KACOU 25: KWA NINI WANAWALI KUMI KATIKA MATHAYO 25:6
(Ilihubiriwa Alhamisi jioni, November 23, 2006 huko Adjame, Abidjan- Ivory Coast)
1 Wakati nabii mjumbe yuko duniani, ni meza ya harusi na Ufalme wa Mbinguni unaorudi duniani. Na huwezi shiriki katika meza ya harusi huko Mbinguni isipokuwa umeshiriki katika ile inayofanyika duniani kandokando ya nabii mjumbe wa kizazi chako. Na huwezi kuingia kupitia lango la mbinguni, na kuketi kwenye meza ya harusi, isipokuwa umeingia kupitia lango ambalo nabii mjumbe ana funguo zake duniani.
2 Ndugu zangu, naendelea kusema kwamba siku inakuja ambapo wana wa Uislamu na wana wa Ukristo watakumbatiana duniani. Kama Esau na Yakobo, wana wa Isaka na wana wa Ishmaeli watafurahi pamoja. Hayo ndiyo wanayoyangojea wanadamu na yatatokea… Na tunapoona kwamba washambuliaji hao wa kujitoa muhanga hawaogopi kufa kwa ajili ya uwongo, unajua kwamba, kile ambacho Mungu amesema lazima kitokee, kuhusu watoto wao ambao watachoma kurani mbele ya misikiti yao, itafika. [Kc13v3]
3 Uislamu utatikiswa kutoka kifuani mwake mwenyewe na kwa wanawe kwa Jina la Mwenyezi Mungu. Watahubiri dhidi ya Uislamu, Ukristo na Uyahudi. Na ni wakati huo ambapo mateso ya mwisho ambayo Kanisa linangoja yataanza na itakuwa hivyo na ni kwa sababu ya saa hiyo Mungu ameruhusu kusimama na kukipa umaarufu mkubwa kitabu ambacho kinaitwa “kurani takatifu”.
4 Ukristo unasonga mbele kama njia ya jua na hautarudi nyuma kamwe. Mnaona? Asia kisha Ulaya kisha Amerika, rangi baada ya rangi, bara baada ya bara… lakini kumbuka kwamba Mungu anapomaliza kuvuna wana wa Ufalme katika nchi, imekwisha. Mengine, ni makuzi ambayo yatavunwa wakati wa hatua inayofuata ya Mungu duniani. Mnaona?
5 William Branham alipokuwa akifanya kazi, Amerika ilikuwa ikichemka lakini Ulaya ilikuwa ya kidesturi karibu kutojali na haikuweza kufanya lolote. Mungu alipaswa tu kukumbuka uzao wa John Wesley, Martin Luther, Whitefield, John Calvin na wengine wengi.
6 Ndugu, jueni kwamba nabii mjumbe kamwe hatainuka tena kutoka Ulaya. Mnaona ? Unapotengeneza shamba la ngano au mchele, kuna machipukizi tena baada ya mavuno. Ndivyo ilivyotokea kwa Asia wakati Mungu alipokuwa akishughulika na Ulaya. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Ulaya wakati Mungu alipokuwa akishughulika na Amerika. Na ndivyo inavyotokea kwa Amerika na Ulaya leo. Huduma ambayo Mungu atabariki Ulaya au Amerika au Asia leo ndiyo itakayochukua Ujumbe wa Kelel ya Usiku wa manane ili kuvuna machipukizi kutoka Ulaya, Amerika na Asia. Amina! Na sasa mnaona kwamba Afrika inazidi kuwa bara moto zaidi la Ukristo.
7 Mungu awabariki! Vema! Jioni ya leo ningependa kuzungumza juu ya mada: Kwa nini idadi ya wanawali wa Mathayo 25 ni kumi ? Mnaona? Kwa nini mabikira kumi kwa ajili ya Bwana? Hilo ndilo ningependa kulizungumzia sasa. Kwa nini wanawali kumi? Je, huu ni mfano wa Bibi-harusi wa Kristo kutoka mataifa yote kama aina ya Sulemani na Daudi inavyoonyesha waliooa wake wengi? Hapana! Sio hivyo.
