KACOU 22: UZOEFU WA YORDANI
(Ilihubiriwa ijumaa jioni, May 14, 2004 huko Locodjro, Abidjan – Ivory Coast)
1 Biblia inasema katika Ufunuo 12:7-9 na Isaya 14 ya kwamba kulikuwa na vita Mbinguni kwa sababu Shetani alitaka kuabudiwa kama Mungu. Shetani alisema: “Nitainua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, nami nitaketi juu ya mlima wa makutano... Nitafanana na Yeye Aliye Juu...”. Malaika wa Mungu walipigana dhidi ya Shetani na malaika zake na kuwatupa duniani.
2 Mabilioni ya malaika walitupwa juu ya ardhi na wakaenda kujificha nyuma ya maji, nyota, vichaka na misitu mitakatifu, sherehe, maagizo ya fumbo katika nchi zote. Badala ya" mapepo" au "malaika walioanguka" , wanaitwa katika Afrika wenye vipaji. Na hawa wajuzi waliwaamsha waganga wenye nguvu. Waliabudiwa na hamu yao ya kwanza ilitimizwa. Wenye nguvu zaidi kati yao walikuwa miungu halisi, hasa katika Misri, kati ya Inka, katika Babeli, katika India na wengine.
3 Kulingana na Ufunuo 14:6-8 , injili iliwaonya wanadamu waachane na haya mapepo maovu. Kwa mara ya kwanza, tulijua kwamba mganga, mwaguzi, mnajimu alikuwa nabii wa Shetani. Baada ya wafalme, ni waganga wa kienyeji na waaguzi ambao waliishi maisha ya starehe: mbuzi weusi, kondoo, kuku weupe, chupa za pombe ...
4 Naaona leo manabii hawa, jinsi walivyo matajiri! Ni makuhani wachawi waliojificha, bila ubaguzi. Madhabahu na mahali pa juu pa 2 Wafalme 17:29-31, madhabahu zile zile za 1 Wafalme 11:5-7 zimekuwa makanisa, misheni na huduma leo. [Kc.15v11] [Kc.32v27-28] [Kc.40v9] [Kc.108v16] [Kc.116v9] [Kc.118v13]
5 Na Serikali inapotoa kibali chake kwa mojawapo ya makanisa haya, misheni na huduma, ni uchawi ambao umehalalishwa.
6 Vema! Hebu sasa tusome 2 Wafalme 5. [Ndl: Ndugu Philippe anasoma sura nzima ya 2 Wafalme 5]… Vema! Kupitia njia ya msichana mdogo, Waziri wa Ulinzi wa Shamu alienda Israeli kwa nabii Elisha, nabii pekee wa kweli wa wakati wake, ili kupata uponyaji wa ukoma wake.
7 Waziri wa kwanza Naamani amwendea Mfalme wa Israeli ili kupokea makaribisho rasmi kwa heshima za kijeshi ili vyombo vya habari vitangaze hili. Walilifanya kama jambo rasmi! Kisha ona mstari wa 9, waziri Naamani akielekea kwenye nyumba ndogo ya nabii Elisha na mizinga, farasi, vitengo vya intelejensia, vikosi vya kijeshi. Haya yote ni kumwambia nabii Elisha kwamba anayekuja si mtu wa kawaida. Watu walitoka pembeni ya barabara kuona msafara wa magari ukipita na ving'ora na gwaride la waendesha pikipiki n.k...
8 Na hayo yote, bila kuhesabu hotuba ambayo angetoa, akitangaza vile vipande elfu sita vya dhahabu na dola milioni kumi kama alivyofanya siku zote katika makanisa mengine huku wakipiga makofi. Kwa mbali tukasikia ving'ora, kisha waendesha pikipiki wakatokea, Waziri Naaman na kikosi kizima hawakuwa mbali...
9 Wakaja na kusimama nje wakingoja heshima kutoka kwa nabii Elisha. Lakini walijipata wamemkosa nabii. Mnaona? Naamani alipofika mbele ya makao ya Elisha, alisema moyoni mwake: “Lakini yako wapi mapambo kuhusiana na ujio wangu? Watoto hawakutakiwa hata kwenda shule leo kwa sababu ya kuwasili kwangu. Au si hapa? ". [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Ilikuwa ni hapo! Mnaona?
