KACOU 24: UFUNUO JUU YA MTI WA UZIMA

 

(Ilihubiriwa jumapili asubuhi, August 21, 2005 huko Locodjro, Abidjan –Ivory Coast)

1 Vema!  Ningependa asubuhi hii nionyeshe kwa usahihi zaidi kile ufunuo ulikuwa juu ya mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya .  Mnaona?  Ninataka kueleza kile Musa alichoona... Na kile Mungu alikuwa anazungumzia  alipoongea  na Adamu...

2 Hebu tusome kwanza Mwanzo 3:22-24 “JEHOVA Elohim akasema, Tazama, mwanadamu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya;  na sasa, asije akaunyosha mkono wake, akatwaa pia matunda ya mti wa Uzima, akala, akaishi milele...! Na JEHOVA Elohim akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.  Alimfukuza Mwanadamu;  akawaweka makerubi, na mwali wa moto wa upanga unaowaka, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, wailinde njia ya mti wa uzima.

3 Hebu tuombe… Bwana Yesu Kristo, bariki wakati huu!  Hakuna piano hapa, hakuna zulia hapa, hakuna kwaya, hakuna feni au kiyoyozi, mahali ni padogo sana kututosha lakini hapa kuna Neno la Mungu lililoahidiwa kwa wakati huu na wote walio hapa asubuhi ya leo waelewe. Ni!  Kwa sababu una uwezo wa kufanya hivyo!  Amina!

4 Vema!  Wakati Mungu alikuwa anazungumza na Adamu  hiyo siku ilikuwa katika Mwanzo 2:16, akimwambia asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, Hawa hakuwepo na Adamu alikuwa vile tutakavyokuwa katika mileniamu.  Kila kitu kilikuwa kizuri na  usawa.  Na Adamu alikuwa Mungu na Adamu aliishi katika hali ya kiroho na kimwili.

5  Adamu alikuwa ameona kwa macho yake ya kiroho jinsi miti hii miwili ilivyokuwa na alikuwa na tafsiri yake, lakini baada ya kuanguka, makerubi waliwekwa pale wakiwa na panga ya mwanga unaowaka yaligeuka huku na kule ili kumzuia asiiendee.  Mnaona?  Dhambi ilimfanya Mungu aanze kumtendea Adamu kana kwamba hakuwahi kumjua kamwe. Na jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba miaka elfu mbili baadaye, makerubi hawa hawangemruhusu nabii Musa kuukaribia mti wa Uzima au kuuona.  Musa alisimama mbali sana… Vema!  Musa, nabii wa sheria, alikuja mbele akiwa na damu ya fahali na mbuzi juu yake.

6 Eh,  maskini Musa!  Alitaka kusonga ili aone ni nini kilihusu, lakini wale makerubi wakamlilia kwa sauti kuu, “Acha!  Acha Musa!!!  Musa akasimama mbali, akalia.  Je! Musa alikuwa amelia alipoona makerubi wakiwa na panga zinazozunguka?  Ndio ndugu, amini tu!  Kwa nini?  Kwa sababu ubinadamu uliangamizwa.[ Kc 23v9]

7  Lakini miaka elfu mbili baada ya Musa, dhabihu ilitolewa kupitia Bwana Yesu...Na katika kisiwa cha Patmo, Yohana ambaye alikuwa mjukuu wa mjukuu wa Adamu alikaribia na makerubi walipomwona, akasema: “Mimi ni Yohana. , mjukuu wa mjukuu wa Adamu na mimi ni nabii wa ukoo wa Musa.  Naja, si kwa damu ya fahali, mbuzi, bali kwa damu ya Bwana Yesu… [Mh: Kusanyiko linasema, “Amina”] Mnaona?  [Kc23v2]

8 Yohana hakuja na damu ya wana-kondoo na mbuzi kama Waislamu, bali alikuja na damu ya hali ya juu, damu ya Mungu, damu ya Mwana-Kondoo wa Mungu.  Na mmoja wa kerubi akamwambia kama sauti ya ngurumo: "Njoo uone!  ".  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina”].  Naye Yohana akasema, “Kisha akanionyesha mto wa maji yaliyo hai, unaong’aa kama bilauri, ukitiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo.  Katikati ya njia yake, na ule mto, na huko na huko, ulikuwapo mti wa Uzima, uzaao matunda kumi na mawili, wenye kuzaa matunda yake kila mwezi;  na majani ya mti huo ni ya uponyaji wa mataifa."  Ufunuo 22:1-2.  Mnaona?  

9 Mti huu ni Bwana Yesu Kristo aliyezaa matunda kumi na mawili, yaani wale mitume kumi na wawili.  Tunaona hile mwanzo, katikati na mwisho wa Biblia.  Na katikati ya Biblia, Yuda Iskariote alikuwa ni uwakilishi wa mti wa ujuzi wa mema na mabaya karibu na Bwana Yesu. 