8 Je, hawa ni wanawali mabikira wanaoandamana na Bibi-harusi kama inavyoonekana katika Esta 2:9? Hivyo ndivyo nilivyofikiri kabla ya ufunuo kuja. Nilidhani kwamba ni kwasababu walitoka kwa mataifa yote. Na mwanatheolojia mzuri anaweza kufundisha hivyo na kwa sababu ya sifa na umaarufu wake, watu wataamini. Wanafundisha chochote chenye mantiki kwao na dunia inawasikiliza kwa sababu ni mantiki.
9 Lakini mtu ye yote ambaye Mungu humtuma, husema Maneno ya Mungu. Mnaona ? Nilipokuwa shuleni, niliweka bidii yangu yote katika mazoezi na kazi za nyumbani ambazo mwalimu alitoa na nilitarajia kupata alama nzuri. Lakini, marekebisho yalipofika, nilisikia: "Kacou Philippe, una sita kati ya ishirini!". Na hilo lilinifanya kuwa na hekima na ufahamu kwa mambo ya Mungu. Kwa maana ikiwa basi katika mambo ya wanadamu sikushinda, si katika mambo ya Mungu kwamba nitashinda kwa ufahamu wangu.
10 Vema! Hebu turudi kwenye kifungu chetu kutoka Mathayo 25:1… Kwa nini mabikira kumi? Sikulijua hilo hadi siku nne zilizopita na ikiwa kuna mtu ambaye alilizungumzia mahali fulani, sijui. Na kama kawaida, ninalifundisha hadharani kabla sijajua kile ambacho mtu yeyote anaweza kufikiria kulihusu.
11 Vema! Sasa na tusome Mathayo 25, mstari wa 1 pekee: “Ndipo Ufalme wa Mbinguni utafanana na wanawali kumi ambao, walizitwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki Bwana-Harusi.
12 Ningependa kubainisha kwamba kutokea wakati wa mitume Bibi-Harusi alipoanza hadi siku zetu, kamwe hakukuwa wanawali wawili au watatu kwa Bwana wetu bali mmoja tu. Paulo hasemi katika 2 Wakorintho 11:2 kwamba alituchumbia kama wasichana bikira kwa Kristo bali kama msichana mmoja, Bibi-harusi mmoja kwa Kristo. Lakini hapa kama katika siku za Yoshua, Israeli wa kiroho anaonekana akiwa amegawanishwa, kila mmoja katika kundi lake, ningesema: kila mmoja katika kundi moja. Tangu wakati wa Yusufu hadi Musa, kamwe Israeli haikugawanyika lakini wakati wa Yoshua hilo lilifanyika, Israeli iligawanyika. Kanisa lilitambulishwa na msichana mmoja hadi usiku wa manane nabii aliwaona wanawali kumi waliokomaa. Na anasema, Ufalme wa Mbinguni utafanana na wanawali kumi...”. Katika siku za usoni. Hiyo ni kusema, siku itakuja ambapo Bibi-harusi Kanisa atatokea kama mabikira kumi. Na hiyo inapaswa kuwa tu wakati wa ukomavu. Amina! Ni hivyo.
13 Vema! Baada ya Musa, kulikuwa na Yoshua na mfano wa pili ulio karibu nasi zaidi ni ule wa Eliya na Elisha. Mnaona ? Musa na Yoshua, Eliya na Elisha hatimaye William Branham na Kacou Philippe. Tatu ni kamilifu. Musa, Eliya na Branham. Joshua, Elisha na Kacou Philippe. Ni kamili na kila kitu ni sawa. Angalieni katika Biblia na mtaona kwamba hakuna mchanganyiko, hakuna machafuko ndani yake. Wala hakuna mchanganyiko kwa yule anayengoja kwake kama mtoto.
14 Biblia na manabii hutuonyesha kwamba Mungu kutokuwa na makosa dhidi ya wanadamu daima ni kupitia mwanadamu aliye hai duniani, na ikiwa ni yeye yule jana, leo, na hata milele, yale aliyoyafanya katika Agano la kale, anaweza kuyafanya vivyo hivyo leo. Na hakuna anayeweza kuwa bila makosa isipokuwa amengojea kwanza ufunuo kutoka kwa Mungu kwa sababu ni Mungu pekee ndiye asiyefanya makosa.
15 Bwana Yesu Kristo ambaye yeye mwenyewe ni Mungu aliyedhihirishwa katika mwili alisema, "Sifanyi jambo lolote isipokuwa nimwone Baba analifanya kwanza." Na ukamilifu na mapenzi kamili ya Mungu na kutokukosea ni matunda ya: "Sifanyi neno wala kusema neno ambalo sioni Baba akilifanya kwanza...".
