabani, aliwaokoa wanadamu wote, pamoja na nyinyi na mimi ninayeongea nanyi. Yohana Mbatizaji alisema: Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aondaye dhambi za ulimwengu . Lakini mwana-kondoo hayuko juu ya kuhani anayemchinja, wala juu ya yule mwenye dhambi ambaye amechinjwa kwa ajili yake. Pili, Bwana Yesu Kristo alikuwa na huduma ya kinabii kama yangu wakati wake. Bwana Yesu Kristo sio nuru yangu. Alikuwa tegemeo na nuru ya watu wa wakati wake kama mimi, Kacou Philippe, niko tegemeo na nuru ya watu wa wakati wangu. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"]. Na leo, nina funguo za Ufalme kama vile alivyokuwa na funguo za Ufalme wakati wake miaka 2000 iliyopita.

11  Katika Ufunuo 1:18, Alisema: "Nina funguo za mauti na za kuzimu, makao ya wafu". Lakini funguo za Ufalme ziko wapi? Funguo za Ufalme ziko duniani na mwanadamu. Kabla ya kuondoka duniani, alimwambia Petro: "Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbingu". Tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu, funguo za Ufalme wa Mbinguni ziko duniani kila wakati na mtu, na leo mtu huyo, ni mimi, mimi ninayesema nanyi. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

12 Leo, katika karne hii ya 21, hakuna mtu anayeweza kuokolewa isipokuwa kupitia mimi, nabii Kacou Philippe anayezungumza nanyi. Na Yohana 3:16 leo ni: Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa nabii wake mpendwa, Nabii Kacou Philippe, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na Uzima wa milele. Bwana Yesu Kristo alikuwa mtu kama mimi ninayeongea nanyi leo na hamuwezi kudhani kuwa mgemwamini Yesu Kristo wakati alikuwa duniani ikiwa amniamini mimi leo. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

13 Na kiburi na ukubwa wa kibinadamu na yale yote yaliyowazuia Wayahudi kumwamini, ndiyo yanayowazuia kuniamini, nabii Kacou Philippe, nabii aliye hai wa wakati wenu. Bwana Yesu Kristo alikuwa mtu kama mimi ninayeongea nanyi. Na hamuwezi kudhani mgemwamini Yesu Kristo au mmoja wa manabii wa Biblia ikiwa h amniamini mimi, nabii Kacou Philippe ninayezungumza nanyi leo. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

14 Vema! Sasa sikilizeni hii: Musa na Bwana Yesu Kristo wanawakilisha picha moja. Musa kwa Agano la kale, Musa mwanzilishi wa Agano la kale. Na kwa upande huu kwa Agano jipya, Bwana Yesu Kristo. Wote wanawasilisha picha moja. 

15 Musa aliwakomboa Wayahudi wote kutoka Misri kwa kulipa malipo kwa Farao lakini nionyesheni jina la Musa katika vitabu vya manabii.  Nionyesheni mahali ambapo manabii Yeremia, Isaya, Amosi na wengine wanahubiri Musa! Nionyesheni mahali ambapo manabii hawa wanarudia kile Musa alisema au kutoa maoni juu ya kile Musa alisema!

16 Mtumishi wa Mungu leo hatakuja kutoa maoni juu ya Biblia, kuhubiri Biblia lakini atahubiri kile ambacho Mungu amempa nabii aliye hai wa wakati wake. Kwanza, Musa hasemi juu ya Nuhu kwa sababu yeye si mwanafunzi wa Nuhu. Hakuishi wakati wa Nuhu. Historia ya Nuhu haimhusu Musa. 

17 Kwa nini Yeremia, Isaya na manabii hawasemi juu ya Musa? Kwa sababu Musa, ni wa wakati mwingine. Musa alikuwa na wanafunzi wake, Musa alikuwa na historia yake, na Isaya, Yeremia na manabii wengine wa Biblia hawawezi kuokolewa pamoja na Musa.