10 Lakini Elisha alikuwa akiona nje Msiria moja maskini aliyepofushwa na utajiri na utukufu wa ulimwengu ambaye mateso ya kuzimu yaliwekwa akiba kwa ajili yake ikiwa hakutubu Elisha aliona ukoma wa mwili , nafsi na roho yake, na tibabu ilikuwa uzoefu wa Yordani. Elisha aliweza kunusa harufu ya ufisadi nyuma ya kombati au koti hilo. Ilikuwa hivyo!
11 Naamani pia alitaka heshima kutoka kwa nabii huyu anayeishi peke yake, lakini Elisha akatuma mjumbe kwake akisema: “Nenda ukajitupe mara saba katika Yordani nawe utakuwa safi. Naamani akakasirika!
12 Alikuwa ameanza kuelewa kwamba yeye, Naamani, mtumishi mkuu wa Mji ndogo wa Siria hakuwa kitu mbele ya yule nabii mdogo wa Mungu mkuu. Namna gani ameniambia niende kujitupa kwenye maji yenye matope kama Yordani!" Je! Farpari na Labana, mito ya Siria siyo bora? ". Naamani akaongeza: “Je! ilipangwa anibatize pia?… Na nabii mwenyewe haji lakini ni mtoto mdogo aneye mtuma ?". Watumishi wa Naamani wakasema: “Bwana, kubali!…” Lakini Naamani akasema: hatukutajarisha hata vazi ya hali moja kwa ajili ya ubatizo! Na watumishi wake Waka jibu tena wakasema : Bwana, ukubali!...". Mnaona? Amina!
13 Alihitaji uponyaji lakini alitaka uponyaji katika ukuu. Naamani hakuwa tayari hata kupiga magoti kwa sababu nguo yake inaweza kuchafuka magotini. Alisema: je ilipangwa nifanye hivi? Je, ilipangwa nifanye hivyo? Watumishi wake wakasema: Bwana [kama] nabii angekuomba [ufanye] jambo kubwa, si ungelifanya? , Kubali!” Vipi zaidi, alikwambia : Jioshe nawe utakua safi. Bwana, kubali. Tazameni mstari wa 11: “Naye Naamani akakasirika, akaenda zake, akasema: Tazama, nilidhani, hakika atatoka na kusimama mbele yangu na ata alika jina la Bwana, Mungu wake, na ku papasa mkono wake juu ya mahali pa ugonjwa; na kuponya ukoma.” Mnaona?
14 Alipofika, Naamani alikuwa tayari amefanya mpango wa kupokelewa kwake, kuponywa kwake. Lakini, akiwa Siria kama angejua kwamba yeye, Naamani, atatendewa kama mtu wa kawaida, hangekuja. Lo! !Maskini Naamani! Lakini mwisho alipojitupa ndani ya Yordani mara saba akatakaswa toka ukoma akawa safi. Amina! akarudi kwa Elisha ambaye alimhubiri Kelele ya usiku wa manane baada ya hapo akamwambia Elisha kwamba hatatoa tena sadaka za kuteketeza kwa miungu mingine katika kanisa lolote. Alikuwa amebadilika, hakutaka tena hotuba ya kukaribishwa, kiti cha kukaribishwa kwa sababu alikuwa amepita Yordani... Oh ! Uzoefu wa Yordani
15 Katika mstari wa 9, Naamani alitaka kusimama kwenye mimbari kutoa hotuba yake ambapo angetangaza vipande elfu sita vya dhahabu na dola milioni kumi za fedha na nia yake ya kuweka lami kijiji cha Elisha na kupeleka huko umeme, maji ya kunywa. na wodi ya uzazi. Licha ya hali halisi, alikuwa anaenda kuonyesha uhusiano mzuri uliopo kati ya Israeli na Siria. Mnaona?