10 Sasa jueni kwamba Yohana alisimama karibu sana na ule mti, karibu sana na kile kiti cha enzi, karibu sana na mto hata hakuweza hata kuyaona yale matawi manne tena kama Musa avyoyazungumzia katika Mwanzo 2:10-14 yaani, Injili nne.  Alipita zaidi ya matawi manne ya Injili.  Hizi si Injili nne bali ni vipengele vinne vya Injili moja.  Musa alisimama mbali sana hata akaona matawi manne tu, mbali, nje ya madhabahu na patakatifu, nyuma ya makerubi pale!

11  Matawi haya manne, Adamu angeweza kuyafikia, Musa angeweza kuyafikia, Wabaptisti na Wabranhamisti wangeweza kuyafikia, hata Wakatoliki wangeweza kuyafikia.  Inamaanisha nini?  Ilikuwa ni ukumbi wa ndani wakati Edeni ilikuwa ukamilifu, yaani uwepo wa Mungu.  Edeni palikuwa patakatifu sana. 

12  Alichokua akikifanya Haruni duniani na damu ya mafahali na mbuzi kilikuwa ni mfano wa kiduniani tu isipokuwa ni damu ya Bwana Yesu Kristo Mwenyewe.  Namaanisha wakati Haruni alikua akiingi mahali patakatifu sana, ilikuwa ni kwa ajili ya siku za kuja ambapo damu ya Yesu ingemwagika.  Je, mnaelewa hili?  Nina imani kwamba Roho yule yule aliye hapa itaongoza huduma nne ili kueleza  haya yote.  Amina!

13 Na sasa, hebu tuchukue matawi haya manne;  Ni Injili gani inayolingana na kila moja ya mito hii kwenye Mwanzo 2:10-14?  Hebu tusome hivyo!… “Mto ukitoka katika Edeni ili kuimwagilia bustani, na kiisha unagawanyika na kuwa mito minne.  »

14 Tuweni makini sasa!  “Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu.  Na dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri;  hapo kuna bedola na jiwe la shohamu".  Ni kitabu cha Mathayo, ni simba.  Amina!  "Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi."  Kushi ni Ethiopia, hii ni Injili ya Marko.  Amina! 

15 "Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaotiririka kwenda Ashuri."  Na Ashuri ni Babeli ambayo ilikuja kuwa Babeli, ni ufalme na sura ya mwanadamu.  Ni kitabu cha Luka.  Amina!  "Na mto wa nne ni Frati."  Na hapa kuna Injili ya Yohana na Ufunuo.  Na anaposema, “Mto wa nne ni Frati” hasemi chochote.  Mnaona ?  Amina!

16 Vema !  Sasa tukirudi kwenye Ufunuo 22:1, Yohana aliwaza moyoni mwake, “Ikiwa huu ndio mti wa uzima,  Nitaangalie upande wa pili maana mti wa ujuzi wa mema na mabaya haupaswi kuwa mbali.” .  Ndiyo, mti huo ungeweza kuwepo lakini dhambi ilipotokea, Mungu aliukata. 

17 Kama vile Mungu alivyomkata nyoka, uwakilishi wake katika bustani ulikatwa.  Dhambi ilipotukia, Mungu aliukata katika Edeni, mti huu uliokuwa na sura ya mti wa asili na ambao ulikuwa karibu na mti wa Ufunuo 22. Kabla ya Mungu kutoa dhabihu, mti huu ulikatwa.  

18 Vivyo hivyo, kabla ya dhabihu ya Yesu kutolewa kwenye msalabani wa Golgotha, Mungu alimkata Yuda Iskariote... Mnaona?  Mungu hakumruhusu Yuda kusimama karibu na Bwana Yesu baada ya ufufuo.  Mungu alikatilia mbali uwakilishi wao wa kiroho na wa kiishara Mbinguni na sasa Mungu alikua akikata tafsiri yao ya kimwili duniani. [Kc23v10]

19  Hivyo, katika bustani hiyo, Adamu alikua na tafsiri, ufunuo kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya uliokuwepo haukuwa mti kama ule wa Ufunuo 22:1-2 bali nyoka, yaani viongozi wa dini.  Ni mti wa theolojia.  Je, mnaelewa hilo?  Kila Kiongozi wa Kiislamu, Mkatoliki, Mprotestanti, Mwiinjili au Mbranhamisti ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya.  Vizuri sana!  Ni hivyo.

20 Kwa hiyo Bwana Yesu Kristo ndiye mti wa Ufunuo 22:1-2 wenye matunda kumi na mawili na ambao majani yake ni wema wa kimiujiza wa kuponya mataifa.  Mnaona?

21 Basi sikilizen initakachosema kwa maana huu ni ufunuo wa kiroho wa mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao mnapaswa kujua: kiroho miti hii miwili ilikuwa Mungu na Shetani, Roho wa Mungu na roho ya shetani. 

