KACOU 21: KUAMULIWA KIMBELE


(Ilihubiriwa jumapili february tarehre 01, 2004, huko Locodjro, Abidjan – Ivory Coast)

1 Sisi si wa muda bali wa milele.  Kabla ya kuwepo malaika au nyota mbinguni au chembe ya jiwe duniani, ninyi na mimi tulikuwepo, tayari tumekombolewa kulingana na Waefeso 1:4.  Lakini miili yetu iliumbwa siku ambayo Mungu alimuumba Adamu. Adamu akamzaa Sethi, Sethi akamzaa Henoko, Enoko akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Mahalaleli… Na hiyo ikaendelea mpaka babu yangu ambaye alimzaa baba yangu.  Ninyi na mimi tulikuwa katika viuno vya Adamu wakati wana wa Ibilisi walikuwa katika viuno vya joka ambaye alitembea na kuzungumza kama mtu katika bustani la Edeni.  Mungu alichukua maji, potasiamu, mafuta, magnesiamu, chuma ... Mungu alichukua vipengele kumi na nane na kuumba mwili wetu.

2 Lakini roho yetu inayokubali Kelele ya usiku wa manane ilikuwa tayari pale kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  Roho yetu tayari ilikuwa pale Mungu alipoumba miili yetu.  Na kwa hivyo ni kwa kuchaguliwa kimbele kwamba mtu anakubali Injili ya wakati wake kulingana na Matendo 13:48 na Warumi 8:29-30 au kwamba anakubali udanganyifu kulingana na Ufunuo 13:8.

3 Nuhu alipokuwa akihubiri hatia na hukumu juu ya mifumo ya kidini ya siku zake na ya kwamba wana wa ibilisi walikuwa wakisaga meno, wakipiga kelele, “Nuhu!  Kamwe hatutakubali Ujumbe wako, tutabaki katika makanisa, misheni na huduma zetu.  Daima tutatumia Biblia zetu za Louis Segond, Thompson, Scofield ambazo unazichoma. Tumepata pia makosa katika toleo la Darby unalotumia… Tunapumzika katika Henoko, baba yetu ambaye alinyakuliwa…”.  Mnaona?  "Tunapumzika katika Yesu Kristo aliyesulubiwa, tunaye Musa, Tommy Osborn, Billy Graham, William Branham...". Walikuwa wakimzungumzia Henoko ijapokuwa, Henoko hakuwa tena duniani. Na leo wanazungumza kuhusu William Branham ijapokuwa William Branham yuko kwenye makaburi ya Jeffersonville.

4 Lakini ikiwa leo mlimwamini Kacou Philippe, nabii aliyeahidiwa kwa wakati wako, ni kwa sababu mlidhihirisha mbegu hii katika wazo la Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!]. 

5 Musa alipokuwa akivuka Bahari ya Shamu pamoja na Wayahudi, tulikuwa pale tukishangilia kwa furaha, lakini hatukuwa na miili bado.  Wakati Yeremia, Isaya, Ezekieli, Amosi... walipokuwa wanatabiri dhidi ya mifumo ya kidini ya siku zao, tulikuwa pale tukipiga kelele, “Amina!  Amina!  Amina!  ".  Wakati Bwana Yesu Kristo alipopaza sauti akisema, "Uzao wa nyoka, nyoka kwenye nyasi, makaburi yaliyopakwa chokaa, wapumbavu!"  …”, wewe na mimi tulikuwa pale tukishangilia kwa furaha: “Haleluya!  Hosana!".

6  Wakati Martin Luther alipokuwa akilihukumu Kanisa Katoliki, wakati John Calvin alipokuwa akiwashutumu Walutheri, wakati William Branham alipokuwa akilaani mifumo ya kidini ya wakati wake kule Marekani, wewe na mimi tulikuwa pale tukisema “Amina!  kwa kila neno lao.  Lakini, hatuwezi kuokolewa na hawa manabii wote hadi William Branham kwa sababu sisi si wa kizazi kimoja.  Hatukuwa nao duniani, hatukuwaamini walipokuwa hai duniani.  [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].