16 Angeweza kusema: “…Mimi, Naamani mnyenyekevu, Waziri wa Ulinzi wa Siria, nimepata nishani ya Heshima mara tatu… heshima ya Tuzo ya nchi kama hii! …”. Mnaona? Alikosa kitu kimoja tu: uzoefu wa Yordani. Alitaka umaarufu na ukuu wa kibinadamu, lakini sio Wokovu! Na ni vivyo hivyo leo, kwa mawaziri na marais wetu mashoga, wanuka pombe na dhambi ambao hawataki uzoefu wa Yordani na nabii ambaye Mungu amemtuma kwao. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. Mnaona?
17 Na ukoma halisi wa waziri huyu, ulikuwa ni cheo chake cha kijeshi, mali zake, magari yake ya vita na nyumba zake za kifahari ambazo zitaangamia duniani na ambazo zilimfanya aamini kwamba yeye alikuwa kitu mbele ya yule nabii mdogo. Mnaona? Naamani alisema katika mstari wa 11 kwamba alifikiri nabii angekuja mwenyewe na kumwomba aidha mfungo kavu wa siku tatu au sadaka kubwa. Hivyo ndivyo alivyokuwa na dola milioni kumi tayari kwa ajili yake, alijua manabii walipenda pesa.
18 Sasa alikuwa amewajua manabii wa Baali pekee hadi wakati huo. Manabii wa makanisa ya Farpari na Abana walipenda pesa. Mnaona? Lakini baada ya uzoefu wa Yordani, alisema: "Sitatoa tena ruzuku au kufadhili chochote, hata kama itanigharimu wadhifa wa uwaziri, ubunge, umeya ... sitaenda tena kuinua Jiwe la uzinduzi bila utaratibu ...".
19 Watu wanataka makanisa ya Farpari yenye fukwe nzuri lakini kinachohitajika ni uzoefu wa Yordani na nabii aliye hai wa wakati wako.
20 Na baada ya tukio la Yordani, waziri Naamani alijifanya mtumishi wa Elisha, akirudia mara tano kwamba yeye ni mtumishi wa Elisha. Kwa mara ya kwanza waziri huyu alitambua kwamba kulikuwa na ibada mbili, aina mbili za makanisa na manabii. Katika mstari wa 10, Naamani hakuwa ameelewa kwamba alikuwa duni mbele ya mjumbe wa Elisha lakini sasa alielewa. Naamani sasa aliona kwamba wafalme, mawaziri, manaibu, mameya, wachungaji, makuhani, manabii, na marais wa dunia walihitaji uzoefu wa Yordani. Mnaona?
21 Nyuma ya mtu huyu mwenye mamlaka na kiburi, nyuma ya utukufu huu na utajiri usio na maana, alikuwa akijificha mtoto wa Mungu, mtu mnyenyekevu ambaye jamii ilikuwa imemwaribu. Jamii ambayo yenyewe inafahamu tu makanisa ya Farpari na Mchungaji Gehazi...
22 Mheshimiwa Waziri, mbunge, Meya, Mheshimiwa Mkurugenzi, wakati nyinyi watu mna mahali pa heshima katika makanisa, wakati wa kuanzisha au kufadhili shughuli za kidini, ukikubali, basi ukoma wa Naamani unakuwa juu yako na wewe unahitaji uzoefu wa Yordani.
23 Ukienda kanisani kutafuta watu kwa ajili ya uchaguzi, ukitoa sadaka kwa kanisa ili kupata kibali cha watu kwa ajili ya uchaguzi, basi ukoma wa Naamani uko juu yako na haya ni makanisa ya Parpar na mheshimiwa Gehazi ndiye mchungaji. .
24 Ikiwa katika kusanyiko, mchungaji ana kiti maalum, si Yordani. Je, Yesu angeweza kutofautishwa na wanafunzi? Je! Yuda hakusema: "Nitakayembusu, ndiye". Je, mtumishi ni mkuu kuliko bwana wake? Watoto wa shetani sasa wameketi juu ya mwana punda wa Yesu.
25 Ninyi manabii na marais wa makanisa shukeni na mje Yordani! Ondokeni kwenye fukwe nzuri za Farpari na Abana!
26 Kanisa lile ambapo mchungaji ama nabii mke ama nabii ameketi pale jukwaani mbele ya kusanyiko, hiyo ni Farpari, na mheshimiwa Gehazi ndiye mchungaji wake. Wanawake wenye jeuri, wanawake wenye hedhi wanaoketi jukwaani, binti za shetani!