16 Hilo ndilo jambo pekee ambalo Mungu anaweza kutambua. Na haya yote hayawezi kufanyika pasipo uvumilivu. Mungu hafanyi lolote bila subira. Bwana Yesu Kristo Mwenyewe angeweza kuanza huduma Yake akiwa ba umri wa miaka kumi na miwili, lakini Alingoja hadi miaka thelathini. Na kutoka miaka kumi na miwili hadi miaka thelathini ilipita miaka kumi na minane. Na kutoka 1993 hadi 2002, hiyo ni miaka tisa. Mnaona? Kwa hivyo, ikiwa unapokea wito na shuguli yako haisitawiwi, na kwamba unahisi msukumo, mganga wa kienyeji ndiye aliye na nafasi nzuri kukuelezea kuwa ni pepo tu ndiye aliyeweka mkono wake juu yako. Mnaona?
17 Vema! Sasa tuchukue 2 Wafalme 2, tukizungumzia Eliya na Elisha... Eliya alikuwa na huduma iliyobarikiwa baada ya huduma hiyo alinyakuliwa katika kundi la malaika. Na aina ya huduma hii ilikuwa ya mwisho ambapo Kanisa la kiroho la Israeli liliunganishwa kikamilifu katika roho na mwili. Pia ilionekana kwamba mtu huyu angeweza kushusha moto kutoka mbinguni katika 1 Wafalme 18 ... kwamba mtu huyu angeweza kuita moto kutoka mbinguni kuteketeza makumi ya wanadamu, kwamba angeweza kufanya mvua inyeshe, kuumba, kufufua. Kulikuwa na kutosha kuweka heshima na umoja, ngano na magugu na zaidi ya yote Bibi-harusi Kanisa katika bikira mmoja.
18 Lakini zaidi ya hayo, hivyo ndivyo Roho alivyowafanya watende. Hivyo ndivyo kipindi cha Roho kiliwapa kufanya. Mnaona ? Hakukuwa wanawali watano au kumi kukutana na Bwana-harusi, bali bikira mmoja tu. Amina! Ikiwa hamuoni au hamuelewi ninachosema, angalieni huduma iliyo karibu zaidi ya aina ya Eliya na Musa, huduma ya William Branham.
19 Wakati William Branham alikuwa akihubiri, hapakuwa na kusanyiko kutoka mtaa huu au ule wa Jeffersonville na hata wale waliokuwa katika miji ya mbali sana waliunganishwa naye kwa simu wakati wa mahubiri. Na mnaona kwamba mwelekeo wa kweli wa kibranhamisti machoni pa Mungu, yaani, ule ulio upande wa Ewald Frank bado unnaitunza roho hii; katika mji mmoja, wana kusanyiko moja tu...si hapa tu bali ni duniani kote.
20 Lakini Elisha alipoanza huduma, wana wa manabii walikuja kushujudu mbele yake. Biblia inasema, “Na wana wa manabii waliokuwako Yeriko, ana kwa ana, wakamwona, na wakasema, Roho ya Eliya ijuu ya Elisha. Nao wakaenda kumlaki, wakamsujudia, na wakamwambia hili na lile…”
21 Roho yoyote inayoweka haja ya usitawi na mashindano juu ya wokovu wa nafsi ni ile ya Gehazi na ni katika enzi ya Elisha kwamba alitenda na uso usiofunikwa. Nami nawaambieni kwamba wana wa nabii wote katika siku za Eliya walikuwa wamemwamini Eliya na walikuwa mwangwi wa Eliya wakati Eliya alikuwa duniani. Biblia inawaita wana wa manabii.
22 Lakini, mwana wa nabii yupi? Wa nabii Eliya, nabii wa wakati wao. Walikuwa wana wa nabii Eliya. Nao walikuwa na ufunuo wa Eliya alikuwa nani na kisha Elisha alikuwa nani, na Biblia inasema kwamba walikwenda na kusujudu mbele ya Elisha. Kwa nini? Kwa sababu walikuwa na roho mmoja. Nabii wa kiinjili kamwe hangefanya hilo kama leo hawawezi kufanya hivyo kwa sababu hatuna Roho Mtakatifu mmoja.