7 Tangu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kila mjumbe alikuwa pamoja na kundi lake katika wazo la Mungu.  Wakati Musa alivuka Bahari ya Shamu, Eliya naye alivuka na nafsi zake elfu saba.  Isaya pia alipita na watu wake.  Yeremia pia akapita na watu wake.  Amosi akapita na watu wake.  Habakuc akapita na watu wake… 

8 Bwana Yesu Kristo, na wale mitume kumi na wawili na wote walioamini kwa wakati wake, akapita na kundi lake.  William Branham, na wote waliokuwa wamemwamini alipokuwa hai duniani, wakapitia pamoja na kundi lake.  Na Kacou Philippe pia alipita pamoja na wale wote wanaomwamini leo. [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina! ”].  

9 Na mnamo Aprili 24, mwaka wa 1993 kabla ya Malaika na Mwana-Kondoo kushuka, wewe na mimi tulikuwa pamoja.  Hebu tusome hilo: “Na mimi, Danieli, nikaona maono peke yangu, na wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono hayo, lakini tetemeko kubwa likawaangukia, na wakakimbia ili kujificha“. Hayo pia yakatukia katika Kutoka 19 na wakamwambia Musa, "Mungu na aseme nawe na wewe utuambie."  Mnaona?

10 Katika maono ya Aprili 24, mwaka wa 1993, sikuwauliza kwamba walikuwa akina nani au walitoka wapi kwa sababu walikuwa pamoja nami bali ni ukubwa wa maono hayo ndio uliowafanya kukimbia ili kujificha.  Nilipokuwa katika roho, Katika maono, nilifikiria kwamba walikuwa pale pia.  Danieli 10:7 inasema kile kilichotukia Aprili 24, mwaka wa 1993. Na Mungu Mwenyewe alikuwa na furaha pamoja nasi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].  

11 Na mimi Kacou Philippe, nilikuwa na furaha pamoja nanyi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  Na kama vile mitume watakavyoketi katika viti kumi na viwili kuhukumu wale waliokuwa duniani wakati wa huduma ya Bwana Yesu, kwa njia hiyo hiyo mimi na nyinyi pia tutawahukumu wale wanaoishi duniani leo. Mnaona? [Kc.117v29] [Kc.129v3] [Kc.135v13] [Kc.136v31]

12 Kabla Yuda Iskariote hajazaliwa, alikusudiwa tangu zamani kumsaliti Bwana Yesu Kristo na kwenda kuzimu.  Bwana alisema, "Mmoja wenu ni pepo."  Na Matendo 13:47 inasema kwamba Neno la Mungu liliendelea kati ya mataifa na wale waliokusudiwa Uzima wa Milele waliamini.  Hii ni chini ya ukuu wa Mungu. 

13 Kabla Yakobo na Esau hawajazaliwa, walipigana ndani ya tumbo la Rebeka.  Kwa nini?  Kwa sababu Mungu alikuwa amewachagua tangu awali kuwa Israeli na Waarabu duniani.  Mungu alimwambia Ishmaeli, baba wa Waarabu na Waislamu, kwamba atakuwa punda mwitu na mkono wa kila mtu utakuwa dhidi yake na mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu.  Wazao wake watakuwa walipuaji, aina ya wanyama wasio na moyo.  

14 Na vivyo hivyo, Mungu alijua kwamba wana wa shetani wangekusanyika katika makanisa ya Kikatoliki, Kiprotestanti, kiinjili na kibranhamisti kwenda kuzimu kulingana na Mathayo 13:24-30.  Kuhusu nyinyi, Mungu alikuwa amewachagua tangu awali mniamini kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.  [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].