18 Ni vile vile kuhsusu Bwana Yesu Kristo. Bwana Yesu Kristo alikuwa na mitume wake mwenyewe: Petro, Yohana, Yakobo. Walikuwa watu wenye nguvu wakati wao na nabii wao, alikuwa Bwana Yesu Kristo ambaye aliwaita. Na baada ya Bwana Yesu Kristo, tunaona Paulo aliyewaita Timotheo, Tito, Swilano na kadhalika. Na leo tuko wakati wa nabii Kacou Philippe. Na ikiwa wewe ni mtumishi wa Mungu, hiyo inamaanisha kwamba umeitwa na nabii aliye hai wa wakati wako, yaani nabii Kacou Philippe. [Mh: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

19 Huwezi kumtumikia Mungu kabla ya kubatizwa na kuwekwa wakfu na nabii Kacou Philippe. Ondoa kiburi chako, nyenyekea na njoo hapa kwa sababu huwezi kuokolewa nje ya nabii Kacou Philippe. Nuhu kwa wakati wake, Isaya kwa wakati wake, Yeremia kwa wakati wake, Bwana Yesu Kristo kwa wakati wake, Paulo kwa wakati wake, Wesley kwa wakati wake, Martin Luther kwa wakati wake na leo, nabii Kacou Philippe kwa wakati tunaoishi. Na kwa ajili ya maono ya Aprili 24, 1993, hiyo haiwezi kushindwa, duniani kama Mbinguni. Amina. Isaya, Yeremia, Amosi, na wale wote hawawezi kusema juu ya Musa kwa sababu hawakumjua Musa.

20 Leo hamuwezi kusema juu ya Bwana Yesu Kristo kwa sababu hamkumjua Bwana Yesu Kristo. Lakini yule mnayemjua ni nabii Kacou Philippe. Na siku ya hukumu, wakati mtakapomwona nabii Kacou Philippe, mtamtambua kama yule ambaye alikuwa akiwagombanisha duniani.

21 Isaya na Yeremia sio wanafunzi wa Musa lakini ni manabii kama Musa. Na mimi, nabii Kacou Philippe ambaye ninazungumza nanyi, mimi si mwanafunzi wa Musa, wala mwanafunzi wa Yesu wa Nazareti au mwanafunzi wa mmoja wa manabii wa Biblia ili nifuate Bibilia, lakini mimi ni nabii mjumbe kama wao.

22 Mko huru kunikataa lakini mjue kwamba, leo, haijalishi wewe ni nani, Kacou Philippe ndiye nabii wako. Muwe Wakristo, au Wayahudi, Waislamu, Wabudhai au wengine, Kacou Philippe ndiye nabii wako. 23 Iwe wewe ni papa wa Roma au rabi katika Israeli au mfalme au rais, Kacou Philippe ndiye nabii wako. Mue ni Waafrika, Wazungu, Waamerika au Waasia, Kacou Philippe ndiye nabii wanu. [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"]. Na ni Mungu Mweza wa yote mnaye fikiri kumwabudu ndiye anayezungumza nanyi kupitia Nabii Kacou Philippe. Mungu aliyekuwa akisema Mbinguni, juu ya Israeli, alikuwa ni yule yule aliye kuwa akitembea na kusema duniani kupitia bahasha ya mwanadamu iitwayo Yeremia na Wayahudi hawakuelewa.

24 Na kuzungumza kwa mfano kuhusu matukio ya Musa na mwanamke Mwethiopia, Kora na Dathani walisema na Miriamu: "Inatosha! Mwanamume ambaye hawezi kudhibiti jinsia yake hawezi kuwa nabii wetu". Na bado, Musa alikuwa zaidi ya nabii kama Kacou Philippe alivyo leo zaidi ya nabii. 

25 Na ninyi viongozi wa dini, watu wenye ndimi zilizogawanyika, hamwezi kuelewa hilo kwa sababu ninyi ni waovu wa dunia. Kama katika wakati wa Nuhu, unalazimika kumwamini nabii Kacou Philippe ili kuokolewa. [Mhr: Kusanyiko linasema, “Amina!”].