27 Na ni Yezebeli aliyewaambia binti zake wafanye hivyo kama yeye mwenyewe anaketi kwenye kiti cha ufalme wakati Ahabu hayupo. Ni mjukuu wa Yezebeli pekee ndiye anayeweza kuketi hapo, mbele ya wanaume, bila kusumbuliwa moyoni mwake. Binti za makahaba, wajeuri kama mama zao! Mnaona? Kanisa la Farpari linaweza kufanya hivyo na mheshimiwa Gehazi ndiye mchungaji wake. [Kc.9v8] [Kc.10v58]
28 Kanisa hili lenye kiyoyozi, zulia, linaloruhusu televisheni, ukumbi wa michezo, mpira kandanda, ufukwe... ni Farpari na mheshimiwa Gehazi ndiye mchungaji wake. Kanisa hili ambalo wanawake wameketi na nywele za bandia, suruali, na rangi za kucha... ambapo wanawake wako kwenye mimbari kwa ajili ya mahubiri au nyimbo, ni Parpar na Gehazi ndiye mchungaji wake.
29 Kanisa hili ambalo mchungaji wake ana gari kubwa na waumini wake ni maskini ni Parpar na Elisha alihubiri dhidi yake katika mstari wa 26. Wana mabasi, teksi za usafiri, hisa katika makampuni, taasisi,na kadhalika ... ni Farpari na mheshimiwa Gehazi ndiye mchungaji wake. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”]. [Kc.9v20-24]
30 Elisha alilaani jambo hili katika mstari wa 26, wao ni watoto wa Gehazi na Elisha aliwahubiria Kelele ya usiku wa manane. Wanachohitaji ni uzoefu wa Yordani. Naamani Waziri wa Ulinzi alitaka kanisa ambalo simu yake ya mkononi inaweza kuita katikati ya mahubiri, ambapo mahubiri hayapingi anasa na starehe; ambapo utalii hauhukumiwi, ambapo ushoga hauhukumiwi, kanisa kulingana na ladha yake ambapo atabatizwa katika bwawa la kuogelea au kisima cha ubatizo.
31 Kwa kweli, Naamani alikuwa akimtafuta mmoja wa hawa makuhani wachawi waliovalia koti na Biblia mkononi na akakutana na nabii wa kweli wa Yesu Kristo
32 Unapoenda kwenye mkesha wa maombi ya makuhani hawa wachawi, iwe unatoka katika kanisa Katoliki, la Kiprotestanti, la Kiinjili au la Kibranhamisti, haijalishi, onyesha shida yako! Lakini Elisha alihitaji uzoefu wa Yordani kwanza, naam! Uzoefu wa Yordani. Alihubiri Kelele ya usiku wa manane kwa waziri huyu!
33 Mawaziri, wabunge, mameya, wakurugenzi na marais... mnataka kuponywa ukoma, saratani, vidonda, UKIMWI ? Nenda kwanza Yordani! Tafuta uzoefu wa Yordani! Ikiwa mtu anajiita mtu wa Mungu na akakubali kuomba kwa kukwepa uzoefu wa Yordani, yeye ni mchawi! [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
34 Wenye mamlaka huomba maombi ya hawa “manabii” katika nyumba zao kwa siri, mara nyingi chumbani kwa miadi. Badala ya mbuzi mweupe au kuku weusi, wanawauliza wafunge na kuona jinsi manabii hao wanavyonenepa kama waganga wa kienyeji kijijini, wakiwa na nyumba za kifahari na magari, koti za Kimarekani badala ya ngozi ya kondoo.
35 Je! si manabii, wasemaji wa Mungu, waliowafundisha ninyi kwamba dhahabu na fedha ni mali ya Mungu na kwamba manabii hao hao, kwa mfano wa Eliya na Yohana Mbatizaji, walivaa ngozi za wanyama? Mnaona? Unahubiri injili nyingine na watoto wa Elisha watakataa! [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
36 Na je, ningeuacha msitu uliobarikiwa na tulivu ambapo nilizaliwa ili kwenda likizo Ulaya? Hatutawahi kupokea ruzuku, hatutawahi kuomba ruzuku na ufadhili kutoka kwa watu. Hatutakubali kamwe ushirikiano na urafiki kutoka kwa kanisa. Furahia Yordani kwanza!