15 Na kwanza, maono ya Aprili 24, mwaka wa 1993 yalitukia Mbinguni kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu katika mawazo ya Mungu.  Kisha yalitukia duniani mnamo Aprili 24, mwaka wa 1993 wa wakati wetu.  Kabla ya kuniona na kunisikia, mliniamini na hayo yanaendelea kutumia sasa, huku wengine wakinichukia na kunitesa.  [Kc.19v42]

16 Na leo, Kelele ya usiku wa manane inaposikika, watakatifu wote pamoja na wale wanaolala husema “Amina!  kwa kila Neno.  Biblia inasema katika Ufunuo 17 na Ufunuo 13 kwamba wale ambao majina yao hayakuandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu watabaki katika makanisa haya ya Kikatoliki, Kiprotestanti, Kiinjili na Kibranhamisti yakiwemo Uislamu na Uyahudi.  Watabaki katika misheni na huduma hizi lakini wateule watalikubali Neno la Mungu si kwa hekima na ujuzi wa Biblia au kwa akili, bali kwa kuchaguliwa tangu hawali.

17   Matendo 13:48 inasema, "...na wote waliokusudiwa uzima wa milele wakaamini."  Sio mwenye kukuesha wala wenye kuwa makini lakini bali walio chaguliwa tangu awali. Sio Mungu anayewasukuma washiriki wa makanisa haya kunikataa, lakini Mungu anajua kwamba watanikataa.

18 Kelele ya usiku wa manane ilipolia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu katika nia ya Mungu, tulikubali na majina yetu yakaandikwa Na damu ya Mwana-kondoo katika kumbukumbu mbele za Mungu.  Na mnamo Aprili 24, mwaka wa 1993, kulingana na Mathayo 25:6, wakati kelele ilisikika duniani, majina yetu yalitamkwa kulingana na Ufunuo 2:17.  

19 Ujumbe wa nabii ni orodha ya majina ya wateule wa kizazi chake.  Na kifo cha nabii kinakuja baada ya mwito wa mteule wa mwisho wa kura yake.  Eliya na Musa hawatakufa kabla ya kuitwa kwa wateule 144,000.  [Ndl: Kusanyiko linasema, “Amina ”].  Na baada ya kusikia Kelele ya usiku wa manane duniani, tuliitikia wito wa harusi.  Kuna kujulikana kimbele.  Naye John Calvin alihubiri jambo hilo na kuliita kuchaguliwa hawali maradufu, ambako ni kuchaguliwa tangu zamani kwa Uzima wa Milele na kuamuliwa tangu zamani kwa upotevu.  [Kc.120v26] [Kc.130v4]

20 Na kama mwana wa Ibilisi akisikiliza hilo, atasema, Lakini ikiwa Mungu amekwisha kuwachagua wengine na kuwahukumu wengine, kwa nini kuenda kanisani?  “Ndugu, msikengeushwe, Mungu ni mjuzi wa yote na ni mkuu.  Ni kama mtihani wa kuingia katika utumishi wa umma ambapo serikali inahitaji watu kumi na uko kwenye orodha ya watahiniwa mia mbili.  Ndugu, ni kwa sababu wagombea mia moja na tisini wataondolewa ndio maana hautakwenda kufanya mashindano?  Nenda ukatunge kwa imani!  

21 Malaika wa nuru akija kuniambia kwamba sitaokolewa, nitamwambia kwamba Mungu ataweka jina langu kwenye orodha ya wana wa Israeli kama Ruthu na Rahabu!  Ni binti za mataifa lakini leo ni Wayahudi.  Nao ni bibi wakubwa wa Bwana Yesu Kristo.  Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.  Na ni kwa sababu jina lako limeandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo ndipo uliamini Ujumbe wa nabii aliye hai wa wakati wako [Mh: Kusanyiko linasema: Amina!]. Na unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba jina lako halifutwi kama Yuda Iskariote.

22  Katika Ujumbe huu wako ndugu walioniambia: “Ndugu Philippe, nilikuwa nimeamini katika ndoa ya wake wengi, nilikuwa nimeamini kwamba kilemba ni kifuniko cha kichwa, niliamini pia kwamba zaka imefutwa lakini nilipouamini Ujumbe huu, hata sikutaka kujuwa, sijawai uliza swali kuhusu mambo hayo… nilizika imani zote za zamani ili kuendana na kile ambacho Ujumbe wa wakati wangu unasema…”. Amina!  Ndugu, Mungu awabariki!  Na hivyo wakajikuta katika Ujumbe huu wa watu wanaotoka katika makanisa na dini zote kwa sababu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, Mungu alikuwa ameamua hivyo.