22 Kisha ni miti ya kiroho tu kama tunavyoona katika Ufunuo 22:1-2 ambayo tafsiri yake ya kimwili ilikuwa kwa upande mmoja Adamu mwenyewe katika hali yake ya kimungu  kabla ya mwanamke kuumbwa, na kwa upande mwingine nyoka wa kabla ya kuanguka.  Na ikiwa tunda lililokatazwa na Mungu ni ni ngono, angalieni pia kila mwana wa Ibilisi kama mti wa ujuzi wa mema na mabaya.  Ninyi wanafunzi wangu, ndugu kama dada, jihadharini na mti huu!

23 Mnasema, “Ndugu Philippe, mwanamke pia?  ".  Ndiyo ndugu, Mungu alipokuwa anazungumza na Adamu katika Mwanzo 2:16, alikuwa anazungumzia mwanamke.  Kwa upande mmoja, mti huu wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa Hawa.  Mkiona mabinti hawa wametoa matumbo nje, miguu nje, sketi zinazochora sehemu za nyuma, hata kama ni dada, jihadhari naye!  Ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya.  Usile! 

24 Mnapowaona wasichana hawa wenye nywele za bandia, hawa wasichana wadogo wamevaa suruali na vifua vyao nje, ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya.  Na hamtaila mpaka Mwenyezi Mungu atakapo ifunika kwa Uzima kama Mariamu na kuwaruhusu kupitia mahari na baraka.  Hamtafanya tendo la ndoa kabla ya ndoa, yaani mahari.  Mnaona ?

25 Tuchukue sasa Ufunuo 12:1 "Na ishara kuu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili."  Hiyo ndiyo picha ya mti wa Ufunuo 22 na huyo ndiye mwanamke.  Na nyie akina dada, mnapowaona kama malaika tayari kuwanunulia nusu ya dunia wakisema maneno kama, "Nitakua siriazi na wewe...", jihadharini!  Ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya.  Mnaona?

26 Na jueni kwamba hapo mwanzo Hawa aliitwa Isha, yaani mwanamke.  Lakini alipozini, jina lake likawa Hawa, yaani, mama wa watu wote walio hai, mama wa wana wote wa Adamu na wa wana wote wa nyoka.  Vivyo hivyo, kanisa linapofanya ukahaba, mtaona jina lingine kuliko Kanisa la Yesu Kristo. 

27 Wakati fulani katika Ukristo, wakati kanisa la Yesu Kristo lilifanya ukahaba jina lake lilibadilishwa kuwa Katoliki.  Kisha likasimama na kufanya ukahaba baadaye, jina lake likabadilishwa kuwa Methodisti.  Na liliposimama karibu na mjumbe mwingine na kufanya ukahaba kisha mjumbe huyo, jina lake lilibadilishwa kuwa Mbaptisti.  Mnaona ?  Wapentekoste, Waadventista, na kadhalika.

28 Na ikiwa katikati ya Biblia, mti wa Uzima ulijidhihirisha kama Neno, pia jueni kwamba mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulijidhihirisha kama theolojia na wapenzi wake ni hawa makuhani na wachungaji wa Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na wa kibranhamisti ikiwemo wale wa kiislamu na kiyahudi.  Na Kelele ya usiku wa manane linasema kwamba hata mkiwa safarini msile wala msinywe kikombe cha mafundisho yao.  Wanahubiri mema na mabaya tu, yaani maadili na Biblia inasema kwamba ni maskini, vipofu, maskini na wako uchi.  

29   Na kwa kumalizia, napenda kusema kwamba hamwezi kuelewa ninachosema kama amzingatia upeo wa kiroho na kimwili wa miti hii miwili.  Kwa mfano katika Yohana 12:28-29 inasemekana: “…Basi sauti ikatoka mbinguni, nilimtukuza, na nitamtukuza tena.  Na umati wa watu uliokuwapo na uliosikia ukasema kwamba kulitokea ngurumo. wengine wakasema: Malaika alisema naye». 

30  Vema !  Mtazingatia nini?  Ngurumo au sauti?  Mnaona?  Ni hivyo.  Na wakati wa jioni siku moja William Branham alipokuwa akiwinda pamoja na ndugu fulani, kulisikika mingurumo mitatu, lakini badala yake, William Branham alisikia maneno matatu yakisemwa kwa sauti kuu: “Hukumu  Pwani ya Magharibi na siku mbili baadaye tetemeko kubwa la ardhi lilipiga Alaska. .

31 Kwa hiyo, mnapaswa kuona mti huu wa Ufunuo 22 kiroho kama mto na mito minne ya Mwanzo 2:10.  Mnasema, “Ndugu Filipo, je, Mwanzo 2:10 inazungumza juu ya mto wa kiroho?  Ndio ndugu, ni katika ono la Musa na tazameni kidogo na mtaona kuwa mto haulishi mito. 

32  Upande wa asili wa Mwanzo 2:10 hauwezekani.  Mto hautiririki kwenye mito bali mito inapita kwenye mto.  Kwa hiyo  kiroho ni Bwana Yesu Kristo na Injili nne, Bwana Yesu Kristo akiwapa uwezo na mamlaka  wanyama wanne wanaozunguka  kiti cha enzi na kwa mitume kumi na wawili.  Amina!


Comments