26 Sasa nina swali: Nabii Kacou, mnamo Mei 7, 1946 jioni, malaika, na kwa sauti ya kusikika, alimwambia William Branham, "Kama vile ishara mbili alipewa Musa, wewe pia umepewa ishara mbili. Kwa hivyo wewe Nabii Kacou Philippe, ni ishara gani ambayo Mungu alikupa, ambayo kwayo tutaamini? "

27 Vema, swali hili linaonyesha jinsi wanadamu wote wako katika kutokuamini na giza la Shetani. Angalia kwamba alikuwa Musa aliyemuomba Mungu ishara hizo kwa sababu ya kutokuamini kwa Israeli. Katika Kutoka 4, Musa alikuwa amemwambia Mungu, "Tazama, hawataniamini, wala hawataisikiliza sauti yangu" na kwa kuitikia hii Bwana akampa ishara mbili. 

28 Wayahudi walikuwa Wamisri na Wapentekoste, walizoea wachawi na ilikuwa njia pekee ya kuwatenganisha na kutokuamini. Vinginevyo, haikuwa katika mapenzi kamili ya Mungu. Lakini baada ya ishara hizi, nini kilifuata? Wote walikufa jangwani.

29  Na kwa upande huu, wakati William Branham alipokuja, ilikuwa ni jambo lile lile, walikuwa Wamisri na Wapentekoste na leo, wamerudi kwa imani yao ya Pentekoste, wakitafuta ishara na kubeba masalio ya nguzo za moto kama Wakatoliki. 

30 Lakini hapa, kuna watu walisema, "Hatuna haja ya kuona au kusikia umeme na ngurumo na hatuhitaji kuona ishara, lakini tunaamini kabisa." Amina! Ni ishara gani ambayo watu hawa wanahitaji kuamini? Kutoa ishara kungepingana moja kwa moja na maono ya Aprili 24, 1993.

31  Nami nawambia , hakika, watu hawa, hapa usiku wa manane, ni bora kuliko hao Wamisri-Wayahudi mbele ya Musa. Watu hawa, hapa usiku wa manane, ni bora kuliko wale Wapentekoste mbele ya William Branham. Ubranhamisti ni Upentekoste, na walirudi kwenye Pentekoste na imani yao ya kitume, wakiwa wamebeba picha za nguzo ya moto. William Branham ni nabii wa kweli lakini Wabranhamani ni watoto wa shetani. Ni kama Biblia na Ukristo. Lakini kwa upande huu, ni imani ya kinabii, imani ambayo inasema, "Hatujaona, hatujasikia lakini tunaamini kabisa." [Mhr: Kusanyiko linasema, "Amina!"].

32 Na Bwana Yesu Kristo aliiona siku yangu, siku ya nabii Kacou Philippe, na kushangilia kwa furaha na kusema, "Heri ninyi mnaoamini bila kuona au kusikia!". Hii ni imani ya kinabii na ni imani kamilifu na imani ya unyakuo. 

33 Mumeamini bila kuuliza ishara kwa sababu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ulikuwa umekusudiwa hiyo na uliidhihirisha katika maono na sasa unadhihirisha hiyo hapa duniani. Sio kwa sababu ulikuwa na busara na akili lakini ni Mungu Mwenyezi ambaye alifanya hivyo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

34 Hebu tuinuke na kumpa utukufu kwa hilo! Haleluya! Haleluya! Pentekoste ni imani ya kitume, ni imani inayoona kabla ya kuamini. Na hii haiwezi kuwa imani kamili. Lakini Mungu alikuwa ameamua mapema imani kamilifu ambayo ni imani ya kinabii na tunafurahi kuishi imani hii ya kinabii. 

35 Imani ya kitume inasema, "Je! Ni ishara gani unayonipa ambayo kwahiyo lazima niamini?" lakini imani ya kinabii inasema, "Hatujaona, hatujasikia lakini tunaamini kabisa". Na hata katika shida, magonjwa, mateso na hata kifo, wana wa Mungu huweka msimamo wao kwa sababu ya imani ya kinabii. Na yule anayeweza kuelewa, na aelewe!

Sura zinazofanana Kc 20, Kc26

Comments