23 Vema! Hebu turudi katika Mwanzo... Nuhu alipokufa, alikwenda kuhubiri kuzimu, watoto wa Kaini walikataa, lakini wa Sethi walikubali. Yeremia alipouawa na wanadini wa wakati wake, alikwenda kuwahubiria wale ambao hawakumwamini Nuhu, lakini licha ya mateso, walimkataa Yeremia, hakuna hata mmoja wao aliyeweza kutubu.

24  Isaya alipokatwa vipande-vipande na makuhani na watu, wakati kila nabii mjumbe, kulingana na Mathayo 23:35, alipokufa, alienda kuhubiri injili yake kuzimu.  Na wale wote ambao katika maisha yao walikuwa wameukataa Ujumbe wa nabii aliye hai wa wakati wao, waliukataa huko pia. Na wale waliowapiga mawe na kuwatesa Manabii wakiwa hai, walitaka kuwapiga mawe na kuwatesa licha ya mateso, lakini wale walioamini ujumbe wao walipokuwa hai walifurahi. 

25 Ayubu alipomwona Bwana Yesu Kristo, alipiga kelele, “Je, sikusema kwamba macho yangu yatamwona Mkombozi wangu!  ".  Ayubu akipiga kelele, Ayubu akiruka-ruka kwa furaha, Ayubu akifurahi.  Mnaona ?  Wakati huohuo, wana wa shetani wa wakati wa Nuhu, walisaga meno yao dhidi ya Bwana Yesu Kristo.  Leo, kama vile Kelele ya usiku wa manane ya Mathayo 25:6 inavyosikika duniani, ndivyo ilivyo kama siku za Nuhu, Bwana Yesu Kristo, na kila nabii.

26 Naye Bwana Yesu Kristo alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa,” bila shaka, pamoja na uwepo wa Nuhu duniani. Ibilisi anazidisha makanisa, anafanya maajabu ili kuwaacha bumbuwazi wana wa shetani na kuwapeleka mbali na kile ambacho Mungu anafanya, na wanaamini kwamba wameokoka. 

27 Bwana Yesu Kristo alisema kwamba kama nyakati hazingefupishwa hakuna mtu ambaye angeokolewa.  Lakini angalia makanisa haya yote ya kikatoliki, kiprotestanti, kiinjilisti na kibranhamisti, na misheni na huduma, na wongofu wao lakini ninawaambia ya kwamba hayo yote ni utongozi wa Shetani.  Wote wataenda kuzimu.  Wokovu haupo katika kanisa, pamoja na mtume, mwinjilisti, nabii wa kanisa, mwalimu na wengine, bali kando-kando ya nabii mjumbe wa kizazi.  [Ndl: Kusanyiko linasema: Amina!].  [Kc.3v26]

28 Tambua kwamba kulingana na siku za Noa, ni wachache sana watakaookolewa.  Na kundi la Mathayo 25:31 hadi 41 linahusiana na wale waliofanya mema kwa  wafuasi m walioleta ukweli tukufu na ambao walichukiwa na kuteswa na kupelekwa mbele ya mahakama na ulimwengu wa kidini.  Hili linawekwa wazi zaidi katika Mathayo 10:41-42. Zaidi ya hayo ni tafsiri potofu.  Mnaona kwamba hapo tena sio jambo rahisi wakati ambapo tunahukumu watu wote.  Utawezaje kumpa glasi ya maji mtu anaye hukumu watu wote ?

29 Kwa hivyo ikiwa utatoa toni za mchele kwa wafungwa wa Kibaptisti, na unafikiri kwamba inahusiana na Mathayo 25:34-40, hiyo ni tafsiri potofu. Bahada ya hiyo inahusu watu waliotenda mema kwa manabii au wafuasi waliosulubiswa na wanadini wa wakati wao.  Kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, walikusudiwa kufanya hivyo.  Na mwenye masikio ya kusikia asikie.


Comments