23 Sasa turudi kwenye andiko letu. Tambueni kwamba wana wa manabii hawa walikuwa katika roho moja na Eliya. Walikuwa wana wa nabii Eliya. Walikuwa wana wa nabii Eliya. Amina! Hebu tusome hilo: “Na watu hamsini kati ya wana wa manabii wakaenda na wakasimama ana kwa ana, kwa mbali; na hao wawili walisimama karibu na Yordani. ". Amina!
24 Kwa Yoshua kulikuwa na wanawali kumi na wawili na hesabu kumi na mbili ilihusiana na makabila kumi na mawili ya Israeli. Hapa inazungumzia kuhusu tano kuashiria neema ambayo kwayo aliokolewa. Hapo mwanzo, kundi lote la Musa lisiloamini lilianguka jangwani. Na kutoka kwa Bibi-harusi wa Kiyahudi walionekana kuwa wengi… na tano ni nambari ya neema kama herufi tano za Yoshua. Na kama Vashti, Wabranhamisti walianguka na Esta alichaguliwa kwa neema kama herufi tano za Hegai.
25 Kwa hiyo hakuna makusanyiko kumi bali kundi mbili za wanawali. Wanawali tano katika kila kikundi kama inavyoonyeshwa katika Wimbo Ulio Bora 6:13. Na haya yote yanaonyeshwa waziwazi katika Ezekieli 1:16 inayosema, “Na kuonekana na muundo wa magurudumu ulikuwa na mwonekano wa krisoliti; kulikuwa na kufanana kwa hizo inne, na sura yao na muundo wao ulikuwa kama gurudumu lililokuwa katikati ya gurudumu. " Mnaona?
26 Angalieni hili: "... sura yao na muundo wao ulikuwa kama gurudumu lililokuwa katikati ya gurudumu." Kuna makusanyiko tano na sura na muundo wao ulikuwa kana kwamba bikira mmoja alikuwa ndani ya bikira. Kwa hiyo si makanisa kadhaa yanayoamini mambo tofauti, bali ni kanisa Bibi-harusi mmoja duniani. Na Kanisa-Bibi-harusi huyu ni watakatifu wote waliokusanyika kandokando ya nabii mjumbe aliye hai wa wakati wao. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. Ni Bibi-harusi Neno!
27 Ndiyo maana anaamini katika Neno linalotoka kwa Mungu na si katika theolojia au mawazo ya wanadamu. Kwa hiyo si suala la Wakatoliki ambao ni makahaba, la Waprotestanti ambao ni makahaba, la wakiinjili ambao ni makahaba, la Wabranhamisti ambao ni makahaba, bali wa Kanisa la kweli linalotembea pamoja na nabii mjumbe katikati yao.
28 Mungu ni Roho na nabii aliye hai ni nafsi na tumbo la uzazi, na Kanisa lililo hai ni mwili. Nje ya nabii mjumbe aliye hai duniani, hakuna Mungu na hakuna Wokovu. [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. Makanisa yote bila tofauti yatashirikiana duniani na makanisa ya mashoga na yataketi pamoja na wanasiasa, na viongozi wa ulimwengu huu. Lakini kuna kanisa moja ambalo litakuwa limejitenga daima, ni lile la Bwana Yesu Kristo, na huwezi kuokolewa mbinguni kabla yakuwa mmoja wa kanisa hili duniani.
29 Kwa hiyo wanawali kumi si Bibi-harusi kumi au makanisa kumi tofauti duniani, bali ni Kanisa moja lenye vipengele viwili. Wanawali watano wapumbavu ni watakatifu waliomtambua Mungu kwa wakati wao lakini ambao mioyo yao imegeuzwa kuelekea hisia tano za mwili au mambo ya mwili wakati wanawali watano wenye busara ni watakatifu wa hilohilo kanisa bibi-harusi lakini wenye mioyo inayoelekea kwenye mambo ya kiroho.
30 Sasa ninakuja kwenye namba kumi. Kwanza, namba 5 ni neema ya Wokovu na namba 10 ni neema maradufu ya Wokovu. Neema ya wanawali watano wenye busara kwa Wokovu kupitia unyakuo na neema ya wanawali watano wapumbavu kwa Wokovu kupitia dhiki. Na aliye na masikio ya kusikia asikie!
Comments
Post a Comment