37 Rais au waziri hatatualika kwenye meza moja na wewe! Hakuna mtu atakayetualika kwenye meza moja kama Wakatoliki, Wabaptisti, foursquare , Kusanyiko la miungu, Wapentekoste… wacha watafute uzoefu wa Yordani kwanza!…
38 Hata kwa ugonjwa wa wazazi, nitamsaidia ashuke kwanza Yordani. Itakuwa ni uovu kwangu kuwaombea wakiwa bado wanaomba kwa wabaptisti, wapentekoste, wabranhamisti, CMA, Wauamsho, Waadventista, Wakatoliki, Wanazarini... Huku wakiruhusu mikono yao kuwekwa na hawa makuhani wachawi katika koti, wanakimbia kwenye mikesha yao ya maombi. Mnaona? Ni lazima wakate uhusiano wote na wachungaji wa Parpar na makanisa. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].
39 Naamani alipoponywa, alitambua kwamba hakuna Mungu ila wa Elisha na hatawahi kumsujudia mwingine. Ningeombeaje Mkatoliki, Mprotestanti, Mwikinjili au Mbranhamisti, mashoga kama hao? Nitafanyaje wakati bado wanaenda kumwabudu mungu wao? Mungu apishe mbali! Je, nitamwombeaje mtu anayesema, “Kanisa ni kanisa, ni [mungu] yuleyule”? Wala kwa baba yangu, wala kwa mama yangu, sitafanya hivyo, ikiwa sivyo kwamba Mungu afungue akili zao kuelewa hili! Na tukishindwa, Mungu atusaidie!
40 Je, Biblia haisemi katika Kumbukumbu la Torati 13:1 kwamba akitokea nabii akifanya miujiza au akitoa ufunuo ya haki na kusema, “Twendeni kwenye kanisa la Baptisti, twende kwenye kanisa la foursquare, twende kwa kanisa la kiinjili. , kanisa la kipentekoste, kanisa la Kusanyiko la miungu... twende kwenye makanisa kama haya, misheni au huduma…”, usiende huko? Je, makanisa haya si mahali pa juu pa 2 Wafalme 17:29-31 na kwamba miungu Dagoni, Adrammeleki, Baali, Rimoni, Baal-Zebubu, Kemoshi, Moloki... si wote wanaitwa Yesu-Kristo leo?
41 Na je, Mungu hakutuma Ujumbe huu kuwafichua? Je, Biblia haikusema katika Mathayo 24:24 kwamba watatokea makristo wa uongo kutoka kuzimu? Je, mtu anawezaje kujiita nabii, yaani, msemaji wa Mungu wakati hana Ujumbe na kila anachosema ni kurejerea Biblia. Anaanza kufanya miujiza ili kuthibitisha Ujumbe gani?
42 Nabii anawezaje kuweka kanisa, misheni au huduma kwenye Biblia badala ya kuleta Ujumbe mpya ambao wanadamu hawaujui? Ni waganga na waganga hata wakiwa kwenye makoti na biblia mkononi. Hakuna Elisha wawili wala Yordani wawili. Wote ni makuhani wachawi na mifungo wanayokuomba ni taswira ya mbuzi mweusi au kuku mweupe.
43 Kwa wateule, Wanaamani wa kweli, Biblia ilisema katika Mathayo 25:6 na Ufunuo 12:14-17 kwamba Injili itakuja na kuwachukua kutoka kwenye upotofu… mbali kutoka katoliki, Kiprotestanti, kiinjili, kibranhamisti na makanisa ukijumuisha Uyahudi na Uislamu mbali na manabii hawa wa uongo. Mnaona?
44 Na kama katika siku za Nuhu, nje ya sauti hiyo unayoisikia leo, hakuna Wokovu popote. Na siku ya hukumu hutasema hukuonywa! Na mwenye masikio na asikie! [Kc.7v49]
Comments
Post a Comment